Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Ni kisa cha Richard ambae alifariki miaka michache iliyopita Richard alitoka kwao baada ya kumaliza kidato cha nne Dar alifikia Mbezi Beach kwa mjomba wake aliyekuwa afisa wa idara serikalini mjomba aliagiza Richard aje Dar baada ya kumkuta kule kwao kijijini akiwa anauza kibiashara chake cha mahitaji muhimu kwa wanakijiji kama sabuni, mafuta, sukari, chumvi nk.
Mjomba aliona ni vyema amsaidie Richard alipata ajira kama mhudumu wa ofisi kabla mjomba hajastaafu baada ya kuajiriwa alijusogeza na kuondoka kwa mjomba kule kazini kuna mama mmoja alimsaidia Richard kupata chumba huku kwetu Kwamtogole.
Baada ya kusoma mtaa ulivyo, Richard alianza biashara ya chips jioni akitoka kazini chips mishkaki, chips kuku na kiepe Richard alinunua freezer la kuhufadhia nyama na biashara ilianza kukua lakini hakuacha kazi.
Ilibidi Richard aajiri wasaidizi wa kumsaidia kazi hasa mataarisho wakati yeye akiwa kazini na watu wa kutafuta kuku na mayai kila siku wakati akiwa kazini katika waajiriwa aliajiriwa sikujua mtoto mrembo, aliyempa Richard ushirikiano wote.
Richard alizama katika penzi la sikujua aliamua kuoa, wazazi wa sikujua walitaka abadili dini. Richard alimpenda sana Sikujua haikuwa shida aliitwa Rashid na tuliitwa kula mpunga baada ya ndoa.
Rashid alimiliki gari na nyumba mtaani lakini hakuacha kazi walipata watoto na kuongeza biashara walifungua bar na mgahawa wa kisasa wa chakula ndani ya usimamizicwa Sikujua.
Sikujua alianza kuwa mlevi, mara nyingi Rashid alimkuta akiwa hajitambui na hivyo kumpeleka nyumbani na yeye kuendelea na biashara alimuonya sana angalau apunguze ulevi lakini ilikuwa ngumu Rashid alikatishwa tamaa na mahusiano ya Sikujua na wanaume mbali mbali pale mtaani kumbe wengi walikuwa wapenzi wake tangu akiwa mwanafunzi.
Rashid aliamua kuhama nyumbani na kumuachia Sikujua kila kitu huko alikokwenda alianza upya alipata kiwanja na kujenga nje ya mji aliendelea na biashara alirudia dini yake na sasa aliamua kuoa mwanamke wa kijijini kwao.
Alikwenda likizo kwao na kumpata binti mzuri mwenye watoto wawili alifiwa na mumewe Richard alitoa posa na kurudi Dar. Sikujua aliyasikia yote hayo. Siku ambayo alimtumia habari kuwa mmoja wa watoto wao ni mgonjwa, Richard alikwenda mbio alimkuta mtoto anaumwa homaya kawaida Richard aliwekewa chakula na alikula. baadaya hapo aliondoka na alipofika kwake hakuamka tena.