Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Bila Wakaidi na Wapingaji tungekuwa hatuna maendeleo huku tukiishi kwenye sayari yetu ambayo ni tambalale na jua linaizunguka....

Na wala tusingehoji wala kutafuta / kujua mazingira yetu ili tupambane nayo sababu tungekuwa tunakengeuka kama waliotaka kujenga mnara wa Babeli (Na bila hao kutaka kujenga huo Mnara huenda hizi lugha tofauti zingekuwa hazipo)

Hence binafsi ninapenda uwepo wa hao so called wakaidi
Kuna vituko sana lakini hakuna zaidi ya ujinga wetu binadamu.

Yaan kama sio wachache kuhoji na kukataa kushikiwa akili dunia ingekuwa bado ndio katikati ya ulimwengu. Kila kitu kinazunguka sayari hii maalum, na sisi wanadamu ndio tungekuwa tumeekewa vitu vyote(sayari za kila aina gesi na jiwe, nyota za kila aina, mawingu yanayozaa nyota, miundo mbalimbali ya vikundi vya nyota n.k) ulimwenguni. Ili tu kuwaaminisha na kushangaza viumbe binadamu uwezo wa mwenyezi mungu. Lengo tuabudu huyo mungu. Mambo yote mwisho ibada!

Lakin wap... sayari yetu ni ndogo, ya kawaida mno. Jua letu nyota kubwa kiasi, isiyo na maajabu yeyote. Mtaa wetu wa nyota umedorora, hamna matukio yoyote makubwa ya kiulimwengu yanayotokea au kuendelea ukitoa kijamii chetu kinachojiita cha pekee. Knachodai kuumbwa na muumbaji wa ulimwengu wote unaotuzunguka sisi(sio kweli). Kwa ajili tu ya kumpunguzia upweke na kumuabudu huyo mungu. Baadae auangamize na wachache wachaguliwe kuendelea na huo utumwa milele kwake, kusikojulikana. Hakuna anayepajua.

Ujinga mtupu!
 
Kusema hayupo hakufanyi asiwepo.

Hayupo kwa sababu hayupo

Sasa kama unajua hivi, kwa nini tunaendelea kubishana.

Na kama unakubaliana na sentesi ya kwanza, sasa hiyo yapili huoni kama unajichanganya mwenyewe.

Maana wewe unakubali kuwa kusema hayupo, hakufanyi asiwepo, kisha unasema hayupo, halafu unalazimisha asiwepo???????

Ndio nini sasa.
 
Huwezi kusema watu wanaohoji ni wajinga... utakuwa una mtanzo kinyume na uhalisia wa mambo!
Wapi nimesema hivyo?

Lakini pia anaehoji huwenda ni mjinga, maana anataka kujua.

Na ujinga sio tusi ni hali ya kutokujua.

Lakini kupinga jambo usilolijua ni.....?

Je wewe unajua kama mungu yupo?
 
Eti mtu anakwambia, katika plane Euclidean geometry:

Duara lina nyuzi 360.

Pembetatu ina nyuzi 180.

Hivyo, pembetatu haiwezi kuwa duara, na duara haliwezi kuwa pembetatu.

Halafu, anakwambia kuna duara moja special ambalo hapohapo ni pembetatu.

Anataka ukubali tu.

Ukikataa, unaitwa mkaidi.
Unajua kama mungu yupo?
 
Quran haiwez kutumika kam reference ya uhakika
mfano mungu wenu naona alijichanganya au alisahau jinsi alivyoiumba dunia
20:53 - tunaambiwa dunia iko kama carpet
79:30- tunaambiwa dunia Ina umbo la yai la mbuni

Inakuaje muumbaji wa dunia anashindwa kutambua umbo sahihi anajichanganya namna hii
Uwe unasoma kijana, aya ya 53 katika sura ya 20 ni hii :

53. Na tulipo mpa Musa Kitabu na pambanuo ili mpate kuongoka. (Taha : 53)

Sura ya 79 aya ya 30 inasema hivi :

30. Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. (an-Naazi'at : 30)

Wapi amejichanganya ?

Halafu kuna wajinga wenzako wamekupa like. Nasubiri uweke aya inayosema kwamba dunia ina umbo kama la Yai.
 
Kwanza kabisa, dhana ya kuwapo Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na ujuzi wote, inajipinga yenyewe kabla mtu yeyote hajaipinga.

Wengine wanaonesha tu dhana inavyojipinga yenyewe.

Unaelewa hilo?
Naomba unionyeshe inavyo jipinga yenyewe.
 
Hayupo kwa sababu hayupo.
Hii haiwezi kuwa sababu. Sasa sisi tutakuuliza umejuaje kama hayupo ? Kwenye jibu la swali hili ndiyo kuna sababu ila hiyo uliyodai si sababu kiuhalisia bali ni mpangilio mwepesi wa sentensi isiyo kamili, yaani hiyo ni sehemu ya sentensi yenye kuihitaji kielezi kufidisha sentensi kamili au ili iwe kamili.
Na hili utaliona kwa kuangalia logical inconsistencies na self contradiction katika dhana ya uwepo wake.
Kingine hii si dhana bali ni uhalisia, dhana unasema wewe kutokana na uchachefu wako wa maarifa juu ya jambo hili.
Uwepo wa Mungu huyo ni sawa na mtu akuambie kwamba kuna duara ambalo hapo hapo ni mraba katika plane Euclidean geometry.
Huu mfano si sahihi, sababu unalinganisha vitu viwili visivyo lingana wala kukaribiana. Una tatizo kubwa la kulinganisha mambo.
Hakuna kitu hicho, ni stories tu za watu.
Naomba uthibitishe ya kuwa hizi ni stori tu za watu.
 
Wewe siku ya kiama ni moto tuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, hawezi kuachia viumbe wake aliowaumba mwenyewe katika dunia yake mwenyewe wachomwe moto.

Hivyo, hata ikiwa kweli nitachomwa moto.

Hilo litathibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
 
masdinero masproblemas
Kumbe hata hujui kama mungu yupo, maana unamaswali kibao juu yake.

Sasa ilikuwaje ukapinga uwepo wake ikiwa hujui kama yupo?

Huoni kama unapinga uwepo wa mungu kwa ujinga wako?

Huu ndio ninaoita mimi ukaidi.
 
Lengo la huu uzi wako ni lipi ?
 
Kuna vituko sana lakini hakuna zaidi ya ujinga wetu binadamu.

Yaan kama sio wachache kuhoji na kukataa kushikiwa akili dunia ingekuwa bado ndio katikati ya ulimwengu. Kila kitu kinazunguka sayari hii maalum, na sisi wanadamu ndio tungekuwa tumeekewa vitu vyote(sayari za kila aina gesi na jiwe, nyota za kila aina, mawingu yanayozaa nyota, miundo mbalimbali ya vikundi vya nyota n.k) ulimwenguni. Ili tu kuwaaminisha na kushangaza viumbe binadamu uwezo wa mwenyezi mungu. Lengo tuabudu huyo mungu. Mambo yote mwisho ibada!

Lakin wap... sayari yetu ni ndogo, ya kawaida mno. Jua letu nyota kubwa kiasi, isiyo na maajabu yeyote. Mtaa wetu wa nyota umedorora, hamna matukio yoyote makubwa ya kiulimwengu yanayotokea au kuendelea ukitoa kijamii chetu kinachojiita cha pekee. Knachodai kuumbwa na muumbaji wa ulimwengu wote unaotuzunguka sisi(sio kweli). Kwa ajili tu ya kumpunguzia upweke na kumuabudu huyo mungu. Baadae auangamize na wachache wachaguliwe kuendelea na huo utumwa milele kwake, kusikojulikana. Hakuna anayepajua.

Ujinga mtupu!
Duuuu umeongea fact tupu Hawa wajinga hudhani Dunia ni special sana na hizo nadharia za Mungu hubase hapa hapa tu Sasa unajiuliza kama huyo Mungu wao yupo Ndio ashindwe kujua formula za ulimwengu zilivyo Mpaka atoe hekayq za kijuha kwenye maandiko aliyoshisha yeye (according to Qureshian mythology/Islam)
Allah claims jua huzama kwenye chemichemi za matope
WTF!
😁😁😁😁🔥
 
Back
Top Bottom