Wanamuziki wa extra musica

Wanamuziki wa extra musica

Nikweli kabisa Abilissi kisauti alifanana sana na christian,sawa na Herman Ngassaki manu manu don mfumu alivyofanana kisauti na Guy guy fall. Na nadhani hii hufanywa makusudi ili kutopoteza identity ya kundi especially wanapotaka kupiga nyimbo za zamani.Lakini bado hujasema Abilisi wapi habari zake zilipo?

Awali nilidhan abilissi ameongozana na oxy oxygen ktk kundi la universal zangul lakn simwoni wala hata kusikia sauti ake.

Nahisi atakuwa kapotea ktk mziki kabisa coz simsikii.


Sikiliza kibao cha Fred Nelson.... uone vijana wanamuonesha kama ni msaliti wa ndoa yake na penzi kubaki ni kwenye simu tu..... huyo mwanaume amekuwa malaya hadi anaasi ndoa yake.
..
Nakipenda sana kibao hiki
 
Roga roga..... sikiliza kibao cha AMIE DETRESSE cha z1 international album ya super helico utamsikia Christian ambe vema sana nenda YouTube upate radha
 
Awali nilidhan abilissi ameongozana na oxy oxygen ktk kundi la universal zangul lakn simwoni wala hata kusikia sauti ake.

Nahisi atakuwa kapotea ktk mziki kabisa coz simsikii.


Sikiliza kibao cha Fred Nelson.... uone vijana wanamuonesha kama ni msaliti wa ndoa yake na penzi kubaki ni kwenye simu tu..... huyo mwanaume amekuwa malaya hadi anaasi ndoa yake.
..
Nakipenda sana kibao hiki

Abilissi aliondoka Extra Musica kabla albam ya Shalai haijakamilika. Ukiifuatilia vizuri albamu hii anasikika vizuri katika nyimbo mbili shalai na Tumemanquse ambayo alitunga yeye, kuondoka kwake kulipelekea hata wimbo wake ushindwe kufanyiwa shooting na ukichukua albam ya shalai upande wa video,wimbo wake wa tumemanguse haupo,na yeye anaonekana tu katika wimbo wa shalai. Lakini upande wa Oxygene ameondoka baada ya albam mbili zaidi tangu itoke shalai,maana yake alikuwemo kwenye Trop c'est trop na Obligatoire.
 
Kundi hili lilianza miaka ya 1990's hivi wakati huo lilikuwa likipiga ktk kumbi za starehe nchini Congo Brazzaville kwa kurudia nyimbo za wakongwe kama akina tabu ley, Franco etc

Ieleweke kuwa lilikuwa na waanzilishi kama ulivotaja yaan hao wawili ambao ndyo walotafuta wenzao wenye vipaji.

Alikuwa ni gii gii falley in French, English anaitwa Guy guy fall alotoa wazo la kulifanya kundi hilo liachane na upigaji wa kumbi za starehe.

Mwaka 1993 walotoa album hyo kweli... jambo lililowastua wakongwe wa muziki congo kuwa hawa vijana si wao bali wanaiba kaz za watu na hasa wenge musica ndo walishutumu sana kund hili...

Vijana hawa hawakukatishwa moyo wakaja na album ya pili.. confirmation...
Kuuthibitishia ulimwengu na ndpo hapa walipa heshima kubwa sana nchini mwao na baran Africa kiujumla na ulimwengu wote.

Ieleweke kuwa ktk album ya kwanza ilipotoka kulitokea msuguano wa madaraka kati ya roga na guy kuwa nan aongoze kundi hlo... jambo hili lilipelekea guy kuonwa kma mwenye uchu wa madaraka ilihali amewakuta humo wakingwe wa kund...

Ukisikiliza album ya pili ni kama Guy fall hasikiki na Christian ambe lakn ukiwa makini utawaskia hapa wawili hawa hawakupewa nafas kubwa sana na pia kunaskika sauti ya doudou copa kwa sana aloletwa kundin na guy akitokea Roman Catholic kma mwanakwaya.

Ni baada ya msuguano huo Guy fall alikuwa wa kwanza kuondoka na kuwa solo artist... baadae waliuata watu watatu akiwemo dullel loemba, Christian ambe na Quentin moyasco sambamba na waimbaji wengne walokuwa benchi toka kwa roga.

Wakali hawa watatu walitoka na album ya super helico ambayo pamoja na ubora mzur ilivuma kidogo sana baadaya hapo walikwazana kimaslahi na alikuwa dullel na cChristian walotoka na kuunda Z1 international extra musica ikipewa jina la ERE D'E VERITE -Wakimshutumu Quentin kuwa si mkweli... neno hlo hapo juu lina maana ya yeye si mkweli...

Na baadae Quentin hakujibu mapigo zaid aliwambia MERCE -akiimaanisha asanten kwa shutuma zenu.

Christian ambe hajafa kimzk ndo kiongoz wa kund la Z1 huko anaitwa papa lutumba akiwa na dullel ambaye pia hukodiwa wakati mwingn na Quentin kpiga rythm gitaa.

kaka bado sijakubaliana na wewe namna hawa wakali watatu walivyoondoka. Baada ya confirmation albam, christian na guy guy fall walijitoa Extra musica. Ukisikiliza albamu iliyofuata ya oragan, waimbaji ni watano tu yaani Moyascko,Oxygene, Abilissi, Doudou copa na Herman Ngassacky. Huku upande wa gitaa yupo Roga roga(solo), espe bass(bass) na durell loemba(rhythm). Drummer ni Ramatoulaye,keyboard ni kingstal,wengine ni pinochet thiery,anaurd laguna,regis touba na cyrill malango japo hawa walikuwa hawapewi nafasi sana yakuonesha mavitu yao. Sasa kwa list hiyo hapo juu ni vp useme christian,durell na moyascko walitoka pamoja wakati christian hata albamu ya oragun hakushiriki?? Nikweli katika super helico ya extra musica international walikuwa pamoja.
 
Amabilis..... Jamaa ana sauti kali sana,mtunzi wa ngoma ya Plus Tard.....one of my favourite song katika album ya Etat Major!! Ila we jamaa uliyeleta uzi huu shikamooooo......
 
Roga roga..... king kistere amefariki jana saa kumi na moja asubuhi ya tarehe 13 February 2014
 
Ulosema ni kweli kabisa... lakn ukifuatilia videos zao Christian ni kama huwa ni mtu wa kujiskia sana cjajua ilikuwaje hadi hakusikika na cjui nn kilimkuta jamaa huyu..
 
Ulosema ni kweli kabisa... lakn ukifuatilia videos zao Christian ni kama huwa ni mtu wa kujiskia sana cjajua ilikuwaje hadi hakusikika na cjui nn kilimkuta jamaa huyu..

Lakini kwanini wengi wao hawajafanya vizuri baada ya kutoka? Ukitazama christian na guy guy fall walikuwa lulu sana na tungetarajia wangetisha zaidi kuliko bendi waliyotokea kinyume chake hawajafanya vizuri tofauti na bendi waliyotokea ilizidi kuimalika, hata alipotoka moyacko na durell bendi ilisimama na kutoa albamu bora kama shalai na etat major huku wao wakitoa nyimbo za kawaida sana tofauti na uwezo wao waliouonesha wakiwa extra musica. Au roga roga ndiye aliyeibeba bendi tofauti na waliokuwa wanatoka katika bendi?
 
Hiyo iko waz sana kuwa Roga ni fundi sana pale kundin ..anauwezo mzur wa kutunga, kupangilia sauti, mashair na mtiririko wake ukweli n fund sana hapana ubish
 
Shukran wadau kwa kutukumbusha mbalikidogo enzi za unjuka, mimi ni mpenzi sana wa boringo za congo kama kuna mwenye historia za Wenge, Coffie na Pepe kalle mtupe uhondo jamani kama wa Zuberi Msabaha.
 
Shukran wadau kwa kutukumbusha mbalikidogo enzi za unjuka, mimi ni mpenzi sana wa boringo za congo kama kuna mwenye historia za Wenge, Coffie na Pepe kalle mtupe uhondo jamani kama wa Zuberi Msabaha.
obwato...... merce...hujawa muwaz zaid unataka history ya wasanii hawa au tafsiri ya nyimbo zao...

Pamoja sana d'e la Congolese
 
obwato...... merce...hujawa muwaz zaid unataka history ya wasanii hawa au tafsiri ya nyimbo zao...

Pamoja sana d'e la Congolese

Mie nadhani njoo na tafsiri kabisa na tuanze na wimbo matongi, Angela, kende,Denide, inondation then racine
 
Ntakuja na tafsiri sahh kabisa wadau punde kaeni chonjo
 
Nitawaletea tafsiri ya wimbo 100 kilos wa ferre golla na maze wa tabuley
 
Back
Top Bottom