Wanaoomba michango ya harusi majasiri sana

Wanaoomba michango ya harusi majasiri sana

Magufuli legeza kidogo jaman watu wanatafuta sababu za kutochangia hapa....nakumbuka enzi hizo uchangiaji harusi ndo ilikuwa ufahari na mbwembwe nyiiiingi
 
mimi harusi sichangiiii hadi uwe ndugu yangu tu...

Ila rafiki, sijui workmate... nakuwaga muwazi kabisa mimi harusi sichangiagi na huwa nasema mapemaaaaa ili usinitumie tumie.sms
 
Mi wiki hii tu nimepewa card ya kualikwa kikao cha kwanza ili ku pledge, nikauchuna nawasikilizia , yaani hawakomi tu kuniletea card maana huwa sichangii, wakishakuona una vihela basi wankutaka uwachangie harusi. Watu wenyewe nawajua wanaishi kinyumba miezi kibao ishapita leo nije niwachangie au mnataka mtaji, mnikome kama mlivyokoma toka kwa mama zenu. nyambaf.
 
Umenichekesha mkuu[emoji1][emoji1]
 
Mimi msimamo wangu mpaka mwisho wa dahari sitakaa nichangie harusi.
Ila akija anayetaka mchango wa ada ya shule au anaumwa au nduguye,period.
 
Mkuu umeongea jambo zito.mimi nimeoa hata ofisini kwangu hawakujua.maana natambua kuwa usiweke bajeti ya ndoa kupitia michango ya watu .kila mmoja ana bajeti yake ya maisha.Mimi nitachangia harusi za familia yangu tu.ujinga mimi sina.ukikaa ofisini kila wiki mchango.Yaani ukiwachekea utazani umejiunga na SACCOS hiyo michango. wengine hawana hata haya wanaandika na kiasi .
 
Yaani imenitokea jana tu , kuna demu tumekuwa naye toka utotoni na bahati mbaya tulipofikia umri fulani tukapotezana, siku moja nakwenda kwao kumuulizia nikaambiwa yupo znz , nikaomba namba zake, nakuanza kuwasiliana naye, lakini chakushangaza simu zangu wala hakuzijali sio kupokea wala kujibu sms zangu, nikaona tabu ya nini, nikauchuna zangu miaka ikakata,

Jana ananibipu, nikapiga akapokea na salamu kibao nikajisema naona.sasa ndio ananikumbuka , basi baada ya salamu nyingi mara ananiambia anaomba mchango wa harusi, nikamuuliza unaozesha au unaolowa, akasema anaolewa, sikumpa jibu kabisa zaidi nikamwambia nimekusikia tu basi, na baada ya hapo nikafuta namba yake kabisaaaaaaa
 
Hata mimi nilikuwa na mtizamo kama wako kwamba siwezi kuchangia harusi lakini ilipofika kwangu nikaona umhimu wa kuwekeza kwa watu huwezi kukwepa kujihusisha kwenye matukio ya kijamii hata kwa kiasi labda uwe huna kitu tusijidanganye hapa usiposhirikiana na mimi kwenye harusi siji kwenye msiba wako/kipaimara n.k ee kila mtu si ana vipaumbele kwenye maisha.
 
Mi wiki hii tu nimepewa card ya kualikwa kikao cha kwanza ili ku pledge, nikauchuna nawasikilizia , yaani hawakomi tu kuniletea card maana huwa sichangii, wakishakuona una vihela basi wankutaka uwachangie harusi. Watu wenyewe nawajua wanaishi kinyumba miezi kibao ishapita leo nije niwachangie au mnataka mtaji, mnikome kama mlivyokoma toka kwa mama zenu. nyambaf.
Najikuta nacheka na kujibana mdomo ili sauti isitoke, ntaonekana chizi.
 
Kutoa ni moyo lakini so kutoa kwako inategemea moyo wako.
 
Back
Top Bottom