Wanaomhujumu Rais Magufuli hawa hapa

Wanaomhujumu Rais Magufuli hawa hapa

Ndugu wanajamvi,
Sisi kama wazalendo na wanaharakati ambao sote tunaipigania nchi yetu kwenda kwenye uchumi wa kati lazima tupaze sauti zetu kila Mara kupinga hujuma mbalimbali zinazofanywa na watu Fulani Fulani kuhakikisha RAIS MAGUFULI anakwama lakini kibaya zaidi hawajui hii nchi ni yetu sote na siyo MAGUFULI peke yakee.

Ndugu wanabodi hakika sasa hivi kuna mambo mengi yanayosemwa kwa RAIS wetu kuhusu utawala wake lakini kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia na huu ni mtandao unaupinga utawala wa awamu ya tano au kwa lugha nyingine wanaomuhujumu RAIS magufuli na hapa wapo watu wa makundi mbali mbali na taasisi mbali ila ngojea nianze kuyachambua kama ifuatavyo;
1: Wafanya biashara ambao walikuwa hawalipikodi;hawa wameunda mtandao wao kwa usiri Mkubwa mno ili kuhakikisha kwa kila namna huu utawala ufe, kwa kuwa walizoea kuishi bila kulipa kodi lakini sasa hivi lazima ulipe kodi kitu ambacho kinawanyima usingizi. Juzi tumesikia kuwa RAIS MAGUFULI analalamika kuna watu wametoa hela benki wameficha nyumbani eti kuzuia mzunguko wa hela inasadikika kuwa kundi hili limo kwenye hii harufu mbaya.
Mfano moja tuu niwape juzi tumemsikia RAIS wa ufilipino Rodrigo Durteze analalamika kuwa anahujumiwa na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya waliounda mtandao wao kuhakikisha huyu RAIS anafeli katika utawala wake kwa kuwa alitangaza operation ya kuwanyonga hawa mabwenyenye.

Lakini akawa na wakati mgumu kwa sababu huu mtandao ulikuwa mpana sanaaa hadi Marekani ameingilia kati kabisa kwa kigezo cha haki za kibinadamu. Swali ni je Marekani hawajawahi kuwanyonga watuhumiwa wa madawa ya kulevya?

Utakuta ni majibu nyepesi kwenye masuala magumu kama haya ukikaa na kufikiri kwa undani utakuta Kuna maslahi ya watu hapa ndo maana wanaingilia mambo yasiyowahusu kwani nani asiyejua athari za madawa ya kulevya inavoangamiza vijana na vizazi katika taifa. Lakini huyu Rais alipoingia madarakani aliivalia njuga kama MAGUFULI alivyolivalia njuga swala la mafisadi na kulipa kodi.

2: Ni genge la watu Wanaodai demokrasia ambayo hata demokrasia yenyewe hawaijui maana yake, eti kwao demokrasia ni kufanya mkutano wa kisiasa na maandamano ambao hauna faida kwa wananchi. Na hapa ndipo kuna upotoshaji mkubwa unaotaka kugawa serikali na wananchi wake, na viongozi wa hii genge hasa ni MBOWE na MAALIM SEIF ambao kwao demokrasia ni ubavu ndani ya vyama vyao na kutunishana msuli usio na faida kwenye ujenzi wa vyama vyao.

Wamejitahidi kutumia vijana wao kama YERIKO NYERERE, MALISA G, BEN SAANANE, JULIUS MTATIRO, katika kuupotosha umma kwenye mtandao wa kijamii kama JF, Facebook na Twiter kuhusu dhana ya demokrasia na wanaenda mbali na kusahau kabisa kuwa wao ndo vijana wa kulisaidia taifa hii kwenda kwenye uchumi wa kati.

Niwasihi hawa vijana waache maramoja kuupotosha umma kuhusu neno demokrasia kama mawazo yao yalivofikia waaache utashi wa kisiasa bali wajenge hoja zenye mantiki ya kutuunganisha sisi wananchi kwenda kwenye uchumi wa kati kwa kuwa Mimi naamini RAIS MAGUFULI angekuwa dikteta wasingetamka hadharani kama wanavolitamka kwa nyakati tofauti Bali huu ni uchochezi wa hali ya juu kuwahi kutokea katika taifa hili.
Kwakuwa hili kundi linasadikika kuwa inapata support kutoka kwenye mtandao wa wafanyabiashara ambao kodi kwao kulipa hawataki na pia inapata support kutoka kwa mtandao wa mabwenyenye wa mataifa ya magharibi wenye mrengo tofauti na RAIS MAGUFULI ambao kwao lengo kubwa ni kutaka kuchuna rasimali zetu na mkakati huu ulianza tokea uchaguzi wa 2015 ambao hawa mabwenyenye wana kiu sanaa na rasimali zetu ndipo wanaungana na mtandao wenye mrengo kama ya kwao wenye kujiita wana demokrasia.

3. Ni taasisi Fulani Fulani zisizo za kiserikali ambao wanatumiwa na wana siasa kwa nyakati tofauti kuja kupotosha umma kuhusu dhana ya demokrasia na utawala wa RAIS MAGUFULI zipo taasisi za kidini na zisizo za kidini kama mnafuatilia mambo kiundani mmemsikia padri Fulani kwa nyakati tofauti amesikika kuupinga utawala wa MAGUFULI hadharani lakini siyo kosa lake ni kosa la waliomtuma.

Hili kundi lina ushirikiano mkubwa na kundi la pili kwa kuwa waga kuna vikao wanafanya kwa usiri Mkubwa na ndipo wakishapewa au wakishaaidiwa vitu Fulani unawasikia wakiropoka bila ata mantiki ya kutuunganisha sisi wananchi hivyo nitoe rai yangu kuvionya hizi taasisi ambao wanashirikiana kwa namna moja au nyingine na hii genge la MBOWE na wenzake kuacha Mara moja kwa kuwa wao ni taasisi bila kujali ya serikali au siyo ya ki serikali kazi yao ni kutuunganisha na si kutugawa na kuleta uchochezi.

4. Baadhi ya vyombo vya habari hapa utakuta kuna media zimenunuliwa na kuna wana habari pia na magazeti yamenunuliwa ili kupambana na serikali ya awamu ya tano juzi tuu ni mfano halisi baada ya waziri NAPE kuvifungia baadhi za station za radio zilizoripoti habari za kichochezi na hili kundi hushirikiana kwa karibu na kundi la pili kwa nyakati na sehemu tofauti.
Kila siku ukisoma gazeti Fulani ambye mmiliki wake ni kiongozi wa chama Fulani utaona na kujiiridhisha kuwa wanapambana na serikali ya awamu ya tano. Rai yangu kwa wanahabari wote kuacha mara moja mambo au kutoripoti kabisa habari za kichochezi zenye mrengo wa kutugawa katika taifa letu pia niwaonye wamiliki wa vyombo vya habari kuacha utashi wa kisiasa kuvitumia vyombo vyao kuripoti au kuandika habari za kichochezi zenye mrengo wa kuligawa taifa letu.

Safari ya kuelekea kwenye uchumi wa kati bado inaendelea:
Ni wako kijana mtiifu,mzalendo na mwanaharakati wa kweli.

SIMON MATO-0762189733.
Jitaid kusifia wanaweza kukuangalia na ww ukawa MKURUGENZI au MKUU WA WILAYA.. Mwanzo wako mzur bro.
Keep it up [emoji115] [emoji123]
 
Machadema hamsifii mtu mpaka aondoke. Mmesahau matusi yote mliyowatukana viongozi hao kweli!?
Swala siyo kusifia au kutosifia bali issue hapa ni kwamba ukifanya vizuri unasifiwa, vile vile ukiboronga unaambiwa ukweli na ukubali kurekebishwa, kwa maana hakuna mwanadamu mkamilifu au malaika, hivyo mtu kukasirika au kuvaa joho la uchochozi kisa kutotaka kukosolewa ni jambo la kushangaza sana na halina mstakabali mzuri kitaifa na hata hulka ya aina hii ikiinuka ndani ya familia ni matatizo makubwa sana kiasi cha kuweza kuisambaratisha familia husika.
 
Swala siyo kusifia au kutosifia bali issue hapa ni kwamba ukifanya vizuri unasifiwa, vile vile ukiboronga unaambiwa ukweli na ukubali kurekebishwa, kwa maana hakuna mwanadamu mkamilifu au malaika, hivyo mtu kukasirika au kuvaa joho la uchochozi kisa kutotaka kukosolewa ni jambo la kushangaza sana na halina mstakabali mzuri kitaifa na hata hulka ya aina hii ikiinuka ndani ya familia ni matatizo makubwa sana kiasi cha kuweza kuisambaratisha familia husika.
Nani mliwahi kumkosoa kwa hekima katika wote uliowataja na mkafanikiwa? Huyo Lissu alimtukana wazi wazi JKN na nyio ndio mlifikia mpaka kumuita jina baya kabisa JK na wengine mkadiriki kuiita serikali dhaifu! Leo unaleta mafyongo gani hapa! Akili zenu sawa na za Ng'ombe tu, hamna kumbukumbu.
 
Nani mliwahi kumkosoa kwa hekima katika wote uliowataja na mkafanikiwa? Huyo Lissu alimtukana wazi wazi JKN na nyio ndio mlifikia mpaka kumuita jina baya kabisa JK na wengine mkadiriki kuiita serikali dhaifu! Leo unaleta mafyongo gani hapa! Akili zenu sawa na za Ng'ombe tu, hamna kumbukumbu.

Tumia busara kidogo wakati wa kujadili hoja.
1. JKN na Mwinyi walikubali kuanzishwa kwa vyama vingi baada ya mawazo ya NCCR kuanzisha platform ya mageuzi.
2. JK alikubali hoja ya kuanzishwa mchakato wa katiba mpya na kuruhusu government transparency vikiwa ni misimamo wa opposition parties and pressure groups
3. Mkapa aliruhusu freedom of speech kufuatia madai mengi ya pressure groups including position parties.
Uliza swali lingine kama bado lipo mkuu.
 
Sijaelewa ulichoandika kwa kuwa Rais magufuli katiba imempa nguvu kubwa sasa inakuwaje ahujumiwe?.anajihujumu mwenyewe yeye ni mkuu wa nchi,amiri jeshi mkuu na mwenyewe kasema Tanzania ni nchi tajiri sasa iweje akina mtatiro,yeriko,malisa watu ambao hawana jeshi wamhujumu mtu mwenye jeshi.muache kumtetea mwambie atekeleze ahadi za kutoa ajira,kuboresha huduma za afya maana kuna baadh ya hospitali baadhi ya chanjo kama ya tetenus,anti rabies ziliadimika,alete viwanda n.k HUU SI WAKATI WA NGONJERA ATEKELEZE AHADI
Mkuu soma vizuri andiko am sure sijatamka mtatiro,yeriko na malisa wanamuhujumu RAIS bali wanatumiwa vibaya na viongozi wa juu kuhakikisha wanapambana na serikali ya magufuli kwa kueneza propaganda humu mtandaoni na hiyo ndo hujuma za waziwazi unaofanywa na mbowe na genge lake
 
Mnapelekwapelekwa na Dj, hamna uwezo wa kujiamulia mambo yenu.
Nadhani shule ni main determinant katika kufikiri na kufanya maamuzi katika mijadala kama hii. Kama upeo wa shule yako umeishia hapo usiulazimishe ukaja ukajikuta unanunua jinai bila sababu za msingi.
 
Watashindana lkn hawatashinda kamwe magufuli ndiyo kila kitu watanyooka tu.
 
Genge LA losawa linalosaka ikulu kwa hali na Mali ni sawa na kansa inayotafuta taifa,
 
Siku tanzania ikipata Dawa ya kutibu tamaa ya kwenda ikulu ilimea katika genge LA wasaka ikulu ak,a oil chafu iliyofukuzwa ccm tutapona
 
Siku tanzania ikipata Dawa ya kutibu tamaa ya kwenda ikulu ilimea katika genge LA wasaka ikulu ak,a oil chafu iliyofukuzwa ccm tutapona
Huu mtandao ni hatari sanaaa usipodhitiwa mapema itatuletea athari kubwa mno!! Asante mkuu
 
Wanakuja na sababu zisizo na kichwa wala miguu ili kuhalalisha utendaji mbovu wa kiwango cha juu katika hii miezi 11 iliyopita.

mimi siko kubishana nikukuweka sawa uache mbwembwe eti magufuli anahujumiwa ili iweje!!acheni porojo kama hamna post zamsingi mkae kimya kunahoja hapo yakukimbia au pumba tu
 
Nadhani shule ni main determinant katika kufikiri na kufanya maamuzi katika mijadala kama hii. Kama upeo wa shule yako umeishia hapo usiulazimishe ukaja ukajikuta unanunua jinai bila sababu za msingi.
Muulize mwenyekiti wako Elimu yake.
 
Back
Top Bottom