Walinzi Wa Nabii Mwingira Wakata Masikio Wananchi Rukwa Shamba la Milonje

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Bi Nuru Togwa(30) alikamwatwa na walinzi wa Nabii Mwingira baada ya kupita karibu na Shamba hilo na kupelekwa katika kambi yao na kukatwa Masikio yote mawili na kunajisiwa.

Bi Alesi Maarifa (77) naye alikamatwa na kuunguzwa na upanga wa moto sehemu za Siri na hadi leo matukio hayo yanaendelea:

Source: Gazeti ,Raia mwema ya Leo.

[h=2]Tuesday, December 27, 2011[/h]

Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa,Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
 
hawa wachungaji wetu wa siku hizi! mali mbele tu. he is responsible kwa watu walio chini yake na unaweza kuta hao walinzi ni waumini wake pia
 
Mwingira umetanguliza mali mno mpaka unapoteza Moral Authority. Tangu mwaka huu uanze haya yote ni yako huoni aibu!
29.04.2012 Jeshi la Polisi lamchunguza Mwingira

Jeshi la polisi linamchunguza kiongozi na watendaji wa Kanisa la Efatha, Nabii na Mtume Josephat Mwingira baada ya kutuhumiwa kuiba mitambo mbalimbali ya Kampuni ya Simon Engineering yenye thamani ya Shilingi bilioni 10.
Akizungumza na NIPASHE Jumapili jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema Taasisi ya Efatha inachunguzwa baada ya mmiliki wa Kampuni hiyo, Richard Moshi kufungua jalada akilalamika kuibiwa mitambo hiyo iliyokuwa ndani ya eneo linalogombaniwa na kanisa hilo.
Kuchunguzwa kwa Mwingira pamoja na Taasisi ya Efatha kunakuja wiki chache baada ya kutokea vurugu iliyosababisha uharibifu wa mali ya kiwanda cha uchapaji cha Afroplusa, ambapo baadhi ya waumini wa kanisa hilo walikamatwa kwa tuhuma ya kuhusika na uharibifu huo.
Kenyela alisema jalada la kesi hiyo limefunguliwa siku nne zilizopita na kazi ya kuchunguza suala hilo imeanza kwa ajili ya kubaini nani anahusika kuchukua sheria mikononi kwa kuondoa mali hizo kinyume na maamuzi ya Mahakama ya Ardhi ambayo ndio inahusika na jambo hilo.
"Polisi tumepata malalamiko kutoka kwa mmiliki wa Simon Engineering, akidai kaibiwa mitambo yake, tunachokifanya ni kuchunguza jambo hili na kama ikifikia hatua ya kuwahoji wahusika tutafanya hivyo," alisema.
Hata hivyo, alisema kesi hiyo haina utofauti na ile ya Afroplus kutokana na unyeti wake, hivyo jeshi la Polisi litakuwa na uangalifu wa kipekee katika kulishughulikia ili lisiingilie Uhuru wa Mahakama inayosikiliza.
"Hapa kuna kesi ya kuchukua hatua mikononi kwa kuharibu mali ndio maana tumeingilia kati, lakini hatutawapeleka mahakamani hadi hapo jalada litakapopelekwa kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ili kupitia kwanza," aliongeza kusema.
Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili Moshi alisema mitambo hiyo iliibiwa kutoka katika eneo la kiwanda hicho na iliibiwa wiki mbili zilizopita na kupelekwa mahali pasipojulikana.
Alisema kiwanda cha Simon Engineering kilisimamisha kazi zake baada ya kutokea mvutano na kanisa la Efatha, ambapo jengo lake pamoja na makampuni mengine yalibomolewa kinyume na sheria na kusababisha kufikishana mahakamani.
Moshi alisema Mahakama ilitoa notisi ya kutaka mali hizo zisiguswe wakati suala hilo likiendelea kusikilizwa, lakini kitu cha kushangaza mitambo hiyo iliondolewa na haijulikani wapi wameipeleka na kwa madhumuni gani.
Alibainisha kuwa mitambo iliyochukuliwa ni ile ya kutengeneza vipuri mbalimbali vya mashine na magari, mitambo ya kutengeneza vyombo vya nyumbani pamoja na zana mbalimbali kwa ma matumizi ya kilimo.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI

10.04.2012
Waumini 53 wa Efatha mbaroni Dar es Salaam

POLISI juzi ililazimika kuwatawanya kwa mabomu ya machozi wanaodaiwa kuwa waumini wa Kanisa la Efatha Foundation baada ya kutokea vurugu eneo la kiwanda cha Afro Plus, jirani na kanisa hilo lililopo Mwenge. Kutokana na vurugu hizo, Polisi inawashikilia watu 53 waliohusika katika vurugu hizo ambazo zilisababisha pia uharibifu wa mali za kiwanda hicho.

Akizungumzia vurugu hizo zilizotokea saa nane usiku wa kuamkia jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema zilikuwa kubwa huku wanaodaiwa kuwa waumini wa kanisa hilo wakikutwa na majambia, panga, nondo na sime.

"Usiku kulikuwa na tafrani kubwa eneo la taasisi ya Efatha Foundation inayomilikiwa na Joseph Mwingira na Kampuni ya uchapaji ya Afro Plus, jambo ambalo lililazimu mabomu ya machozi kutumika, lakini tulituliza vurugu hizo bila kupoteza uhai wa mtu yeyote," alisema Kamanda Kenyela.

Efatha Foundation na Afro Plus wamekuwa na mgogoro wa muda mrefu na kila mmoja akidai kuwa mmiliki halali wa eneo hilo na suala lao lipo mahakamani.

Akizungumzia tukio hilo la jana, Kenyela alisema Polisi ilipokea taarifa za kuwapo moto katika kiwanda cha Afro Plus ambapo askari wake na kikosi cha zimamoto kilifika eneo la tukio lakini walizuiwa na walinzi wa Efatha Foundation kuuzima moto huo.

"Walinzi wa Efatha Foundation walituzuia, hatujui kama walifanya hayo kwa maelekezo ya mwajiri, na jambo baya zaidi walikuwa wamewashikilia mateka walinzi wa kiwanda na taarifa tulizozipata walikuwa wameandaa greda (tingatinga) la kuvunja kiwanda," alidai Kenyela.

Kenyela alisema walinzi wa Efatha waliokuwa na silaha aina shotgun walipiga risasi mbili kutaka polisi waondoke eneo hilo.

Alisema kuwa ilipofika saa 11 alfajiri, polisi walifanikiwa kuingia ndani wakakuta kundi la wanaodaiwa waumini wa Efatha wakiharibu samani za kiwanda hicho na ndipo polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya na waumini hao kukimbilia ndani ya kanisa.

"Polisi walikwenda kuwakamata watu hao 51 ambao walikutwa wakiwa na nondo, jambia, panga, sime na vyote pamoja na gari lililotumika kuwaleta watu hao vimechukuliwa kama kielelezo wakati watu hao watakapochukuliwa hatua za kisheria," alidai.

Kenyela alisema Polisi inaangalia kama watu hao wameshawishiwa na mtu au kikundi fulani kufanya uvunjifu wa amani na watakayembaini kuhusika ataunganishwa kwenye makosa hayo.

"Suala hili liko mahakamani, lakini kwanini watu wanataka kufanya uvunjifu wa amani badala ya kuacha Mahakama ikatekeleza wajibu wake. Polisi tunalaani kabisa vurugu hizi na yeyote tutakayebainika kuhusika kuandaa vurugu hizi tutamuunganisha katika mashitaka," alisema.

Source: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=28808

NA Elvan Stambuli
TUHUMA nzito ya ubakaji imemwangukia Nabii na Mtume wa Kanisa la Efatha la Jijini Dar es Salaam, Josephat Elias Mwingira (pichani) ambapo Wakili Eliya Hubert Mbuya amedai katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kuwa, kati ya mwaka 2005 na 2009, mtumishi huyo wa Mungu alimbaka mkewe, Risasi Jumamosi lina A-Z ya sakata hilo.

KESI YA MSINGI
Kesi ya msingi yenye namba 226/2010 ilifunguliwa mwaka jana na Nabii Mwingira ikimtaka Wakili Mbuya ambaye ni mlalamikiwa awe amefika mahakamani hapo Novemba 10, 2011 mbele ya Jaji Nchimbi ili ajibu madai ya mlalamikaji anayemshitaki kwa suala lenye utata wa umiliki wa kiwanja nambari 548 (a) kilichopo Kawe, Dar es Salaam.
Mwingira anamlalamikia Mbuya kwa kuvunja mkataba wa kumpa sehemu ya kiwanja hicho ambacho tayari nabii huyo amejenga nyumba na kuboresha miundombinu kwa thamani ya shilingi 1,000,000,000.
Katika majibu ya Mbuya yayowasilishwa mahakamani hapo na Kampuni ya Mawakili ya Ngalo (Ngalo and Advocates), Mbuya amedai kuwa mke wake alibakwa na Mwingira, hivyo akaghairi kutoa kipande cha ardhi kwa mlalamikaji kama alivyofanya awali.

MWANZO WA SAFARI
Akieleza kwa urefu sakata hilo, Wakili Ngalo alidai kuwa, Julai 2003, Mbuya akiwa na mkewe Betha alihudhuria semina iliyoendeshwa na Mwingira katika Kanisa la Efatha, Mwenge Jijini Dar es Salaam ambapo kutokana na mahubiri yake, waliamua kuokoka na kuwa wanachama wa kanisa hilo.
Wakili Ngalo akaongeza kuwa, Mbuya alidai kwamba Oktoba 2003, katika kanisa hilohilo, iliendeshwa semina nyingine iliyokuwa chini ya Ibrahim Mlay na mlalamikiwa (Mbuya) alichangia basi dogo aina ya Toyota Coaster.
Alisema kuwa baada ya muda Mlay aliendesha semina tena katika kanisa hilo ambapo Mbuya na mkewe walihudhuria na walichangia kipande cha ardhi kilichopo Ploti Namba 548, Kawe Beach.
Sehemu ya majibu hayo ya kinga ikasema kuwa mwaka 2005, Mwingira alimtaka mlalamikiwa kutafuta mnunuzi wa kiwanja hicho ambapo fedha ambazo zingepatikana, zingejenga makanisa ya Efatha sehemu nyingine.
Ikadaiwa kuwa, alijitokeza mnunuzi aliyekuwa tayari kulipa shilingi 176,000,000, mwingine akiwa tayari kwa kulipa shilingi 450,000,000 kwa lengo la kujenga hoteli.
Ikasemekana kwamba, Novemba 2006, mlalamikaji alimwambia mlalamikiwa kuwa Mungu alimwonesha maono yakimtaka mlalamikiwa asikiuze kiwanja hicho, bali amkabidhi mlalamikaji hivyo amwandalie ‘dokumenti' za makabidhiano ya kiwanja hicho, naye akatii.

DALILI ZA UBAKAJI
Akizungumzia madai ya mkewe kubakwa, Wakili Ngalo alisema kuwa mwaka 2009, mke wa Mbuya alitubu kwa mumewe kwamba siku moja mwanaume huyo akiwa kazini, yeye alizini na mtumishi huyo wa Mungu kwenye ndani ya nyumba yao.
Sehemu ya waraka huo ikasema kuwa, mke huyo aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kupata ugonjwa mbaya (tunausitiri) uliomsumbua kwa muda wa miaka mitatu ambapo katika kumwomba Mungu, aliisikia sauti ikimwambia ili apone lazima atubu dhambi ya uzinzi kwa mumewe.

MUME NA MKEWE WANAMKABILI MWANGIRA
Baada ya kusikia hayo, mlalamikiwa akiwa na mkewe walikwenda kumkabili mlalamikaji ofisini kwake ambapo walimkuta akiwa na mkewe.
Kwa mujibu wa wakili huyo, mke wa mlalamikiwa aliweka wazi uhusiano wake wa mapenzi na mtumishi huyo wa Mungu ambapo mke wa mlalamikaji naye akasema amewahi kusikia tetesi za kuwepo kwa uhusiano huo.
"Mke wa mlalamikiwa alimuomba radhi mke wa mlalamikaji ambapo alimsamehe lakini mlalamikaji hakujibu chochote," ilisema sehemu ya nyaraka ya Wakili Ngalo iliyopo mahakamani.
NINI KIINI CHA TATIZO?
Aidha, Mbuya alinukuliwa na wakili wake akidai kwamba kwa sababu walikuwa wakihudhuria hafla mbalimbali za maombi kanisani hapo na kutoa michango hiyo ndiyo ilikuwa kivutio cha Mwingira kumtembelea nyumbani kwake mara kwa mara na kutenda hayo.

KWANINI MUME ALIGHAIRI KUTOA KIWANJA?
Nyaraka hizo zimesema kuwa kutokana na Mbuya kugundua uhusiano huo usiofaa ambao mke wa mlalamikaji alikiri kuusikia, aliamua kufuta uamuzi wake wa awali wa kugawa ardhi aliyokusudia kumpa Mwingira na akaifahamisha Wizara ya Ardhi, mlalamikaji pamoja na mkewe (Mbuya).
Wakili Ngalo amesema Mbuya aliiomba mahakama hiyo kuitupilia mbali kesi hiyo na mlalamikaji aamuriwe kulipa fidia.

ANACHOTAKA NABII MWINGIRA
Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali za kimahakama (nakala tunazo), Mwingira alifungua kesi Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi Agosti 23, 2010 akiitaka itoe amri ya utekelezwaji wa kile alichokiita ‘mkataba wa ugawaji eneo.'
KUTOKA MHARIRI WA RISASI JUMAMOSI
Mhariri anaamini kuwa, mahakama itatenda haki kulingana na sheria kwani imekuwa ikifanya hivyo kila mara linapotokea tatizo lenye utata wa kisheria.

31.01.2012
KIONGOZI wa Kanisa la Efatha, Nabii na Mtume Josephat Mwingira amekamatwa na polisi katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam, akituhumiwa kuharibu mali za mfanyabiashara, Zain Sharifu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, ACP Charles Kenyela, Mwingira alikamatwa wiki iliyopita na kushikiliwa kituoni hapo.
Hata hivyo, Kenyela alisema, Mwingira alidhamiwa baada ya kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za kuvunja na kuharibu mali ndani ya Kiwanda cha Uchapaji cha Afroplus kinachomilikiwa na mlalamikaji.

"Tumemkamata kiongozi huyo ili atoe ufafanuzi wa kina baada ya kupokea malalamiko hayo, " alisema Kenyela alipozungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita ofisini kwake.
Kenyela alisema, mashtaka hayo yalifikishwa polisi na Zain, Januari 8, mwaka huu, akidai kwamba walinzi binafsi wa kiongozi huyo wa kanisa, walivamia kiwandani kwake na kuharibu mali baada ya kufanya fujo.

Aliongeza kuwa polisi baada ya kupata taarifa hizo, walikwenda eneo la tukio kushuhudia na kukuta mali zilizoharibiwa, hivyo walimtaka Mwingira kufika polisi ili atoe ufafanuzi lakini alikaidi ndipo polisi ikatumia nguvu kumkamata.

"Alipoulizwa Mwingira kuhusu madai hayo alijitetea uwa eneo hilo ni mali halali ya Efatha tangu Juni 17, 2005, baada ya kulinunua kutoka kwa mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Mangula, hivyo anasubiri tamko la Mahakama ya Ardhi Tanzania ambako shitaka limepelekwa," alisema.
Baada ya Mwingira kuhojiwa kituoni hapo, Kenyela aliwakutanisha na Zain ambaye ni mlalamikaji na kuwataka wasiendelee kugombana, badala yake wasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu kesi hiyo.
Kamanda Kenyela alifafanua kuwa mwanamke aliyemshitaki Mwingira ni mmoja wa wamiliki 11 wa viwanda vilivyokuwa ndani ya Kitalu namba 90, Mwenge, Dar es Salaam.

Awali, Mwingira alisema, aliwataka wamiliki wa viwanda hivyo kuhama ili kupisha upanuzi wa kanisa na viwanda 10 vilitekeleza ombo hilo.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa makampuni 10 ambayo yalitakiwa kuhama na Mwingira na kutekeleza ni Metal Works, Timber Malt Tech, Auto Ran Makongo, Container Global, Simon Engineering, Safe Man, Profession Investigation, Elbe Ltd, Zana za Kilimo Mbeya na Kilimanjaro Machine Tools Ltd.

Januari 17 mwaka huu, katika toleo lake namba 721 gazeti hili liliripoti kusakwa kwa Mwingira na askari 20 waliofika kanisani kwake kwa lengo la kumkamata.
Askari hao waliokuwa katika magari mawili aina ya Land Rover ‘Difenda' walifika kanisani kwa Mwingira baada ya kupata taarifa za kutokea kwa fujo kati ya wafuasi wa kanisa na wafanyakazi wa viwanda cha Afroplus kinachopakana na kanisa hilo, Mwenge, Dar lakini walimkosa.

Kamanda Kenyela alisema alimtuma mkuu wa polisi wa wilaya (OCD) kumpelekea Mwingira barua ya wito ili afike ofisini kwake na kutoa onyo kwamba kama akikaidi, wao polisi wasilaumiwe.
Baadhi ya wananchi waliokuwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay baada ya kumuona Mwingira walisema ni kitendo cha aibu kwa viongozi wa makanisa ya kiroho kufikishwa polisi.

"Siyo Mwingira tu, tumekuwa tukiona viongozi wengi wa makanisa ya kiroho wakifikishana polisi na watu au wao kwa wao, ningeshauri haya mambo wayamalize kwa kuelewana uraiani. Wana uwezo wa kuombea matatizo, hilo linawashinda nini? Zamani ilikuwa ni mwiko kuona kiongozi wa dini akifika polisi kulalamika au kulalamikiwa," alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Frida Gabriel aliyedai kuwa ni mlokole.
 
Bi Nuru Togwa(30) alikamwatwa na walinzi wa Nabii Mwingira baada ya kupita karibu na Shamba hilo na kupelekwa katika kambi yao na kukatwa Masikio yote mawili na kunajisiwa.

Bi Alesi Maarifa (77) naye alikamatwa na kuunguzwa na upanga wa moto sehemu za Siri na hadi leo matukio hayo yanaendelea:

Source: Gazeti ,Raia mwema ya Leo.

Tuesday, December 27, 2011

Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa,Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Mola, kweli haya yapo na hakuna wa kumchukulia hatua? Haki za binadamu hapa Tanzania zipo? Hebu kina TAMWA, na TNGP, na Mama Bisimba shughulikieni hili jambo. Halafu yule Engineer Mkuu wa Mkoa Manyanya alikuwepo juzi akishuluhisha or what na hakuna la maana lenye utekelezaji alililotamka zaidi ya kuacha tatizo kwa uongozi wa serikali ya kijiji ambao umeshindwa kutatua tatizo!!! Kweli engineer na Siasa!!! Hivi vigezo vya kuteuzi wa wakuu wa wilaya na mkoa vinazingatia nini?
 
hawa wachungaji wetu wa siku hizi! mali mbele tu. he is responsible kwa watu walio chini yake na unaweza kuta hao walinzi ni waumini wake pia
acheni ujinga, where is the connection between walinzi wa kifipa wanaolinda shamba la kanisa la efatha kule sumbawanga/rukwa na Mwingira? yeye alikuwepo wakati hayo yanatokea? any proof anyway?.....kama yeye alikuwa zake hapa dsm anahubiri walinzi wa shamba lake kule wakafanya hivyo sasa mbona mnaanza kumlaumu yeye utafikiri mwingine personally ndo alifanya hivyo?...na je? kuna ushahidi wowote? peleka polisi basi....na sidhani kama polisi wana urafiki wowote na mwingine kwasababu siku zote anagombanana nao hapo mwenge hadi walikamata wafuasi wake karibia hamsini na kuwaweka ndani kwa suala la kile kiwanja nje ya jengo lake.....kama mwingira amefanya makosa yeye binafsi ndo muongee kwa kumlaumu yeye na kanisa lake pengine, lakini kama watu binafsi vibarua wanaolinda shama lake wamefanya hivyo kama mna ushahidi basi kawalaumuni wale wale....kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe...unless una chuki binafsi na mwingine/efatha...
 
naona umeanza na kashfa, kiongozi wa dini anawajibika kuchagua watu makini katika kazi zake na pia mara nyingi wanakuwa watumishi wa kanisa lake.mfano rahisi ni shule za st. marys ambapo watumishi wengi ni waumini wake. na hii si mara ya kwanza kumkuta mwingira, kumbuka waumini wake walipovamia kile kiwanda walipokurupushwa na polisi wakakimbilia church wakajifanya wanasali, alipovunja nyumba za watu kule kerege kwa kutumia mabaunsa
 
Bi Nuru Togwa(30) alikamwatwa na walinzi wa Nabii Mwingira baada ya kupita karibu na Shamba hilo na kupelekwa katika kambi yao na kukatwa Masikio yote mawili na kunajisiwa.

Bi Alesi Maarifa (77) naye alikamatwa na kuunguzwa na upanga wa moto sehemu za Siri na hadi leo matukio hayo yanaendelea:

Source: Gazeti ,Raia mwema ya Leo.

[h=2]Tuesday, December 27, 2011[/h]

Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa,Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

mungu ibariki Tanzania
 
Wabongo kwa kufuata maneno ya magazeti hatujambo...especially vichwa vya habari....kuna maneno katika moja ya habari eti wameandika waumini wa kanisa la Efatha Foundation...hivi kweli kuna kanisa lenye hilo jina jamani!
 
Efatha Ministry muangalizi mkuu ni Apostle and Prophet J.E.Mwingira,
Efatha Bank ni chombo cha fedha chini ya hii huduma lakini kina bodi ya wadhamini (trustees) ambao ndio wafanya maamuzi.
Heritage Insurance ni chombo cha bima chini ya Efatha foundation
Heritage Farm, Sumbawanga ni moja ya miradi ya Efatha foundation kwenye kilimo.
Efatha seminary ni shule ya sekondari chini ya Efatha foundation.
EFATHA maana yake ni funguka.
 
duh! huyu jamaa inabidi afuatilie hao watu anao waajiri...
 
Bi Nuru Togwa(30) alikamwatwa na walinzi wa Nabii Mwingira baada ya kupita karibu na Shamba hilo na kupelekwa katika kambi yao na kukatwa Masikio yote mawili na kunajisiwa.

Bi Alesi Maarifa (77) naye alikamatwa na kuunguzwa na upanga wa moto sehemu za Siri na hadi leo matukio hayo yanaendelea:

Source: Gazeti ,Raia mwema ya Leo.

[h=2]Tuesday, December 27, 2011[/h]

Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa,Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Nafukua makaburi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom