Mrimi
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 1,691
- 635
Kwa sasa watu wamegawanyika ktk makundi mawili.
Kuna linaloona kwamba maandamano wanayofanya CDM ni uvunjaji wa sheria, na kukaidi amri halali ya jeshi la polisi.
Lakini lingine linaona kwamba ni haki yao ya kikatiba kufanya maandamano ya amani ili kuonesha hisia zao juu mambo yale wanayoona ni kinyume na haki yao kikatiba.
Sasa tena jambo lingine ni kuhusu kibali cha kufanya maandamano:
-Chadema wanasema utaratibu halali si kuomba kibali bali ni kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kisha jeshi hilo lisimamie usalama katika maandamano hayo. Na kuhakikisha kwamba maandamano yanafanyika kwa amani bila uvunjifu wa sheria.
-Upande wa jeshi la polisi unasema Chadema wanawajibika kuomba kibali polisi, kisha polisi wana opt kutoa au kutokutoa hicho kibali kulinagana sababu za kiusalama.
Sasa tulio wengi si wajuzi wa sheria, tunaendeshwa zaidi na emotions. Kwa hiyo basi naamini kuna wanasheria wengi tu mnapita humu JF naomba mtuweke sawa katika hili. Napenda sana michango inayozingatia uhalisia wa mambo kuliko ushabiki usiokuwa na maana.