Nchi za Ulaya zina historia ya kuwa na ugomvi na Urusi

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,314
3,444
Nchi za Ulaya zina historia ya kuwa na ugomvi na Urusi

Ugomvi huu una udini ndani yake

Isingekuwa mkono wa Marekani, Urusi ingekuwa imeshavamia leo hapo Ukraine

Ugomvi wa Ulaya magharibi na Urusi haujaegemea tu kwenye siasa na uchumi bali na katika dini pia ambayo ndio kiini cha mzozo wote. Nchi za Ulaya magharibi zilikuwa ni nchi za Kikatoliki na nchi za Ulaya mashariki zilikuwa za kiorthodoksi. Urusi ilikuwa ni mlinzi wa kanisa la mashariki huku Roma ikiwa mlinzi wa kanisa la magharibi. Ugomvi, uhasama na vita havikuepukika. Ndio maana hakuna Papa awaye yote aliyekanyaga ardhi ya Urusi, maana Warusi hawamtaki. Papa Yohana Paulo II alitaka kwenda huko akazuiliwa. Na leo Papa Francis ameonesha nia hiyo lakini hajakubaliwa. Warusi wana uchungu wa kihistoria kwa madhira ambayo yalifanywa nchi za magharibi zikiongozwa na kanisa hasa Ufaransa, Finland, Uingereza na Italia kuanzia karne ya 13. Hii ilikuwa Nato ya kale ambayo ilivamia Urusi na kuipiga sana, na tokea hapo mpasuko wa kutoelewana ukatokea.

Sababu kuu ya vita

Ubaba (patriaki) wa kanisa la Urusi unaongoza Waorthodoksi zaidi ya milioni 100 duniani na wote hawamtambui Papa kama mwakilishi wa Yesu na khalifa wa mtume Petro. Na vita vya kwanza kati ya Ulaya magharibi na Urusi vilitokea sababu hiyo. Mnamo karne ya 11 naam mwaka 1050 ulitokea mpasuko mkubwa kati ya kanisa la magharibi na lile la mashariki. Mpasuko uliokea baada ya Papa kumtuma mwakilishi wake huko Kostantinopo kumtaka patriaki mkuu ajisalimishe chini ya Ukulu mtakatifu (holy see) kwa kumtambua Papa kuwa ni Vicar of Christ na mrithi wa Petro. Akakataa na kumfukuza mwakilishi wa Papa, na mwakilishi wa papa akatoa matusi mabaya na kuahidi mabaya kwa Kostantinopo. Mnamo 1204 katika vita vya nne vya msalaba, vikaishia katika kuvamiwa kwa Kostantinopo na kutawaliwa kwa miaka 70. Waorthodoksi hawajawahi sahau jambo hili, walimlaani Papa kwa madhira aliyowafanyia. Kostantinopo ikadhooifika na kuliacha kanisa la magharibi kuwa na nguvu sana kiasi ambacho Kostantinopo ilitegemea ulinzi wake ili kujilinda dhidi ya Waislamu. Vatican ilishinikiza kutambuliwa kwa Papa katika baraza la Frolence. Lakini mwana mfalme wa Moscow alipinga maamuzi ya baraza la Frolence lililoongoza na patriaki mkuu wa Kostantinopo kwa ajenda ya kumtambua papa kama mkuu wa kanisa la kiulimwengu na mwakilishi wa Yesu duniani na khalifa wa Petro. Mwana mfalme huyo alijitenga na ushirika wa Kostantinopo na kumshinikiza patriaki ajiuzulu. Hivyo mpango wa Roma ukavunjika na wakaingia vitani naam vita vya msalaba dhidi ya Urusi na kuharibu miji mingi na kuleta kuzorota kwa uchumi wa Urusi. Kuanzia hapo uhasama ukaongezeka hadi leo hivi. Baada ya Kostantinopo kuanguka mikononi mwa waislamu mnamo 1453 (karne ya 15), Moscow ikasimama kama mlinzi wa kanisa la Orthodoksi hadi leo hivi. Mapatriaki wakaitangaza Moscow kama Rumi ya tatu baada ya Rumi ya pili (Kostantinopo) kuanguka. Juu ya anguko la Kostantinopo kuna mikono ya kanisa la magharibi. Waorthodoksi wanamsemo huu "bora kukaa chini ya kilemba cha Sultani kuliko kukaa chini ya tiara (taji) ya Papa". Waorthodoksi wana ajenda ya kuirejesha Kostantinopo, mnamo karne ya 19 ilikuwa manusura Kostantinopo irudi mkononi mwa Waorthodoksi baada ya Urusi kuipiga Othoman hadi ikaunyanyapaa mji huo na kukimbia. Lakini ajabu Wakristo toka magharibi wakiongozwa na Uingereza na Ufaransa na Italia wakaingilia vita na kuipiga Urusi na kuirejesha nyuma. Wakaishinikiza itoke Kostantinopo na Crimea na irejeshe maeneo yote kwa Othoman iliyoyatwaa, ikafanya hivyo. Othoman ikabakia kuwa mgonjwa wa magharibi (sick man of the west) ikilindwa na Ulaya dhidi ya Urusi. Chuki ikainuka zaidi kwa Waorthodoksi dhidi Wakatoliki, na Waprotestanti walioungana na Wakatoliki dhidi yao. Ndio maana katika vita vya Ukraine, Kiril patriaki mkuu wa kanisa la orthodoksi la Urusi alitangaza vita vya Ukraine kuwa ni vita vitakatifu vya kulinda kanisa na Urusi. Makasisi wake wanabariki silaha za Urusi kabla ya kwenda vitani. Na Urusi imetwaa maeneo yote matakatifu ya orthodoksi huko Ukraine katika eneo la Donbas. Na Zelenky yeye akijibu kwa kuondoa jadi za kiorthodoksi mfano tarehe ya Krismas na pasaka kufuata jadi ya katoliki na zaidi akiunga sera za ushoga jambo ambalo limelaaniwa na kanisa la Moscow. Huku Papa Francis yeye akiombea uongofu wa Urusi kwa moyo wa Maria ili kutimiza moja ya siri tatu za Fatima (nitakuja kueleza hapa kwa upana). Na akiyakosoa majeshi ya Urusi kuwa ni ya kikatili sana na kutaka dunia iwasaidie Waukraine. Akiwa Kazhkastan alikutana na wajesuiti wa kanda hiyo na kuwaambia wajipange zaidi maana dunia imeingia katika vita vya tatu vya dunia. Na zaidi anarushiana maneno na Patriaki Kiril kwamba Kiril amekuwa altar boy wa Putin, na Kiril naye akimkosoa kwa ajenda za ushoga.

Mabadiliko katika Ulaya ya zama za kati

Baada ya uprotestanti kuinuka mnamo karne ya 16, siasa za Ulaya zilibadilika kwa kiasi kikubwa. Wafalme wa Ulaya walibadilika kimtazamo, wale waliomuunga Papa na wale waliokuwa kinyume chake. Shirika la Jesuits liliundwa sababu hiyo naam kuua nguvu ya uprotestanti (counter reformation) ili kurudisha enzi ya Papa na nguvu ya kanisa la Roma katika Ulaya magharibi na duniani kote. Kupitia mwamvuli wa Wajesuiti wa Ukumene, Waprotestant wamerejea tena kwa kuchukua msimamo wa kati. Si rahisi leo kusikia mahubiri kutoka kwenye mimbari za Waprotestanti kwamba Papa ni mpinga kristo kama baba zao walivyofunza. Leo zimebakia injili za maridhiano, umoja wa dini, midhaha, miujiza na utabiri wa mambo ya siasa na mipira katika mimbara za Waprotestanti. Mafundisho ya mababa zao yamefungiwa kwenye makabati ya kanisa, hayajulikani na waumini. Waroma wanashangaa maana hawakufikiria hali hiyo kwa wepesi wanaouona. Kupitia baraza la pili la Vatican, Roma ilipunguza makali (ikajiweka low), ikajifanya imebadilika kimsimamo. Vitabu vingi vikaandikwa vya mapenzi kwa waprotestanti waliolaaniwa na mapapa wa zamani kwamba hawatakanyaga mbinguni maana Petro hawatambui. Roma sasa imechukua msimamo wa kati hadi kuchukua baadhi ya mafundisho kadhaa ya waprotestanti ili kulaanisha umoja. Roma imefanya hivyo kijasusi tu, Waroma wasioelewa wanakwazika hasa wanapoona kanisa lao linalaanisha mambo. Waprotestanti wanaona Roma imebadilika, rejea baraza la umoja wa waprotestanti wa Marekani mnano 2014 huko Marekani katika ukumbi wa kanisa la Kenneth Copeland. Tonny Palmer kama mwakilishi wa Papa, alimwakilisha papa katika mkutano huo, akatoa hotuba ambayo ilipokelewa na umoja huo na akatoa kauli tata kwamba uprotestanti "UMEKWISHA". Akashangiliwa na wote wakaingia kwenye maombi ya pamoja yaliyoongozwa na Kenneth wakimwombea Papa na kunena kwa lugha ngeni. Papa Francis akawapigia simu na kutoa maneno mazuri ya umoja na kuwakaribisha Vatican kwa mvinyo na chakula. Na walienda wote. Roma haijabadilika ipo pale pale ni Uprotestanti ndio uliobadilika, hayo ni maigizo tu. Roma injili yake ni ile ile ya kuokolewa kwa matendo na si kwa njia ya imani, Roma bado inaomba kwa Maria, Roma bado inaombea wafu na kuomba watakatifu wake. Tuachane na hili, turejee pale tulipoishia.

Kwanini Marekani inakataa vita vya moja kwa moja dhidi ya Urusi?

Marekani ndio kizuizi cha nguvu ya Ulaya iliyopotea baada ya vita vya kwanza na vya pili vya dunia. Ulaya magharibi haikuwa na jinsi zaidi ya kuegemea Marekani kiulinzi, kisiasa na kiuchumi. Urusi nayo ikakuwa kijeshi, kisiasa na kiuchumi na ikawa na umoja mkubwa ulioitwa USSR. Ulaya ikaogopa, nayo ikaunda NATO lakini hawakuwa na uwezo dhidi ya Moscow. Ikabidi waishawishi Marekani kujiunga na Nato pamoja na Canada. Ndipo Nato ikawa na nguvu na kujisalimisha totally kwa Marekani kiulinzi. Ingawa Ulaya ilikuwa na ajenda fiche ya kuwa na umoja wenye nguvu wa kiuchumi na kijeshi nje ya Marekani. Hivyo umoja wa Ulaya ni hatua ya kufikia malengo yao. Umoja wa Ulaya (EU) umeasisiwa na Vatican, hawa ndio wapo nyuma ya pazia. Mjeruman na Mfaransa ni wasimamizi maana wao zamani ndio walikuwa nguvu na jeshi la Papa na kanisa la Rumi. Hawa wanahamu sana Urusi ivamiwe kijeshi, Macron na Kansela wa Ujeruman wameshatoa kauli tata za uvamizi lakini Marekani hataki, ndio maana Macron ametoa kauli kwamba Ulaya iachane na USA na kuunda jeshi lake. Kwanini Marekani haitaki vita vya moja kwa moja?

Marekani na Urusi wanahusiano wa jadi, wote walikuwa na adui mmoja naam VATICAN. Na ndio maana Mrusi alimuuzia Marekani Alaska akiwa hana shaka na Marekani. Sahivi wanajuta sana. Na zaidi wanamikataba ya ulinzi ya kutovamiana na kuchunguzana. Ugomvi wa Marekani na Urusi ni wa kutengeneza kutoka Ulaya, maana katiba ya Marekani hairuhusu Marekani kujitanua kijeshi ama kuingilia mataifa mengine. Uongo ulitengenezwa kwamba Urusi ni tishio la usalama wa Marekani na dunia, hivyo bunge la seneta likapitisha ajenda kwa Marekani kulinda uhuru wake nje ya mipaka ya Marekani, hivyo CIA ikaundwa kwajili hiyo. Hapo ndipo Marekani ikaanza kuvamia nchi ambazo ziliunga sera za USSR kama Vietnam nk. Lakini cha ajabu huko Veitnam walimpanda Rais mkatoliki aliyeuwaua mamilioni ya Wabudha na kuleta ubaguzi wa kidini. Rais Jeff Kenned alipoingia madarakani, alikomesha msaada kwa rais huyo na kukomesha vita hivyo kwa hoja kwamba vita hiyo si kwa faida ya Marekani bali kwa kikundi cha siri. Vita vilikoma na rais wa Vietnam akakamatwa na wananchi na kunyongwa. Jeff hakuishia hapo, akairudi na CIA ili kuivunja kwa hoja kwamba haipo kwajili ya Marekani bali kikundi cha siri aka Vatican. Wakaona kijana ni msaliti, wakamuua haraka. Lakini raia wakaandamana wakitaka haki ya kifo chake, serikali ikadanganya. Tokea hapo ajenda za kikundi cha siri zikakwama hadi alipokuja rais Reonald Reagan aliyefanya mahusiano ya kibalozi na Holy see -Vatican na kuanza vita kamili dhidi ya Urusi na Soviet kwa ujumla. Huyu alivunja daraja la utengano kati Marekani na Vatican toka karne ya 19 hadi karne ya 20. Utengano huu ulitokana na kuingilia mara kwa mara kwa Vatican dhidi ya katiba ya kiprotestant ya Marekani ambayo Papa aliilaani na kutamka kwamba inapaswa kuangamizwa. Na kwa wakati huo rais kipenzi wa Marekani Abraham Lincon mtetezi wa katiba ya Marekani na mpinzani wa Vatican aliuawa kwa kifo cha kutatanisha ambacho kilileta sintofahamu kubwa sana. Hivyo Vatican ikatuhumiwa maana Lincon aliisema vibaya Vatican kwamba inataka kumuua kupitia jeshi lake la Wajesuiti. Tokea hapo baada ya kifo chake, uhusiano kati ya USA na Vatican ukakoma hadi enzi za Reagan. Ukumene ndio sehemu ya mapatano kati ya Kanisa la Rumi na Waprotestanti. Na huko ndio mwanzo wa kuharibika kwa sera za nje za Marekani na kuumbika kuwa taifa la kifashisti duniani hadi kutetea demokrasia ya kigiriki ya ushoga na kutwaa ubabe wa Rumi.

Kwanini baadhi ya nchi za kiorthodoksi zipo Nato?

Kwanini Macron anataka liundwe jeshi la umoja wa Ulaya na kuachana na Marekani kiulinzi?

Vatican inahusika vipi na umoja wa Ulaya?

Kwanini Vatican inaitaka sana Urusi?

Itaendelea......zaidi utayapata kwa upana katika kitabu kijacho cha SIRI YA UASI KUTOKA MTO HIDEKELI (Seh 3)

Na Jeff Massawe
The watchman
0757722557
FB_IMG_1714671029879.jpg
 
0757722557View attachment 2979273
Waswahili tunawaza udini wakati wenye akili wanawaza haki na maendeleo, toa mambo yako ya udini kichwani kama hujaenda shule ,hujasoma kuhusu historia ya dunia kuhusu socialism na capitalism na sisi nam, wewe unawaza udini tu
 
Urusi pia in Ulaya.

Wazungu wa Urusi ni Wazungu wa Kabila/Jamii ya Slavs.

Wanapatikana Urusi hadi Czech
 
Waswahili tunawaza udini wakati wenye akili wanawaza haki na maendeleo, toa mambo yako ya udini kichwani kama hujaenda shule ,hujasoma kuhusu historia ya dunia kuhusu socialism na capitalism na sisi nam, wewe unawaza udini tu
Historia haijaanzia kwenye socialism na capitalism,, anachosema mleta mada hajakosea ........asili ya kanisa la orthodox la urusi ni Ukraine, huku sie hizi dini tunazichukulia kama sehem tu yakuweka hisia zetu ila huko zilipotoka ni vyombo vya utawala japo kwa sasa wanavaa sura nyingine
 
Mi mwenyewe nashangaa kuna kipi kipo nyuma ya pazia kinachopelekea Ufaransa kuwa na msimamo kiasi hiki kufikia hatua ya kufanya maamuzi magumu kupeleka askari wake Ukraine.
 
Lakini hii si ndo ile dini ya mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie na la kulia,, 😳, dini ya amani hii kumbe na nyie mnadundana
 
Uko sahihi, hata sasa kuna crack down ya kanisa la Othodox la mashariki huko ukraine, waumini wake wanakamatwa
 
Utakapo endelea nistue.Usisahau kuelezea tofauti iliyopo kati ya Roman na Orthodox Church.

Naanza kukubaliana nawe pale Ukraine kwenye ule mji Mariupol (bikira maria),ulitandikwa mabomu yakutosha kiasi kwamba mpaka papa aliguna.
 
Roman kiongozi wao mkuu ni papa wa Vatican ila wa orthodox viongozi wao wapo kutokana na eneo la utawala wa kanisa hawana kiongozi mmoja kwa kanisa lote, orthodox ya urusi ina kiongozi wao, ukija ya wagiriki, Syria nazo hivyo hivyo zina viongozi wake wakuu, pia ishara ya msalaba ya orthodox inaelekea kulia halafu kushoto wakati roman ni kushoto halafu kulia,, pia orthodox wanaamini roho mtakatifu anatoka kwa Mungu (baba) tu huku roman wanamini roho mtakatifu anatoka kwa Mungu pamoja na mwana (Yesu),,,wote ni wakatoliki sema vipengele vichache ndo wanapishana
 
Back
Top Bottom