Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Wanaokana mungu huwa wanahoja mbalimbali katika kupinga uwepo wa mungu, pia huwa wanakosoa mafunzo ya dini ili kutilia mkazo zaidi katika hilo.

Lakini ukweli ni kwamba, sio kama hoja zao zinathibitisha kutokuwepo kwa mungu, hapana.
Bali hoja zao zinathibitisha kuwa wao ni wapingaji, hivyo hakuna andiko wala muujiza utakao wafanya waamini, sembuse hizi hoja ambazo huwa wanarumbana na watu Kila kukicha.

Na hivi ndivyo walivyo tangu enzi na enzi, hoja zao ni zilezile, na hata katika Quran, imeelezwa jinsi hawa watu walivyowakaidi.

Walipoonyeshwa miujiza waliita uchawi, maneno ya mwenyezimungu waliyaita hadhithi za kutunga, mitume waliwaita wachawi, machizi n.k.
(rejea; Quran 6:7,10:2,15:6, 46:17, 44:14, 40:56...)

Na katika kudhihirisha zaidi ukaidi wao, walifikia hadi kusema kumwambia mwenyezimungu, eti kama kweli hii (yaani yale aliyokujanayo mtume) ni haki kutoka kwako basi tuteremshie mawe kutoka mbinguni, au ututeremshie adhabu yenye kuumiza.(rejea; Quran 8:32)

Hii inaonyesha ni kiasi gani hawa watu ni wakaidi maana wangetaka kujua, wangeomba kuongozwa ila kwakuwa ni wakaidi wakaomba kuangamizwa.

Atakwambia thibitisha kama mungu yupo.

Sasa kama dalili alizoziweka mungu mwenyewe kuthibitisha uwepo wake hazijakukinaisha kuamini, unadhani hoja gani itakayokukinaisha.

Muktadha wa kupinga kwao ni kwamba mungu hayupo, hivyo hoja za kuthibitisha uwepo wake zote ni batili, lakini hata kama mungu yupo na hizi ndizo dalili alizoziweka kuthibitisha uwepo wake, basi ndio tayari wameshazipinga, maana hawakubalianinazo, hivyo ni wapingaji.

Kwahiyo tatizo sio ubora wa dawa ya sikio katika kutibu, bali tatizo ni kuwa hili ni sikio la kufa, hivyo halisikii dawa.
Quran haiwez kutumika kam reference ya uhakika
mfano mungu wenu naona alijichanganya au alisahau jinsi alivyoiumba dunia
20:53 - tunaambiwa dunia iko kama carpet
79:30- tunaambiwa dunia Ina umbo la yai la mbuni

Inakuaje muumbaji wa dunia anashindwa kutambua umbo sahihi anajichanganya namna hii
 
Hii ndio maana ya ukaidi, kwa sababu kupinga hakulazimu kutokuwepo, mtu anaweza kupinga hata kitu ambacho kipo.

Ndio maana sitaki kubishana na wewe.

Ngoja nikusaidie kuelewa mada yangu.

Kwa kusema hivi:-

Siamini kama wewe upo.

Na huwezi kuthibitisha kama wewe upo.

Kwa sababu haupo.

Sasa wewe endelea kuhangaika kunithibitishia uwepo wako, maana nakuhakikishia, hata uje nyumbani kwangu nikuone bado nitaendela kupinga tu.
Nakwambia hivi, hata kama mimi sipo.

Bado hujathibitisha Mungu yupo.

Na huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.
 
Nakwambia hivi, hata kama mimi sipo.

Bado hujathibitisha Mungu yupo.

Na huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.
Kwani nimesema kuwa huu ndio uthibitisho kuwa mungu yupo?

Ninachosema ni kuwa wewe unapinga uwepo wa mungu.

Kwani na wewe kusema hayupo ndio hayupo?
Ni kama mimi tu ninavyosema wewe haupo.
 
Quran haiwez kutumika kam reference ya uhakika
mfano mungu wenu naona alijichanganya au alisahau jinsi alivyoiumba dunia
20:53 - tunaambiwa dunia iko kama carpet
79:30- tunaambiwa dunia Ina umbo la yai la mbuni

Inakuaje muumbaji wa dunia anashindwa kutambua umbo sahihi anajichanganya namna hii
Kumbe reference ya uhakika ni ipi?
 
Wanaokana mungu huwa wanahoja mbalimbali katika kupinga uwepo wa mungu, pia huwa wanakosoa mafunzo ya dini ili kutilia mkazo zaidi katika hilo.

Lakini ukweli ni kwamba, sio kama hoja zao zinathibitisha kutokuwepo kwa mungu, hapana.
Bali hoja zao zinathibitisha kuwa wao ni wapingaji, hivyo hakuna andiko wala muujiza utakao wafanya waamini, sembuse hizi hoja ambazo huwa wanarumbana na watu Kila kukicha.

Na hivi ndivyo walivyo tangu enzi na enzi, hoja zao ni zilezile, na hata katika Quran, imeelezwa jinsi hawa watu walivyowakaidi.

Walipoonyeshwa miujiza waliita uchawi, maneno ya mwenyezimungu waliyaita hadhithi za kutunga, mitume waliwaita wachawi, machizi n.k.
(rejea; Quran 6:7,10:2,15:6, 46:17, 44:14, 40:56...)

Na katika kudhihirisha zaidi ukaidi wao, walifikia hadi kusema kumwambia mwenyezimungu, eti kama kweli hii (yaani yale aliyokujanayo mtume) ni haki kutoka kwako basi tuteremshie mawe kutoka mbinguni, au ututeremshie adhabu yenye kuumiza.(rejea; Quran 8:32)

Hii inaonyesha ni kiasi gani hawa watu ni wakaidi maana wangetaka kujua, wangeomba kuongozwa ila kwakuwa ni wakaidi wakaomba kuangamizwa.

Atakwambia thibitisha kama mungu yupo.

Sasa kama dalili alizoziweka mungu mwenyewe kuthibitisha uwepo wake hazijakukinaisha kuamini, unadhani hoja gani itakayokukinaisha.

Muktadha wa kupinga kwao ni kwamba mungu hayupo, hivyo hoja za kuthibitisha uwepo wake zote ni batili, lakini hata kama mungu yupo na hizi ndizo dalili alizoziweka kuthibitisha uwepo wake, basi ndio tayari wameshazipinga, maana hawakubalianinazo, hivyo ni wapingaji.

Kwahiyo tatizo sio ubora wa dawa ya sikio katika kutibu, bali tatizo ni kuwa hili ni sikio la kufa, hivyo halisikii dawa.
Msingi wa Imani ni kutojua jambo kiundani. Nadharia za imani zimejaa uongo.

Kuhusu mungu wengi wasiofata imani na kuabudu ni kutokana na sababu nyingi sio ukaidi. Kusema hoja ni zilezile ni uongo. Watu wa kale walikuwa na hoja za kifalsafa, wakati sikuhizi kuna hoja za kiushahidi na vipimo. Watu wa zaman hawakuwa na uelewa kama wa siku za karibuni. Zama hizi mtoto wa miaka 10 anayepata elimu iliyoshiba ana uelewa mkubwa zaidi wa jinsi dunia inaenda na nafasi yake kwenye ulimwengu kuliko wanazuoni wa zama za giza au kale.

Kiujumla ukielewa mambo utaona jinsi mungu hana nafasi katika kuanza na muendelezo wa vitu vyote, kila siku mwanya unavyozidi kupungua nafasi ya mambo ya imani inavyopunguwa. Mifano iko mingi kuonyesha vyanzo vyote vya imani leo hii havina mashiko tena.

Dalili unazoongelea hazina mantiki. Hakuna dalili isiyopingika au kukosa udhaifu. Kwahyo kulingana na shida ya kukosa ushahidi au hoja zenye nguvu ya kutosha, kwann uwe na imani?
 
Tunapinga uwepo wa Mungu kwa nadharia za vtabu vya dini , Ila kwa uhalisia wa uwepo wa supernatural power iliyofanya creation hatupingi kabsa , Natharia ya uwepo wa Mungu iliyopo kwenye vtabu vya dini inapotosha ukweli , kwasababu inamwelezea Mungu kuwa hashindwi chochte ili ndani kabsa ime mlimit kwenye baadhi ya mambo , mfano wa uwepo wa Mungu mbinguni akiwa na makerubi na wazee 24 ,hauoni umepunguza nguvu ya Mungu na kumlimiti kwenye sehemu moja tu anayoweza kuooperate kutokea apo? Pili Mungu anaweza kukasirishwa au kufurahishwa na binadamu , hauoni binadamu kuwa anaweza kucontrol hisia za Mungu !? Ila kwa tunaoishi ukweli wa kuwa kunasupernatural power inayo operates hii universe na universe nyingne hauoni tupo sahihi because energy can not be created no destroyed? Usione watu hawaamini vitabu vya dini hivhiv tu tunasababu za msingi tu ata huyo Mungu wa kwenye vitabu tunaweza tukamhoji kwanini maneno yako yanapinga baadhi ya tabia zako
Una maana gani kwa supernatural power? Ni nn hyo?
 
Hujafanya chochote mkuu kwakuwa bado umenukuu Quran ambayo hao wapinga mungu kwa hoja za kimantiki hawaiamini.

Huwezi kuwaaminisha kwa kwenda kunukuu biblia au quran.
Ifike muda twende mbele zaidi ya kuamini tu... tueleweshane. Kama kitu hakina mantiki hakina maana, na kwa msingi hakina msaada kwa watu zaidi ya kuongeza uharibifu wa rasilimali kama muda, pesa, mawazo n.k. ambazo pasipokuwa na hivi vitu visivyokuwa na msingi mali hizo zingetumika kuboresha hali za watu.
 
Na hii ndio maana ya ukaidi.

Wanaipinga Quran kwa sababu wanasema haijatoka kwa mungu, lakini hata kama inatoka kwa mungu ndio tayari wameshaipinga.
Kwann wasikaidi kama hoja haina mashiko? Itakuwa ni uzembe wa kutumia ufahamu kuona kitu hakiko sawa na kukipokea hvyo hvyo. Pengne hata unafiki, ujifanye una imani wakati kiundani huielewi na kuwa na hoja za kuitetea ipasavyo.
 
Kwani nimesema kuwa huu ndio uthibitisho kuwa mungu yupo?

Ninachosema ni kuwa wewe unapinga uwepo wa mungu.

Kwani na wewe kusema hayupo ndio hayupo?
Ni kama mimi tu ninavyosema wewe haupo.
Umeambiwa huwezi kuthibitisha kwa sababu Hayupo
 
Thibitisha Mungu yupo, na kwamba hizo habari za kuwepo kwa Mungu si hadithi za kusadikika zilizotungwa na watu tu.

Twende pointi moja bada ya nyingine katika uthibitisho wako.
Sawa sawa... nadhani mzigo wa ushahidi huwa upande wa wanaodai uwepo wa kitu.

Huu mzigo ulikuwa mkubwa kupita uwezo wa kutunga uongo kiasi cha hizi imani kuchukua njia za kulazimisha watu wazifate kupitia mfano wa ukamdamizaji wa kiuchumi (kulipisha wasiofata imani husika kodi kubwa kuliko wafuasi, kunyima haki za msingi kama kumiliki mali kwa wasiofata, au kuwafanya watumwa kabisa) na kuua kwa vita waliokuwa na mashaka na madai ya uongo mwingi kwemye hizi imani.
 
Kwann wasikaidi kama hoja haina mashiko? Itakuwa ni uzembe wa kutumia ufahamu kuona kitu hakiko sawa na kukipokea hvyo hvyo. Pengne hata unafiki, ujifanye una imani wakati kiundani huielewi na kuwa na hoja za kuitetea ipasavyo.
Mtu anaweza kupinga uwepo wa kitu ambacho kipo.

Kwa ujinga, ukaidi, ubishi, kiburi kuipumbaza akili yake n.k, na haya ndio yanampelekea kujenga hoja juu ya hilo.
 
Kwani nimesema kuwa huu ndio uthibitisho kuwa mungu yupo?

Ninachosema ni kuwa wewe unapinga uwepo wa mungu.

Kwani na wewe kusema hayupo ndio hayupo?
Ni kama mimi tu ninavyosema wewe haupo.
Kusema hayupo hakufanyi asiwepo.

Hayupo kwa sababu hayupo.

Na hili utaliona kwa kuangalia logical inconsistencies na self contradiction katika dhana ya uwepo wake.

Uwepo wa Mungu huyo ni sawa na mtu akuambie kwamba kuna duara ambalo hapo hapo ni mraba katika plane Euclidean geometry.

Hakuna kitu hicho, ni stories tu za watu.
 
Mtu anaweza kupinga uwepo wa kitu ambacho kipo.

Kwa ujinga, ukaidi, ubishi, kiburi kuipumbaza akili yake n.k, na haya ndio yanampelekea kujenga hoja juu ya hilo.
Kwanza kabisa, dhana ya kuwapo Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na ujuzi wote, inajipinga yenyewe kabla mtu yeyote hajaipinga.

Wengine wanaonesha tu dhana inavyojipinga yenyewe.

Unaelewa hilo?
 
Kwann wasikaidi kama hoja haina mashiko? Itakuwa ni uzembe wa kutumia ufahamu kuona kitu hakiko sawa na kukipokea hvyo hvyo. Pengne hata unafiki, ujifanye una imani wakati kiundani huielewi na kuwa na hoja za kuitetea ipasavyo.
Eti mtu anakwambia, katika plane Euclidean geometry:

Duara lina nyuzi 360.

Pembetatu ina nyuzi 180.

Hivyo, pembetatu haiwezi kuwa duara, na duara haliwezi kuwa pembetatu.

Halafu, anakwambia kuna duara moja special ambalo hapohapo ni pembetatu.

Anataka ukubali tu.

Ukikataa, unaitwa mkaidi.
 
Bila Wakaidi na Wapingaji tungekuwa hatuna maendeleo huku tukiishi kwenye sayari yetu ambayo ni tambalale na jua linaizunguka....

Na wala tusingehoji wala kutafuta / kujua mazingira yetu ili tupambane nayo sababu tungekuwa tunakengeuka kama waliotaka kujenga mnara wa Babeli (Na bila hao kutaka kujenga huo Mnara huenda hizi lugha tofauti zingekuwa hazipo)

Hence binafsi ninapenda uwepo wa hao so called wakaidi
 
Kwanza kabisa, dhana ya kuwapo Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na ujuzi wote, inajipinga yenyewe kabla mtu yeyote hajaipinga.

Wengine wanaonesha tu dhana inavyojipinga yenyewe.

Unaelewa hilo?
Wewe unaelewa hilo ndio maana unapinga uwepo wa mungu.

Sawa.
 
Back
Top Bottom