Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

Ni kweli kumezuka wimbi la wakosoaji wengi wa Nyerere siku za hivi karibuni. Mimipia naafiki kwamba Nyerere hakuwa malaika lakini bado naamini ni kiongozi aliyefanya kila awezalo kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wake. Nahisi kuna agenda ya siri ya kumchafua na inawezekana kabisa ni fitna za baadhi ya viongozi aliowaacha waliomsaliti na kusababisha chama na nchi kwenda arijojo.
 
Duh! Mkuu ASANTE SANA kwa ulichokiandika.Kitufe cha Thanks sikioni, ila nakupa hongera kwa kufanya summary nzuri sana khs utawala wa Mwl. Mpendwa wetu, Julius Kambarage Nyerere. Kwa kweli Mkuu, umenifanya nitake kuwa kama Mizengwe Iliyoanza Kupinda kwa kulialia, sijalia ila machozi yamenirengarenga kwa jinsi watu wanavyomkosea heshima Mwl. Nyerere kwa mema na mapenzi aliyojitolea kwa Nchi hii, hadi hawa Vilaza wa sasa hivi wanapata sehemu ya kutamba ''Kisiwa cha Amani''....wanafikiri kilijiweka tu kama walivyokuta rasilimali za nchi hii alizowahifadhia vizuri Mwl??? M...a...t...a...k...o....yao!!! MOD nisamehe ni hasira tu zimenijia kwa hawa jamaa wanao mchezea Nyerere! MTOA MADA ULICHOTAKA KUFAHAMU KHS NYERERE AMBACHO HATA MTOTO WA CHEKECHEA ANAWEZA KUKIONA NA KUKIELEWA ENZI HIZO ZA NYERERE ALICHOKIFANYA NDIO HICHO HAPO JUU JAMAA KAWAKILISHA. Achana na rongorongo za hawa WanaInterejensia Uchwara wanaojidai wanafahamu mengi ya Mwl yasiyoonekana!
 
Mkuu Asante Sana!
 


Unapozungumzia "school of taught" unazungumzia schools of economic thought? Socialism vs. free enterprises? Unajua kabisa nani mshindi, I hope.
Socialism-Ujamaa system ambao Nyerere alikuwa ana practice unajua kabisa ilifeli kwa sababu ya matatizo gani. Tunachozungumzia hapa ni jinsi Nyerere alivyoshindwa kuimplemet hizo fundamentals principles za uchumi kwa makusudi kwa sababu ya Udictator wake.

Unapouliza definition ya Udictator, na kama Nyerere aliqualify kuwa Dictator; jibu Yes, Nyerere alikuwa Dictator. Mfano, na ushahidi ni Azimio la Arusha. Nyerere kwa nguvu alitumia kuwahamisha watu na kuwapeleka vijijini kwa nguvu. Tatizo kubwa lilotokea ni mauaji yaliyotokea ni kwamba WTZ walikuwa wanakufa kwa njaa, maradhi huko vijijini. Utawahamisha vipi WTZ kutoka ktk sehemu zao na kuwapeleka vijijini kulima, bila ya kuwa na mahitaji muhimu kama maji, hospital? Hayo ni mauaji. Nyerere alifanya hayo kutekeleza Azimio la Arusha. Huo ni Udictator.

Unazungumzia kuhusu video documentary. Hii video clip in MANENO yake mwenyewe Nyerere, na ANAKUBALI ALIKUWA DICTATOR. Angalia hii clip ili usikilize na umuone Nyerere mwenyewe anasema maneno hayo, please.
Films On Demand - View Playlist#
 
Asante sana Mkuu kwa ulichoandika, ongezea na hii: Ukitaka kuona kirahisi kwamba Mwl. Nyerere bado anahitajika sana ktk nchi hii, angalia baadhi ya watu wanavyosema kuhusu viongozi wanaofanya mabaya utasikia ''Mwl angekuwepo angewachalaza viboko'' kama hiyo haitoshi, utakumbuka Mrema kipindi kile alivyojipatia umaarufu hadi akawa anatembea na kitabu cha Mwl na watu walijitokeza kwa wingi kumsikilizia, hata Kikwete ukiuliza alichofanya hadi watu wakampenda ni kipi ktk uchaguzi wake wa kwanza?? Kama utakumbuka watu wengi walivutika kutokana na hisia kwamba ana dalili za kufuata hatua za Mwl, tena kulikua na tetesi zimezagaa kwamba kakataa nyumba za mgao wa bure wa serikali, wananchi wengi waliguswa na kumpa matumaini yao ya ukombozi wakiamini angerejesha heshima serikalini baada ya Mkapa kuonekana kama kawaachia Viongozi wa serikali wajimwaemwae wanavyotaka kwenye matumizi ya mali za uma. Ninacho sisitiza hapa, Watanzania bado wanamwitaji sana Nyerere hivyo hata akitokea Kiongozi mwenye dalili za kufuata nyayo zake...lazima atafanikiwa. Baadhi yao aliojivika ngozi ya Mwl kumbe ni Matapeli ni hawa kwa uchache: Mrema, Kikwete, Pinda, Sita, Mwakyembe, etc. Wako wengi!
 
Kauli zote za kumhujumu Mwalimu zitachuja na hazitawafanya watanzania wamchukie. Ni nyie wachache mliofilisika kifikra. Fikra mbovu. Upuuzi uliokubuhu. Toka lini gunia la mchanga likawa sawa kwa uzito na gunia la pumba? Acha hizo pumba. Jua namna ya kuweza kumridhisha mke uliyemwoa. Maana watu wa jamii hii ni hatari kwa taifa hili. Ni hesabu rahisi, kama huioni, ni watanzania wangapi ambao hawajui mazuri na mabaya ya mwalimu? Iweje watanzania hao hao ndio wanaomwenzi mwalimu. Bora hata wakristu wangekuwa wanamlaani kuliko waislamu maana alitaifisha shule za kikisto kuwa mali ya serikali yake ili pamoja na wengine watoto wa kiislamu nao wasome.

Na ni waislamu hao hao waliokuwa wanamchenga mwalimu na kuwaelekeza watoto wao kuzingatia elimu ya madrasa. Leo mwalimu anaonekana mtu ovyo kwa hao hao. Mfano wangekuwa wanachukulia maanani jinsi mwalimu alivokuwa akiwapigania kielimu wangekuwa mbali. Lkn wapi. Leo hii mna watu kama kiwete, magamba,nk nk waliokuwa wanasoma shule za misheni , leo huyu kiwete angekuwa anauza mabumunda. Acheni upuuzi, ushenzi, ukoram, upumbavu, ufuska wa kimawazo. Kaa na wake zenu; wawafunze: maana mama zenu walishindwa.
 
Films On Demand - View Playlist[/URL]#

Shamu, kama umeisikiliza hiyo video nakusikiliza maneno ya sekunde tano tena yanayoeleweka vizuri na bado hukuelewa!! I am so sorry for you! It's too low. Duh! Huyo amini hakuweza kusema yeye ni dikteta seuse Nyerere!! pick up one word and make your own phrase. Being a hater for nothing is not good for your health, it may complicate to serious problem in future dude!
Naomba mtu mwingine asipoteze muda kusikiliza huo 'ushahidi' maana ni tatizo la chuki la mtu mmoja.
 
Unapozungumzia "school of taught" unazungumzia schools of economic thought? Socialism vs. free enterprises?
School of thought definition:
A collection or group of people who share common characteristics of opinion or outlook of philosophy,discipline,belief, social movement,cultural movement or art movement

It doesn't mean 'economy' Shamu!
 

wow! you can say it again!

ukisoma african societies unaweza kumtetea Nyerere many ways, kitu ambacho sijakiona kwa Nyerere defenders! nasoma. I will be one to my own kids...is natural!
 
Nimesoma Raia Mwema nadhani kuna watu watarudi post zangu za mwanzo, kukubaliana na mimi kuwa Nyerere atajitetea

Raia Mwema

mwandishi yuko shallow kidogo, article haijashiba, HASA SWALA LA POSHO, NA WAISLAMU HALIJASHIBA

Ni ukweli Nyerere alivunja shirikisho la east africa la waislamu, lakini ni ukweli usiopingika ni yeye pia alivunja Assemblies of God vipande viwili!! ka kutaka dini zisiwa na nguvu, na kipindi hicho Aseemblies of God church lilikuwa na nguvu na lilihisiwa kupokea misaada kutoka Marekani

waandishi issue za dini kwa Nyerere mzi-balance, sioni tatio la udini

Nyerere hakuwa mdini!! UGONJWA WAKE MKUBWA ULIKUWA ALITAKA UJAMAA na katika jitihanda hizo aliharibu hapa na pale
 
Ndugu kambota: Unajua katika kipindi chake Nyerere vijana wengi wa low income erners families na son and doughters of peasants walikuwa wanarudia darasa la saba mara kumi hata kumi na mbili kwa kiu ya kupata elimu ya secondari. Yeye nyerere hakuona hilo ni kama tatizo. Makweta mwaka 1983 alifanya tume ya kuboresha elimu na alikuja na ripoti ya kwamba tanzania tupo nyuma sana ki elimu ni lazima serikali ijenge secondari mpaka ngazi ya kata. Lakini Nyerere alikataa kwa kujibu eti wewe unataka kuimarisha paa badala ya msingi, kimya. Alipotoka madarakani alikuwa napeleka wanafunzi 900 kwa mwaka chuo kikuu lakini mkapa alipotoka madarakani alikuwa anapeleka wanafunzi 40,000.00! Mazuri ya nyerere mimi nimemtetea sana ila mabaya yake ni lazima yuyaweke wazi pia ili viongozi wetu wasije wakaiga bure. Katika utawala wake aliondoa hati miliki kwa wanamuziki hivyo kuwafanya wanamuziki wengi kufa masikini. Lakini walioona hilo pungufu wamerudisha hati miliki kwa wanamuziki wa Tanzania , ona sasa wanamuziki wetu wanavyo ishi maisha ya mboga saba mezani! Ona sasa Kikwetae alivyo boresha maisha ya vijana wetu wenye kipaji cha soka na muziki. Jiulize kwa nini watanzania hawapati kazi Kenya na Uganda ila waganda na wakenya wanapata kazi kirahisi Tanzania? Hayo yote tumtwishe nani lawama? Watu walikaa na jazba moyoni kwa kuogopa utawala wake ,ila sasa wanatoa jazaba yao.
 
lakini ni ukweli usiopingika ni yeye pia alivunja Assemblies of God vipande viwili!! ka kutaka dini zisiwa na nguvu, na kipindi hicho Aseemblies of God church lilikuwa na nguvu na lilihisiwa kupokea misaada kutoka Marekani

Naomba utufill details za hili; maana so far Nyerere kalaumiwa sana kwa kuanzisha BAKWATA na kuwagawa Waislamu. Ilikuwaje katika hili la kuivunja Assemblies of God?
 
School of thought definition:
A collection or group of people who share common characteristics of opinion or outlook of philosophy,discipline,belief, social movement,cultural movement or art movement

It doesn't mean 'economy' Shamu!


Umemiss point here. Tunapozungumzia "school of thought" lazima ujue unazungumzia kuhusu point gani. Kwa Nyerere, ni philosophy katika school of economic thought. Hiyo uliyotoa ni definition ya school of thought. Ukienda kwenye share common hapo inabidi uzungumzie philosophy ya Nyerere ambayo ni Ujamaa. Sasa unapozungumzia "school of thought" lazima uelezee ni school of thought ipi? Ujamaa, au free market economy.
 


Walioiweka hiyo video wanajua zaidi kile wanachozungumza. Wametumia kauli ya Nyerere kucite ushahidi wa maneno waliyotoa. Sasa wewe kama unasema Wazungu pia hawajui maana ya lugha yao, itakuwa ni ubishi wa ligi usioisha. Fuatilia vizuri hiyo video clip ili ujue ukweli.
 
Nguruvi3;2178484]Asichokijua ni kitu kinaitwa 'school of thought' yaani kuna vyuo duniani haya mambo wanayajadili kila uchao, tofauti na Shamu wanaangalia mambo kwa mtazamo mpana bila hisia wala chuki
Nilisema kujadili mambo kwa ujumla bila ya hisia au chuki iwe ya kisiasa, kiuchumi au kiutamaduni. Kauli yangu ni general na haikutaja mahali kuhusu Nyerere au ujamaa. Hayo umepandikiza wewe kwa kuongozwa na chuki na hisia, nadhani unaona hatari yake. Often unakuwa off point.
 
Nadhani kukosolewa ni jambo la kawaida kwa kila mtu. Ata wale wale manabii na makuani walikuwa na makosa yao kama wanadamu.
 
nani anaweza kutuwekea tafsiri hasa ya neno DIKTETA? hapa kuna tatizo, nyerere aliongoza kwa kufuata sheria zilzokuwepo, hizo sheria ndo tuite kuwa zilikuwa katika mfumo wa kidikteta, tofauti na sheria za sasa, hizi za leo ni zakidikteta zaidi tena udikteta wa kimfumo hasa.
 
Uliusoma vizuri mpango wa maendeleo wa Nyerere wa mwaka 1963? Unaweza kunithibitishia kuwa suala la sekondari za 'kata' halikuwepo? Unaamini kuwa Makweta na Lowasa ndio walioanzisha mpango huo? Je Mwalimu alikuta sekondari ngapi alipochukua nchi. Kama angeendeleza sekondari huduma za afya alizopata baba au mama yako zingetoka wapi?
Alipotoka madarakani alikuwa napeleka wanafunzi 900 kwa mwaka chuo kikuu lakini mkapa alipotoka madarakani alikuwa anapeleka wanafunzi 40,000.00!
Alipoingia madarakani alikuta wanafunzi wangapi wa chuo kikuu? Je kulikuwa na chuo kikuu Tanganyika. Hao walimu waliofundisha 40,000 ya Mkapa walizaliwa siku moja na kuwa walimu(maprofesa). Je ubora wa 40,000 unawezaje kuuweka katika mizani na 900 wa mwalimu?Mkapa alijenga vyuo vikuu vingapi? Na ona sasa mamilioni ya wahitimu wasivyokuwa na kazi achilia mbali mamilioni wanaoteseka bila hata kumaliza shule. Hao wa mboga saba wanaweza kuzidi 20 labda! nisaidie kwa hili
Jiulize kwa nini watanzania hawapati kazi Kenya na Uganda ila waganda na wakenya wanapata kazi kirahisi Tanzania? Hayo yote tumtwishe nani lawama? Watu walikaa na jazba moyoni kwa kuogopa utawala wake ,ila sasa wanatoa jazaba yao
Nyerere amezuia watu kupata kazi duniani? Kama huna elimu au hujui kujieleza kupata kazi Nyerere angetakiwa aje kukusaidia Interview.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…