Wanashikiliwa kwa kumkashfu mtume

getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,150
1,821
Hii imekaaje wadau? Kuna watu wanashikiriwa na polisi zanzibar eti kwa kosa la kumkashfu mtume.! Kwa wanaojua zaidi mtujuze..
Chanzo star TV.

========

JESHI la Polisi Zanzibar linatarajia kumfikisha mahakamani mtu anayedaiwa kumkashifu Mtume Muhammad (S.A.W).

Mtuhumiwa huyo, Dk. Abdallah Saleh Abdallah (50), mkazi wa Kikwajuni mjini Unguja, baada ya kutoa maneno hayo ya kashfa juzi na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Unguja, Kamishna wa Jeshi la Polisi visiwani hapa, Hamdan Omar Makame, alisema walimtia mbaroni daktari huyo wa binadamu baada ya taarifa zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwamo wa Facebook.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumkashifu Mtume Muhamad na waumini wa dini ya Kiislamu.
“Tumemkamata mtuhumiwa na tayari tumeshakamilisha kila kitu, ikiwamo taarifa za upelelelezi. Hivyo kilichobaki ni kumfikisha makahamani tu ili aweze kujibu mashtaka yake,” alisema Kamishna Makame.
Akiongezea kuhusu ukusanyaji wa taarifa za upelelezi, alisema wamelazimika kumshikilia kijana Ali Juma Makame (30) mkazi wa Michenzani mjini hapa ambaye anatuhumiwa kusambaza video hizo mitandaoni.

“Tunawanasihi waumini wa dini ya Kiislamu kutokubali kuyumbishwa na kufanya maandamano kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria, ni bora kujiepusha na jambo hili kwani tayari vyombo vya ulinzi vimeshachukua hatua kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Kutokana na video hiyo, taasisi mbalimbali za dini ikiwamo Jumuia ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) na Ofisi ya Mufti, zimelaani tukio hilo na kutoa wito vyombo vya sheria kuchukua hatua na kufanya kazi bila upendeleo.
 
Taarifa ya habari star tv. Kuna watu wawili wanashikiliwa na polisi zanzibar kwa kosa la kumkashfu mtume kupitia mitandao ya kijamii...!
Polisi wanasema watuhumiwa wanao na upelelezi unaendelea na watafikishwa mahakamani.. Ninatamani watu walio znzbr watupe ufafanuzi zaidi katika hili jambo.
 
Sijawai kuona sehem yesu anakashifiwa wala mtume anakashifiwa na kama imethibitika wamefanya ivyo basi wachukuliwe hatua...ila tu najaribu kuwaza ingekua waislam ndiyo wamekamatwa kwa kumkashifu yesu, sijui ndugu zetu wa kiislam wangeichukulia vipi?
 
Hawajaandamana hao. .??...maana huwa hawachelewi eti. ...ila muheshimu dini za watu kashfa siyo nzuri. ....
 
Hii imekaaje wadau? Kuna watu wanashikiriwa na polisi zanzibar eti kwa kosa la kumkashfu mtume.! Kwa wanaojua zaidi mtujuze..
Chanzo star TV.
Nimeisikia hiyo taarifa ss sijajua kama serekali ina aheria zinazojihusisha na maswala ya kidini
 
Back
Top Bottom