Wanasheria, hukumu ya DOWANS na doctrine ya RES JUDICATA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasheria, hukumu ya DOWANS na doctrine ya RES JUDICATA

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by KAUMZA, Jan 12, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  LEARNED BROTHERS AND SISTERS!!!
  Tuachane kidogo na majukwaa mengine, hasa jukwaa la siasa. Maana siasa hupandisha jazba hasa mnapotofautiana kimawazo na kimtazamo. Naombeni tuliangalie hili kwa umakini. Wasomi wetu wa sheria wanataka kwenda mahakamani kupinga serikali kuilipa Dowans mabilioni ya shilingi wakati Mahakama ya usuluhishi ya kimataifa ilishatoa hukumu, JE DOCTRINE YA RES JUDICATA na ESTOPPEL OF JUDGEMENT(RECORD) haita-function hapo na kuwa kizuizi?
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Tulianza toka mwanzo kuiita ile hukumu ile sio hukumu kwani hukumu hutolewa na mahakama tu, waliosikiliza ule mgogoro sio mahakama bali ni chombo cha kawaida tu kilichopewa jina la International Chamber of Commerce (ICC). Suala likiwa kwenye usuluhishi hivyo kinachotolewa hapo ni tuzo au kwa kiingereza ni award.

  Wanaharakati wanavyokwenda mahakamani wanaenda kwa sababu sheria ya usuluhishi inaruhusu mtu asiyeridhika na tuzo ( sio hukumu ) kupinga tuzo hiyo kwenye mahakama ya kikweli.

  Katika misingi na mantiki hiyo res judicata na au estoppel haiwezi kuapply.
   
 3. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama watashinda, maana mlalamikaji na mlalamikiwa kwa pamoja walikubaliana kuipeleka kesi yao katika mahakama ya usuluhishi. Tungekuwa na nafasi nuri ya kushinda kama kesi ingekuwa imesikilizwa kwa upande mmoja tu i.e upande wa mlalamikaji bila mlalamikiwa kuwepo. Lakini kwa hili, serikali iliridhia na upande wa mlalamikaji uliridhia pia. Ingawa ktk sheria 1+1 si lazima iwe 2, inaweza kuwa 1 na muda mwingine inaweza kuwa 3, 4 na kuendelea
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Hebu fafanua kidogo maana naona kizunguzungu kutokana na reasoning yako
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Jan 12, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Naomba tu-digest maana ya phrases zifuatazo:

  1. "The decision of the arbitrator shall be final and binding upon the parties and shall not be subject to appeal. Either party may petition any court having jurisdiction to enter judgment upon the arbitration award. At the request of either of the parties, the Arbitrator shall cause such arbitration to be filed with the High Court of Tanzania."

  2. "The Parties waive any right to challenge or contest the validity or enforceability or any arbitration proceeding or award brought in conformity with this Section, including any objection based on venue inconvenient forum."

  3. "Every Award shall be binding on the parties. By submitting the dispute to arbitration under these Rules, the parties undertake to carry out any Award without delay and shall be deemed to have waived any recourse in so far as such waiver can validly be made."

  Kwa hiyo naomba tuchanganue Rules of ICC nilizoziandika hapo juu, hasa maeneo niliyoya-underline! Kwa haraka haraka sijaona sehemu ambao High Court inaweza ku-challenge kesi ambayo imetoka kwenye utaratibu wa Arbitration ila bado sijaelewa vizuri kama wasipoisajili Award hiyo itakuwaje! What is the effect of registration or non-registration? Let's discuss!
   
 6. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mi ninavyoelewa ni kwamba maamuzi ya msuluhishi yanakuwa ni ya mwisho. Kama ingekuwa ni hapa Tanzania ni kama vile kusema maamuzi ya mahakama ya rufaa. Ndipo mimi kwa uoni wangu nadhani hatutaweza kufanikiwa. Lakini kama mwenye kujua zaidi atupe darasa. Bado tunahitaji ufafanuzi juu ya jambo hili
   
 7. NyaniMzee

  NyaniMzee JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 80
  Ni kweli uamuzi wa msuluhishi ni wa mwisho, kutokusajili award ni kuvunja mkataba wa kimataifa wa kuheshimu maamuzi ya international tribunals ambao Tanzania tuliuridhia, pili kutokusajili tozo( award) kunafanya riba iongezeke ( in Dowans case ni 7.5% compound interest of the 94bn computed from 15th Nov. 2010 when the award was delivered). Kusajili tozo kunafanya tozo iwe enforceable by parties. tatizo linionalo mimi ni kuwa hawa wanaharakati pamoja na nia njema ya kulinda public interest watawezaje kusajili petition kupinga award ambayo is not properly before the court? Na petition yao lazima iambatanishwe na nakala ya Award ambayo haijasailiwa rasmi. hapooo sasa!!!!
   
 8. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ila nasikia mshitaki na mshtakiwa ni wamoja ni kiasi cha kuwahadaa watanzania kuwa kuna kitu kilifanyika. Mwanasheria mkuu wa serikali alikuwepo kwenye hiyo kesi au ni Rex Attorney pekee? Kwanini TANESCO wasiachiwe wakafanya mambo yao wenyewe bila kuingiliwa na executive government?
   
 9. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  NAFIKIRI WANASHERIA WETU NA WANAHARAKATI WAMEONYESHA NJIA wao wanafungua shauri Mahakama kuu kupinga uhalali wa tuzo iliyotolew kwa DOWANS isisajiliwe na kuwa Tuzo ya Kimataifa kwa sababu mikataba ya awali ilipatikana kwa rushwa na maslahi ya umma yalikiukwa this means the contract was NULL AND VOID ABINITIO AND U CANT DERIVE ANY RIGHT FORM NULITY CONTRACT,
   
 10. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  cha muhimu hapa ni kwamba pamoja na kujaribu kila njia kuepusha balaa hilo ila pia serikali ichukue hatua za madai dhidi ya REX ATTORNEY ambao walitoa muongozo batili,waliiruhusu serikali kuvunja mkataba na Dowans ilhali wakijua hatma hii na leo wanaishauri serikali kuilipa dowans,hii haiko sawa
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Jan 13, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo wakuu kama award haitakuwa registered effect yake ni ipi?
   
 12. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Wajomba"nchi wahisani" wataweza kutukatia misaada na pia uwekezaji utashuka nchini kwa kuwa tutaonekana wahuni. Tatizo hapa ni kwamba, wanasiasa waliingilia sheria. Inatugharimu na itatugharimu
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Jan 15, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nilikuwa namaanisha kwamba Award isipokuwa registered DOWANS hawatakuwa na haki ya kulipwa? Na kama watakuwa na haki ya kulipwa bila registration, sasa maana ya registration ni nini?
   
 14. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Hivi kuna mtu angetabiri kampuni kubwa kama BAE systems kuchunguzwa na kukutwa na hatia? Mi bado nashikilia kuwa ICC siyo infallible na tukiweza ku-prove kuwa wame-favour kampuni ambayo ni feki tunaweza tukawa na ushindi mkubwa zaidi. Sidhani ICC watataka kashfa. Mi naona hamna haja kuwafanya miungu mtu!
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Watanzania kweli mnanichosha, hivi hiyo Dowans inatoka kwenye nchi ipi muhisani na imeajiri watu wangapi huko? In impact gani kiuchumi kwenye nchi husika kiasi kwamba ikifa itaathiri uchumi wa eneo, state au nchi hiyo? Hao mnawaita wafadhili ina maana ni maroboti? Kwamba wakisikia tu Tanzania imegoma kuilipa Dowans bila hata kujua undani wake basi tayari wanakata the so called misaada? Ni mwekezaji gani genuine nayeweza kuwa in favor na jinsi Dowans ilivyoingia nchini, ilivyooperate na inavyotaka kulipwa? Hao Dowans wamewekeza $$ ngapi Tanzania so far mpaka wawe ni tishio kiasi hiki?
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Sheria ya Arbitration ipo wazi kuruhusu Mahakama Kuu kutobanwa na chombo cho chote hata kama mlikubaliana kuchunguza na kufanya maamuzi sahihi kuhakikisha haki inatendeka...................................unaloliongelea wewe ni kama limefanyika mahakamani lakini siyo kwa msuluhishi...................................na isitoshe TAnesco ni mali ya umma ilipaswa kiwepo kibali cha Bunge cha kuondoa mamlaka ya Mahakama Kuu kuchunguza TUZO ya Msuluhishi jambo ambalo hata hivyo halikufanyika......................

  Watendaji serikalini hawana mamlaka ya kisheria ya kuzuia TUZO kuchunguzwa na mahakama zetu kwa sababu wao siyo wamiliki wa hiyo taasisi..............wamiliki halisi ni raia kupitia Bunge lao.......................
   
 17. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #17
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimefuatilia mjadala na kupata ufahamu wa baadhi hoja kwa mtazamo wa sheria. Ila kuna suala moja tusaidiwe na wanasheria: Hivi ilipobainika kuwa mkataba wa Richmond na baadae ni haramu fake sbb unakiuka sheria, je justification na nguvu ya tozo ya ICC ipo wapi? Je kuvunjwa sheria ktk mkataba hakumaanishi ni makubaliano batili ambayo ICC haipaswi kuyazingatia kufikia uamuzi? Nchi na muwekezaji int. wakikubaliana biashara ya vichwa vya watu na mnoja kuvunja mktb je Icc itasikiliza shauri?
   
 18. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hivi kuandika kwako kote hapa ni kuogopa wahisani kutukatia Misaada??? Du!! kweli tunasafari ndefu sana ya kwenda huko miguu yetu itupelekako.
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Katika hili la Dowans hakuna anaeweza kuzuwia award ya ICC. Simpo.
   
 20. s

  smz JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi siko kisheria zaidi:

  Hapa ni kwmba halipwi mtu hata shillingi moja, kama serikali watafanya unyemela, hakuna siri tutagundua tu. hapo sasa ndipo tutaanzia hapo. Baba wa taifa alimwambia Kabila (marehemu) kwamba ana roha ngumu sana, kulipa madeni ambayo hayana kichwa wala miguu, akamwambia asilipe, nadhani kweli hakuwalipa, kwani walimfanya nini.

  Sisi hapa kupitia Ngeleja anasema lazima tulipe, lakini hasemi wale waliosababisha hadi tulipe hayo mabilioni yetu serikali inawachukulia hatua gani, huu ni zaidi ya uhujumu uchumi, lazima waseme watawafanya nini, na siyo kusema tu, lakini wote tuone wanafanya hayo watakayosema. kidogo hata tunawalipa angalau tunaona waliosababisha wananyea ndoo.
   
Loading...