Waziri wa Fedha, Mambo ya ndani, Waziri wa Kazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali msaidieni Rais kudhibiti wageni wanaoajiriwa bila vibali nchini

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,125
Nimefanya utafiti mdogo kuhusu Sababu za kuongezeka Kwa wageni wanaofanya kazi nchini kinyume cha sheria na mbinu za ukwepaji Kodi wanazotumia nikadhani sheria zetu ni rafiki Sana Kwa wafanyabiashara wakubwa kukwepa Kodi nchini.

Nimesoma sheria ya za Uhamiaji nikashtuka kubaini kwamba kampuni ya Dangote ikiajiri wageni kinyume cha sheria na wakakamatwa na polisi au magresheni mwajiri atalipa faini ya shillingi laki tano na kila mtuhumiwa atalipa shillingi laki tano.

Sheria hiyo upande wa vibali inasema mwajiri utawajibika kumlipia mgeni kibali cha shillingi dola elfu mbili (2000usd ) kufanya kazi nchini. Naomba Mawaziri wenye dhamana mtusaidie Watanzania, dola elfu mbili NI Sawa na milioni karibia tano, lakini endapo ntakwepa kulipa milioni tano nitalipa faini ya shillingi laki tano: do you think mwekezaji atakimbilia laki tano ay atalipa dola elfu mbili?

Nchi za wenzetu makampuni na waajiri wamewekeza adhabu kubwa za faini karibia mara hamsini ya kiasi cha compliance hili kuwafanya watii sheria Bila Shuruti. Kwetu tunashindwa nini kuboresha sheria zetu ziwabane wageni wanaoajiri wageni nchini?

Hali ipo hivyohivyo kwenye sheria inayosimamia ajira nchini na hata uwekezaji. Nataka kusema nini kwenu watunga Sera, fanyeni mapitio la eneo hili kuboresha kanuni na Sheria

1. Mhe. Waziri wa Fedha; eneo la kuishi kwenye nchi za ugenini Bila vibali linamomonyoa Sana uchumi WA nchi. Ntakupa mfano

Mgeni anayeishi Bila vibali; halipi Kodi za serikali, analipwa Mshahara usiolipiwa Kodi, Hana Makato yoyote ya serikali, mwajiri anatumia akaunti za nchini kwake kumwingizia fedha au kumlipa cash kumwezesha kuishi, anapokonya ajira za Watanzania wenye sifa na baya zaidi upo uwezekano fedha anazolipwa zikachepushwa na kufuel corruption au kufanya matendo ya jinai ikiwemo utakatishaji fedha

Kwa msingi huu nataka kuamini kwamba juhudi za Mhe. Rais zakuleta wageni nchini zinahujumiwa kwa kiasi kikubwa bila wasaidizi wake ninyi kujua mnamhujumu. Badilisheni sheria za kazi, Uhamiaji na uwekezaji ziwe rafiki Kwa wageni lakini zitoe adhabu Kali Kwa yeyote atakayebainika kuzikiuka ikiwemo waajiri na waajiriwa.

Mkiwabama waajiri watawekeza zaidi kutumia waajiriwa WA ndani na kama wataona IPO faida ya kuajiri wageni basi watafanya juhudi waajiri watu potential na wenye integrity. Sheria nzuri zitapunguza Sana watendaji wa serikali kutengeneza mianya ya rushwa na kwenda kusumbua wageni kwenye makampuni bila intelligent yakutosha.

2. Waziri wa kazi na Waziri wa Magresheni; msiposimamia taasisi zinazodhibiti wageni zikawa na mifumo ya taarifa kila penye kiwanda au taasisi inayoajiri wageni mnamhujumu Mhe Rais. Msipoweka vitendea kazi na incentive kwenye eneo la kukabiliana na wageni wasiotaka kulipa Kodi na Tozo za serikali mtakuwa mnafanya hujuma Kwa Mhe.rais. Lakini pia msipoweka adhabu Kali Kwa waajiri wanaokwepa kulipia vibali bado hujuma Kwa serikali itakuwa wazi. Someni sheria ya NEMC mtaona namna ambavyo kutiririsha maji machafu kunaweza kuathiri kiwanda na wakati mwingine kufungwa. Kama NEMC wanatambua madhara ya uchafu kwanini ninyi msitambue madhara ya kuajiri wageni Bila vibali?

Katika utafiti wangu mdogo nimebaini pia kuwa; Viongozi wa Tanzania mmekuwa na Tabia ya kuwaaddhibu Sana Watanzania, kuwatengenezea by laws mbovu Watanzania lakini siyo wageni.

Naomba niwakumbushe kwamba Mh. Rais anapowaleta wageni nchini Hana miujiza yakuwafanya wageni hao wachangie pato la Taifa. Anategemea wafike wafuate sheria na kupitia ufuataji wa sheria basi nchi ikusanye Kodi na mapato mengine. Mnasubiri Hadi Mhe. Rais aje awaambie kwamba sheria za nchi zinavutia Uhamiaji usiofuata sheria?

Lakini pia wenzetu mnaodhibiti fedha haramu, mnadhibiti vipi fedha haramu Kwa hawa watu wasiotaka kufuata sheria? Suala la fedha haramu na utakatishaji fedha linatumika Sana Duniani kufadhili Uhalifu; nimeweka mazingira yakuziona fedha zinazochepushwa Kwa kukosekana sheria madhubuti? Potential investors kwanini wawe wahifadhi wakuu wa Wilaya wageni wasio na sifa?

Mapendekezo ya kisera kwenu
1. Sheria zote zinazosimamia ajira ya wageni nchini zipitiwe upya na kuwekewa masharti au vifungu vinavyosaidia kupambana na fedha haramu, money laundering na pia kumpa adhabu kali mwajiri atakayebainika kuajiri wageni kinyume cha sheria. Minimum kama wapo wawekezaji wakubwa basi watozwe hata bilioni moja itasiadia Sana kuwa na wawekezaji wanaoheshimu sheria lakini wanaoheshimu utu.

2. Serikali iboreshe mindset za maafisa wanaotoa huduma katika eneo hili. Nchi za wenzetu ukisikia kiwanda kinakaguliwa na watumishi wa serikali tayari wanakua Wana taarifa hivyo wakija ndani ya muda mfupi wanachukua wavunja sheria wanachama shughuli zinaendelea. Kwetu huku tunatumia zaidi mabavu kuliko akili. Kulinda uwekezaji mkubwa uliowekwa na endapo sheria itakuwa inatoa adhabu Kali basi hatutategemea ukaguzi kila siku kwenye makampuni.

3. Angalieni namna yakuwekeza kwenye technology ambapo mgeni akiwa nchini anajulikana alipo na siku akitaka kutoka nchini kwenye mpaka wowote wanaotoa huduma wakibaini alikwepa sheria wanamkamata na kumfikisha kwenye dola. Wageni awatakaa nchini kizembe Kwa Sababu wanajua watakataliwa kutoka.

4. Punguzeni waajiri vibarua wanaoomba vibali vya muda mfupi. Nchi nyingi ukienda Kwa agenda ya kufanya KAZI Kwa muda mfupi unafanya unaondoka. Hapa kwetu watu wengi anafanya kazi holela tu hakuna anayeangalia mgeni amekaa muda gani akidhurura. Hapa taasisi zinazohusika zizibitiwe

5. Taratibu za mgeni kufanya kazi au kupata kibali ziboreshwe. Urasimu mara nyingi uchangua wageni kuishi Bila vibali. Tutoe vibali Kwa muda mfupi na asiyestahili ajulishwe na aisimamiwe aondoke nchini

6. Mgeni akivunja sheria za magresheni asiruhusiwe kuingia tena nchini Kwa kipindi flani kama tulivyofurumishwa south. Miaka mitano hakuna kuingia nchini na hapo umepigwa faini, mwajiri ametoka bilioni imeenda kununua madawa nk

MKifanya haya mtasiadia mambo yafuatayo;
1. Waajiri wanategemewa kuheshimu sheria

2. Waajiri wataajiri watu makini na wengi Watakuwa Watanzania

3. Tutaondokana na ajira za vibarua Kwa wageni badala yake ajira nyingi za vibarua zitafanywa na Watanzania na hivyo kupunguza changamoto ya ajira.

4. Waajiriwa sekta binafsi Watakuwa na nidhamu ya KAZI.

5. Tutaondoa makanjanja na kuweka watu makini eneo la utoaji huduma Kwa wageni.

6. Wadhibiti utakatishaji fedha watapata taarifa sahihi

7. Kodi na mapato ya serikali yataongezeka.

8. Tutapunguza wimbi la wahamiaji wasio na sifa nchini.

9. Usalama utaimarika Kwa Sababu kupitia mifumo tutakuwa tunafahamiana.

10. Wageni kutoka nchi jirani watadhibitiwa Kwa Sababu soko la ndani litatumika zaidi

Naomba kutoa mchango wangu kumsaidia Mhe. Rais katika eneo la kuvutia wageni lakini pia kuwadhibiti wasiwe chanzo cha Uhalifu kama inavyotokea south Afrika.

Wenye dhamana msiwaonee huruma waajiri lieni nao; hakuna generosity kwenye mtiguano WA kiuchumi. Ukarimu wetu hautajenga shule wala zahanati; ukarimu wetu wa kijamaa tusipouondoa kwenye mindset tutazidi kuwaumiza Watanzania na kuwapa wageni.

Natamani ningekuwa mshauri WA kiuchumi WA Mhe Rais.......simple issues zinafanya mengi kuliko big issue. Ulaya potential business man and women together with investors wamebanwa hapa, nchi zinafanya vyema....FBI wanapata data na kuzotumia kufanya policy reform. Trump alikuwa na Sera ya Uhamiaji ilitibgisha Dunia, natamani kuziona sheria tamu za kudhibiti wageni zisizoweka urasimu WA huduma tutakimbia kiuchumi.

NAKALA
MHE. RAIS
 
Back
Top Bottom