Wanasiasa msitufanye wajinga kuhusu mikutano ya kisiasa

MEXICANA

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
1,772
2,032
Specifically naongea na wanaodai kwamba hakuna uhuru wa kufanya mikutano ya kisiasa. Rais kasema hajazuia mikutano yenu ya wanachama wenu ndani ya chama. Wabunge wafanye kwenye maeneo yao pia.

Marekani wametoka kwenye uchaguzi juzi kati, je? Bado wanaendelea na mikutano ya siasa?

Tunataka demokrasia gani, Unataka uweke mkutano wako ili ueleze nini? Si ueleze wanachama wako kile unachotaka kueleza.
Mbona mataifa mengine hawana huo utopolo mnao claim?

Je, Demokrasia ya Tanzania ni so special sana kuliko demokrasia za nchi zingine duniani? Nakuuliza wewe unayepinga kila kitu.

Najua jambo moja tu juu yenu, nyie si wa kuwachekea chekea au kulia lia, maana hamuchelewi kusema hamtaki kuchekewachekewa kama Mfalme fulani hivi mlivyokuwa mnamuita miaka ya nyuma, na sasa hivi nmesikia mnasema hamtaki mfalme anayelialia.

Kiuhalisia siasa ya Tanzania imejaa unafiki mwingi Sana, ni biashara kama biashara zingine.
 
Mpuuzi wewe, makongamano ya dini, michezo, harusi, matamasha, mikutano mbalimbali mbona inafanyika isipokuwa tu ya vyama vya siasa tena vya upinzani? kwanini mambo yote yasisimame mpaka hapo atakaponyoosha nchi?
 
Msipende kutumia mifano ya nchi ambazo hamzijui. Marekani mikutano inaendelea kama kawa kwa sababu hakuna mwanasiasa mwenye mamlaka ya kuzuia chama, kikundi au mtu binafsi kufanya mkutano wake popote anapotaka.

Hamuoni kuwa kwa kudai kuwa Chadema wakifanya mkutano wa hadhara watu wataacha shughuli zao ili wakahudhurie mnakiri kuwa Chadema kinakubalika sana kwa sababu mwananchi ana haki ya kutohudhuria bila kutoa sababu yeyote!

Amandla...
 
Mleta mada unakosea na unafanya watu humu hawana kumbukumbu au ufahamu. Mosi, wabunge wa CCM hawana cha kuwaambia wananchi waliopigika kwa uchumi mbovu na umasikini. CCM inahofia vyama vya siasa kuwakumbusha wananchi machungu ya kimaisha wanayopitia.

Wakati Rais hana jimbo, na mwenye kofia ya Mwenyekiti wa chama, atatumia ziara za kiserikali kwenye mikoa na wilaya kama sehemu za shughuli za chama. Nikikumbushe machache:

a) Dr. Tulia Ackson kutambulishwa kwa wanaMbeya katika ziara ya Rais.
b) Kupokelewa kwa madiwani wa Chadema waliohamia CCM katika kamisheni ya wanajeshi Arusha
c) Kutambulishwa kwa Katibu Mkuu wa CCM katika sherehe za Mei Mosi Mwanza.
d) Kupokelewa kwa wabunge na madiwani waliohama katika ziara za Rais JPM ikiambatana na Dr. Mashiru na Polepole na wenyeviti wa mikoa na wilaya kupewa nafasi ya kutoa neno kwa umma huku wakiwa wamevalia sare za CCM.
e) Rais kuongea na wananchi "waliomsimamisha" na kuwazodoa kwa kuwaambia "walichagua vibaya" pale inapokuwa ni eneo la wapinzani.

Alichokisema SSH sio tofauti na alichokifanya JPM. Ilifikia hata mikutano ya ndani na waandishi wa habari ya hasa Chadema ikizuiliwa kwa kisingizio cha "taarifa za kijasusi" ili mradi tu wanasiasa wasiongee, huku mawaziri, wakuu wa wilaya na mikoa wakifanya kazi za CCM.

Unaweza kudhani watu ni wapumbavu hawatambui mambo haya, lakini huwezi kudhani hawakumbuki. Nakukumbusha hilo!
 
Mpuuzi wewe, makongamano ya dini, michezo, harusi, matamasha, mikutano mbalimbali mbona inafanyika isipokuwa tu ya vyama vya siasa tena vya upinzani? kwanini mambo yote yasisimame mpaka hapo atakaponyoosha nchi?
We mpuuzi Sana, unataka mkutano wa nje ueleze nini, mda wa kampeni umeisha , au unataka uandamane
 
Mleta mada ni mpumbavu, mikutano ya kisiasa ni sehemu pia ya kutafuta wanachama na ni takwa la kikatiba! Yaani unachekelea kuvunjwa kwa katiba? Una akili timamu kweli? Kama mnataka hivyo basi badilisheni katiba ili ipige marufuku mikutano hiyo!Shwain
 
Ila wapinzani kwani mbunge na wawakilishi wengine wa wananchi hawatoshi kusimama kwenye maeneo yao na kuzungumza na wananchi wao juu ya mustakabali wa malengo yao mpaka mchukuane wanachama wote wakuu kuzururua na kuleta jam isiyo ya lazima kwetu? Loooh! hatutaki tumewachoka bana hizo pesa za bajeti mpeni diwani wenu atujengee ofisi ya chama chetu pendwa.
 
Mama nchi imemshinda,alifikiri kuongoza nchi ni sawa na kuongoza kikundi cha taarabu cha kugeuza geuza makalio
 
Ila wapinzani kwani mbunge na wawakilishi wengine wa wananchi hawatoshi kusimama kwenye maeneo yao na kuzungumza na wananchi wao juu ya mustakabali wa malengo yao mpaka mchukuane wanachama wote wakuu kuzururua na kuleta jam isiyo ya lazima kwetu? Loooh! hatutaki tumewachoka bana hizo pesa za bajeti mpeni diwani wenu atujengee ofisi ya chama chetu pendwa.
Kigoli, kwa hakika hutaolewa. Utabaki kuosha vyombo, kudeki na kuteka maji na kufua nguo za watu. Bado hujitambui na utu uzima wote huu??
 
Marekani mbona mbali sana nchi gani ya Africa chama cha siasa kinafanya mikutano ya hadhara baada ya uchaguzi.

Uwezi kufanya political campaign kwa miaka mitano mfulululizo. Hayo mambo yanamuda wake, uchaguzi ukiisha kazi.
 
Hivi wabunge wa upinzani wapo wangapi wenye sifa za kuweza kufanya mikutano yao ya kisiasa katika majimbo yao? Hivi viongozi wetu wanapoapa kuitunza, kuilinda na kuitii katiba ya JMT kabla kushika madaraka yao ya uongozi huwa wanamaanisha kweli?
 
Mpuuzi wewe, makongamano ya dini, michezo, harusi, matamasha, mikutano mbalimbali mbona inafanyika isipokuwa tu ya vyama vya siasa tena vya upinzani? kwanini mambo yote yasisimame mpaka hapo atakaponyoosha nchi?
Ni mpuuzi si kidogo, yupo tayari akajazane uwanja wa taifa kumuona diamond Ila eti sio kumsikiliza mtu Kama Lissu
 
Back
Top Bottom