Je, kinachoendelea sasa katika nchi tajiri ya Marekani ni uthibitisho kwamba pesa sio kila kitu (Money can't buy everything)?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Good evening jamiiforums

Je, kinachoendelea sasa katika nchi tajiri ya Marekani ni uthibitisho kwamba pesa sio kila kitu (Money can't buy everything)?

Marekani ana-sign peace deal na wanamgambo? How comes? Americans have enough cash, fully equipped military/intelligence machinery plus overwhelming political influence lakini bado wanaomba poo?

gfghytgb.jpg


Marekani (USA) ndio nchi yenye pesa nyingi, teknolojia ya kutisha pamoja na mifumo imara ya ulinzi na usalama hapa duniani ikufuatiwa na mataifa kama China, Uingereza na Ufaransa.

Kwa namna Marekani ilivyo na "assets" za kila namna sikutegemea kabisa kama wange-sign peace agreement na wanamgambo wa Taliban ambao hata ndege vita moja hawana.

Taliban wanapigana kwa kujificha, silaha duni, pesa za kuungaunga na Intelligence gathering mbovu leo wanaingia makubaliano ya kusitisha vita na nchi yenye mihela?

HATA MIMI NINAPENDA KUJA KUWA TAJIRI SIKU ZA MBELENI

Ninaomba ieleweke kwamba mimi sichukii watu wenye pesa nyingi/matajiri hata siku moja. Matajiri wamenisaidia sana na ninatamani kuwa kama wao hapo baadae.

Pesa ni kitu kimoja muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Ukosefu wa pesa umefanya watoto kufa mapema sana kwa sababu ya kukosa matibabu stahiki ambayo laiti kama wazazi wao wangekuwa na pesa ya kutosha, wangeweza kuishi muda mrefu zaidi na kufika hata miaka 80.

Umuhimu wa pesa unaweza pia kuonekana linapokuja suala zima la elimu. Mimi ni mmoja wapo wa wahanga wa suala zima la kusoma pasipo kuwa na pesa za kutosha.

Ningekuwa na uwezo wangu wa ku-upload vyeti vyangu vya kidato cha nne na sita humu JF mngeshangaa sana.

Matokeo yangu ya mitihani ya vidato hivyo viwili yanatofautiana kwa mbali mno. Nilifaulu kwa alamu za juu kidato cha nne kwa maana shule niliyopangiwa ilikuwa na walimu wazuri waliofundisha kwa juhudi pasipo mtoto kuhitaji kusoma masomo ya ziada.

Kidato cha tano na sita, nilienda kusoma katika shule ambayo ilikuwa ni lazima mwanafunzi asome masomo ya ziada (tuition) ili aweze kufaulu.

Sasa mimi baba yangu atapata wapi pesa ya kunipa nikasoma tuition wakati nguo/t-shirts tu za kuvaa nikiwa nyumbani nilikuwa nazo mbili mpaka watu wamenikariri wakawa wananiita "yule jamaa anayevaaga t-shirt nyekundu".

Kuna kipindi niliacha kabisa hata kwenda kanisani kwa maana nguo ni hizo hizo tu kila jumapili mpaka wasichana wakawa wananicheka.

Siku moja nikiwa kidato cha tano nilienda ofisini kwa mwalimu wa taaluma nililia saaana kama dakika 10 mbele ya yule mama nikamsimulia shida nilizokuwa ninapitia nyumbani kesho yake akaniletea nguo kadhaa za mtoto wake wa kiume.

Keep resting in peace madam Rosemary, sitakuja kukusahau shujaa wangu. Hakika umasikini ni mbaya sana.

Juzi hapa kuna watoto waliuawa wakiwa wameenda kuiba kuku. Just imagine mtoto anauwawa kisa kuku wa 15,000/= tu?

Ndugu zangu madhila ya umasikini ni mengi sana na ninaweza kuandika hata kurasa 1000 zinazohusiana na kadhika ya kutoka katika familia fukara. Nimeishi katika umasikini hivyo ninaujua from A to Z.

Kwa kipindi kirefu sana watu wamekuwa wakihusisha matukio ya uhalifu na viwango vya umasikini huku reference kubwa ikifanywa kutoka katika nchi zilizomo ndani ya bara la Afrika kama vile Tanzania.

Kwa namna nyingine tunaweza kusema kwamba "the higher the the poverty level, the higher the crime rate".

gfgtghnbgf.jpg


Katika page ya Facebook ya kaka/mdogo wangu Millard Ayo nimekutana na taarifa hii inayohusu maamuzi ya bunge la huko kuruhusu watu kutembea na silaha hata kama hawana vibali kutokana na matukio ya "random shooting" ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika majimbo mbalimbali huko nchini USA;

"Wabunge wa Texas Marekani wamepitisha muswada utakaoruhusu Wakazi wa Jimbo hilo kubeba bunduki na kutembea nazo mtaani hata kama hawana vibali vya kubeba silaha tofauti na sasa ambapo sheria inataka yeyote anaebeba bunduki kuwa na leseni, awe pia na mafunzo ya kuitumia lakini pia historia yake lazima ichunguzwe.

Wanaounga mkono sheria hiyo mpya wanasema itaruhusu Raia wa Texas kujilinda wenyewe huko mitaani na huenda ikasaidia Raia kujibu mashambulizi pale Mtu mwenye silaha anapofyetua risasi bila sababu kwenye eneo la umma kama ambavyo imetokea Watu kuua Watu kanisani, super market na sehemu nyingine za umma"


SWALI: Je, kinachoendelea katika nchi tajiri ya Marekani kwa sasa ni uthibitisho kwamba pesa sio kila kitu (Money can't buy everything)?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Nimekula saaaaana pesa za boyfriends wa mashosti zangu. Nimewachuna haswaaa. Nilifanya sana umalaya enzi nipo chuo IFM na mabosi wa pale town hivyo ninajua ninachokisema.

Sasa nimeolewa, nipo na watoto 2 Iringa. Njoo unywe ulanzi.
sasa mbona kama unafukua makubiri yako mkuu!!?
 
Kuwa na moral na Tabia nzuri ni kitu kizuri sana kwenye maisha,

Wazungu wengi hasa wa Right wing hawana moral, wao ni maslahi tu kwenda mbele, kama kuna maslahi kushirikiana na Taliban watashirikiana nae na haijaanza leo, wakati Osama anapigana na Urusi Marekani walikuwa wakimpa support.

Ndio maana maisha yao wengi wanaishia kuwa wapweke na wasio na furaha, wengi sio emotional na wenye mpenzi, wanajali tu maslahi.
 
Shida na matatizo ni part ya kuwa mwanadamu Infantry Soldier
Kuna solution moja tu iliyothibitika juu ya shida, nayo ni kuacha kuishi, kufa.

Haya maisha ni Comedy ukitizama kwa angle fulani. Mfano Marekani ana kombora na silaha za gharama/aghali sana, sasa kudondosha kombora la mill mia tano kwa hema la talibani ni kichekesho. Kama akiamua kumpa nusu ya gharama ya kombora la kumwangamiza kwa makubaliano kutokuingiliana katika maslahi inakuwa win win situu kama wachumi wasemavyo

Kwa mada yako kapiga ndege wawili kwa jiwe moja. Kwanza talibani, pili kapunguza gharama za jeshi
 
Back
Top Bottom