Wanaowasha full light barabarani usiku

Wanaowasha full light barabarani usiku

Tena ukiwa maji......unaona kama ni pikipiki mbili zinakuzengua............bora kusiwe na hizo taa kabisa...........

Hahaa!unaona km pikipiki mbili afu unaamua kukaa katikati yao ili zikupite pembeni kinachofuatia ni 🎶parapanda italia...🎶🎵
 
Maelezo yako yanakiri kuwa matumizi ya taa FULL yapo na yanakubalika. Sijui hapa unabishia nini.
 
tembea na kioo cha kijiangalia , akikupiga full unakiweka mbele apate reflection yake mwenyewe tena unamuelekezea machoni, mm nimefanya ivyo wanazima haraka sana
 
kiukweli hili swala hata mimi lina nikela sana.
tatizo watu baadhi ya madereva hawajui matumizi ya taa. Kuna hizi taa nyeupe ndio zinaumiza balaa yani kama ulikuwa kwenye kona mkatana na yupo full light anakupoteza kabisa...

KWA MIMI nafikiri kutembea full light sio kosa ila inshu je hiyo full light unaitumia sahihi?
na hili huwa lina tunatokea sana sans kwa waendeshaji magari magodo, wengi wana shidwa kutumia hizii taa na baadhi hata ukimwonyesha ishara ya kuwa apunguze hapunguzi.
HAKIKA INAKELA
 
Ila kuna hizi taa za HID nazo zinamwanga mkali hata kama sio full japo kuwa sio sawa na full.
 
Kwanza nionavyo mimi tatizo hili lipo sehemu mbili kuu ya kwanza ni adjustments za taa zenyewe kwani wengi wa madereva hawajui taa ziko sawa na zinamulika kama zilivyotengenezwa? Maana kuna gari zingine ukipanda unashangaa zinamulika angani utafikiri ni ndege, zingine zinamulika pembeni ya barabara utafikiri anawinda. Hapa ushauri ni wangu kama una gari sogeza karibu na ukuta washa taa za gari na uangalie zinamulika straight kama la rekebisha ukishindwa peleka kwa mechanic arekebishe. La pili ambapo ni kwa madereva wanaotumia full light kila wakati hilo ni kosa kubwa lakini hilo ni jukumu la traffic kuwasimamisha na kuwatuma hospital wakapime macho. Amini usiamini wengi wa madereva wanaowasha full hawaoni vizuri. Jiulize ni wangapi humu wamewahi kujitolea tu kupima macho kwa optician. Think big
 
hii nimekubali sana tena mimi naweza kuwa katibu mwandamizi wa kuisaport team ya ktengeneza circuit hiz
 
Back
Top Bottom