Wanaume hatufaidi ndoa, tunatumika tu kama tingatinga

Wanaume hatufaidi ndoa, tunatumika tu kama tingatinga

Mkiwa na nguvu na pesa mnajijua bana mambo yenu.....anyway poleni kwa mnayopitia.
Tatizo wanawake huwa wanatengeneza chuki kwa watoto, hivi hata kama sawa wanaume wanakosea ina maana hata mema yake hayaonekani kipindi chote hiko? Watoto wanasoma wanapata kazi halafu mnaangalia mabaya tu, mnatumia udhaifu huo kuwahadaa watoto na kutengeneza chuki ili kusudi muonekane wa maana sana kuliko wanaume.

Hio mitoto ya hivyo ni upumbavu mtupu.

Hakuna mwanadamu hakosei.
 
Tatizo nyie hampo wazi!
Mtoto nina shida nakupigia simu kukuomba hela unaniambia utatuma siku zinapita hata 3 days nakupigia hupokei!
Mimi kama mtoto nitajisikiaje?

Baada ya siku unatuma, kumbe ulikua hupokei sababu huna hela.. kwanini usiseme nijue mzee hana lkn ananitafutia

Wanaume ni watu wazuri! Lakini wakina mama wanajua kucheza na akili za watoto kujichukulia points😂
Sivyo hata kuchukua points, ni wazuri kutengeneza chuki kwa watoto dhidi ya baba. Wabadilike sio wote.
 
Muwamba ngoma.....hii part ya mwanaume inaelezewa mwanaume katenda memaaaa katenda memaaaa maishani mwisho kazeeka katengwa, serious????

Hii situation sometimes iko hivi, mwanaume ukiwa na nguvu zako unakua kivuruge, kivuruge kweli, kama ni mlevi mlevi mbwa kero nyingi....unavumiliwa tu, wakati unavumiliwa hata mioyoni watu wanakutoa inabaki ile basi tuuuu.....ukishazeeka sasa huna nguvu za kupiga sarakasi muda huo unataka urudishe mapenzi na upendwe huo moyo wa kupendwa haupooo inabaki tu huruma ya kibinadamu, ndo muda huu zinaibuka ngonjera za kutengwa.

Kuwa mwema wakati wote, usisubirie kipindi huna nguvu
Wanasahau fainali uzeeni, wakati yanasumbua ujanani kuchochora na wanawake wa nje hayatulii yanajua yatakuwa na nguvu muda wote..!!! Waache kulalamika wawachukue vimada wao wapeane faraja.
 
Tatizo wanawake huwa wanatengeneza chuki kwa watoto, hivi hata kama sawa wanaume wanakosea ina maana hata mema yake hayaonekani kipindi chote hiko? Watoto wanasoma wanapata kazi halafu mnaangalia mabaya tu, mnatumia udhaifu huo kuwahadaa watoto na kutengeneza chuki ili kusudi muonekane wa maana sana kuliko wanaume.

Hio mitotio ya hivyo ni upumbavu mtupu.

Hakuna mwanadamu hakosei.
Kweli hapo kinamama wengi hukosea.....kwa kusambaza sumu kwa watoto tupo vere kwakweli, sio kitu kizuri
 
Na wanakuwaga majeuri sana, ndani wanaona km wanaishi na ng’ombe, wakichoka wanarudi mikono nyuma wanataka faraja thubutuuuuu!!!!
Yani waenjoy ujanani na uzeeni pia 🤣🤣🤣
Watavuna walichopanda
Tuwafariji wazee wetu na kuwaonesha upendo ambao wanauhitaji sana uzeeni kuliko sasa 🤣🤣🤣
 
Mke ndo mbinafsi...
Yeye ndo alitakiwq aopt kubaki na mumewe wale uzee pamoja.
Binafsi wanangu kunichukua labda niwe mjane and jobless, otherwise ntabaki na mume wangu au mishe zangu.

Marry your person and treat her right, ni mara chache sana kukutelekeza
 
Nani ni mfaidi wa ndoa, kati ya mke, watoto na mme? Mstaafu wa miaka 68 alifanya kazi maisha yake yote ili familia yake iishi katika first class life style, na kulinda hiyo 'status quo' limemgharimu karibia maisha yake yote, hassling for the wife and children, akijinyima kila kitu kuhakikisha watoto wake wanasoma shule nzuri za private na wapate kozi nzuri vyuoni.

Mke wake ambaye amefikisha 60yrs amechukuliwa na mtoto wake wa mwisho Amsterdam in the Netherlands, mzee anapambana na high blood pressure, na kisukari, lakini upweke kwenye bagalow lake ndo shida kubwa kuliko, mzee hakuzaa watoto wengi aliza wawili tu. Ambao wameamua kuchukua na kulea mama yao na kuacha baba yao.

Hivi kwanini watoto hususani wa kiume wakikua wana tuchukia sisi Baba wakati sisi ni factor kubwa katika mafanikio yao?

Wanatutenga na kuthamini mama zao wengine wanatamani tufe mapema wachukue urithi loh!

NB.

1. Wanaume tujiandeni kwa wakati wa kustaafu hao watoto na wake zetu hubadilika na kuwa adui zetu tukistaafu (nolonger productive)

2. Early birth and late birth ni muhimu Zaeni watoto wa ukubwani kwa mke mdogo ukiwa 55 to 60yrs ( ukistaafu angalau uwe na wakukaa nao nyumbani, monogamy ina maumivi badaye polygamy inatatua shida zingine badaye.

View attachment 2948887
Kama walivyo mfanyia baba yao... Nao watafanyiwa hivyo hivyo....

Watoto tusiwe wabaguzi kwa wazazi wetu... Tusipende kuruhusu story za upande mmoja zistawi katika akili na mioyo yetu hasa za upande wa mama zetu (ingawa sio wote) maana tukizitilia maanani adhali zake ndo hizo.. sikiliza afu potezea tu...


N:B hata wazee wetu (mababa) wana mengi yakusema ila tu wanaamuaga kukausha kwa ustawi wa maisha ya uzao wao... Bahati mbaya uzao wenyewe wa smartphone, Instagram, na kujiona maasla hawajui hilo na ujinga wao......
 
Basi utaanza kumnunia huko ndani, dada wa watu anabaki na maswali kumkichwa "nimemkosea nini hubby mbona amenuna kavimba" kumbe umevimbishwa na comments za jf.....
Jf ndo hao watu tunao ishi nao mitaani kazini misibani michango na mawazo yao hayana tofauti na maisha halisi, na wanacho sema hapa ni ukweli mtupu sio imagination, kaa mbali na mwanamke mwenye roho mbaya.
 
Jf ndo hao watu tunao ishi nao mitaani kazini misibani michango na mawazo yao hayana tofauti na maisha halisi, na wanacho sema hapa ni ukweli mtupu sio imagination, kaa mbali na mwanamke mwenye roho mbaya.
Sio sababu ya kutoka kwenda kumnunia.....au umpe sababu basi
 
Kama hukuwa na mahusiano mazuri na huyo mwanao usitegemee maajabu.

WaMama wanabembeleza, wanaonya kwa upole.

Baba wewe unataka uogopwe kama Simba, unakoroma tuu.


Fainali uzeeni.
Kwahiyo wewe mtoto akosei eti umbebeleze, kisa unataka akupende uzeeni, hapana hiyo biashara sifanyi, kama kaamua hivo basi ni kudra za Mungu siwezi kujipendekeza kwa mtoto kisa kupendwa uzeeni.
 
Back
Top Bottom