Wanaume hatufaidi ndoa, tunatumika tu kama tingatinga

Wanaume hatufaidi ndoa, tunatumika tu kama tingatinga

Dawa yao ni kuponda mali zako zote ulizotafuta kabla hujazeeka,,
Kuna mzee jirani na ninapo ishi hapa ni aged around 60+ lakini bado yupo kitengo huko bandarini sijui ndo wale mnawaita 'seniors'. Huyu mzee ana mke mmoja na watoto watatu wakubwa wawili walishapata ajira zao ila mmoja mdogo ndo yuko high school .

Baada ya hawa watoto kupata kazi walianza kumdharau mzee wao na kuzidisha mapenzi kwa mama yao, walianzisha miradi yao ya maendeleo lakini msimamizi mkuu akawa mama yao. Mzee akasoma alama za nyakati akaziba mirija yote ya fedha zinazofujwa na mkewe. Si haba huyu mzee ni mtu wa maji yaani anapiga haswaa na hazimi hovyo hivyo basi akauza nyumba mbili kati ya alizonazo hapa dar, akaacha kujishughulisha na biashara alizokuwa akifanya awali akaanza kuponda mali.

Mara kadhaa huwa napata wasaa wa kukaa na huyu mzee na huwa ananiambia yeye kwa sasa hela alizonazo na umri wake hana cha kupoteza hivyo kaamua kuponda Mali
 
Ule ukaribu walio nao na mama unajengwa hautokei tu....

Mama ndo anatumia muda mwingi kukaa na watoto, wanakua na ukaribu.

Sasa kina baba tunaona kuogopwa ndo sifa, humfuatilii mtoto, huna hata muda wa kumsemesha, hata mtoto akijaribu kukuambia mambo yake labda ya shule, michezo, unapuuza.

Mwisho wa siku mtoto hana chochote cha kumfanya akukumbuke.

Tengeneza ukaribu na watoto, kuitwa baba haitoshi, onesha juhudi.
Kibongo bongo maisha yalivyo mpelampela ukitengeneza ukaribu na watoto na kuishi kifamilia utajikuta hauna ata Mia mbovu uzeeni , bongo ukiwa na familia na unajitafuta unatakiwa uonekane jpili tu tena jioni na alfajiri na mapema utokomee , labda kama una kaajira ka serikali unaweza ishi kifamilia ila usitegemee makubwa.
 
Dawa yao ni kuponda mali zako zote ulizotafuta kabla hujazeeka,,
Kuna mzee jirani na ninapo ishi hapa ni aged around 60+ lakini bado yupo kitengo huko bandarini sijui ndo wale mnawaita 'seniors'. Huyu mzee ana mke mmoja na watoto watatu wakubwa wawili walishapata ajira zao ila mmoja mdogo ndo yuko high school .

Baada ya hawa watoto kupata kazi walianza kumdharau mzee wao na kuzidisha mapenzi kwa mama yao, walianzisha miradi yao ya maendeleo lakini msimamizi mkuu akawa mama yao. Mzee akasoma alama za nyakati akaziba mirija yote ya fedha zinazofujwa na mkewe. Si haba huyu mzee ni mtu wa maji yaani anapiga haswaa na hazimi hovyo hivyo basi akauza nyumba mbili kati ya alizonazo hapa dar, akaacha kujishughulisha na biashara alizokuwa akifanya awali akaanza kuponda mali.

Mara kadhaa huwa napata wasaa wa kukaa na huyu mzee na huwa ananiambia yeye kwa sasa hela alizonazo na umri wake hana cha kupoteza hivyo kaamua kuponda Mali
Hao wazee wanao fanya hivo wanakua na roho mbaya zaidi na ni hatari kwa maisha yake unaweza akalishwa sumu na mkewe, hamna kitu wanacho chukua wake zetu kama kuponda mali hususani nyumba.
 
Unawezaje kuwa baba usiekoroma ndani ya nyumba eti unaogopa watoto watakuwa hawakupendi ukizeeka?,hilo kwa msio na ndoa mnajidanganya,wamama wana mapenzi ya kupitiliza na huruma inayowafanya hata mtoto akikosea anashindwa kumuadhibu,wanachofanya ni kuwaambia watoto ngoja baba ako arudi,na ukirudi kweli anamshtakia,na wewe unachukua action kama baba,mtoto akianza kulia huyohuyo mama ndio anakuja kubembeleza,sasa hapa chuki ya mtoto kwa baba utaikwepa vipi?ile hali ya kumuona mama ana huruma na mapenzi haifutiki kichwani mwake.Mwanaume pia usipokoroma ndani kwako nyumba inakuwa haina ladha,hata mkeo mwenyewe ataanza kukudharau,wanawake wanapenda ile hali ya kuishi na mwanaume ambaye ana mambo ya kiume na sio kike,yani a little bit aggressive,unakuwa na kaubabe flani hivi,hii ipo hata kwa madume ya wanyama it is nature.Wewe tafuta hela,acha kuishi kinyonge humu duniani kwa kutafuta sympathy za mke na watoto,katika maisha yako"mjue sana Mungu ili uwe na amani na ndipo mema yatakapokujia-Ayubu 22:21"...
 
Unawezaje kuwa baba usiekoroma ndani ya nyumba eti unaogopa watoto watakuwa hawakupendi ukizeeka?,hilo kwa msio na ndoa mnajidanganya,wamama wana mapenzi ya kupitiliza na huruma inayowafanya hata mtoto akikosea anashindwa kumuadhibu,wanachofanya ni kuwaambia watoto ngoja baba ako arudi,na ukirudi kweli anamshtakia,na wewe unachukua action kama baba,mtoto akianza kulia huyohuyo mama ndio anakuja kubembeleza,sasa hapa chuki ya mtoto kwa baba utaikwepa vipi?ile hali ya kumuona mama ana huruma na mapenzi haifutiki kichwani mwake.Mwanaume pia usipokoroma ndani kwako nyumba inakuwa haina ladha,hata mkeo mwenyewe ataanza kukudharau,wanawake wanapenda ile hali ya kuishi na mwanaume ambaye ana mambo ya kiume na sio kike,yani a little bit aggressive,na moja wapo ni kuwa na kaubabe flani hivi,hii ipo hata kwa madume ya wanyama it is nature.Wewe tafuta hela,acha kuishi kinyonge humu duniani kwa kutafuta sympathy za mke na watoto,katika maisha yako"mjue sana Mungu ili uwe na amani na ndipo mema yatakapokujia-Ayubu 22:21"...
Mtoto yoyote mwenye hofu ya Mungu hata humtese je akikua lazima atakupenda na kukujali........ila mwanamke hata umbebe je wakati wa kukusaliti ukifika atakusaliti tu.
 
Mama hawezi kuwapa watoto sumu kama mna mahusiano mazuri!! Afanye hivyo ili iweje? Halafu kwani hao watoto hawaoni mambo yalivyo humo ndani? Hata kama bado ni wadogo but with time wataelewa. Mimi siamini huu msemo eti watoto wanapewa sumu na Mama eti wachukie baba zao; why? Kuna mambo mnafanya mnatengeneza chuki nyinyi wenyewe bila kujua.
Umesema but with time wataelewa,kwa hiyo kipindi watakapoelewa ndio wanakuwa hawajapewa sumu?

Lkn pia mbona kuna maandiko mengi tu ya baadhi ya wajumbe wakiwaomba msamaha baba zao kwa madai ya kupewa sumu na mama zao hali iliyo pelekea kuwachukia baba zao.
 
Ule ukaribu walio nao na mama unajengwa hautokei tu....

Mama ndo anatumia muda mwingi kukaa na watoto, wanakua na ukaribu.

Sasa kina baba tunaona kuogopwa ndo sifa, humfuatilii mtoto, huna hata muda wa kumsemesha, hata mtoto akijaribu kukuambia mambo yake labda ya shule, michezo, unapuuza.

Mwisho wa siku mtoto hana chochote cha kumfanya akukumbuke.

Tengeneza ukaribu na watoto, kuitwa baba haitoshi, onesha juhudi.
Na hiki ndicho ambacho mimi na mzee kilivyokua..
Yani ni wale wazee waliokua hata ukiwa na shida huna awezo wa kumwambia mpaka umwambie mama..
Madhara yake yapo mpaka leo mimi na yeye pamoja na ukubwa nilionao hatuna mazoea.. ni kitu ambacho naona kinauuma sana na si kwamba sitaki ila ni automatic tu unakuta sioni ile connection
 
Muwamba ngoma.....hii part ya mwanaume inaelezewa mwanaume katenda memaaaa katenda memaaaa maishani mwisho kazeeka katengwa, serious????

Hii situation sometimes iko hivi, mwanaume ukiwa na nguvu zako unakua kivuruge, kivuruge kweli, kama ni mlevi mlevi mbwa kero nyingi....unavumiliwa tu, wakati unavumiliwa hata mioyoni watu wanakutoa inabaki ile basi tuuuu.....ukishazeeka sasa huna nguvu za kupiga sarakasi muda huo unataka urudishe mapenzi na upendwe huo moyo wa kupendwa haupooo inabaki tu huruma ya kibinadamu, ndo muda huu zinaibuka ngonjera za kutengwa.

Kuwa mwema wakati wote, usisubirie kipindi huna nguvu
Umenena vyema
 
Jijengee akili ya kukubaliana na matokeo kuwa ndiye Baba yako pekee basi utaanza kubadili mtizamo na kumpenda Baba yako.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo wanawake huwa wanatengeneza chuki kwa watoto, hivi hata kama sawa wanaume wanakosea ina maana hata mema yake hayaonekani kipindi chote hiko? Watoto wanasoma wanapata kazi halafu mnaangalia mabaya tu, mnatumia udhaifu huo kuwahadaa watoto na kutengeneza chuki ili kusudi muonekane wa maana sana kuliko wanaume.

Hio mitoto ya hivyo ni upumbavu mtupu.

Hakuna mwanadamu hakosei.
Jenga ukaribu na watoto wako toka wakiwa wadogo.. ili wawe connected na wewe.. kwa mwendo huo hata ufanye jambo gan la maana sheikh bado utapigwa bao tu uzeen na mwanamke
 
Muwamba ngoma.....hii part ya mwanaume inaelezewa mwanaume katenda memaaaa katenda memaaaa maishani mwisho kazeeka katengwa, serious????

Hii situation sometimes iko hivi, mwanaume ukiwa na nguvu zako unakua kivuruge, kivuruge kweli, kama ni mlevi mlevi mbwa kero nyingi....unavumiliwa tu, wakati unavumiliwa hata mioyoni watu wanakutoa inabaki ile basi tuuuu.....ukishazeeka sasa huna nguvu za kupiga sarakasi muda huo unataka urudishe mapenzi na upendwe huo moyo wa kupendwa haupooo inabaki tu huruma ya kibinadamu, ndo muda huu zinaibuka ngonjera za kutengwa.

Kuwa mwema wakati wote, usisubirie kipindi huna nguvu
wewe ndo umeongea ninachokijua mimi kwenye hili suala la wanaume walio wengi kuhisi wametengwa wakizeeka
 
Kwahiyo wewe mtoto akosei eti umbebeleze, kisa unataka akupende uzeeni, hapana hiyo biashara sifanyi, kama kaamua hivo basi ni kudra za Mungu siwezi kujipendekeza kwa mtoto kisa kupendwa uzeeni.
Wewe nani kakwambia kumnyoosha mtoto akikosea kunahusiana na kupendwa?
 
Hiyo inatokea mostly na specifically kama baba alikuwa kauzu kwa watoto na mama badala ya rafiki. Subconsciously watoto wataweka mpaka ambao hautovunjika mpaka ukubwani. Ambapo utakuwa umezeeka, huna nguvu na unaanza kuhitaji kupendwa na kuhudumiwa. Hapo ndipo utaanza kunotice kwamba watoto na mama walikuwa wanakuvumilia tu.

Hata ukijaribu kuwa karibu na mzee unaona tu kuna kitu hakipo sawa. Tofauti kabisa ukiwa na mzazi wa kike.

Kama hutaki watoto wakukimbie uzeeni basi acha ubabe wa kifala kwa familia. Ikiwezekana upeleke nje ili wakuone bora zaidi. Mwisho wa siku badala ya kukukimbia, watakaa chini na wewe mpige story na kinywaji baridi pembeni.

Otherwise utabaki peke yako kwenye hiyo nyumba. Hichi kitu nimejiandaa kabisa kukiepuka nikipata familia yangu.
Hii ndio scenario Ilivyo mimi na mzee, ule ukuta kati yangu na yeye uko mpaka leo hata kwenye simu haizid dakika mbili mazungumzo yashaisha na si kwa makusudi ila kutokana na ukauzu wake aliokuaga nao..
Ilifika muda mzee atasubiri ukosee ndio akuseme, ukiwa na shida basi huna uwezo wa kumwambia mpaka umwambie mama ndio amwambie mzee.. Automatically ile connection unashtuka haipo mpaka uzeen na hapo yeye wala hajui kwann watoto hatuna story nae
 
Ule ukaribu walio nao na mama unajengwa hautokei tu....

Mama ndo anatumia muda mwingi kukaa na watoto, wanakua na ukaribu.

Sasa kina baba tunaona kuogopwa ndo sifa, humfuatilii mtoto, huna hata muda wa kumsemesha, hata mtoto akijaribu kukuambia mambo yake labda ya shule, michezo, unapuuza.

Mwisho wa siku mtoto hana chochote cha kumfanya akukumbuke.

Tengeneza ukaribu na watoto, kuitwa baba haitoshi, onesha juhudi.
Kitu ulichoandika hapa unaonekana una umri mdogo sana yaani chini ya miaka 25.

Jukumu la msingi la Baba ktk familia ni kuhakikisha familia iko salama na kupata mahitaji yote msingi ndani uwezo wake.

Ukiwa mwanaume (Baba) siku zote jambo la msingi kwetu ni kuheshimika tu sio kupendwa. Watoto wajinga wajinga ndio huwa wanamsahau Baba.
 
Back
Top Bottom