Wanashikiliwa kwa kumkashfu mtume

Wanashikiliwa kwa kumkashfu mtume

Mi nazungumzia utata wa Paulo kwenye Matendo 9:6 "Lakini simama uingie mjini nawe utaambiwa yakupasayo kutenda".

Yesu anamwambia Paulo aingie mjini ndiyo ataambiwa apasayo kutenda,lakini kwenye Matendo 26:15-18. Ambalo ni tukio hilohilo ila huku Yesu tayali anamwambia Paulo nini cha kufanya na si hadi aingie mjini kama ilivyoelezwa kwenye Matendo 9:6.

Wala hapo hakuna kujichanganya hata kidogo.
Mat.9:6 inaeleza jinsi Sauli alivyotokewa na Yesu na maono mbalimbali aliyopewa wakati Mat.26:15-18 Paulo alikuwa anatoa utetezi wake mbele ya Mfalme Agripa.
Hapa kwenye utetezi alikuwa anatoa muhtasari wa yaliyotokea kwa ufupi ambayo alikuwa hajyajaandikwa katika vifungu vilivyotangulia.Anania huko Damascus alimwombea Paul na hatimae kujazwa Roho mtakatifu.
Roho Mtakatifu ndio mwongozo na Roho ya utendaji kwa Wakristo.Bila Roho Mtakatifu huwezi kutenda mambo yoyote ya kimungu. kwa hiyo Yesu alipomwambia aende mjini na ataambiwa yaliyo sahihi kufanya alimaanisha atapokea Roho Mtakatifu.vifungu vyote vipo sahihi.
 
Kwani mtume ni nani?mbona mitume na manabii ni wengi mno,mtume ni kwako,kwa wengine hana maana wanaweza hata kumuona ni kinyago
 
Basi tukubaliane ya kwamba biblia inajichanganya yenyewe. Maana mimi nimekupa maandiko yote yanaonesha yesu sio Mungu bali yesu ana Mungu wake ambaye ndiye anayemtegemea katika biblia hiyo hiyo. Kwa kifupi ni hivi:

Yohana 20:17

Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

Biblia haijichangaji bali binadamu ndio tunajichanganya.
Yesu mara nyingi alikuwa anaongea kwa Mafumbo na Mifano kiasi kwamba hata wanafunzi wake waliwahi kumuuliza kuhusu kadhia hiyo.

Mafumbo huwa yanawashinda sana watu kuyafafanua.
 
ni hivi zanzibar ni nchi ya kiislamu, hii inamaana kuwa katba ya nchi yao msingi mkuu ni quran. mahakama nyingi zipo katka msingi wa SHARIA, kwa hiyo mtu kumtukana au kumkashifu mtume na uislamu kwa ujumla ni kuvunja SHARIA. pia zanzbar iko katka shirikisho la nchi za kiislamu duniani. kwa kifup zenchi ni kama vile MISRI, ALGERIA, SAUDIA ARABIA, QATAR nk
 
Hicho ni kielelezo kizuri kwa wasio heshimu Mira na desturi za wengine.
 
Biblia haijichangaji bali binadamu ndio tunajichanganya.
Yesu mara nyingi alikuwa anaongea kwa Mafumbo na Mifano kiasi kwamba hata wanafunzi wake waliwahi kumuuliza kuhusu kadhia hiyo.

Mafumbo huwa yanawashinda sana watu kuyafafanua.
Haya toa maana ya hili fumbo: yaani maandiko yaliyowazi kabisa yesu anasema anaye Mungu wake wewe unasema yesu kasema kwa mafumbo. Maandiko uliyotoa wewe mbona hukusema yana mafumbo? Haya nifumbulie hili fumbo basi.

Yohana 20:17

Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.
 
Haya toa maana ya hili fumbo: yaani maandiko yaliyowazi kabisa yesu anasema anaye Mungu wake wewe unasema yesu kasema kwa mafumbo. Maandiko uliyotoa wewe mbona hukusema yana mafumbo? Haya nifumbulie hili fumbo basi.

Yohana 20:17

Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

Kwanza nikushukuru kwa kuendelea kusoma neno la Mungu aliye hai maana imeandikwa kwa Yesu Kila Goti litapigwa.

Yoh.20:17 inaeleza mazingira ya Yesu baada ya kufufuka.Hakutaka kutoa mafundisho au kufanya kazi yoyote kwa sababu yote aliyamaliza pale msalabani.Alichokuwa anafanya ni kutaka kuwaaminisha wanafunzi wake na wengine kwamba kweli amefufuka kama alivyosema.

Kuhusu Swala la Baba na Mungu nimeshaliongelea sana hapa na kutoa vifungu vya Biblia.
Itoshe kusema tu kwamba Mungu ana nafsi tatu yaani BABA,MWANA(YESU) na ROHO MTAKATIFU-UTATU MTAKATIFU MUNGU MMOJA.Kikikosekana kimoja hapo Umungu haujakamilika.
Akisema anaenda kwa Baba ni sawa,Akisema Mungu wangu ndie Mungu wenu ni saw vilevile.
Mfano.Magufuli akisema Rais wa Tanzania hataki mzaha kwenye kazi,sidhani kama atakuwa amekosea.
 
Yesu ni habari nyingine, mtume alikuwa binadamu Kama wewe wakati Yesu hakuwa binadamu wa kawaida.
Soma matendo 2:22 alafu urudi hapa useme yesu alikua ni Mungu na wala hakua binadamu anayeenda chooni kama wewe..
 
Serikali haina dini., wawachie tu wanawaonea Kama ni kashfa kwa mtume wao wawasubiri sku wakiingia msikitini kwao kuswali ndipo wawahukumu,,
La sivyo ni uonevu tu.
 
Kwanza nikushukuru kwa kuendelea kusoma neno la Mungu aliye hai maana imeandikwa kwa Yesu Kila Goti litapigwa.

Yoh.20:17 inaeleza mazingira ya Yesu baada ya kufufuka.Hakutaka kutoa mafundisho au kufanya kazi yoyote kwa sababu yote aliyamaliza pale msalabani.Alichokuwa anafanya ni kutaka kuwaaminisha wanafunzi wake na wengine kwamba kweli amefufuka kama alivyosema.

Kuhusu Swala la Baba na Mungu nimeshaliongelea sana hapa na kutoa vifungu vya Biblia.
Itoshe kusema tu kwamba Mungu ana nafsi tatu yaani BABA,MWANA(YESU) na ROHO MTAKATIFU-UTATU MTAKATIFU MUNGU MMOJA.Kikikosekana kimoja hapo Umungu haujakamilika.
Akisema anaenda kwa Baba ni sawa,Akisema Mungu wangu ndie Mungu wenu ni saw vilevile.
Mfano.Magufuli akisema Rais wa Tanzania hataki mzaha kwenye kazi,sidhani kama atakuwa amekosea.
Haya tuje kwenye huo utatu wako kama ulivyodai.

Baba (B) ni Mungu, Mwana (M) ni Mungu na Roho Mtakatifu (R) ni Mungu, lakini Baba si mwana, na Mwana si Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu si Baba”. Kwa hesabu rahisi na kwa kanuni inakuwa hivi, ikiwa B = G, M = G na R = G; kwa kufuatanisha inakuwa B = M = R, wakati sehemu ya pili ya maelezo hayo inaonesha kuwa B№ M№ R (inamaanisha haziko sawa). “Sasa je, huo si mkanganyiko juu ya utatu wenyewe?
 
Alikuwa nani kiongozi...?
Alikuwa ni Mungu,, aliponya,, aliokoa,, alifufua,, na kutenda miujiza mingi sana ., hivyo huyu hakuwa mwanadamu wa kawaida,,hakuna mtu awezae kutembea juu ya maji au kukemea pepo zivumazo baharini Bali ni Yesu tu.
 
Aliyekashifiwa kalalamika? Au kuna mtu analalamika kwa niaba
Hapana ni mafunzo mema aliyofunza kwa waislamu, pale aliposema''imani ya muislamu haijakamilika hadi pale mimi (mtume) nitakapokua napendeza zaidi kuliko mtu kupenda nafsi yake '' hili linaushahidi pale sayyidna umar alipomwendea mtume Muhammad na kumwambia '' hakika mimi nakupenda sana ewe Muhammad kuliko vitu vyote isipokua nafsi yangu'' jibu alilojibiwa ni '' bado hujanipenda, ili mapenzi yako yakamilike unipende mm zaidi kuliko nafsi yako ''
Hii ndio maana anapotokea mtovu wa adabu yeyote awae akamkashifu mtume Muhammad lazima waislamu wa kweli wasimame na kumtetea. Ukitaka kulijua hili kwa undani soma kitabu BIOGRAPHY OF THE PROPHET MUHAMMAD S. A. W. (SEALED NECTAT) BY safiu rahman al-mubarakpur, uone waislamu walivyo mlinda na kumtetea mtume wao ktk vita ya uhud.
 
Alikuwa ni Mungu,, aliponya,, aliokoa,, alifufua,, na kutenda miujiza mingi sana

Kwa hiyo mtu akifanya hayo mambo anafaa kuitwa MUNGU ikiwa tu amejaaliwa uwezo huo na MUNGU MUUMBA WA VYOTE ambaye ni MMOJA TU...?

hivyo huyu hakuwa mwanadamu wa kawaida,,hakuna mtu awezae kutembea juu ya maji au kukemea pepo zivumazo baharini Bali ni Yesu tu.

Watu wanatembea mpaka angani ndugu kila mtu kwa uwezo aliokuwa nao haijalishi anatumia uwezo gani, hao pia twaweza kuwaita MUNGU...?

Tuanzie hapo kwanza then tutaendelea.

Karibuni Sana.

Shukran.
 
Haya tuje kwenye huo utatu wako kama ulivyodai.

Baba (B) ni Mungu, Mwana (M) ni Mungu na Roho Mtakatifu (R) ni Mungu, lakini Baba si mwana, na Mwana si Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu si Baba”. Kwa hesabu rahisi na kwa kanuni inakuwa hivi, ikiwa B = G, M = G na R = G; kwa kufuatanisha inakuwa B = M = R, wakati sehemu ya pili ya maelezo hayo inaonesha kuwa B№ M№ R (inamaanisha haziko sawa). “Sasa je, huo si mkanganyiko juu ya utatu wenyewe?

Wewe utakuwa si wa kwanza kuchanganywa na hili swala la Utatu Mtakatifu.
Kadri unavyotafuta kuujua ndivyo unavyozidi kuchanganyikiwa.
 
Hupaswi kukashifu imani ya mwenzako wala eneo au sehemu wanayoitumia kuabudu kulingana na imani yao. Tanzania haina dini ila inalinda na kuheshimu imani za raia wake as long as hazikiuki sheria na taratibu za nchi. So kutukana, kukashimu ama kudhalilisha kwa namna yoyote imani ya mtu jambo hilo halikubaliki LAKINI lisiwe na upande mmoja haki itendeke kote sio wakikosea waumin wa iman fulan wanakushiwa ila wakikosea wa upande mwingine ndio inaonekana kosa tena kubwa kama uhaini vile. Ieleweke wazi siungi mkono tabia za kukashifu imani za watu.
Na kama kaelezea mashaka juu ya imani yake je
 
Wewe utakuwa si wa kwanza kuchanganywa na hili swala la Utatu Mtakatifu.
Kadri unavyotafuta kuujua ndivyo unavyozidi kuchanganyikiwa.

Wewe usiyechanganyikiwa kwa nini usimueleweshe inawezekana akaelewa nae akavutiwa pia akaja kwa yesu.

Mueleweshe mkuu.

Shukran.
 
Wewe utakuwa si wa kwanza kuchanganywa na hili swala la Utatu Mtakatifu.
Kadri unavyotafuta kuujua ndivyo unavyozidi kuchanganyikiwa.
Wewe unaejua ndio unieleweshe. Kama una amini kuwa Mungu ana nafsi tatu basi hakuna Mungu aliyekamili.
 
Back
Top Bottom