Wananchi wavamia shamba la Nabii Josephati Mwingira Break Throw Mapinga

Wananchi wavamia shamba la Nabii Josephati Mwingira Break Throw Mapinga

Je Ni yeye mwenyewe au wafuasi wake wanamwita Nabii ? au ni hapa JF tu
 
Yani huyo jamaa hizo mali na mashamba ni mali yake Au mali ya kanisa?
 
Wananch wa Bagamoyo eneo la Mapinga Wamevamia Shamba la Nabii na Mtume Josephati Mwingira. Juzi Mwingira alikwenda huko akiwa na walinzi wa Kimasai walioambatana Na Mabounce na kuendesha operation ya kuwaondoa kwa nguvu wananchi hao na kuzua mapigano makali ambapo leo kuna kikao cha ulinzi na usalama kujadili suala hilo kinachofanyika shule ya Sekondari ya Lord baden MEMORIAL SCHOOL inayomilikiwa na Col Kipingu.

Mgogoro huo unasululishwa na Polisi Bagamayo na polis DSM na watendaji wa Serikali. Hii ni mara ya pili kwa Mwingira kuvamiwa ambapo kule Sumbuwanga anamiliki shamba zaidi ya ekar 500 alilouziwa Tshs 600m na wananchi wanapinga.


Mtume na Nabii Josephat Mwingira na ghiriba kwa Watawala mkoa wa Rukwa


[h=2]Monday, April 25, 2011[/h] [h=3]MTUME NA NABII JOSEPHAT MWINGIRA NA KIKWETE NA PINDA[/h]
​


http://www.blogger.com/post-edit.g?blogID=6603747238927766074&postID=2459875649829979800&from=pencil Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa,Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
hapo hakuna nabii.walinzi wa kimasai kumlinda nabii wa Mungu. Hii ni ya mwaka!!!!!
Hali ya Mgogoro wa Nabii na Mtume Josephat Mwingira huko Mapinga Bagamoyo ni kwamba , Yeye Mwingira aliwapa baadhi ya Wananchi pesa na kununua eneo hilo kwa njia ya kuwarubuni wachache sasa baada ya mgao huo kuleta mgogororo wale ambao walikosa mgao ndio wamerudi kwenye maaneo hayo wakidai haki yao na kesi ipo mahakamani!!!

Sasa Nabii Mwingira akaamua kuwaondoa hao waliorejea kwa maelezo kwamba MUNGU Kamutuma yeye kama Mtume wala hana haja ya Mahakama!!!

Katika kutekrleza hilo , amekodi majeshi ya aina tatu :
1. Mabounce Wana bastola
2.Wamasai wana mishale
3.Askali wa Kampuni ya Ulinzi wanao miliki silaha

Yeye Mwenyewe Josephati Mwingira Yupo hapa na ndiye anasimamia operation Zote za kuamurisha Askali na kubomoa Nyumba za watu anao dai wamevaimia ili hali kesi yao ipo mahakamani!!!

Askali wote waliokodishwa na Nabii Josephati wanalipwa Posho ya Tshs 45,000/- na Tshs 60,000/- kwa siku kutokana na kazi hiyo ya dharura ambayo itadumu kwa miezi mitatu!!

Mpaka sasa Katapila linaunguruma huko na Wanaendelea na operation Hiyo.


Hatua ya Mwingira kuchukua sheria mkononi ilifanyika tena kwwenye kiwanja ambacho kipo karibu na Kanisa lake Mwenge ambapo aliamuru nyumba zibomolewe wakati kesi ipo mahakama kuu!!
Hadi sasa mgogoro huo unaenderea ambapo Mahakama kuu ilisha toa hati za kukamatwa Nabii Josephati Mwiongira kwa Kuingilia uamuzi wa Mahakama lakini mpaka sasa haja kamatwa!!!


Wapo watu wanaoamini kuwa Mwingira na Rais Kikwete ni Marafiki lakini wengine wana amini kuwa serikali inamuogopa Nabii Mwingira !!!!
 
Idadi ya Askali waliokodishwa na Nabii Mwingira wanakadiriwa kuwa 50 ambapo kampuni ya Ulinzi inayo linda EFATHA BENKI MWENGE imeongeza Nguvu kubwa kwa sakata hilo!!!


Hata hivyo Walimu wa Shule ya Break Through wanamulalamikia Nabii Mwingira kwa Kuwatapeli mishahara yao ya Miezi sita na mpaka sasa walimu hao wamehama na kutafuta kazi sehemu zingine!!!

Walimu hao walalamikia utapeli huo huku yeye Nabii Mwingira akishirikiana kufanya utapeli huo na mWANAMKE ANAEYE TAJWA KWA JINA LA ROZI MFANYAKAZI WA AKIBA BENK!!!
 
[h=2]Mwingira aporomosha matusi ya nguoni ibadani baada ya kuumbuliwa na JF[/h]
Katika ibada ya jumapili iliyokuwa inafanyika kwenye kanisa la EFATA Nabii na mtume mwingira aliporomosha matusi ya nguvu kwenye ibada hiyo kwa watu wote wanaokwenda Loliondo na waandishi wa habari wanaojifanya kumuandika kwenye vyombo vya habari baaadhi ya maneno yenye lugha iliyopitiliza sitaweka ila mojawapo ni haya " Nasema wale wanaokwenda Loliondo ni wajinga!! nasema niwajinga!! waandishi wa habari ambao wanatabia ya kuniandikaandika kwenye vyombo ya habari ni wajinga'' nasema niwajinga, mawaziri wanaokwenda Loliondo ni wajinga!!! wanaonisema kuwa ninalaaana ya Kanisa la Moja ni wajingaaaa!!! baada ya kuporomosha maneno ambayo sio rahisi kwa mtu yeyote wa mungu kuyatamka alimalizia kwa kuwataka wamumini waitikie kwa kusema ameeen. Hata hivyo alibainisha wazi kuwa anajua kuna waandishi wa habari wapo ibadani hapo hivyo waandike wanavyoweza maana ni wajinga.

Kwenye Ibada ya jumapili ya tarehe 13/03/2011 mwingira alitoa amri mafundi waliokuwa wanarusha ibada ya jumapili kwa njia ya TV wazime ili wanachi wanofuatilia ibada hiyo wasione kashfa aliyoitoa kumkashifu babu wa loliondo hata hivyo bila kujua kuwa JF member alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wametinga ndani ya ibada hiyo. Hata hivyo inaonesha kuwa mwingira anashida kubwa kiroho hivyo kwani taharuki na ghadhabu aliyoionyesha ibadani juu ya kuanikwa na vyombo vya habari mimi binafsi sijui nitafanyiwa maombi gani ili niamini kuwa mwingira ni nabii. Baada ya ibada baadhi ya waumini wake walisikika wakimlaumu kwa lugha alizotumia kuwasilisha hisia zake!! nimeona niwajuze wenzangu ili mjue msimamo wa nabii huyu!!!!​
 
[h=2]Ranchi ya ngombe songea;mkurugenzi miwgira meneja mke wa mwingira..tutafika??yesu tusaidie[/h]
Ndugu wapendwa ktkt bwana
wakati waumini wa makanisa mbali mbali wakiangaika kutafuta nauli za kwenda ibadani..,mtume na nabii mwingira amekuwa akiombwa kununua usafiri kwa ajili ya watumishi wake kuja na kurudi at least kuondoa adha ya wapendwa kutembea mpaka ubungo....

Narudi Songea;Mh Mtume na Nabii Mwingira unaweza kutueleza ile ranchi ya ngombe ilio kule songea ya jina la efatha iweje mkurugenzi wewe na meneja wa ranchi mama mwingira...je hii ranci ni ya efatha ama familia ya mwingira..unajua mtumishi ndio pale tunarusi kuuliza n kweli unaweza ona babu anakula 500 kwa siku kama laki 2..lakini unaona watu wanakiri uponyaji ..sasa turudi kule songea ambako tangu nianze kusali efatha nina miaka 2.5 sijawahi sikia matumizi na mapato ya ranchi ya efatha..nafikiri watumishi wanaitaj kujua kinachopatikana na si kupigwa geresha

Ajabu nilishangaa sana siku waziri mkuu pinda anashirikia kampen za kuchanguia mfuko wa songea ukatoa MILLION kUMI KASH na huku watumishi wako wakikosa nauli na kulilia hata kabasi cha kuwapeleka pale ubungo..embu tuwaangalie wenzetu jaman tusiwe wakina RAIS GABGO ...unaweza kuwa gabgo huku ukiwa kanisan...mwisho nashauri mpendwa jitahdi uwe unahubiri NENO LA MUNGU na si story za babu kama babu tumechoka kwenye magazeti zinatutosha..inashangaza unatangaza waumini wachunguzane mbona kwenye kupona wasiambiane???

NI VIZURI KANISA KUWA NA KITEGA UCCHUMI LAKINI UMILIKI WA VITEGA UCHUMI KWA JINA LA FAMILIA ZA WACHUNGAJI NAOMBA UFE ITAPENDEZA ZAID NA ZAIDI KUWAPA MATUMAINI WAUMINI..PIA KILA MNACHOKIANZISHA EMBU WAUMINI FUNGUKEN KUULIZIA KINACHOENDELEA..HIZI NI SADAKA ZENU ATI MNA HAKI YA KUHOJI NA KUULIZA KINACHOENDELEA MWISHO WA SIKU MTASIKIA UWANJA WA EFATHA MWENGE UMEUZWA MNAKUMBANA NA KIBAO CHA

TUMAHAMIA

SONGEA​
 
Nabii Josephati Mwingira na Misukule
Kiongozi wa Kanisa la Efatha la jijini Dar es Salaam, Nabii Josephat Mwingira (pichani) amewashangaza waumini wake alipodai Jumapili iliyopita kuwa, kuna mabinti wawili wachawi waliomfuma na kumvamia kanisani humo na akadai wametoka Loliondo katika Kijiji cha Samunge, hivyo amewakamata.

Tukio hilo lililowashtua waumini wake lilioneshwa moja kwa moja na televisheni ya kanisa hilo. Kiongozi huyo akadai kuwa, kitendo cha kuwakamata wachawi hao ni ushujaa na ushindi kwake.

Kiongozi mmoja mwandamizi wa kanisa hilo aliliambia Uwazi kuwa, Mwingira ana maono ya aina yake na mabinti hao wamejitokeza wenyewe na kudai kuwa walikuja kumdhuru.

"Wakati nabii huyo alipokuwa akiendesha ibada kanisani hapo ndipo binti mmoja alipoibuka na kudai kuwa ameagizwa kuja kuwanga kanisani hapo," alisema kiongozi huyo aliyeomba jina lake kutoandikwa gazetini kwa kuwa siyo msemaji.
Mwandishi wetu alishuhudia binti huyo akihojiwa na Mwingira na kukiri mbele ya hadhara kuwa, yeye anafanya ulozi pamoja na mwenzake ambaye yupo kanisani humo. Muda mfupi baadaye naye alijitokeza na kwamba alifundishwa na bibi yake ambaye hakumtaja jina.

Hata hivyo, uongozi wa kanisa hilo uliwawekea ulinzi mkali na ukakataza mtu yeyote kuwapiga picha, hali iliyosababisha minong'ono kwa watu.

"Kama kweli ni wachawi kwa nini wanakataza wasipigwe picha?" Alisikika mtu mmoja akihoji kwa sauti ya chini na akadakia mwingine aliyehoji kwa nini majina yao hakutajiwa mwandishi?

Mwandishi wetu alifuatilia kuona hatma ya mabinti hao lakini akashuhudia wakiingizwa katika gari na kutoweka eneo la kanisa na mmoja wa viongozi wa kanisa hilo na kuelekea kusikojulikana.
 
[h=2] Mtume na Nabii Mwingira awakera majirani zake
[/h]
"Mtume" na "Nabii" Mwingira azidi kuwakera majirani zake
Na Mwandishi Maalum

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, ambayo inaendelea kuwashangaza watu wengi, hususan wanaoishi jirani na "kanisa" la EPHATA, mtu anayejiita "Mtume na Nabii", Askofu Josephat Mwingira, amezidi kuwakera watu hao kutokana na vituko vyake visivyoisha kila uchao.

Kwa mujibu wa watu hao, Askofu huyo ambaye ndiye kiongozi wa juu na wa mwisho wa kanisa hilo, amekuwa akiwafanyia vitendo vya hujuma, vitisho na ubabe, majirani zake hao, kiasi cha hata kuhatarisha maisha yao, au kuwafanya waishi kwenye maisha ya hofu nyingi na woga.

Siku ya Jumamosi, Mei 26, 2007, kuanzia majira ya saa moja asubuhi, "kijiko" kinachomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, kikisindikizwa na askari wa kawaida na wa kikosi cha kutuliza ghasia, wakiwa wametokea Kituo cha Polisi cha Oyster Bay, pasi na kutoa hadhari yoyote, kilianza harakati za ubomoaji wa ofisi na vibanda vya wafanyabiashara mbali mbali, ambao walikuwa wakifanya shughuli zao kwenye eneo ambalo liko jirani na kanisa hilo, hapo Mwenge, Dar es Saalaam.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, eneo hilo hapo awali lilikuwa kiwanja ambacho hakikuwahi kupimwa, jambo ambalo lilikuwa kivutio kwa watu walioona upenyo wa kufanyia shughuli zao za kibiashara. Mwekezaji mmoja aliamua kujenga vibanda na kuwakodisha wafanyabiashara ambao waliweka maduka yao hapo. Eneo hilo linapakana na eneo la iliyokuwa kampuni ya Mangula Makongo Metalworks and Tools Limited, (MMMTL), ambayo imefilisiwa chini ya Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC).

Kwa mujibu wa taarifa mbali mbali zilizopatikana, mnamo mwaka 2001, PSRC ilitangaza kuifilisi kampuni ya MMMTL, na kuwakaribisha wawekezaji kujenga ofisi zao kwenye eneo la iliyokuwa kampuni hiyo. Kiwanja hicho, ambacho kinatambulika kama Kitalu Namba 90, Mikocheni Light Industrial Area, kilitumiwa, kwa sehemu ndogo, na kampuni tatu za Simon Engineering Works Limited, Afro Plus Industries Limited na Elbe Tanzania Limited, ambazo ziliingia kwenye eneo hilo kwa nyakati tofauti, kuanzia mwaka 2001.

Wakiongea kwa masharti ya kutotajwa majina kwa kuwa wao sio wasemaji husika, watu waliohojiwa wakiwa ni wafanyakazi katika maeneo ya nje ya Kitalu Namba 90, na wafanyakazi katika makampuni yaliyomo ndani ya eneo hilo, wamesema kwamba wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa kwa watendaji wa kanisa la EPHATA, ambalo limesajiliwa kama Taasisi Isiyo ya Kiserikali (Trust), kwa jina la EPHATA FOUNDATION.

"Hawa watu wamekuwa wakitusumbua kwenye maeneo yetu, mara kwa mara tunafuatwa na askari polisi kwa amri yao, eti tumetishia kuwaua.
"Mara nyingi hili geti unaliona (akiashiria geti linaoingia ndani ya eneo hilo) linakuwa linafungwa, watu wanazuiwa kuingia hapa kwenda ofisi kwao, wanalazimika kuyaacha magari yao nje, ambako hakuna usalama.

"Ndugu mwandishi hapa ni kero tupu," alisema mmoja wa watu waliohojiwa.

Mdau mwingine alisema Askofu Mwingira amekuwa akiendesha maombi maalum ya kuwaombea kifo wakurugenzi na watendaji wakuu wa makampuni ambayo yamepangishwa na PSRC kwenye kitalu hicho.

"Ni Mungu gain anayeombwa aue viumbe wake? Hawa hakika wanamwabudu shetani, sio Mungu. Sijawahi kusikia kwamba eti unamwomba Mungu aue mtu fulani, mnakaa, mnakula pilau, mnafanya ‘hitma' ya kuwaombea watu wafe, usiku kucha? Hakika sijawahi kuona!" alisema mdau huyo.

Wakizungumzia tukio la Jumamosi, Mei 26, 2007, watu mbali mbali wamepokea tukio hilo kwa hisia tofauti.

"Kwenye hili eneo kulikuwa na taarifa ya watu kuondoka, ambayo ilitolewa siku nyingi na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

"Watu walikuwa wakifanya shughuli zao hapa, na kulikuwa na kesi mahakamani. Lakini hawakuwa na leseni za biashara, wala hawakuwa wanalipa kodi zinazoambatana na leseni hizo.

"Alichofanya Mwingira, kwa kuwa alikuwa anajua kwamba hata wakienda wapi, ameenda kule Manispaa, sijui kaongea na nani, wakampa eneo hili alimiliki. Na yeye kwa roho yake mbaya, akaamua kuja kuwabomolea watu bila taarifa yoyote kwamba siku bulani anabomoa. Watu wameshtukizwa tu!" alisema mdau mmoja.

Taarifa za kuaminika kutoka kwa baadhi ya watu wanaofanya kazi ndani ya kanisa la EPHATA zimesema kwamba Askofu Mwingira aliwachangisha waumini wa kanisa hilo kiasi cha Shilingi Milioni Kumi za Kitanzania, ambazo zilitumika katika kuwalipa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni pamoja na Askari Polisi kutoka Oyster Bay na wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia, ili kuendesha zoezi la bomoa-bomoa bila kupingwa.

"Sisi tuliona kijiko cha Manispaa, Mgambo wa Manispaa na Askari Polisi, tukajua kwamba hili zoezi linaendeshwa Kiserikali. Kwa hiyo hatukuwa na ujanja wa kulalamika wala kuzuia, tulichofanya ni kuokoa mali zetu, zile ambazo tuliziwahi.

"Nyie wenyewe mmemuona yule jamaa alivyopigwa na hawa Mgambo wa Manispaa, alipokuwa akijaribu kuokoa mali zake. Ninavyosikia, huyu jamaa ana wake wawili na watoto saba, jina simkumbuki. Wamempiga, wamemjeruhi, na mali zake wamepora. Kuna haki hapa? Huyu mtu kweli ni Nabii na Mtume, anayewatuma watu kufanya udhalimu wote huu?" alisema mdau mwingine.
Wakihojiwa katika nyakati tofauti na ITV pamoja na vyombo vingine vya habari, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Shaban Londa, alisema kwamba yeye binafsi hakuwa na taarifa kuhusu zoezi la bomoa-bomoa hiyo siku hiyo ya Jumamosi, Mei 26, 2007. Aidha, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni naye alikiri kutokuwa na taarifa zozote kuhusu bomoa-bomoa hiyo.

Kuhusu utendaji wa kanisa hilo, mdau mmoja ambaye naye aliongea na mwandishi wetu kwa masharti hayo hayo ya kutotajwa jina lake, alisema: "Huyu jamaa ni mfanya biashara tu! Anachangisha pesa nyingi za watu, anawadanganya, anawapa matumaini ya uongo. Ameshavunja ndoa za watu wengi, na wale ambao wanaondoka kwenye kanisa lake kwa kukatishwa tamaa na vitendo vyake, wanaogopa kujitokeza kutokana na kanisa hilo kugubikwa na imani za kishirikina."

Watu wengi waliohojiwa walisema, kwa nyakati tofauti, kwamba Askofu Josephat Mwingira anasadikika kutumia nguvu za giza kuendesha shughuli zake za kidini. Aidha, wameongeza kwamba kiongozi huyo mwenye utata mwingi, anadaiwa kuwahifadhi raia wa Nigeria, ambao wanaaminika kuwa wachawi wanaomsaidia kuendesha shughuli zake hizo.

"Tumeona mengi hapa, tunaogopa kusema mzee, tukisema hatujui kama tutaishi mpaka kesho. Dunia nzima inajua kwamba Nigeria ndio inaongoza kwa ushirikina! Utajaribu kaka?" alisema mdau huyo.

Wakati yote haya yakiendelea, taarifa za kuaminika ni kwamba, licha ya kudai kwamba anamiliki kihalali eneo la Kitalu Namba 90, kwamba amenunua eneo hilo kutoka PSRC, taarifa kutoka ngazi za juu serikalini zimekanusha kuuzwa kwa eneo hilo kwa EPHATA FOUNDATION. Jitihada za kupata taarifa za uhakika kutoka PSRC zimekuwa zikigonga mwamba kutokana na watendaji wa PSRC kuwa na kigugumizi kuhusu suala hilo. Licha ya malalamiko ya muda mrefu, pamoja na kuwapo kwa kesi mahakamani kuhusu mgogoro unaolikabili eneo hilo, PSRC wameshindwa, ama kukanusha ama kuthibitisha kuuzwa kwa eneo hilo, Mahakamani au mahala popote pale ambapo wametakiwa kufanya hivyo. Uthibitisho pekee kwamba EPHATA FOUNDATION walipewa nafasi ya kumiliki eneo hilo ni barua iliyoandikwa mnamo mwaka 2005, kwenda kwa "Mtume na Nabii" Josephat Mwingira, ikitolewa nakala kwa Simon Engineering, Elba na Afro Plus Industries, kwamba EPHATA FOUNDATION ilikuwa imetoa malipo ya awali ya ununuzi wa kiwanja hicho, kwa makubaliano ya kuuzwa kwa kiwanja hicho kwa thamani ya Shilingi Milioni Mia Nne za Kitanzania (TShs. 400,000,000/=), kwa kutoa malipo ya asilimia kumi (10%) ya thamani hiyo. Kwa mujibu wa barua iliyotumwa kwa EPHATA FOUNDATION na kutolewa nakala kwa wapangaji wa eneo hilo, EPHATA FOUNDATION ilipewa muda wa sio zaidi ya miezi mitatu kukamilisha malipo hayo, la sivyo ingekuwa imepoteza haki ya kumiliki kiwanja hicho.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa wadau mbali mbali wa kampuni hizo tatu, Mahakama Kuu ilitoa amri (zuio) kwamba EPHATA FOUNDATION na watendaji wake wasiwazuie wamiliki, wakurugenzi, watendaji, wafanyakazi na wageni wa kampuni hizo tatu ambazo zimepangishwa na PSRC kwenye eneo hilo, kutowabugudhi au kutowazuia kufanya shughuli zao, ikiwa ni pamoja na kutowazuia kuingia na kutoka kwenye sehemu zao za kazi.

Hata hivyo, kwa mara kadhaa sasa, licha ya amri zilizotolewa na viongozi mbali mbali wa Serikali, pamoja na maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi, akiwemo Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, Askofu Mwingira na watendaji wake wamekuwa wakipinga amri hizo halali, kwa kufunga geti lililojengwa kwenye njia ya kuingia kwenye eneo hilo.

Wakihitimisha taarifa zao kwa mwandishi wetu, wadau wa Kitalu Namba 90, ambao ni majirani wa kanisa la EPHATA FOUNDATION, wamesema kwamba wamekerwa na unyanyasaji wanaofanyiwa na "Nabii na Mtume" Josephat Mwingira, na kuhoji, "Je, yeye yuko juu ya Sheria za nchi?"

Aidha, wadau hao wamesema kwamba wameazimia kupeleka malalamiko yao Mahakama Kuu, kutokana na kuonekana wazi kwamba amri halali ya Mahakama Kuu imepingwa na Mwingira na wafuasi wake, jambo ambalo ni kosa la jinai.

Juhudi za kumpata Nabii na Mtume Mwingira kuyazungumzia madai haya zilishindikana kutokana na kutokuwepo ofisini kwake na kutopatikana kwa njia ya simu.

Tutaendelea kuwapa taarifa nyingine mbali mbali kuhusu sakata hili kadri zitakavyopatikana
​
 
[h=2]Mzee Wa Upako kasema hakuna nabii mwingine duniani isipokuwa yeye!!!
Wednesday, December 28, 2011[/h] [h=3]BREAKING NEWS....![/h]






Mzee wa Upako Mchungaji Anthony Lusekelo ametangaza hivi sasa kupitia kituo cha television cha Channel Ten....kuwa mvuo kubwa iliyotangazwa na mamlaka ya hali ya hewa kuwa itanyesha jijini Dar es Salaam kwa siku tatu na kuwa italeta maafa haitaleta; haitaweza kuleta maafa kwa kwa neno lake na yeye kama mtumishi wa Mungu anao uwezo wa kuzuia na kuleta mvua.Akiongea kwa kujuiamini na mamlaka kubwa amesema kuwa anaongea wazi wazi bila kificho kupitia TV usiku huu ili kila mtanzania afahamu na kujua kuwa yeye anaye Mungu aliye hai na ni mtumishi wa Mungu.Amesema kuwa kama mvua hiyo itanyesha na kusabaisha maafa makubwa kama yaliyotokea basi yeye atajiuzuru uchungaji.Ila kama haitanyesha basi watu wasione aibu kukiri kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu....amesema mvuo hiyo itanyesha kwa kawaida tu na haitakuwa na maafa makubwa kama ilivyotarajiwa kwani yeye ameshamuomba Mungu isilete maafa na imeshakuwa hivyo.Akianza kwa kusema kuwa maafa yaliyotokea Dar es Salaam wiki iliyopita ni kwa sababu yeye hakuwepo mjini Dar es Salaam ndio maana ilinyesha ila hii ya sasa haitanyesha....!
 
Temitope Joshua
tb_joshua3.jpg

Church: Synagogue Church Of All Nations (SCOAN)
Estimated net worth: $10 million – $15 million (N1.5b- N2.5b)
 
Huyo ni tapeli tu anakula hela za wajinga wanao mwamin na na kuabudu katika kanisa lake nina ndugu yangu mmoja kesha wahi fanya kazi mashamba yake ya sumbawanga unaambiwa ni katili huyo shetan huko hafai hata bure yaan huyo ni nabii wa kuzim kabisa wooote wanao amini katika kanisa lake wametekwa na ni mateka wa shetan ingawa wao hawajitambui na ukiwaambia wankuwa wakali, nabii mwenyewe mtume mwenyewe khee hii noumaaaaa
Ni kweli hao waumini wake ni wakali sana unaoonyesha kumpinga nabii wao na SAW wao! nakumbuka nilinuniwa na gf baada ya kumwambia anapotea kufata dhehebu la namna hiyo!
 
Ni wakati muafaka sasa Serikali ikaingilia kati hawa wachungaji uchwara ambao kazi yao kubwa ni kupora sadaka kutoka kwa wananchi maskini na hasa wanawake.Kwa kuanzia wafuatao wanatakiwa serikali iwachukulie hataua hawa wezi haswa Mwingira, Lusekelo na Kakobe


Wewe makupa, shikilia adabu yako vizuri, isikuponyoke. Jifunze kuwa na adabu kwa Watumishi wa Mungu. Ukimtaja Kakobe katika orodha yako, basi uwataje pia Pengo, Malasusa na Mokiwa!
 
Nikumbushe mkuu, kule swanga yale mashamba yako malonje, ulinji au mawenzusi? Nacho kumbuka ni kanisa lake pale darajani upande wa kulia kabla ya polic post unavyoelekea swanga town fro tunduma.
 
sipendi kuhukumu watu lakini huyu bwana nina mashaka nae sana
kazi ya Mungu inaonekana hata kwa macho.
Kuna mfano wa Yesu alipojaribiwa na ibilisi alimwambia kama atamsujudia atampa
milki zote za dunia, kumbe mtawala wa dunia ni Ibilisi
Kwa hivo mtawatambaua wafuasi wake kwa mienendo yao na mali zao.
yesu hakuwa na hata pa kuweka kichwa hakuwahi kumiliki kitu
hata mitume wake waligawana kila walichonacho kwa faida ya kueneza injili
hawa wanaotembea na hammer,viwanja vikubwa bank nk mtapima wenyewe,
 
Ni wakati muafaka sasa Serikali ikaingilia kati hawa wachungaji uchwara ambao kazi yao kubwa ni kupora sadaka kutoka kwa wananchi maskini na hasa wanawake.Kwa kuanzia wafuatao wanatakiwa serikali iwachukulie hataua hawa wezi haswa Mwingira, Lusekelo na Kakobe

ushahidi unao kwamba walikuibia ww!if yes ishawishi serikali but if is just usikike,EPUKA SANA KWANI UTATOLEA HESABU YOTE UYASEMAYO.Usiwaguse watumishi wa bwana kwa maneno ya uzushi...
 
Kwa hiyo Wakuu kwa maoni yenu,Ukiwa mchungaji,Mwinjilisti,Mwalimu,Nabii na Mtume hutakiwi kumili mashamba makubwa kama hayo ya Mwingira.
Je hata kuendesha gari yenye thamani kubwa haitakiwi?
 
Nabii mussa, daudi, selemani, mtume mudi nk ni manabii walikuwa na majeshi kuliko hata mwingira hata yesu alikuwa anatumia nguvu eg hekaruni, kwa hiyo Mwingira kutumia nguvu kudai mashamba yake ni jambo la kawaida sana kwenye biblia.KUMBUKA BWANA YESU NI BWANA WA VITA
 
nabii mussa, daudi, selemani, mtume mudi nk ni manabii walikuwa na majeshi kuliko hata mwingira hata yesu alikuwa anatumia nguvu eg hekaruni, kwa hiyo mwingira kutumia nguvu kudai mashamba yake ni jambo la kawaida sana kwenye biblia.kumbuka bwana yesu ni bwana wa vita

acha kupotesha umma kwa maelezo yako ya jumla jumla. Huwezi kumfananisha huyu mtumishi wa giza na watu wa mungu waliodedicate maisha yao kwa mungu. Kwamba yesu ni bwana wa vita, hivyo unahalalisha ayofanya huyu mchungaji wako? Kumbuka kwamba, haya yote yalitabiriwa na manabii mbalimbali kwamba lazima manabii wa uongo watatokea siku za mwisho. Asikudanganye mtu kwamba kwasababu anamuita yesu kwenye mambo yake, basi ni mtumishi wa mungu aliyehai? Kumbukashetani ana uwezo mkubwa sana, na shetani anajua kwamba miujiza ndiyo dawa yenu nyie msiotaka kusoma biblia takatifu ili mdanganywe kwa urahisi na hawa watumishi wanaojiita manabii wkt wanajua kwamba unabii wao wameutoa baharini, nigeria au marekani kwa yule mfalme wa giza.

My take: Wewe na waumini wengine ombeni mungu sana na kusoma maandiko ili muweze kuonyeshwa yanayoendelea nyuma ya pazia ya hawa mnaowaita manabii wa mungu.
 
Back
Top Bottom