Wanaume mkiondoka nendeni moja kwa moja.

Wanaume mkiondoka nendeni moja kwa moja.

Hiyo hali ya ww kumtukana inadhihirisha kwamba bado hujamove on! Una hasira naye na usimcheke kwakuwa hata ww hiyo hali itaendelea kukuandama tu hadi pale utakapokuwa tyr kusamehe kutoka moyoni kisha aidha myasuruhishe mmalizane au kila mmoja ashike za kwake.

Ogopa sana mtu ambaye umemtenda ukahangaika weeee na vidampa huko kisha baadaye unakuja kurudi kwake hakutukani wala nini , hakutolei shombo, ila anakuhurumia kwa kukupa maneno ya kukutia nguvu na kukutaka usikate tamaa maisha ndivyo yalivyo na mwishoni anakwambia yy ameshapiga hatua haupo tena moyoni mwake - weeeeeeeee utajuta nakwambia.

Nakuahauri kama utaamua kumsamehe hakikisha hamgusani hadi mpime afya zenu kwa utaratibu unaotakiwa ili kuilinda afya yako maana huwezi kujua huko alikopita kapewa mangapi
Neno mujarabu...!
 
Habari za mida?
Mimi ni mdada niliyewahi kutendwa na nikaumia sana sana sana hata niliwahi kuona maisha yangu hayana thamani yoyote.
Nilishawahi kujaribu kujiua mara kadhaa lakini ilishindikana. Maisha yakaendelea na nikazoea kidogo kidogo. Mwenzangu akaenda kwa wanawake wengine kwa sababu tu kuwa amenichoka.
Amebadilisha wanawake kwa karibia miezi saba sasa toka aniache. Kila wiki ana mpya hata akawa anapitia hadi wauza baa na wamama walioolewa. Sasa ametendwa na huyo mpenzi wa baa, amepigwa na kuumizwa sana na huyo msichana, amerudi tena kwangu kuwa mimi ndiye mtu wa kweli kwake, hataki niondoke maishani mwake. Muda huu hata hamu ya mwanaume sina kabisa. Nikimtazama kama mpenzi napata hasira na sifurahii kuwa naye.
Sasa namtukana lakini bado ameganda tu jamani. Wanaume mkitaka kuondoka nendeni kimoja, hata tukiwapenda vipi kuna muda mioyo yetu inabadilika khaaaaaaaaa....
bahari ina sifa moja tu, nayo ni kupokea maji,
 
Maintain your position ukiyumba kidogo umeisha
Wanaume si watu wazuri
 
Hadi anarudi kwako inaonekana haujamsahau na una mazoea nae sana. Huyo anakuchukulia msukule wake usio na nguvu ya kumpinga.

Mtu akikuumiza kihivyo mfungie vioo kila kona sio anatuma sms moja unajibu mara nne,anapiga unapokea haraka na kuongea kwa furaha kama vile umeambiwa ulitumbuliwa kwa bahati mbaya hivyo urudi kazini na mishahara yote utalipwa.
Naona kuna ka ukweli....lakini ni mchungu.
 
Hapo wewe ndio mwenye maamuzi yaliyo sahihi
sababu ndio unayemuona alivyokuwa nyuma na sasa tofauti iko wapi.

Ila pia nikwambie umakini naye unahitajika kwani huenda ikawa ana lake jambo ndio sababu anajifanya kukuganda.
Neno la nguvu...mleta uzi chukua hatua.
 
Tumeyaongea jana kwamba sitakuacha tena mpaka kifo, ila hujaridhika umeamua kuyaleta JF.
Tulia mama nakupenda sana.
 
Ukimwi upo na unauwa mtapima, lakini tabia
Tabia ni kama ngozi vile..... Ngumu sana kubadili rangi yake....!!! Kupima watapima.... Lakini pia si wapo ambapo mwanzo wa mahusiano walikuwa negative.... Baada ya miaka 7-10 ya NDOA... Kuna mmoja kamuambukiza mwenzie....!!!!

Tabia ya mtu ni ngumu sana kubadilika.... Asidanganywe na vimachozi uchwara....!!!! Tehe....!!😉
 
Kifupi ni kwamba alipokuacha huku move on, yaani ulikuwa unasubiria ipo siku atarudi. Kama uliamua kusonga mbele ni wazi ungefunga kila njia ya yeye kukutafuta tena na wala usingejua ishu zake za kutembea na wanawake wa bar. Msamehe tu
 
Ulitaka ujiue kisa mwanaume ambaye hata si mmeo!

Kila wiki anabadili wanawake, unajua updates zake zote, hukuwa tayari kumove on.

Kwa kiwango hiki Cha ujinga ulichonacho, utamkubalia, atakutumia na kukuacha tena.. and oh good luck with them STDs
 
Sasa ukimkubalia hapo kuendelea na wewe ndio penzi litanoga,futa yote aliyokutendea moyoni mwako,anza naye upya,tena kwa style unayotaka wewe,nisikilize mimi hutajutia,unaweza ukasema ngoja nitafute miwngine akaja kukutenda zaidi hata ya huyo na ukija kumrudia tena wa kwanza unakuta naye kaghairi hakutaki tena...
 
Nimeipenda sana
Hiyo hali ya ww kumtukana inadhihirisha kwamba bado hujamove on! Una hasira naye na usimcheke kwakuwa hata ww hiyo hali itaendelea kukuandama tu hadi pale utakapokuwa tyr kusamehe kutoka moyoni kisha aidha myasuruhishe mmalizane au kila mmoja ashike za kwake.

Ogopa sana mtu ambaye umemtenda ukahangaika weeee na vidampa huko kisha baadaye unakuja kurudi kwake hakutukani wala nini , hakutolei shombo, ila anakuhurumia kwa kukupa maneno ya kukutia nguvu na kukutaka usikate tamaa maisha ndivyo yalivyo na mwishoni anakwambia yy ameshapiga hatua haupo tena moyoni mwake - weeeeeeeee utajuta nakwambia.

Nakuahauri kama utaamua kumsamehe hakikisha hamgusani hadi mpime afya zenu kwa utaratibu unaotakiwa ili kuilinda afya yako maana huwezi kujua huko alikopita kapewa mangapi
 
Achana naye bhana,lijitu limetembea mpaka na makahaba wa baa,wa kazi gan sasa na usikute keshalivaa gonjwa huko sasa hataki kufa peke yake anataka mfe wote...TAKE CARE MY DEAR DON'T BE LIKE A FOOL TO HIM,HE IS LIKE A DEVIL TO YOU...Wanaume nanyi hebu jaribuni kuthamini mlivyonavyo maana wazuri hawaishi kila siku wanazidi kuzaliwa tu...
 
Hiyo hali ya ww kumtukana inadhihirisha kwamba bado hujamove on! Una hasira naye na usimcheke kwakuwa hata ww hiyo hali itaendelea kukuandama tu hadi pale utakapokuwa tyr kusamehe kutoka moyoni kisha aidha myasuruhishe mmalizane au kila mmoja ashike za kwake.

Ogopa sana mtu ambaye umemtenda ukahangaika weeee na vidampa huko kisha baadaye unakuja kurudi kwake hakutukani wala nini , hakutolei shombo, ila anakuhurumia kwa kukupa maneno ya kukutia nguvu na kukutaka usikate tamaa maisha ndivyo yalivyo na mwishoni anakwambia yy ameshapiga hatua haupo tena moyoni mwake - weeeeeeeee utajuta nakwambia.

Nakuahauri kama utaamua kumsamehe hakikisha hamgusani hadi mpime afya zenu kwa utaratibu unaotakiwa ili kuilinda afya yako maana huwezi kujua huko alikopita kapewa mangapi
Unaposema huko alikokuwa hapaaminiki kwa yeye mme wake alipoondoka aliziba pasipite kitu? Twende mbele na kuludi nyuma!
 
Back
Top Bottom