Mkuu naheshimu sana Dini ya Kiislam na two of my best friends ni Muslims
Ninajua baadhi ya maandiko yaliyopo katika qur'an na yanafundisha mema kbs.
Ninachowapingaga hawa waislam hewa hapa ni unakuta anasimamia kitu ambacho hakijui effectively na hata kukitetea kimaandiko hajui isipokuwa kulalamika na kuuponda Ukristo.
Have peace mkuu.
Kweli baadhi yao wanakuwa ni hewa kweli,
Kwanza haipaswi kuponda Ukristo wala kumtukana mkristo...siku moja nilisikiliza mawaidha IQRA TV sheikh akasema, sisi binadamu tunakosea, akataja baadhi ya maandiko kuwa,
Hatupaswi kumchukia mtu kwa tabia yake wala matendo yake au dini ya mwenzio bali Tunapaswa kumuweka karibu, kumpenda na kumuelimisha pale alipopotoka...Tunatakiwa tutende mazuri, mema ili yule aliyepotoka avutiwe kuwa karibu na mema.
Sasa ikiwa wewe kisa ni kumpinga mwenzio unamkashifu, unamponda bila kumuelimisha na kumuonesha upendo huyo mwenzio atakufuata vipi? Naimani mwisho wa yote nyote mtakuwa ni mliopotoka.. hakuna atakayeona uzuri wa kumfuata mwenzie uko wapi.
Ukitaka kujua Uislam umeamrisha mema ila tuu ni binadamu ndio Mashetani angalia kipindi cha MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN.
Humsikii mtu akitukana hovyo
Wanakuwa wakarimu,
Hawanywi wala kula vilivyokatazwa,
Wanakuwa ni wenye kutoa sadaka kwa wale wasiokuwa na uwezo,
Upendo unakuwa ulio jaa kwa kila namna...
Ila mwezi huu ukimalizika kila mmoja aliyeshetani anakuwa kama liyeshukuru kuwa alikuwa jela sasa ameachiwa....
Basi ukiona hivi ujue kuwa sio DINI YA UISLAM iliyoamrisha uovu bali NI BINADAMU TUU NDIO WAOVU, NDIO MAANA MWEZI ULE WANATENDA SANA MEMA....hatukuamrishwa kutenda mwema wakati mmoja tuu ila ni wakati wote..Na mwezi ule ni moja ya mifano ya miezi yote uliotilia mkazo kuwa uliyoamrishwa ni yapi.