Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 57,239
- 90,296
Ukiacha vichwa panzi wachache na mapoyoyo wa hali ya chini na wale wenye maisha duni wanaoimbishwa wimbo wa amani bila haki na wanaimba kwa sababu ya ukosefu wa maarifa, taarifa sahihi au udini wengine wote wanaoimba zaidi amani badala ya kuimba zaidi haki ni wanufaika wa mfumo ulioondoa mazingira ya haki na kuifanya nchi kuwa ya kakikundi kadogo cha watu wanaoamua watu wengine waseme nini, wapate habari gani, wanaoteka, kupoteza, kuua watu na kufanya ufisadi uliopindukia.
Ukweli ni kwamba uwepo wa haki katika nchi utaondoa mahubiri, mawaidha, kelele na harakati zote za amani katika nchi.
Uwepo wa haki utafanya uchaguzi ufanyike bila mitutu ya bunduki na magari ya kutisha ya polisi.
Uwepo wa haki utasababisha watu waendelee na biashara zao bila hofu yoyote hata wakati wa uchaguzi.
Uwepo wa haki utaondoa harakati na ngonjera zote za manabii wa mchongo kama Mwamposa na taasisi kama BAKWATA kila inapofika wakati wa uchaguzi
Uwepo wa haki utasababisha hata kamati za mchongo za amani na maridhiano kama hizo za Sheikh Alhad Musa kukosa kazi na kujifia zenyewe.
Msisitizo na kelele nyingi sana kuhusu amani ni kwa sababu HAKI haijatamaliki katika nchi yetu kwa muda mrefu sana. Ni kupoteza muda tu kupiga kelele za amani kama hakuna HAKI, ni sawa na kutumia dawa ya kutuliza maumivu ya kichwa wakati unaumwa Malaria.