Wanasheria tupeni maelezo kwanini kesi zinachukua muda mrefu?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
4,702
2,000
Nilivyokuwa na miaka 14 nilipata ajali mbaya ya kogogwa na Gari Arusha. Mimi na rafiki yangu wakati huo tulikuwa kwenye baiskeli tunashangilia kuchaguliwa kuingia form 1. Mimi ndiyo nilikuwa abiria na bahati mbaya ndiyo niligogwa na gari la kampuni ya caterpillar na dereva akakimbia. Bahati nzuri gari lilikuwa na namba kubwa ubavuni na boss yule akashikwa baada ya uchunguzi.

Hii kesi yangu ilianza mwaka 1990 na mpaka leo sijui iliendeleaje lakini mpaka namaliza form 4 mwaka 1993 watu watatu mashahidi upande wangu walikuwa wamekufa kwa ulakini mmoja alikiwa polisi. Baada ya kuona watu wanakufa na mahakama inachukuwa muda yawezekana kesi waliamua kuifuta. Lakini cha ajabu mpaka leo kesi za Tanzania zinachukuwa muda sana na sijajua vizuri hasa sababu ni nini?

Naomba watu ambao ni mawakili, majaji au waendesha mashitaka watueleze ni kwanini kesi zinachukuwa muda mrefu sana na kunyima watu haki zao za msingi.
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,967
2,000
Mawakili na wanasheria ni kama mafundi ambao ukiwapelekea gadget/device yako wakutengenezee, mkapatana something like laki au laki 2, kwa mfano, hata kama tatizo ni dogo tu la elfu kadhaa, atalazimisha atumie hata ^we-key tea-sir^ :) au zaidi, ilimradi tu awianishe urefu wa muda aliotumia na kiwango cha fedha alichokutajia. USA waliitwa Kangaroo Courts!!!

NB: Chanzo cha tatizo ni walimu kuleeee shuleni ambao walituaminisha kwamba ukitumia booklets nyingiiiiiii kujibia mtihani (such as Essay), basi wewe moja kwa moja umejibu vema. Wanakuawadi maksi hata bila kusoma ulichoandika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom