Wanaosema 'Money Can't Buy Happiness...'!

Kwani asiyekua na hela hafiwi mkuu? Kuna vitu haviepukiki uwe na hela au huna, lakini kufiwa na ndugu mkakosa hela ya kumtoa hospitali kisa bill kubwa maumivu yake hayaelezeki.
Nani kasema asiye na hela hawezi kufiwa tunazungumia hao madogo ambao wanasema unaweza kuwa na furaha kisa tu unapesa wakati Kuna wenye pesa wa misongo ya mawazo. Ukiacha kutokuwa na pesa Kuna mambo kibao tu duniani yanaweza kukuondolea furaha
 
NDIYO, pesa inaweza kununua furaha, Una uwezo wa kukifikia kila unachokita, kwa nguvu ya pesa huzuni inatoka wapi.
.
.Ndiyo maana kuna neno Pesa inaweza kupafanya pa Giza kuwa mchana na mchana kuwa usiku.
 
Siyo kweli mkuu. Unaweza weka tafsiri yako na isifanye kazi. Furaha haitokani na tafsiri yako juu ya furaha yenyewe bali inatokana na tafsiri yako juu ya mafanikio na kumbukumbu zinazokuzunguka.
Hapo tayari umeshaweka tafsiri yako ya furaha kwa kusema inatokana na mafanikio yako, bado nitarudi kukuuliza mafanikio kwako ni nini? Bado kila mtu atabaki na tafsiri yake
 
Wakuu pesa ndo furaha yenyewe, hata kama unaumwa ukajua unauwezo wa kwenda India ni furaha pia 😂😂, bora kulia kwenye Nissan Terra tena nipige na mayowe poa tuu kuliko furaha huku unapiga miayo
 
Back
Top Bottom