Wananchi wawashambulia wabunge kufuatia adhabu kwa Askofu Gwajima na Silaa

Kwahiyo watz watakuwa wengi sana ni wapumbavu?

Yani katika watu milion 60 hakuna werevu walau milion 1 wa kwenda kushambulia zile chanjo chap?

Yani hata wasomi wetu wa vyuo vikuu, madaktari, manesi, na watumishi wengine wa umma?

Chadema ina wafuasi manasema zaidi ya milion 7, nao siyo werevu kiasi cha kwenda kushambulia zile chanjo milion 1 chap ziishe?
Yes, nchi ina wajinga wengi sana, hata hilo kundi la wasomi uliloorodhesha hapo nao ni wajinga, huwa hawana misimamo wanayumbishwa kama matawi ya miti ili wapate kula yao, kama mnawategemea Chadema kumaliza hizo chanjo msijali.
 
walioharibu ni hao akina Gwajima na Mollel walianza kwa kuisema vibaya chanjo lakini ndiyo hao hao leo wanasema ni nzuri, wananchi washike lipi?

Wewe kama una akili timamu kirusi cha kwanza cha corona kiliitwaje na kasi yake ilkuaje na ss kirusi kinaitwaje na kasi yake ikoje? Kama kirusi kinabadilika unashangaa kubadilika watu? Acha hizo tafakari
 
Ndio kwa sababu hii nchi inaimani za kichawi top 5 Afrika,imeshikwa na makanisa ujasiliamali kama ya kina Gwajima,mwamposa nk na ina watu wenye elimu duni ,idadi kubwa ya maskini top 5 Afrika,around 90% wameisha la saba au hawakusoma na hata waliosomea walienda kujibia mitihani sio kuelimika thus why wakishahitimu kila kitu kinaishia hapo.

Sasa kwa hali hii unategemea nini? Ndio maana Mwendazake alifaulu kueneza propaganda na pia ccm wanafaulu kuwashika watu.
Hiyo ni kusema kwamba jamaa wamechagua Vita zao na wanashinda! Unabakiwa na chaguo chache Tu chagua Vita yako ikiwa ni kurekebisha Hizo fikra za watu, kujiunga nao au kuwa mtazamaji Tu
Ila upuuzi ndio utadumu kuwa na wafuasi wengi ndio maana watu wa Aina ya Gwajima Mimi nabaki kuwa mtazamaji Tu wa matukio Yao hata kuwachukia ni matumizi mabaya ya chuki
 
Wewe kuandika tu kiswahili ni majanga, unadhani unaweza kujua na kuchambua vizuri hoja za Askofu Gwajima kama “sauti ya nyikani” na kinachoendelea nchini!

Kiswahili ni lugha nyepesi kwangu. Lakini wewe unaleta ulimbukeni wako wa jiwe, na jiwe wako ameshaenda harudi tena
 
Sawa ila kumbe ukichanjwa bado kuumwa unaumwa ...Maana ya chanjo si ni kinga ya kuzuia ugonjwa fulani ukiingia mwilini usilete madhara sasa mbona hayo madhara ya corona bado yatatokea hata kama nimechanjwa hebu nipe elimu
Una ushahidi wa watu waliopata chanjo na kupata madhara kufikia kulazwa "sadaruki-ICU"?!!!

Ni hivi.....

Unapopata chanjo haina maana kuwa HUWEZI KUPATA MAAMBUKIZI....bali Kuna "chance" KUBWA ya kutofikia hatua mbaya.....

Watoto wadogo wanachomwa chanjo dhidi ya INFLUENZA(FLU)....kwani huwa hawapati mafua?!!!

Wazungu wanapokwenda maeneo yenye KIPINDUPINDU huchomwa chanjo dhidi yake siku 7-10 kabla....wakija maeneo yenye malaria(epidemic) humeza dawa za kuzuia kupata maambukizi makali yatakayopelekea "severe malaria"....

Kwa hiyo kwa kuwa mtu amepata hizo chanjo (KIPINDUPINDU+MALARIA) ndio akanywe maji machafu(yenye vinyesi vya binadamu) na kulala pembeni ya mabwawa yenye VIDUDU VYA MALARIA?!!

Kwako mkuu mwenye cheo kikubwa "kisichopewa jina bado ndani ya CCM".......
 
Kupata takwimu ya WANANCHI WENGI HUMU MITANDAONI kuko "biased" sana......

Juzi baada ya mh.Spika kuteleza ulimi na kutamka "jina la bwana Yesu badala ya bwana Yusufu" hukohuko ulipotuchukulia TAKWIMU zako ,HAO WANANCHI USEMAO NAO WALILIPUKA kuanza kumshambulia kwa KUKOSEA KULE ijapokuwa ULIMI HAUNA MFUPA NA YEYOTE ALIYEKUWA ANAFUATILIA VYEMA MTIRIRIKO WA MAELEZO YAKE alimuelewa vyema tu......

Hizo takwimu zako unazichukua kutokana na makundi yafuatayo:

1)Wasio na uelewa mpana juu ya nchi na taasisi ya bunge la JMT

2)Vijana wa upinzani wenye kupinga kila jambo linalofanywa na utawala ulio chini ya CCM

3)Vijana walio "desperate" kimalezi ,kifikra na kimtazamo wasiojishughulisha TAFAKURI zaidi ya "KULIPUKA" katika kila jambo kuntu"substantial"....

Binafsi ninaiunga mkono KAMATI YA BUNGE YA MAADILI ,HAKI NA KINGA kwa kuwahoji akina Askofu Gwajima na kutoa MAAZIMIO YALE....

#NchiHaiendeshwiKwaMihemkoKoko
#NchiKwanza
#SiempreJMT
Mkuu sikubaliani na wewe ktk hoja zako tatu hapo juu.
Wanaopinga chanjo ya corona wanao uelewa wa kutosha tu kuhusu masuala ya serikali na bunge. Tunafahamu kwamba kwamba wabunge ni wawakilishi wa wananchi na kwa hivyo ni vyema wakaangalia changamoto/mawazo yao na kuipelekea serikali kupitia bunge.
Si kweli kwamba mawazo/maoni ya wapinga chanjo yanatoka mitandaoni tu, kwani mkuu wewe hufuatilii media zingine? Wewe hufalii vipindi kwa mfano tu kama malumbano ya hoja na vingine vingi tuu ambavyo mtu yeyote, wa itikadi yoyote ananafasi ya kushiriki?
Wewe hufatilii hata watu wanaopiga simu kutoa maoni juu ya chanjo ya corona? Vinginevyo ungetoa njia mbadara ambayo ni sahihi kwako kupata data sahihi.
Pia si kweli kwamba wenye mawazo tofauti na chanjo ni vijana wa upinzani na wasio jielewa. Hapa umetukana watu wengi sana mkuu. Mbona kiongozi mkuu kabisa wa upinzani(Freeman Alkael Mbowe) alitoka hadharani na kutaka chanjo iwe lazima kwa wote na akapata uungwaji mkono na vijana wake maelfu kwa maelfu. Mbana wapo vijana wa ccm tena wanaolifahamu vizuri bunge na serikali hata kukuzidi, mfano akina polepole, jerry na wengine wengi wanamawazo tofauti na chanjo?
Ninachotaka kuuliza hapa ni kwamba, ni ipi njia sahihi ya kupata mawazo ya hao wanaojielewa?
 
Swala la chanjo Gwajima kapata uungaji mkono kwa wananchi wengi kwasababu kuu moja ni Legacy ya upumbavu wa Mwendazake kuwaongopea wananchi na kuwashawishi wananchi kuwa chanjo ni feki na kutumia kivuli Cha dini
Hahah such clown, thinking you know so much than most people about the vaccines?. We'll Never give in to their coercion or fear, once they put it in your blood, it cannot be removed. I am not getting it regardless and the more government tries to force it the more resistance. It's that simple.

Wewe unaona vaccines hazina shida kachome na familia yake usiwe na hasira au wivu kwa wale ambao hawajachoma, wakifa itaku athiri nini wewe? Sababu wewe ukichoma si unakuwa salama na familia yako? Then do just that to stay safe, but the majority have spoken hawataki chanjo. Don't blame it on Magu.
 
Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa wananchi wengi hawakubaliani na serikali kwenye suala la chanjo za korona.

Huhitaji kufanya utafiti wa kina kujua ukweli wake kwa sababu utapata maoni ya wananchi kwenye video za YouTube katika channel kama Millard Ayo ambazo hazifungamani kisiasa katika kutoa habari.

Kama ukitaka kujua mawazo ya wananchi wengi angalia sehemu ya maoni hasa kama wachangiaji wamekuwa zaidi ya 800.

Wabunge waliochangia maazimio ya Kamati ya bunge ambao waliwashambulia Askofu Gwajima na Jerry Silaa wameshambulia sana na wananchi kwenye sehemu ya maoni.

Kwa taasisi yenye watu mwenye akili timamu na ambao wanatumia fikra timamu katika kuchambua maswala mbali mbali watayachukua maoni ya wananchi kama picha na kiakisi kwa yale wanayofanya kama bunge na serikali.

Mfano ni hii video ya YouTube ambayo baadhi ya wabunge walikuwa wanawashambulia kina Askofu Gwajima na Jerry Silaa ambayo imepata wachangiaji zaidi ya 1000. Soma maoni ya wachangiaji utagundua kinachoendelea katika fikra za watanzania wengi.

VIDEO:

Kwa maoni haya ya wananchi ni lazima Bunge na Serikali wajitathimini kwa yale wanayoyafanya kwa sababu inaonekana hayana maslahi kwa wananchi wengi!

Bunge na serikali wanatakiwa wajue Askofu Gwajima na Jerry Silaa ni sauti ya watanzania wengi walioko “nyikani”.

Serikali na bunge waache “kushupaza shingo” kama hawataki kuvunjika kwa sababu kwenye siasa hakuna watu wajinga na wasio wajinga bali kuna watu wanakubaliana na serikali au hawakubaliani na serikali.

Mmarekani aitwaye George Carlin aliwahi kusema, “Never underestimate the power of stupid people in large groups.”

Muda ni mwalimu wa kweli!

Hoja dhaifu sana hii kuchukulia data za mitandaoni kuwa ndio sauti ya wote. Hatuwezi kuwa upande wa upotoshaji kuwa ndio ulioshinda. Huwezi kutofautiana na Chama na Serikali yako mwenyewe huwezi jiuzulu na utoke au uanjishe chama chako.
 
Mkuu sikubaliani na wewe ktk hoja zako tatu hapo juu.
Wanaopinga chanjo ya corona wanao uelewa wa kutosha tu kuhusu masuala ya serikali na bunge. Tunafahamu kwamba kwamba wabunge ni wawakilishi wa wananchi na kwa hivyo ni vyema wakaangalia changamoto/mawazo yao na kuipelekea serikali kupitia bunge.
Si kweli kwamba mawazo/maoni ya wapinga chanjo yanatoka mitandaoni tu, kwani mkuu wewe hufuatilii media zingine? Wewe hufalii vipindi kwa mfano tu kama malumbano ya hoja na vingine vingi tuu ambavyo mtu yeyote, wa itikadi yoyote ananafasi ya kushiriki?
Wewe hufatilii hata watu wanaopiga simu kutoa maoni juu ya chanjo ya corona? Vinginevyo ungetoa njia mbadara ambayo ni sahihi kwako kupata data sahihi.
Pia si kweli kwamba wenye mawazo tofauti na chanjo ni vijana wa upinzani na wasio jielewa. Hapa umetukana watu wengi sana mkuu. Mbona kiongozi mkuu kabisa wa upinzani(Freeman Alkael Mbowe) alitoka hadharani na kutaka chanjo iwe lazima kwa wote na akapata uungwaji mkono na vijana wake maelfu kwa maelfu. Mbana wapo vijana wa ccm tena wanaolifahamu vizuri bunge na serikali hata kukuzidi, mfano akina polepole, jerry na wengine wengi wanamawazo tofauti na chanjo?
Ninachotaka kuuliza hapa ni kwamba, ni ipi njia sahihi ya kupata mawazo ya hao wanaojielewa?
Sawa mkuu....

Ingetokea hayati JPM(RIP) asingepinga chanjo...."huo usemao umma wa wapinga chanjo" WANGEPINGA LEO HII?!!!

WANGEPINGA kwa hoja zipi za KISAYANSI??!!

Ama wanapinga tu "kimbango" na kuongozwa na "conspiracy theories"?!!!

Nakukumbusha kuwa MAJIBU YANGU HAPO JUU nimeyatoa kwa yule aliyesema kuwa "Mh.Gwajima na Mh.Silaa" wameonewa na kamati ya BUNGE.....

Kesi ya Silaa(KODI YA MISHAHARA YA WABUNGE) ni tofauti na ya Gwajima....

Mh.Gwajima hakupewa adhabu na BUNGE kwa kuwa na hoja kinzani dhidi ya CHANJO bali kwa kusema UONGO USIO NA USHAHIDI KUWA VIONGOZI WAMEPEWA "MLUNGULA" ILI WAPOKEE CHANJO....je hapa umemletea ushahidi wake huo?!!!
 
Hiyo ni kusema kwamba jamaa wamechagua Vita zao na wanashinda! Unabakiwa na chaguo chache Tu chagua Vita yako ikiwa ni kurekebisha Hizo fikra za watu, kujiunga nao au kuwa mtazamaji Tu
Ila upuuzi ndio utadumu kuwa na wafuasi wengi ndio maana watu wa Aina ya Gwajima Mimi nabaki kuwa mtazamaji Tu wa matukio Yao hata kuwachukia ni matumizi mabaya ya chuki
Kuna mambo fulani unakuta ni ya lazima kwa Taifa sasa kuwazima wapotoshaji wakati fulani ni muhimu maana ukiwaacha wataonekana ndio washika hatamu.

Unapokuwa na nchi yenye sifa nilizotaja hapo awali na waliojaaluwa mdomo kama Tzn hii ni muhimu kuwa partial dictator vinginevyo wenye Nia ovu wanaweza kukutoa kwenye reli.
 
Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa wananchi wengi hawakubaliani na serikali kwenye suala la chanjo za korona.

Huhitaji kufanya utafiti wa kina kujua ukweli wake kwa sababu utapata maoni ya wananchi kwenye video za YouTube katika channel kama Millard Ayo ambazo hazifungamani kisiasa katika kutoa habari.

Kama ukitaka kujua mawazo ya wananchi wengi angalia sehemu ya maoni hasa kama wachangiaji wamekuwa zaidi ya 800.

Wabunge waliochangia maazimio ya Kamati ya bunge ambao waliwashambulia Askofu Gwajima na Jerry Silaa wameshambulia sana na wananchi kwenye sehemu ya maoni.

Kwa taasisi yenye watu mwenye akili timamu na ambao wanatumia fikra timamu katika kuchambua maswala mbali mbali watayachukua maoni ya wananchi kama picha na kiakisi kwa yale wanayofanya kama bunge na serikali.

Mfano ni hii video ya YouTube ambayo baadhi ya wabunge walikuwa wanawashambulia kina Askofu Gwajima na Jerry Silaa ambayo imepata wachangiaji zaidi ya 1000. Soma maoni ya wachangiaji utagundua kinachoendelea katika fikra za watanzania wengi.

VIDEO:

Kwa maoni haya ya wananchi ni lazima Bunge na Serikali wajitathimini kwa yale wanayoyafanya kwa sababu inaonekana hayana maslahi kwa wananchi wengi!

Bunge na serikali wanatakiwa wajue Askofu Gwajima na Jerry Silaa ni sauti ya watanzania wengi walioko “nyikani”.

Serikali na bunge waache “kushupaza shingo” kama hawataki kuvunjika kwa sababu kwenye siasa hakuna watu wajinga na wasio wajinga bali kuna watu wanakubaliana na serikali au hawakubaliani na serikali.

Mmarekani aitwaye George Carlin aliwahi kusema, “Never underestimate the power of stupid people in large groups.”

Muda ni mwalimu wa kweli!

GWAJIMA, asitetewe , tatizo lake nikutaka kujifanya anajua kila kitu, kwamba dunia NZIMA inachanja kuangamiza watu wake, na Kama sivyo inawezekanaje iwe TZ

Yeye KWA imani yake hakulazimishwa chanja, na hakuna anaelazimishwa chanja , ila ni kosa pale msimamo wako unapoutumia shawishi ,na katisha watu wengine kupata chanjo Ili Hali unajua, kufa KILA mtu atazikwa na kaburi lake Wala huwezi kuwa na msaada WOWOTE siku ya kifo Cha mtu kikifika Kama ASKOFU,

Ni mtu wa ajabu tu anaweza kubaliana na Gwajima kwenye hoja zake za chanjo,
 
Binafsi nawaunga Mkono Mhe Askofu Gwajima na Mhe. Jerry Silaa. Yale yalikuwa mawazo yao binafsi na yangejibiwa kwa hoja.
 
Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa wananchi wengi hawakubaliani na serikali kwenye suala la chanjo za korona.

Huhitaji kufanya utafiti wa kina kujua ukweli wake kwa sababu utapata maoni ya wananchi kwenye video za YouTube katika channel kama Millard Ayo ambazo hazifungamani kisiasa katika kutoa habari.

Kama ukitaka kujua mawazo ya wananchi wengi angalia sehemu ya maoni hasa kama wachangiaji wamekuwa zaidi ya 800.

Wabunge waliochangia maazimio ya Kamati ya bunge ambao waliwashambulia Askofu Gwajima na Jerry Silaa wameshambulia sana na wananchi kwenye sehemu ya maoni.

Kwa taasisi yenye watu mwenye akili timamu na ambao wanatumia fikra timamu katika kuchambua maswala mbali mbali watayachukua maoni ya wananchi kama picha na kiakisi kwa yale wanayofanya kama bunge na serikali.

Mfano ni hii video ya YouTube ambayo baadhi ya wabunge walikuwa wanawashambulia kina Askofu Gwajima na Jerry Silaa ambayo imepata wachangiaji zaidi ya 1000. Soma maoni ya wachangiaji utagundua kinachoendelea katika fikra za watanzania wengi.

VIDEO:

Kwa maoni haya ya wananchi ni lazima Bunge na Serikali wajitathimini kwa yale wanayoyafanya kwa sababu inaonekana hayana maslahi kwa wananchi wengi!

Bunge na serikali wanatakiwa wajue Askofu Gwajima na Jerry Silaa ni sauti ya watanzania wengi walioko “nyikani”.

Serikali na bunge waache “kushupaza shingo” kama hawataki kuvunjika kwa sababu kwenye siasa hakuna watu wajinga na wasio wajinga bali kuna watu wanakubaliana na serikali au hawakubaliani na serikali.

Mmarekani aitwaye George Carlin aliwahi kusema, “Never underestimate the power of stupid people in large groups.”

Muda ni mwalimu wa kweli!

Unaonekana unafarajika sana kuona baadhi ya watu wanakataa chanjo! Wewe hauitaki chanjo ukikaa kimya na mamno ya chanjo ukatuachia wajinga kunashida gani?

IMG_20210803_101338.jpg

IMG_20210803_101338.jpg
 
Swala la chanjo Gwajima kapata uungaji mkono kwa wananchi wengi kwasababu kuu moja ni Legacy ya upumbavu wa Mwendazake kuwaongopea wananchi na kuwashawishi wananchi kuwa chanjo ni feki na kutumia kivuli Cha dini
Haya wewe mwerevu tusaidie haya majibu.
Chanjo Zina usalama kiasi gani? Zinaweza kumkinga mtu kwa muda gani?
Short term na long term side effects ni zipi?
Kwanini ujaze consent form wakati chanjo zote hatukuwahi kujaza consent form?
Je ukichanjwa hutaugua?
 
Yes, nchi ina wajinga wengi sana, hata hilo kundi la wasomi uliloorodhesha hapo nao ni wajinga, huwa hawana misimamo wanayumbishwa kama matawi ya miti ili wapate kula yao, kama mnawategemea Chadema kumaliza hizo chanjo msijali.
Unasema wanachi ni wapumabavu!

Je nyie chadema ina maana siyo werevu pia? Mbona chanjo bado zipo na zilikuja milion 1 tu?

Ina maana nyie hamfiki milioni hapa nchini?
 
Huo ni ushahidi kuwa chadema hawafiki milioni, hivyo kelele za kuibiwa kura waachane nazo
 
Back
Top Bottom