Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Huo bado ni uhuru sababu ya lile lengo la wewe kuumbwa.
Bado unatoa majibu ya kihuni

Uhuru wa huyo mtu uko wapi kama amezuliwa kufanya jambo fulani?

Mtoto namba 1 anafungiwa ndani na mzazi wake kwa kuzuiwa kwenda kucheza na wenzake.

Na pia kuna mtoto namba 2 ambaye wazazi wake wammpa uhuru wa kwenda kucheza na wenzake pale atapojiskia

Ni mtoto namba ngapi mwenye uhuru wa kuchagua leo nikacheze na wezangu au nisiende na ikawezekana?
 
Mwisho wako unaujua ?
Hapa ungekuwa wewe ungesema jibu kwanza swali langu

Mwisho wangu siujui, lakini najua sifa za Mungu zinazoniwezesha ku reason kuwa kila kitu kilipangwa kabla hata sijazaliwa

Kwa mantiki hiyo nafata njia ambayo nilitengenezewa kupita, kwa hoja hiyo naelewa kila kitu kinafanyika kwa makusudi na hata kama nitaona nakosea lakini hiyo itakuwa katika fikra zangu na watu walionizunguka lakini sio katika perception ya Mungu

Kwa hiyo hilo swali nimehoji kwa kuzingatia view point ya upande wa Mungu.

Nikweli sijui ila najua kuwa yeye ndio mpangaji wa fate kwasababu hakuna kitu kipya machoni kwake, sasa je naweza badilisha fate ambayo yeye alinipangia?
 
Ameshiriki kivipi ? Nilikuuliza ukifanya mabaya huwa unaamua kwa hiari yako au unafanye ? Haya maswali ungekuwa unajibu yangekuepusha na makosa.
Ameshiriki kivipi

Nakurudisha kwenye mfano wangu wa duka la silaha hapo juu

Mabaya sifanyi kwa hiari yangu natimiza fate ambayo aliiweka kabla sijazaliwa

Nina uwezo wa kubadilisha fate?
 
Nakuuliza swali, unajua mwisho wako utakueaje ?
Nimekujibu lakini nakujibu tena

Sijui mwisho wangu utakuwaje, lakini pia hapo inaonesha dosari nyingine kuwa sio kweli tuna uhuru wa kuchagua kwasababu hatuwezi kujua hata mwisho wetu

Najua Mungu ni muweza wa yote na mjuzi wa yote

Kupitia sifa hizo najua alijua maisha yangu yote kabla sijazaliwa

Najua hakuna bahati mbaya katika maisha yangu, yani kila kitu kimepangika na mimi sina ujanja wa kufanya kinyume

Kwa mantiki hiyo chochote nacho kifanya ni muendelezo wa kukamilisha yale aliyonipangia na sina uwezo wa kwenda vice versa.

Kwa hiyo sijui mwisho wangu utakuwaje, ila najua kivyovyote itavyokuwa sio kwa hiari yangu ni kwa kutimiza mipamgo yake

Juhudi zozote zinazoweza kuonekana kama nazifanya kwa utashi wangu zitabaki kama mtazamo wa kibinadamu na kujiona nafanya kwa uhuru wangu lakini haiko hivyo, kwasababu kila kitu kilishakuwa arranged kabla sijazaliwa

Sasa je nina nafasi ya kubadili fate aliyoiona?
 
Kujua kwake hakukuzuii wewe kufanya unachotaka. Unarudia swali ambalo nimeshakujibu.

Unajua kwanini mwanadamu ameumbwa na matashi, akili na mfano wake ?
Kwa maana Mungu anaweza akajua muuaji anaenda kuua, halafu muuaji akabadili gia na kuhairisha kutekeleza hayo mauaji?

Kama hawezi utasemaje anaweza fanya anachotaka?
 
Ndiyo maana kuna mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu, si kwa mtoto mchnga tu bali kwa mtu yoyote.
Kama unakiri kuna mambo yapo nje ya uwezo wetu na bila shaka utakubaliana kuwa tungepewa huo uwezo tungefanya mazuri, kwanini Mungu hakufanya hivyo?

Kwanini Mungu amuadhibu kiumbe kwa kufanya jambo ambalo limechangiwa na uwezo wake kuwa nje ya kiwango?

Kwanini Mungu hakumpatia mtu uwezo wa kutosha kuweza kufanya mambo katika utimilifu?

Mtoto wa miezi mitatu tumboni kwa mama yake anauwezo wa kujitetea kutokufa pindi mama yake akitaka kumuua kwa kuitoa mimba?
 
Kwanini Mungu amuadhibu kiumbe kwa kufanya jambo ambalo limechangiwa na uwezo wake kuwa nje ya kiwango?
Kama jambo gani ? Hivi huwa unasoma ninachokiandika ?
Kama unakiri kuna mambo yapo nje ya uwezo wetu na bila shaka utakubaliana kuwa tungepewa huo uwezo tungefanya mazuri, kwanini Mungu hakufanya hivyo?
Tungepewa uwezo gani tungefanya mazuri ? Hali ya kuwa kila kitu kimeshawekwa wazi ? Jitahidi kujenga hoja vizuri na ujenge hoja kwa mujibu wa kile nilicho kiandika.

Kwanini Mungu hakumpatia mtu uwezo wa kutosha kuweza kufanya mambo katika utimilifu?
Ukamilifu wa mwanadamu unaingia katika sheria alizoziweka Mola mtukufu. Ya kwamba amuumba mwanadamu mwenye madhaifu ila akaweka sheria za kutimiza ukamilifu. Mathalani leo hii mwanadamu amewekewa sheria ya kuomba msamaha, kadhalika na mambo ambayo akiyafanya hufuta makosa aliyo yafanya, akaweka sheria ya mambo ambayo akiyafanya analipwa mema na mema zaidi.
Mtoto wa miezi mitatu tumboni kwa mama yake anauwezo wa kujitetea kutokufa pindi mama yake akitaka kumuua kwa kuitoa mimba?
Kila jambo lina hatua. Ndiyo maana kuna hatua ya ukuaji na utendani mambo. Mtoto akiuliwa huo unakuwa wakati wake umefika, ila hatohukumiwa kwa hilo, mwenye makosa ni yule aliye muua.
 
Kwa maana Mungu anaweza akajua muuaji anaenda kuua, halafu muuaji akabadili gia na kuhairisha kutekeleza hayo mauaji?

Kama hawezi utasemaje anaweza fanya anachotaka?
Bila shaka kabisa, mara ngapi tunabadilisha nia zetu ?

Hawezi vipi wakati amepewa uwezo wa kufanya na kutofanya ?
 
Sijui mwisho wangu utakuwaje, lakini pia hapo inaonesha dosari nyingine kuwa sio kweli tuna uhuru wa kuchagua kwasababu hatuwezi kujua hata mwisho wetu
Mwisho wako huujui, ila ushaambiwa ukifanya mema unaenda sehemu fulani na ukifanya mabaya kadhalika, kwanini usifanye mema ukaenda peponi ?
 
Hakuna mwingine Mwenye uwezo zaidi ya Mungu wa kuchanganya shahawa za baba yako na yai la mama yako ukapatikana wewe

Ila kama wewe unamjua aliyoifanya hiyo kazi hadi wewe Leo upo hapa duniani nitajia ni nani na kama humjui pia sema kuwa hamjui aliyefanya hadi Leo hii wewe upo hapa duniani

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Mimi simjui aliyefanya hivyo vipi Wewe mwenzangu unamjua na ulishawahi mwona?
 
Quran 35:11
Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii.

Quran 23:14.
Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.

Umeumbwa kupitia hizo process na hizo process naamini unazikubali ila maandiko yanazema Mungu ndio aliyefanya hayo

Najua kuwa wewe hauamini Quran nataka unitajie kwa upande wako ni nani alifanya hizo process hadi Leo hii wewe upo hapa duniani

Sent

Hizo ni Mythology za waarabu Tena walizicopy kutoka Kwenye Maandiko ya Israelites
Hizo zimeeleza Nadharia za uumbaji bila uthibitisho Zaidi ya masimulizi yaliyojaa Ngano ambazo Kila jamii inazo
Mpaka Leo Moja ya theory Bora ya uumbaji ni Ile ya SUMERIAN tables ambayo ni kongwe Sana Kuliko bible na Quran verses
Sumerian tablets zinawaelezea ANNUNAK kama viumbe waliofanya human cloning na human manipulation Kwa
Homo Electus na akabadilika na kua Homo sapiens Sapiens,
Nadharia ya Annunak inakubalika kisayansi na imesaidia kufanya cloning Kwa viumbe mbali mbali unaowaona Leo kuanzia wanyama mpaka binadamu na hii inamake sense katika Ulimwengu wa Leo Kuliko Vitabu vyenu vilivyojaa Ngano na hekaya za kijuha
Summeria tablets zimeandikwa Zaidi ya Miaka 450,000 BCE
Kwenye clay tablets na zinasema binadamu alifanyiwa cloning na human manipulation Ili awe kibarua wa kuchimba Dhahabu za ANNUNAK kutoka Huko sayari ya Nibiru na Leo watafiti wa mambo kale wanazidi gundua machimbo ya kale sana kuzidi historia ya Uwepo wa Mwanadamu na watu mengine wameyagundua Huko South Africa na Maputo msumbiji,mengine ni Yale ya grand Canyon Huko America
Sasa Wewe ndio utafute maarifa Acha kuariri Vitabu vya Dini za kuletewa bila kutafuta maarifa mengine Nje ya Hizo mythology!
 
Mtiririko wako una hitilafu kubwa sana. Hitilafu ya lazima chanzo cha kwanza cha ulimwengu kiwe mungu. Kwanini ulazimishe umungu kwenye kila hali? Hakuna hali ya kwamba mungu akakosekana? Anayesema hydrogen atoms mungu wake hizo atoms. Atakayekuja kusema strings utasema mungu wake ni strings? Au weak force? Quantum dynamics? Undefined probabilities?

1. Uchawi ni nn? Uchawi unafanyikaje? Unaathiri vipi vitu na watu? Kiimani na kisaikolojia au ina athari za kihalisia? Wewe ndio wale wanaodhani ukiomba kabla ya kuanza safari au mtihani utafika salama au kufaulu? Unadhani mtu akikuendea kwa mganga ufilisike utafilisika kweli bila wewe kusababisha au sababu ingne isiyohusiana na uganga uliofanywa? Nawe ni mmoja wao? Kama ni hivyo pole sana mkuu.

Lakini tuendelee. Ukielewa na kufata taratibu za kitafiti na uchunguzi utagundua hakuna uchawi, wala bahati, wala mkosi, wala miujiza wala viumbe visivyofata sheria asilia. Hakuna anayepaa tu hivihivi. Hakuna anayepona ghafla bila uhalisia wa kibaiolojia. Hakuna anayekufa pasipo sababu za msingi. Hakuna anayedhuriwa kichawi au kwa nguvu zisizopimika. Kila kitu duniani lazima kifate sheria asilia. Hakuna njia ya mkato. Uchawi haupo. Upo kichwani mwako tu. Hakuna haja ya kuongelea sana hili liko wazi sana kwa wenye kufatilia kiundani mambo ya kwenye jamii zetu.

2. Mungu ni nini au nani? Kwa maana za kibinadamu za kawaida hakuna ushahidi wa uwepo wake. Mungu ana ufahamu? Kama ndio basi atoms haziwezi kuwa miungu. Hazina ufahamu wowote. Kama mungu hana ufahamu basi pengine atoms kweli(unajua kuna vipengele ndani vinavyoathiri na vidogo zaidi ya atoms?) ndio miungu yetu. Miungu hii haihitaji imani za kuombwaombwa au kujengewa mahekalu, kutengewa muda na siku fulani na taratibu fulani ili ziridhike kututimizia mambo yetu hapa duniani. Sadaka zetu zitasaidia nn atoms? Ibada zinakuwa hazina maana. Dini zitatakiwa kutoweka kwenyw jamii watakaoelewa miungu hii. Hoja yako ya atoms ni miungu inafaa kupuuzwa mara moja.

Kuna wanasanyansi wana hoja zao kwamba kama uwepo wa kitu mungu unawezekana basi sio mungu aliyehai na kuwepo kila saa na sehemu. Kuna jina wanapenda kulitumia kuongelea hili kundi la imani; Deism. Yaan madai ya hii ni yawezekana alitenga mafiga matatu akainjika chungu akasepa. Kwahiyo mkono wa mungu kwenye dunia hii wala ulimwengu kiujumla. Hayupo tena alishaondoka akatusahau yapata bilioni kadhaa ya miaka. Hapa hakuna mambo ya miujiza, maono, uchawi sijui mapepo, mikosi, bahati, nyota yako sijui na takataka zingine.

Mimi binafsi, kama walivyo wanasayansi na wasio wengi, nasema ulimwengu ulianza bila ya uwepo wa mungu. Kuweka hoja kwamba alianzisha au yupo siyo suluhisho. Bali ni kuongeza tatizo jipya kwenye mtiririko wa suala hili la chanzo cha ulimwengu. Sana sana unaongeza maswali zaidi. Alitoka wap? Ametengenezwaje(hakuna kisichokuwa na mwanzo wa hivihivi tu. Kama ulimwengu lazima uliumbwa basi hata huyo muumbaji wake aliumbwa. Tusizushe umaalumu kama kinga ya hoja)‽ Kwann aanzishe?(Jibu liwe la maana sio ili "aabudiwe" utaanzisha kingine kwann aabudiwe? Bila kuabudiwa hajatimia?) Kwann alilipua muda husika? Alilipuaje? Alikuwa na lengo la kufikia hapa tulipo sasa?

Ukikaa peke yako na imani zako jitathmini sana na mwisho ujikubali kwamba unaamini lakini hujui unachokiamini hata ukisoma likitabu gani la imani haisaidii!
Wasipokuelewa hapa Hawa viumbe hakika vichwa vyao ni mizigo mizigo Sana Mkuu!
 
Tungepewa uwezo gani tungefanya mazuri ? Hali ya kuwa kila kitu kimeshawekwa wazi ? Jitahidi kujenga hoja vizuri na ujenge hoja kwa mujibu wa kile nilicho kiandika.
Kwanini kuna mambo yametuzidi kwasababu yako nje ya uwezo wetu na hatuwezi kuya control?
 
Ukamilifu wa mwanadamu unaingia katika sheria alizoziweka Mola mtukufu. Ya kwamba amuumba mwanadamu mwenye madhaifu ila akaweka sheria za kutimiza ukamilifu. Mathalani leo hii mwanadamu amewekewa sheria ya kuomba msamaha, kadhalika na mambo ambayo akiyafanya hufuta makosa aliyo yafanya, akaweka sheria ya mambo ambayo akiyafanya analipwa mema na mema zaidi.
Alivyokua anamuumba kwa kumuwekea udhaifu hakujua kuwa huo udhaifu utasababisha kufanya yale yasiyo mpendeza?

Kwanini mtu akifanya dhambi kwa msukumo wa udhaifu ambao Mungu kamuwekea, Mungu huyo aje amuadhibu?

Hata katika mahakama zetu ikigundulika kichaa kafanya mauaji hakuna kesi itayomkabili kwasababu amefanya hayo akiwa hayuko kwenye utimilifu

Kwanini Mungu kazidiwa standard za busara na mahakama zetu, kwanini amekuwa sadistic kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom