Soma hivyo vitabu ndugu vina majibu ya maswali yako, ni vema wakati unavisoma ungepata ufafanuzi kutoka kwa watu wenye maarifa zaidi ya dini ya UISLAMU yaliyo sambamba na huo ufahamu mfano: ABU RASLAAN MUSSA KILONGOZI, ABU FADHIL QASSIM MAFUTA, ABU ABDI-SALAAM MUJAAHID, ABU UMAYR ADAM MANDHUMATUL na wengine wengi, visome hali ya kuwa moyo wako upo huru - ruhusu kupokea haki ijapokuwa ladha yake ni chungu, hivyo ndivyo mambo yalivyo
Hii ni moja ya mada ngumu sana kuwahi kuwepo kwenye ulimwengu wa imani na wanazuoni wakubwa wa UISLAMU wanakiri juu ya hilo hadi kufikia kuonya waumini kufikiri sana na kuhoji sana juu ya masuala yanayohusiana na haya kwa kuchelea wengi ni wenye maarifa madogo wanaweza wakatatizika na wakatoka kwenye mstari, masaili mengi ya kidini hayapimwi kwa hoja za kiakili, mantiki wala falsafa, ulimwengu wa imani ni ulimwengu wa yakini, hivyo kwenye ulimwengu huu baadhi ya mambo yamewekewa mipaka na tahadhari, baadhi ya mambo yanahitaji mapokeo na kuyaitakidi tu kama yalivyokuja - si kila jambo ni la kutafakari kwa 100% au kuhoji sana mfano: MWENYEZI MUNGU asili yake ni nini? ametokana na nini? yeye ni wa kwanza na mwisho, wa kwanza kwa maana gani? chanzo chake ni nini? haya ni baadhi tu ya maswali ambayo si salama kujiuliza kwa waumini wa imani mbalimbali, hivyo inashauriwa watu wayapokee kwa uchache wake na yanawakinaishe
Sisi ambao ni waumini wa imani mbalimbali, tunafahamu na tunaheshimu nafasi za wasiosadikisha uwepo wa MUNGU kwa hoja mbalimbali, kila mtu ana uhuru wa kuamini anachoamini na haifai kuwalazimisha wala kuwashurutisha waamini vile tunavyoamini, wanadamu hatufanani kwa hali zote - si kifikra tu na uwezo wa kupambanua mambo, na kamwe hamna jambo ambalo wanadamu wote tutakuja kuwa na ufahamu mmoja, haitakuja kutokea na haijawahi kutokea, kwa hali hii ni vema kila mmoja aheshimu msimamo wa mwenzake pasina kubezana, bali kueleweshana tu kwa nia njema na kwa lugha nzuri
Suala jingine: waumini wa imani mbalimbali mfano: WAYAHUDI, WAKRISTO, WAISLAMU, WABAHAI, WAHINDU na wengine mnatakiwa mfahamu kwamba, unapojadiliana na wapagani au watu wasioamini uwepo wa MUNGU mara nyingi hatuhitaji kutumia maandiko ya vitabu vitakatifu au vyanzo vingine vya maandiko ya kiroho kama marejeo yetu, wao hawaviamini - si rahisi andiko likawakinaisha hata liwe na tija kwenye imani zetu isipokuwa mara chache sana - hususani wanapofanya mifananisho au wanapokuwa wameuliza swali linalohitajia jibu la kiakili kutoka kwenye vitabu, wao sanasana wanatumia ELIMU ZA MANTIKI, SAYANSI, FALSAFA na HISTORIA, hivyo unapojadiliana nao hakikisha nawe upo njema kwenye mambo hayo na unajua kujenga hoja mfano: anaweza akawa anapinga uwepo wa MUNGU kwa hoja ya kutokuonekana kwake, kwa hoja yake hiyohiyo waweza kumuuliza: mbona hapingi uwepo na maumivu na hali hayaonekani? hivyo ndivyo mijadala yetu dhidi yao inavyoendeshwa, na baadhi ya nyakati ni kwa kumpatia marejeo au andiko linalofafanua mada inayomtatiza kwa lengo la kuongeza maarifa yatakayomsaidia kumuondoa kwenye mabano
View attachment 2170227View attachment 2170226