Habari za jioni waheshimiwa, mo naomba bunge lijalo lipitishe sheria kali kwa wale wanaowasha taa full wakati wa usiku kwani huwa zinaumiza sana, kitu ambacho kinaweza kusababisha kutokuona vizuri na wakati mwingine ajali.
Unakuta madereva wengine wanawasha taa kali kama vile wanawinda maporini usiku. Huwa inakera sana wajameni.
Au kama sheria ipo tafadhali nijulishwe hatua za kufuata.
Ni hayo tuu kwa leo, nawasilisha ....
sheria ya usalama barabara no.30 ya mwaka 1973 na marekebisho yake no 16 ya 1996 sehemu ya 39 kifungu cha 39c kifungu cha 5 inasema: dipped (beam) itaruhusiwa kwenye
(a) mitaa ya watu wengi na zipo taa za kandokando mwa barabara,
(b) iwapo anamkaribia mwenzake ili wapishane vizuri
(c) iwapo anataka kulipita gari la mbele yake
(d) mtu yeyote akitenda kinyume cha hapo atakuwa ametenda kosa.