GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,584
- 127,934
Hivi inaingia akilini kabisa Janamume zima tena limekomaa kabisa asubuhi anagombana na Mkewe kuwa kwanini hajamchemshia maji ya Kuoga.
Hivi kwa baridi au kipupwe hiki cha Dar es Salaam ni cha kumfanya kabisa Mwanaume mzima na urijali wake kuoga maji ya moto?
Nyie Wanaume mbona " mmelegea " hivi? Kinachoniuma kabisa kuna " njemba " moja nimekutana nayo mahala inampiga Mtu " mkwara " kuwa yeye ni ngangari na mtoto wa mjini wakati kabla ya hapo nilimsikia akimuwakia Mkewe katika Simu kuwa kwanini leo kamwekea maji ya baridi bafuni.
Nilikuwa nadhani Watu wanatania tu kuwa baadhi ya wanaume ni " sleki sleki " na " maboflo " nikawa nakataa na hata kuwatetea ila kwa aina hii ya " ulegevu " na kung'ang'ania kuoga maji ya moto kwa kisingizio cha baridi kali ya Dar sasa nakubali kuwa mnastahili " kuchapiwa " wenza wenu na Wakomavu Special wa Mikoani ambao wao iwe baridi ya aina yoyote ile maji watakayooga ni ya baridi tu.
Mijanamume mizima " hovyo! ". Badilikeni......