tikatika
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,330
- 4,119
Nikiwa ni mwanadamu nimeona mengi, mtu aliyekosa na akaomba msamaha mbele ya watu wengi husamehewa. Lakn mtu kibri mara nyingi huvuna kiburi chake. Watanzania kama binadam kwa umoja wetu kuna wakati tulipatia kufanya maamuzi ya Taifa letu na kuna wakati tulikosea na tukajutia mbeleni. Kuna wakati tumejutia kwa wabunge wetu na kuna wakati tumefurahia kuwachagua baadhi yao
Mara nyingi nimemsikia rais wetu akijutia kwa tawala zilizopita kwamba zilikua za kifisadi. Anasema walifanya dili kila sehem. Kwa lugha rahisi yeye kama mtanzania na alipiga kura anajutia kura yake kumpa mtangulizi wake maana alifanya vibaya. Hivyo sioni ubaya watu amabao watakuja hapa na kujutia maamuzi yao ya kumchagua yeye endapo tu kile walichotegemea toka kwake hawakioni.
Naomba nieleweke kujutia maamuzi yaliopita sio kosa ni jambo la kawaida ili kutorirudia hapo mbeleni. Kumbukeni awamu iliyopita viongozi wa ccm walipita huku na kule na kusema katika serikali yao kuna mawaziri mizigo. Mawaziri hao kama wabunge wao katika majimbo ina maana wanajuta kuwachagua hadi kufikia kuwa mawaziri.
Kupitia ukurasa huu nitaomba kuona wale ambao wanajutia kura yao kumpa rais tuliye naye . Maana kwa kipindi kifupi kilichopita tayari amefanya mengi yenye kuonyesha njia ya wapi anatupeleka. Wale watakao jutia maamuzi yao tutawasamehe lakn wanaoona walikua sahihi wajue Mungu anawaona watakuja kukiri wakiwa wamechelewa. Maana mficha ukame njaa itamuumbua. Hii ya kujutia haichagui chama kuna wana ccm na kuna wasio na chama ila ulipiga kura.
Karibuni