1. Kichwa kinalalama wanaume hawafaidi ndoa.....!!! Kwanza kufaidi ndoa ni kupi? Ninini ama ni kitu gani ambacho huyu mume hafaidi na anaona wanaofaidika na ndoa ni wanawake na watoto.....
2. Mwanaume kutumika kama tingatinga....
Bado najiuliza, hapa mwanamke hatumiki..??? Mtoto hatumiki?
Ama, kutumika ni nini? Ama kutumikaje?
Mada ni pana sana, licha ya maswali hapo juu twende nayo hivyohivyo kwa upana kufikia muafaka ama maelewano, maana ndo suluhu kubwa jamii inataka.
Kwanza hakunaga formula kwenye ndoa kwa maana namna ya kuendesha ndoa, kila ndoa inanendeshwa kutokana na yanayoikabili. Pia hakuna formula ya kulea watoto, mtoto yuko kwa namna yake na hulka zake, unakuta wamezaliwa 5 wote wamelelewa nyumba 1 na wazazi aina 1 ila 3 wanakuwa na adabu na maisha, 2 hawashikiki yaani wameshindikana...
Nikirudi kwenye mada, wacha niende kwa mifano kama 2 au 3 hivi kama hali itaruhusu.
1. Dingi mhasibu na mkewe mkunga wote dini moja wamepata watoto 5. Dingi anakuwa na safari za kikazi na kusafiri na mkewe na watoto hadi nje ya nchi, dingi ni mhasibu mbobezi. Kazi yake ilimfanya asionekane nyumbani, ila jumamosi na jumapili haendi kazini anashinda siku nzima kalala, ikifika saa 10 jioni anaamka, mke anamuandalia mlo anakula kisha anatoka kurudi usiku mnene. Watoto wamekua wanamuona mdingi anafatwa na SU tai kila siku kurudishwa jioni na SU, akirudi analala hadi saa 11 au 12 jioni anajiandaa kutoka na kurudi usiku mnene. Kesho tena mzunguko unaendelea. Dingi anaghqrimia familia mahitaji yote maana saa ingine anasema kuna hela nimemuachia mama yenu kwa matumizi fulani hivyo watoto wanatambua wajibu na mchango wa baba.
Mama ndo anaamshana na watoto jumatatu hadi ijumaa kuwaandaa shule, wakirudi wakute chakula tayari, mama awafundishe kufua nguo zao, usafi wa vyumba vyao. Mama aende kanisani na watoto awafundishe kutoa sadaka, kupanda daladala, kutengeneza bustani za maua na mbogamboga, kufuga kuku, kushona nguo iliyochanika na huku mama ni mkunga....
Mdingi anajisahau au sijui ndo asili, anaanza kutupa mbegu huku na kule, watoto wa nje wanazaliwa kunakuwa na tafrani, mke anakuwa kimyaaa, watoto wanaletwa ndani ya nyumba mke anawalea pamoja na watoto wake wa mwanzo. Hawa watoto wa nje hawaishi kiasi cha dingi kustaafu bado anarusha mbegu tuu.... ila mke yuko kimya analea.
Wale watoto wana mamazao ambao waliwatelekeza wakalelewe kwa baba yao wakakuta mke kajaa, ila wale watoto wakiita mama basi ujue wanamuita huyu mama mlezi sio mama zao wazazi. Dingi kuona haitoshi 60+ anahamia shamba anavuta binti na kuendelea kupata watoto....!!! Okay....
Wakati dingi ameenda shamba, kamuacha mke kwenye mji mwenyewe, mke nae kajistaafia anaendelea kumuabudu Bwana wa Mabwana..... miaka 5 mbele watoto wanamvuta mama na dingi ulaya kwa matembezi, maana baadhi ya watoto wanaishi huko. Dingi anaona hakuna raha huko bora akae shamba anazungukwa na watoto wajukuu...!
Watoto wakamchukua mama ulaya mazima, dingi shamba kukawa shubiri, mafao ya EA yalikata, hela hakuna watoto wadogo wanataka kusoma intanesheno dingi nehi, ila nyumba na mashamba anayo.
Ile kero ya matumizi ya anasa anayodaiwa na watoto kule shamba akaona bora are arejee mji wake mjini, hakuna neno..... yuko pekeyake anaishi mwenyewe....
Sasa huyu katengwa, kajitenga au karma imemtenga na familia japo katengeneza ya uzeeni pia...? Mke huko ulaya hana mpango wa kurudi bongo amenawiri na kuwa bimbi bomba...!
2. Dingi mtumishi wa umma, miradi yote ya serikali yeye ndo anafanya bajeti, anaandikia propozo na ikipita anafanya kazi na makandarasi na kutoa ripoti kwa wakuu wake. Huyu anaondoka nyumbani saa 1 au 12 asubuhi kurudi saa sita usiku.... sii jumapili wala siku za sikukuu yeye ni workaholic, ila familia anaihudumia vyema. Na mara nyingi (watoto 3) anawapa watoto pesa mkononi wanunue wanachotaka na saa ingine anatoka nao kwenda matembezini ila akipotea nyumbani humuoni.
Mkewe mama wa nyumbani anapambana na malezi ya watoto na ndugu wanaokuja kutaka msaada, mume alitumbuliwa...... (uzuri alikuwa na HELA) hivyo maisha hayakubadilika hakuna aliyejua kama dingi hana kazi, alijua kutunza hela zake alizokuwa anazikusanya. Mtoto mdogo keshamaliza chuo saa hii wanasuguana mgongo na mkewe,hawa walioana kabila moja japo mkewe ni chapombe.
3. Dingi alikuwa na kazi shirika binafsi pesa ipo, wanawake kila kona ila mke anavumilia. Safari moja hakurudi nyumbani ambapo si kawaida yake, mama kumekucha anasema ngoja nikanunue vocha anakutana na gari la mumewe limepaki mtaa wa 2, kugonga mlango mumewe anatoka na taulo....!!!
Mke akarudi nyumbani kimyaaaa maisha yakaendelea, hawa walipata watoto 2. Mke nae alikuwa anafanyq kazi UN huko anacheocheo tuu. Sasa baba akaanza kustaafu mama kaendelea na kazi alipogonga 60 nae kastaafu. Muda wote huo mke anavumilia mapichapicha ya mume, kumbe ana hesabu zake.
Wiki 1baadq ya mama kustaafu akawaita mumewe na watoto wao ambao wameshaanza kazi, akawaambia, nilikaa kwenye hii ndoa sio kwa raha ni ilinyie mpate malezi ya baba na mama na mkue vyema. Wajibu huo nimeumaliza, nimewaita hapa nahamia kwangu (mke kajenga kajumba ka vyumba 2 kinachojitegemea hapo Tegeta). Anaacha jumba la kifahari la mumewe na magari yake, pension ya UN sio ya kitoto.
Watoto wako mama kwanini, sasa huu si ndo muda mzeeshane mkae pamoja hakuna tena matatizo, mke akasema nimewaita kuwapa taarifa sio ushauri, hapa naondoka na nguo zangu tuu.
Dingi akaanza kulia, watoto kuita ndugu waingilie kati mke anasema fanyeni mnalotaka hapo sirudi.
Huyu mke alifikwa? Utajiulizana mhehe huyu? Mbona hakujinyonga wakati anapigwa matukio? Dingi bado ana mshiko pia sema uzee, upweke....
Ogopa ama kaa mbali na mtu anayeweka vinyongo na kupanga mipango yake ya baadae bila kukushirikisha hata kama si ya kukudhuru.
Sina jibu la nini kifanyike, ila walau kila mmoja ajue kula na kipofu,hakuna aliyemkamilifu. Funika kombe mwanaharamu apite.
Ukiweza acha mambo yatayoleta doa kwa mwenzano, ukishindwa fanya asijue, akijua omba upate patna anaye react hapohapo, wale wanaokaa kimya wakisubiri muda ukifika wakuachie pira, aahaha unalooo.
Unajikuta uji unaupoozea tumboni.
Kasinde Matata.