Wanaume mamwinyi

Hujaelewa sijamaanisha hivyo. Majukumu ya mke yanaeleweka lkn kuna vitu vidogo vidogo kama nguo zako chafu unashindwaje kuziweka sehemu husika?
 
ndio maana nimesema waliopita waliona ni kawaida tuu mswaki akiukuta mezani atamtolea mumewe na kuuweka unapostahiri ila kwa zama hizi ndio imekuja kuwa tofauti na hii ni kawaida tu,babu mpaka ananmfulia bibi nguo anajua thamani ya bibi na bibi thamani yake aliitunza kwa kujali thamani ya babu,unatendewa kulinganya na unavyotenda
 
Hapa sawa.mapenzi ni njia mbili daima na siyo moja kama wengi wanavyotaka kusema.
 
Wanaohudumia wapo wachache. Wengine wanahudumiana
basi huna haja ya kuwa na mume kwa kuwa anayoyafanya mumeo na wewe unaweza kuyafanya,wacha mwanaume akamtafute asiyeweza kuyafanya anayoweza (mwanaume) kuyafanya
 
Ninachoweza kusema ni pamoja na majukumu mazito tuliyo Nayo lakini wanawake kwenye ndoa tutimize ahadi yetu ya ndoa ya kuwahudumia na kua wasiri wao mpaka kifo! Ukimpenda mapungufu yake hutoyaona kero Bali ni changamoto ya kufikia marekebisho ya tabia ya mumeo namaana kila akosealo tutafute muda mkiwa wawili mweleze kwa upole,mueleze siku ukiugua na yeye na hiyo tabia yake ya kubwaga Nguo hovyo hovyo itakuaje? Mweleze upande wa pili wa kila tabia aifanyayo naamini japo mwanaume ni mtoto lakini ni mtu mzima kwa umri hivyo atakuelewa,ataelewa linalokusononesha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe kila siku unalialia kuhusu mume wako,.. Na sifa zote za Mwanaume mbaya unaziandika wewe... Sasa kwanini usiachane nae!.. Kila siku mumeo tuuuuu mbaya, kwani wewe hauna weakness yoyote Ile...
Unalalamika lakini hutoki, sasa kuna faida gani..

"Ukifuga njiwa utajua bei ya mtama"
 
Aongeze mke wa pili tu kwa kweli maana kazi zinakuelemea kama ni mwanamme mwinyi au mvivu namna hiyo.
 
Hapa sawa.mapenzi ni njia mbili daima na siyo moja kama wengi wanavyotaka kusema.
shida ya wanawake wa leo you are so fine in judging small issues kuliko mambo makubwa,huwa mnahisi mko sahihi nyie kwanza kuliko mtu mwingine yoyote,unataka upendwe,upewe kila kitu wewe,ufanyiwe yote unayoyakuta kwa jirani na rafiki zako ajabu ni kwamba wewe hutaki na huwezi kufanya hata moja unalotaka ufanyiwe,mahusiano ni kama maji ukiyasafisha na kuyatunza nawe yatakutunza badae utakapo yanywa
 
Mwanaume unatuangusha, maisha ya ndoa sivyo, ni kushirikiana na sio kumfanya mke mtumwa, unashindwa hata kuchukua kijiko jikono? Je kupika, akiugua mke utaajiri mpishi? Jirekebishe

Sent using Jamii Forums mobile app
We sio mwanaume, huitwi joseph na wala hauna mke.

Kwa hiyo asiungue mke wangu niungue mimi, ili huko njiani mpaka kazini niseme nimeungua kwa nini, kwa kumpikia mke wangu na watoto?

Kwa taarifa yako mke kama anaumwa atatafuta hata mdogo wake aje kupika na kufua nguo zangu,zake,za watoto na kama si vibaya kama mke kazidiwa sana aniliwaze kidogo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…