Hivi huyo mwingira anamtafuta mungu au mali? Manake simwelewi mara anamiliki mashamba, bank, viwanja vikubwa anatembelea magari ya gharama sasa huyu ni mtumishi wa mungu au mtafutaji. Huyu jamaa anatia shaka.
Biblia inasema huwezi kutumikia mabwana wawili yaani pesa na mungu. Sasa mtume anamuhubiri mungu gani.
Makanisa mengi ikiwemo Roman Catholic.hayategemei sadaka wanaamini asiyefanya kazi na asile hata kama ni kanisa au ni padre lazima ajishughulishe.Ndio maana Roman catholic wana miradi ya mashule,vyuo vya VETA na vikuu kama st augustine ,miradi ya mashamba,hostel,miradi ya kupangisha maduka kama ilivyo msimbazi Centre,Vituo vya Radio,Television,Magazeti,Bank ya Mkombozi kwa ajili ya kuweka sadaka zao na ada za mashule yao na pesa za waumini wao na kuzikopesha,kuziwekeza n.k Makanisa mengi yamegundua kuwa ukitolea macho sadaka pekee kanisa haliwezi kujitegemea na kuendelea kwa kasi litakuwa tegemezi kwa watoa sadaka waumini ambao kila siku wanapungua kwa kupenda dunia,kwa kuhama hovyo makanisani na wabahili wa kutupwa kutoa sadaka na hata wakitoa midomo juu padre hapumui mara kala hela zetu hela zenyewe hazijai kibaba.
Hivyo Usishangae Mwingira anachofanya kanisa ni sehemu ya jamii linapatikani kanisani na sokoni pia llinapatikana likiuza bidhaa zake ili lipate pesa za kujiendesha.Na ni kitu kizuri.Sababu wanaweza hudumia yatima,wenye shida n.k wakiwa na mapato mazuri kuliko waanzishe mfano kituo cha yatima kinachotegemea huruma ya maruhuni mtoa sadaka ambaye mpaka apende siku ya sikukuu ndio alete mlo mmoja akiwa kazungukwa na vyombo vya habari kibao kwa katukio ka kutoa mlo mmoja.
Kutafuta mali kwa ajili ya kuhudumia jamii kwa shule,bank,n.k sidhani ni kosa.Sidhani mbinguni watu wanaenda tu kwa kujisalia na kusalia wengine tu inataka watu wahudumie wengine pia kwa mahitaji na huwezi hudumia mwingine wakati ni lofa huna kitu.Yesu aliwahi kulalamika kuwa nilikuwa sina nguo hukunivika,nilikuwa sina kile hukunipa nenda motoni.Ina maana anaendelea kulalamika nilikuwa sina shule hukunijengea,nilikuwa sina hospitali hukujenga,sina benki hukunianzishia,sina sehemu ya kupangisha maduka hukunijengea nenda motoni.Makanisa yasiyofanya hayo yajiulize tena.Vigezo vya kwenda motoni viko vingi si tu kwa sababu wewe huibi huzini basi wewe wa mbinguni.Vimo vigezo pia hivyo vya huduma kwa jamii.
Lakini una haki ya kuamini chochote hata katiba ya nchi inakuruhusu.Imani ni kitu cha mtu binafsi sikupingi unachoamini natoa maoni yangu.