Yuyo Ahumile Shamalendi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2018
- 993
- 782
Wakuu habari, kama nilivozungumzia kwenye kichwa cha habari.
Nina shida na mawasiliano ya TAMISEMI kwa anayeelewa niingieje kwenye website yao au email yao, vilevile sina email yao wala website yao, naombeni anayefahamu mawasiliano yao anisaidie.
Bila kujali ngoja niwaeleze tatizo linalonituma niwatafute hao.
Nina watoto wawili ambao majina yao yalikosewa shuleni, na sasa hivi wapo sekondari, mmoja yuko form four na mwingine yuko form one.
Nataka nifuatilie kama kuna uwezekano wa majina yao kurekebishwa, maana nimekuja kugundua hicho kitu baada ya kwenda kuwakatia vyeti vya kuzaliwa, wale watumishi wa ofisi ya usajili wa vizazi na vifo waliniambia niende shuleni kwao nikachukue majina yao ndipo niwapelekee.
Sasa baada ya kwenda shuleni kwao nikakuta naandikiwa majina ambayo yana makosa ya baadhi ya herufi, huyu wa form four jina la tatu limekosewa ni herufi moja tu ndo iko sahihi, na huyu wa form one jina la pili limekosewa herufi mbili na la tatu limekosewa kabisa.
Naombeni wakuu mwenye uelewa wa hivi vitu anieleweshe nifanyeje ili kurekebisha haya majina, maana hawa wa usajili wa vizazi na vifo walinishauri niende ofisi za elimu sekondari wilaya lakini baado maelezo walionipa hayakua ya kunisaidia.
Na ni lazima watoto niwakatie vyeti vya kuzaliwa.
Karibu kwa ushauri wenu na msaada pia wa mawasiliano ya TAMISEMI.