Wanamuziki wa extra musica

Wanamuziki wa extra musica

nawakubali sana kuliko bendi yoyote ile duniani mpaka sasa,ya pili ni wenge mesomere ya werason ngiama makanda

Uko sahihi tu mkuu kwa vile hukuwahi kuwajua Wenge BCBG kabla hawajatengana Werason,JB Mpiana,Allain Makaba na wengine ilikuwa balaa na mimi binafsi nasema sijawahi kusikia tena kama hao jamaa

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Anaitwa Roberto Wuunda Ekokota...
Haya sahihisha hilo jina lako kabla sijarudi

Hata na Wewe pia Umekosea Anaitwa Roberto Wunda Enkokota au WABINTUNGA WAJINERO ambae Alikuwa ndiyo Repa au ATALAKU Kwa Kilingala au ANIMATEUR Kwa Kifaransa na Aliacha Kughani ( KUREPU ) Mara baada tu Ya Kutoa Album Yao Ya PENTAGONE baada Ya Kujulikana Akisumbuliwa na Tatizo La Kansa Ya Koo. Ukitaka Mengine Uliza tu Kwani GENTAMYCINE na MIZIKI Ya Congo DRC ni Kama Vile Samaki na Maji au Chupa na Kizibo. Karibu!
 
Habari wanajamii,napenda kuulzg maswal yafuatayo; kila mbongo wa extra musica yu wapi sasa bend hyo maendeleo yake yakoje na huyu ramatoulay ndo yule aliyeimba ule wimbo wa alaj maana majina yao na saut vinanichanganya sana.
Naomba msaada wenu wadau

Kila Mbongo Aliamua Kuacha Muziki na Kujikita Zaidi na Biashara na Kutengeneza Matangazo Nchini Ufaransa na Ubelgiji baada Ya Kundi Zima La Extra Musica BPBL ( Bon Pied Bon Look ) ikimaanisha Wajuao Kuvaa na Wenye Mwonekano Mzuri Lilipogawanyika baada Ya Mvurugano Kati Ya Manguli Wawili Ibambi Ikombi au Wengi Mnamjua Kama Roga Roga La Liberateur na Abilisi ambapo Wakagawanyika na Pakawa na Extra Musica Zangul chini Yake Roga Roga na Extra Musica Internationale chini Yake Abilisi ila hadi Sasa Extra Musica Ya Roga Roga ndiyo Inatamba Sana Kwani Ilibaki na Watu Muhimu Sana ktk Bendi Kama Mpiga Drums Maarufu na Anayetisha Aitwae Ramatoulaye Diabate na Mpiga Solo Akiwa Mwenyewe Gwiji Roga Roga na ktk Mpini wa Bass Akiwa Mwenyewe Espa Bass na Kwa Mliokuwa Mkidhani Kuwa Labda Kuondoka Kwa Kila Mbongo au ( Mazikou Ghislain ) ktk Upande wa Kughani au Kurepu Mlikosea Mno Kwani Alikuja Mtu Mwingine Hatari Kwa Kurepu Aitwae ARAFATE WANYA na Ukitaka Usikie Shughuli Yake Fuatilia Albam Yao Ya Trose Trop Utaijua Habari Yake na Sasa hivi Kimeongezeka Kingine ktk Kurepu Kinaitwa ZAPARRO DEGAIRE ni Hatari Tupu na Wana Album Yao Mpya Iitwayo KINDOKI Ikiimanisha UCHAWI au NDUMBA. Kila la Kheri!
 
Extra Musica ni kundi la muziki linalotoka katika nchi ya Congo Brazzaville. kundi hili lilianzishwa mwaka 1993 na wanamziki walioanzisha kundi hili ni Roga Roga na Espe Bass. Pamoja nakuanzishwa mwaka huo 1993, walifanikiwa kutoa albamu yao ya kwanza mwaka 1995 iliyoitwa Les Nouveaux Missiles. Albamu zingine ni Confirmation (1996), Ouragan 1997(Champions d’ Afrique), Etat-Major (1998) , Shalai (1999), Trop C’est trop(2001), Obligatoire(2004), La main noire(2006), Sorcellerie (Kindoki)-2011. Wanamziki waliokuwepo tangu albamu ya kwanza ni
Ø Waimbaji ; Guy Guy Fall, Quentin Moyascko, Oxygene (Mbon Sylvain), Dou dou copa (Elenga Laka Bienvenu Dominique), Christian na Herman Ngassaki (Don Mfumu).
Ø Atalaku ; Kila Mbongo
Ø Gitaa la solo; Roga Roga (Ibambi Okambi Rogatien)
Ø Gitaa la base; Espe Base
Ø Gitaa la Rhymes ; Durell Loemba
Ø Drummer; Ramatoulaye (Ngolali G)
Ø Keyboard & Horns; Christian Kingstall

Wanamziki wengine wa kundi hilo wa mwanzo walikuwa Pinochet Thierry, Regis Touba, Cyrille Malonga na Arnaud Laguna. Albamu ya kwanza Herman Ngassaki na Dou dou Copa hawakupata nafasi kubwa sana ya kuimba kutokana na uwepo wa mtu kama Guy Guy Fall, Oxygene, Christian na Quentin Moyascko katika safu ya waimbaji.

Baada ya kufanya vizuri sana albamu yao ya kwanza Mwanamziki Abilissi (Samba Brice) alijiunga na Extra Musica hivyo naye kuwemo katika safu ya waimbaji ya Extra Musica walipotoa albamu yao ya pili ya Confirmation. Ujio wake ulifanya jumla ya wanamziki saba kuwa katika safu ya uimbaji wa Extra Musica ambao ni Guy Guy Fall, Dou Dou Copa, Christian, Oxygene, Herman Ngassacky, Abilissi na Quentin Moyascko. Safu hii ilifanya albamu yao ya pili kuwa moto kuliko ya awali na hivyo kuteka hisia toka sehemu mbalimbali Afrika na duniani kote huku ikichombezwa na atalaku za Kila Mbongo na gitaa la Roga Roga.

Baada ya kufanya vizuri sana albamu yao ya pili, mgogoro wa kimaslahi na kiuongozi ulilikumba kundi hili na kupelekea wanamziki kama Christian na Guy Guy Fall kujitoa na kutokuwepo kwenye albamu ya tatu ya kundi hili. Nafasi zao zilijazwa vyema na Herman Ngassaki aliyechukua nafasi ya Guy Guy Fall na Abilissi aliyechukua nafasi ya Christian na huwezi sikia kutajwa kwa Guy Guy Fall na Christian albamu ya Oargun. Herman Ngassaki alifanikiwa sana kuitumia sauti ya Guy Guy Fall katika album zote ambazo Guy Guy Fall na ukitaka ujue jinsi wanavyofanana kisauti sikiliza wimbo wa Success Extra anavyoanza Guy Guy Fall na usikilize wimbo wa Lolango katika album ya Oaragan namna anavyoanza Herman Ngassaki, usipokuwa makini unaweza jua ni mtu mmoja kumbe sio.

Pamoja na kukimbiwa na waimbaji hao wawili bado kundi lilbaki imara sana na kufanikwa kutoa albamu yao ya tatu huku Guy Guy Fall akienda kufanya kazi kama mwanamziki wa kujitegemea(solo Artist) na mpaka leo yupo kivyake na habari za Christian kimziki kuishia hapo.

Lakini pamoja na kutoa albamu hii ya tatu, kundi liliingia tena kwenye mgogoro mkubwa na kusababisha wanamziki wapatao sita kuondoka na kwenda kuunda kundi la Extra Musica International. Wanamziki hao ni Pinochet Thierry, Regis Touba, Cyrille Malonga, Durell Loemba ,Quentin Moyascko na Arnaud Laguna. Huko nako baadae Extra Musica International iligawanyika na kundi la ZI International kuundwa chini ya uongozi wa
Durell Loemba, Pinochet Thierry, Regis Touba na Cyrille Malonga, huku Extra Musica International ikibakiwa na Quentin Moyascko na Arnaud Laguna.

Baada ya kukimbiwa na wanamziki hawa Extra musica chini ya uongozi wa Roga Roga walijipanga na Ku-recruit wanamziki wapya kama Sonor aliyechukua nafasi ya Durell Loemba katika gitaa, Gildas Pozzi na Emery Mbona wakisimama katika Tumbas. Safu ya uimbaji ikabakiwa na wanamziki wanne tu ambao ni Oxygene, Herman Ngassaki, Dou Dou Copa na Abilissi. Atalaku ikiongozwa na Kila Mbongo huku kwenye drummer akisimama Ramatoulaye, keyboard kama kawaida ni Christian Kingstall, Gitaa la base Espe Bass na la Solo ni Roga Roga na kufanikiwa kutoa albamu ya nne iitwayo Etat-Major ambayo inaaminika kuwa ni albamu bora ya kundi hili. Albamu hii sio tu ilivunja rekodi ya mauzo ya kundi hili bali pia iliwafanya kupata mialiko mbalimbali ya kimataifa ikiwepo Tanzania. Pia album hii iliwafanya kuchukua tuzo nyingi Afrika ikiwepo tuzo ya Kora kama kundi bora la mziki kwa Afrika.

Baadae walitoa albamu yao ya tano iliyokuja kujulikana kama Shalai na ndiyo ilikuwa albamu ya mwisho kwa Rapa wa muda mrefu wa kundi hili Kila Mbongo baada ya kujiengua na kundi hili na kuchana na mziki. Pia ilikuwa ni albamu ya mwisho kwa Abilissi. Pia katika albamu hii wanamziki kama Papy Batin Maboulango na Boudouin Massipi walishiriki baada ya kujiunga na kundi hili kwa mara ya kwanza.

Kimya kidogo kilipita kabla ya kutoa albamu ya sita ya kundi hili iitwayo Trop c’est trop huku rapa akiwa ni mpya baada ya Kila Mbongo kuacha muziki. Rapa huyu mpya aliitwa Arafat.
Baada ya albamu hii ya sita ya, kundi hili lilibadili jina na kuwa Extra Musica Zangul.

Mwaka 2004 wakafanikiwa kutoa albamu yao ya saba iitwayo Obligatoire. Mwaka huohuo baada ya kutoka albamu hii Dou Dou Copa Alijitoa na kuwa mwanmziki anayejitegemea (solo Artist) na Oxygene alijitoa mwaka 2005 na kuunda kundi lake la Universal Zangul huku akiondoka na baadhi ya wanamziki ambao walikuwa hawapati nafasi ya kuimba katika Extra Musica Zangul.
Pamoja na kuondoka Oxygene na Dou Dou Copa bado kundi hili lilitoa albamu yao ya nane mwaka 2006 iitwayo La Main Noire na albamu ya tisa ambayo nikama ya Roga Roga iitwayo Sorcellirie(Kindoki) na imetoka mwaka 2011.

Kwasasa kundi lipo kisasa zaidi na linapiga Rhumba ya kisasa zaidi huku rapa wake ni Zaparo. Wanamziki wa awali waliopo mpaka leo ni Roga Roga,Espe Bass, Ramatoulaye na Herman Ngassaki. Pia kwa habari zisizoaminika ni kuwa Rapa wao wa zaman Kila Mbongo naye amerudi kundini. Mwaka jana 2013 HermanNgassaki alitoa nyimbo kadhaa kama solo artist lakini bado yupo na kundi hili. Wasiomjua Herman Ngassaki waangalie wimbo Etat-Major mwishoni anavyokata mauno.

Zifuatazo ni Albamu za Extra Musica na nyimbo katika albamu hizo tukianza na albamu ya kwanza mpaka ya mwisho.

v 1995 Album Les Nouveaux Missiles
- Amie reviens (Duller Loemba)
- Chagrin plus plus (Pinochet Thierry)
- Detresse
- Dieu L'eternel (Roga Roga)
- Freddy nelson (Quentin Moyasko)
- Na Ko Bala Yo Na Ko
cd1.jpg
v 1996 Album Confirmation
- Success Extra
- Inondation
- Angela
- Ziya
- Denide
- Etape
- Kende
- Love in love
ib421464.jpg

v 1997 Album Ouragan
- Losambo
- Melenge (Roga Roga)
- M'ere S (Duller Loemba
- Panique totale (Quintin Moyascko)
- Reconnaissance (Espe Bass)
- Lolango (Duller Loemba)
- Hommage (Roga roga)
- Generation Mechante (Oxygene)
51+khU0m-ZL._SY300_.jpg

v 1998 Album Etat-Major
- Etat-major
- Raccine (Roga Roga)
- Patience (Kila mbongo)
- Vertige D'amour (Ramatoulaye)
- Villegiature
- Plus tard(Abillisi)
- La plule (Roga Roga)
- Ecart (Dou Dou)
- Cri Du Coeur (Oxygene)
3138.jpg

v 1999 Album Shalai
- Aministe Shalai
- Matongi
- A vous de voir
- Complainte
- Horizon 2000
- Laissez passer
- Ndzima
- Sissi limperatrice
- Solitude
- Tu me manques(Abillisi)
- Zineba
EXTRA_MUSICA_Shalai-worldzik.jpg
v 2001 Album Trop C’est Trop
- Trop c’est trop
- Gambala
- Zangul Zangul
- Moselekete
- N’julie
- Guivano
- Papato
- Polemique generale
- Probleme sur problem
- 12 Balles
- Zongi Sanga
- Bikisa Nga’ (chez Ntenda)
- Kared Amour
4907.jpg
v 2004 Album Obligaitore
- Obligaitore
- Honorablement
- Epaka
- Racini II
- Gyrophare
- Aigle Impérial
- Rufin Bouka (Oxygene)
- Radoutable
- Boss chez Trimba
- Foundation Muller
- L’oublier
- Honorablement
3246.jpg
v 2006 La Main noire
- La main noire
- Racine III
- Rosalain
- 72 minutes de silence
- Mban-Antoine
- Eternite d,amour (Espe Bass)
- Magomboro
- Noces de bois(Roga roga)
- Parfum mondial
- Petit mais costaud
- Mack Serge
EXTRA-MUSICA_LaMainNoire.jpg
v 2011 Sorcellerie (Kindoki )
- Sorcellerie
- Kindoki
- La sape
- Le meilleur
- Marriage
- Les gouts et les couleurs
- Congo United
- Brice Anga Golo
- Flo Miokono(Roga roga)
- Jules Maswa
- Gael Bitoma
- Racine IV
- Gaetan Kodia
- Supreme
- Musicien
- Vrai PDG
- Rosalin
b0298b5d.jpg

africa.jpg cat918.jpg cd4.jpg Roga-Roga_chez_Zaiko_640.jpg QuentinMoyascko3.jpg 0-1.jpg mq1.jpg 0.jpg 51767_142091439170839_100001099525145_214667_6021172_o.jpg Extra_Musica_Concert_1.JPG 2126621-2962337.jpg Guyguy_Fall_extra_musica_nouvel_album_NDOKI_ZOBA_deja_dans_bacs.jpg alloco-party-660x320.jpg 220px-Doudou_Copa.jpg

View attachment Extra Musica ni kundi la muziki linalotokea katika nchi ya Congo Brazzaville.docx
Sehemu ya pili itahusu nini wanafanya Extra Musica International, ZI International, Universal Zangul, Dou Dou Copa na Guy Guy Fall.
More information & Contacts ................Bislisk@yahoo.com
 
Ntakutafta tuweke sawa mambo hapa kuna sehem unapotosha mambo jitokeze hapa mi ni mfuas mkubwa wa makund haya ya extra musicians..... reference; Raphael kubona gmail. Com
 
Last edited by a moderator:

karibu sana,unaweza weka hapa jamvini huo upotoshaji ili tuujue vizuri, napatikana kupitia bislisk@yahoo.com
 
Last edited by a moderator:
Extra Musica ni kundi la muziki linalotoka katika nchi ya Congo Brazzaville. kundi hili lilianzishwa mwaka 1993 na wanamziki walioanzisha kundi hili ni Roga Roga na Espe Bass. Pamoja nakuanzishwa mwaka huo 1993, walifanikiwa kutoa albamu yao ya kwanza mwaka 1995 iliyoitwa Les Nouveaux Missiles. Albamu zingine ni Confirmation (1996), Ouragan 1997(Champions d' Afrique), Etat-Major (1998) , Shalai (1999), Trop C'est trop(2001), Obligatoire(2004), La main noire(2006), Sorcellerie (Kindoki)-2011. Wanamziki waliokuwepo tangu albamu ya kwanza ni
Ø Waimbaji ; Guy Guy Fall, Quentin Moyascko, Oxygene (Mbon Sylvain), Dou dou copa (Elenga Laka Bienvenu Dominique), Christian na Herman Ngassaki (Don Mfumu).
Ø Atalaku ; Kila Mbongo
Ø Gitaa la solo; Roga Roga (Ibambi Okambi Rogatien)
Ø Gitaa la base; Espe Base
Ø Gitaa la Rhymes ; Durell Loemba
Ø Drummer; Ramatoulaye (Ngolali G)
Ø Keyboard & Horns; Christian Kingstall

Wanamziki wengine wa kundi hilo wa mwanzo walikuwa Pinochet Thierry, Regis Touba, Cyrille Malonga na Arnaud Laguna. Albamu ya kwanza Herman Ngassaki na Dou dou Copa hawakupata nafasi kubwa sana ya kuimba kutokana na uwepo wa mtu kama Guy Guy Fall, Oxygene, Christian na Quentin Moyascko katika safu ya waimbaji.

Baada ya kufanya vizuri sana albamu yao ya kwanza Mwanamziki Abilissi (Samba Brice) alijiunga na Extra Musica hivyo naye kuwemo katika safu ya waimbaji ya Extra Musica walipotoa albamu yao ya pili ya Confirmation. Ujio wake ulifanya jumla ya wanamziki saba kuwa katika safu ya uimbaji wa Extra Musica ambao ni Guy Guy Fall, Dou Dou Copa, Christian, Oxygene, Herman Ngassacky, Abilissi na Quentin Moyascko. Safu hii ilifanya albamu yao ya pili kuwa moto kuliko ya awali na hivyo kuteka hisia toka sehemu mbalimbali Afrika na duniani kote huku ikichombezwa na atalaku za Kila Mbongo na gitaa la Roga Roga.

Baada ya kufanya vizuri sana albamu yao ya pili, mgogoro wa kimaslahi na kiuongozi ulilikumba kundi hili na kupelekea wanamziki kama Christian na Guy Guy Fall kujitoa na kutokuwepo kwenye albamu ya tatu ya kundi hili. Nafasi zao zilijazwa vyema na Herman Ngassaki aliyechukua nafasi ya Guy Guy Fall na Abilissi aliyechukua nafasi ya Christian na huwezi sikia kutajwa kwa Guy Guy Fall na Christian albamu ya Oargun. Herman Ngassaki alifanikiwa sana kuitumia sauti ya Guy Guy Fall katika album zote ambazo Guy Guy Fall na ukitaka ujue jinsi wanavyofanana kisauti sikiliza wimbo wa Success Extra anavyoanza Guy Guy Fall na usikilize wimbo wa Lolango katika album ya Oaragan namna anavyoanza Herman Ngassaki, usipokuwa makini unaweza jua ni mtu mmoja kumbe sio.

Pamoja na kukimbiwa na waimbaji hao wawili bado kundi lilbaki imara sana na kufanikwa kutoa albamu yao ya tatu huku Guy Guy Fall akienda kufanya kazi kama mwanamziki wa kujitegemea(solo Artist) na mpaka leo yupo kivyake na habari za Christian kimziki kuishia hapo.

Lakini pamoja na kutoa albamu hii ya tatu, kundi liliingia tena kwenye mgogoro mkubwa na kusababisha wanamziki wapatao sita kuondoka na kwenda kuunda kundi la Extra Musica International. Wanamziki hao ni Pinochet Thierry, Regis Touba, Cyrille Malonga, Durell Loemba ,Quentin Moyascko na Arnaud Laguna. Huko nako baadae Extra Musica International iligawanyika na kundi la ZI International kuundwa chini ya uongozi wa
Durell Loemba, Pinochet Thierry, Regis Touba na Cyrille Malonga, huku Extra Musica International ikibakiwa na Quentin Moyascko na Arnaud Laguna.

Baada ya kukimbiwa na wanamziki hawa Extra musica chini ya uongozi wa Roga Roga walijipanga na Ku-recruit wanamziki wapya kama Sonor aliyechukua nafasi ya Durell Loemba katika gitaa, Gildas Pozzi na Emery Mbona wakisimama katika Tumbas. Safu ya uimbaji ikabakiwa na wanamziki wanne tu ambao ni Oxygene, Herman Ngassaki, Dou Dou Copa na Abilissi. Atalaku ikiongozwa na Kila Mbongo huku kwenye drummer akisimama Ramatoulaye, keyboard kama kawaida ni Christian Kingstall, Gitaa la base Espe Bass na la Solo ni Roga Roga na kufanikiwa kutoa albamu ya nne iitwayo Etat-Major ambayo inaaminika kuwa ni albamu bora ya kundi hili. Albamu hii sio tu ilivunja rekodi ya mauzo ya kundi hili bali pia iliwafanya kupata mialiko mbalimbali ya kimataifa ikiwepo Tanzania. Pia album hii iliwafanya kuchukua tuzo nyingi Afrika ikiwepo tuzo ya Kora kama kundi bora la mziki kwa Afrika.

Baadae walitoa albamu yao ya tano iliyokuja kujulikana kama Shalai na ndiyo ilikuwa albamu ya mwisho kwa Rapa wa muda mrefu wa kundi hili Kila Mbongo baada ya kujiengua na kundi hili na kuchana na mziki. Pia ilikuwa ni albamu ya mwisho kwa Abilissi. Pia katika albamu hii wanamziki kama Papy Batin Maboulango na Boudouin Massipi walishiriki baada ya kujiunga na kundi hili kwa mara ya kwanza.

Kimya kidogo kilipita kabla ya kutoa albamu ya sita ya kundi hili iitwayo Trop c'est trop huku rapa akiwa ni mpya baada ya Kila Mbongo kuacha muziki. Rapa huyu mpya aliitwa Arafat.
Baada ya albamu hii ya sita ya, kundi hili lilibadili jina na kuwa Extra Musica Zangul.

Mwaka 2004 wakafanikiwa kutoa albamu yao ya saba iitwayo Obligatoire. Mwaka huohuo baada ya kutoka albamu hii Dou Dou Copa Alijitoa na kuwa mwanmziki anayejitegemea (solo Artist) na Oxygene alijitoa mwaka 2005 na kuunda kundi lake la Universal Zangul huku akiondoka na baadhi ya wanamziki ambao walikuwa hawapati nafasi ya kuimba katika Extra Musica Zangul.
Pamoja na kuondoka Oxygene na Dou Dou Copa bado kundi hili lilitoa albamu yao ya nane mwaka 2006 iitwayo La Main Noire na albamu ya tisa ambayo nikama ya Roga Roga iitwayo Sorcellirie(Kindoki) na imetoka mwaka 2011.

Kwasasa kundi lipo kisasa zaidi na linapiga Rhumba ya kisasa zaidi huku rapa wake ni Zaparo. Wanamziki wa awali waliopo mpaka leo ni Roga Roga,Espe Bass, Ramatoulaye na Herman Ngassaki. Pia kwa habari zisizoaminika ni kuwa Rapa wao wa zaman Kila Mbongo naye amerudi kundini. Mwaka jana 2013 HermanNgassaki alitoa nyimbo kadhaa kama solo artist lakini bado yupo na kundi hili. Wasiomjua Herman Ngassaki waangalie wimbo Etat-Major mwishoni anavyokata mauno.

Zifuatazo ni Albamu za Extra Musica na nyimbo katika albamu hizo tukianza na albamu ya kwanza mpaka ya mwisho.

v 1995 Album Les Nouveaux Missiles
- Amie reviens (Duller Loemba)
- Chagrin plus plus (Pinochet Thierry)
- Detresse
- Dieu L'eternel (Roga Roga)
- Freddy nelson (Quentin Moyasko)
- Na Ko Bala Yo Na Ko
View attachment 136084
v 1996 Album Confirmation
- Success Extra
- Inondation
- Angela
- Ziya
- Denide
- Etape
- Kende
- Love in love
View attachment 136085

v 1997 Album Ouragan
- Losambo
- Melenge (Roga Roga)
- M'ere S (Duller Loemba
- Panique totale (Quintin Moyascko)
- Reconnaissance (Espe Bass)
- Lolango (Duller Loemba)
- Hommage (Roga roga)
- Generation Mechante (Oxygene)
View attachment 136086

v 1998 Album Etat-Major
- Etat-major
- Raccine (Roga Roga)
- Patience (Kila mbongo)
- Vertige D'amour (Ramatoulaye)
- Villegiature
- Plus tard(Abillisi)
- La plule (Roga Roga)
- Ecart (Dou Dou)
- Cri Du Coeur (Oxygene)
View attachment 136087

v 1999 Album Shalai
- Aministe Shalai
- Matongi
- A vous de voir
- Complainte
- Horizon 2000
- Laissez passer
- Ndzima
- Sissi limperatrice
- Solitude
- Tu me manques(Abillisi)
- Zineba
View attachment 136088
v 2001 Album Trop C'est Trop
- Trop c'est trop
- Gambala
- Zangul Zangul
- Moselekete
- N'julie
- Guivano
- Papato
- Polemique generale
- Probleme sur problem
- 12 Balles
- Zongi Sanga
- Bikisa Nga' (chez Ntenda)
- Kared Amour
View attachment 136108
v 2004 Album Obligaitore
- Obligaitore
- Honorablement
- Epaka
- Racini II
- Gyrophare
- Aigle Impérial
- Rufin Bouka (Oxygene)
- Radoutable
- Boss chez Trimba
- Foundation Muller
- L'oublier
- Honorablement
View attachment 136109
v 2006 La Main noire
- La main noire
- Racine III
- Rosalain
- 72 minutes de silence
- Mban-Antoine
- Eternite d,amour (Espe Bass)
- Magomboro
- Noces de bois(Roga roga)
- Parfum mondial
- Petit mais costaud
- Mack Serge
View attachment 136110
v 2011 Sorcellerie (Kindoki )
- Sorcellerie
- Kindoki
- La sape
- Le meilleur
- Marriage
- Les gouts et les couleurs
- Congo United
- Brice Anga Golo
- Flo Miokono(Roga roga)
- Jules Maswa
- Gael Bitoma
- Racine IV
- Gaetan Kodia
- Supreme
- Musicien
- Vrai PDG
- Rosalin
View attachment 136111

View attachment 136113View attachment 136114View attachment 136115View attachment 136116View attachment 136117View attachment 136123View attachment 136124View attachment 136125View attachment 136126View attachment 136127View attachment 136128View attachment 136129View attachment 136130View attachment 136132

View attachment 136083
Sehemu ya pili itahusu nini wanafanya Extra Musica International, ZI International, Universal Zangul, Dou Dou Copa na Guy Guy Fall.
More information & Contacts ................Bislisk@yahoo.com

Kaka Mbeya Hawajambo Lakini? Naona Umeamua Kutoka Kivingine na Kufunguka Zaidi. Naona Umelitendea Haki Jina Lako. Hongera Sana Kwa Uchambuzi Wako Mzuri na Nimekukubali na Hakuna Ulipokosea ktk Maelezo Yako ila Sasa Nitaomba Uje na Uchambuzi wa Kina wa Bendi Yangu Kipenzi Ya Wenge Musica BCBG Chini Yake Jean Bedele Tshituka Mpiana a.k.a ( Munkulu Ya Bamukulu, Leadere Charismatique, Souverein, Papa Cheri, De La Patria, Lonkia Milo Da Nkoko, Excel De Ja Pon, Moto Pamba ) Nitashukuru Sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Nisalimie huko Kwa Wambeya.
 
Kundi hili lilianza miaka ya 1990's hivi wakati huo lilikuwa likipiga ktk kumbi za starehe nchini Congo Brazzaville kwa kurudia nyimbo za wakongwe kama akina tabu ley, Franco etc

Ieleweke kuwa lilikuwa na waanzilishi kama ulivotaja yaan hao wawili ambao ndyo walotafuta wenzao wenye vipaji.

Alikuwa ni gii gii falley in French, English anaitwa Guy guy fall alotoa wazo la kulifanya kundi hilo liachane na upigaji wa kumbi za starehe.

Mwaka 1993 walotoa album hyo kweli... jambo lililowastua wakongwe wa muziki congo kuwa hawa vijana si wao bali wanaiba kaz za watu na hasa wenge musica ndo walishutumu sana kund hili...

Vijana hawa hawakukatishwa moyo wakaja na album ya pili.. confirmation...
Kuuthibitishia ulimwengu na ndpo hapa walipa heshima kubwa sana nchini mwao na baran Africa kiujumla na ulimwengu wote.

Ieleweke kuwa ktk album ya kwanza ilipotoka kulitokea msuguano wa madaraka kati ya roga na guy kuwa nan aongoze kundi hlo... jambo hili lilipelekea guy kuonwa kma mwenye uchu wa madaraka ilihali amewakuta humo wakingwe wa kund...

Ukisikiliza album ya pili ni kama Guy fall hasikiki na Christian ambe lakn ukiwa makini utawaskia hapa wawili hawa hawakupewa nafas kubwa sana na pia kunaskika sauti ya doudou copa kwa sana aloletwa kundin na guy akitokea Roman Catholic kma mwanakwaya.

Ni baada ya msuguano huo Guy fall alikuwa wa kwanza kuondoka na kuwa solo artist... baadae waliuata watu watatu akiwemo dullel loemba, Christian ambe na Quentin moyasco sambamba na waimbaji wengne walokuwa benchi toka kwa roga.

Wakali hawa watatu walitoka na album ya super helico ambayo pamoja na ubora mzur ilivuma kidogo sana baadaya hapo walikwazana kimaslahi na alikuwa dullel na cChristian walotoka na kuunda Z1 international extra musica ikipewa jina la ERE D'E VERITE -Wakimshutumu Quentin kuwa si mkweli... neno hlo hapo juu lina maana ya yeye si mkweli...

Na baadae Quentin hakujibu mapigo zaid aliwambia MERCE -akiimaanisha asanten kwa shutuma zenu.

Christian ambe hajafa kimzk ndo kiongoz wa kund la Z1 huko anaitwa papa lutumba akiwa na dullel ambaye pia hukodiwa wakati mwingn na Quentin kpiga rythm gitaa.
 
KUna mengi tungeongea humu natumia simu sna computer
 
Maelez ya nyongeza ni kuwa...
Huyu sonor digital na herman ngasacky ukitizama vizuri album ya kwanza na hsa kibao kile cha ukumbn utawaona pia kibao cha kanisan pale yan dieu et...... utamwona abilisi nyma hawa ni moja wa waimbaji walokuja chukua nafas za wakongwe wa kundi lile walikuwa ni vijan wazur sana lakn walikosa nafas hivo wakabak kuwa na mapenz mema na kund lao had wakasajiliwa
 
Kuhusu kila mbongo huyu yeye ni mtumishi mwema sana wa kundi hili na kama hujui ama la ni kwamba ma rapper wengi hupatwa na tatizo la sauti ktk zao za sauti kwa sababu ya kugeuza mara kwa mara sauti zao ili kuleta radha zao ktk koras...

Hyu kma utakumbuka album yke ya mwisho ilikuwa shalai na ktk album hii ndo aliletewa msaidiz baada ya yeye kukiri kuwa sasa anatatizo la sauti kuanza kukoroma... mskilize nyimbo za awali na za mbelen hasa mwishon utagundua hlo tatizo.

Ikamlazmu akafanyiwe upasuaji wa koo la hewa na sauti nchini France na sasa anaendelea vema..

Sina uhakika kma kweli amerudi kundn mwaka jna lakn zaid naona rogaroga akimpa heshma jukwaan had leo hii na ni mtu mwema sana kwakweli
 
Kimsingi nawapenda sana watu hawa ktk makundi haya

QUENTIN, DULLEL, CHRISTIAN AMBE
 
Kaka Mbeya Hawajambo Lakini? Naona Umeamua Kutoka Kivingine na Kufunguka Zaidi. Naona Umelitendea Haki Jina Lako. Hongera Sana Kwa Uchambuzi Wako Mzuri na Nimekukubali na Hakuna Ulipokosea ktk Maelezo Yako ila Sasa Nitaomba Uje na Uchambuzi wa Kina wa Bendi Yangu Kipenzi Ya Wenge Musica BCBG Chini Yake Jean Bedele Tshituka Mpiana a.k.a ( Munkulu Ya Bamukulu, Leadere Charismatique, Souverein, Papa Cheri, De La Patria, Lonkia Milo Da Nkoko, Excel De Ja Pon, Moto Pamba ) Nitashukuru Sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Nisalimie huko Kwa Wambeya.

Usijari baada ya sehemu ya pili ya hawa jamaa,nitakuja na Wenge generation( bcbg,el paris, maison mere,bles bula etc)
 
Kundi hili lilianza miaka ya 1990's hivi wakati huo lilikuwa likipiga ktk kumbi za starehe nchini Congo Brazzaville kwa kurudia nyimbo za wakongwe kama akina tabu ley, Franco etc

Ieleweke kuwa lilikuwa na waanzilishi kama ulivotaja yaan hao wawili ambao ndyo walotafuta wenzao wenye vipaji.

Alikuwa ni gii gii falley in French, English anaitwa Guy guy fall alotoa wazo la kulifanya kundi hilo liachane na upigaji wa kumbi za starehe.

Mwaka 1993 walotoa album hyo kweli... jambo lililowastua wakongwe wa muziki congo kuwa hawa vijana si wao bali wanaiba kaz za watu na hasa wenge musica ndo walishutumu sana kund hili...

Vijana hawa hawakukatishwa moyo wakaja na album ya pili.. confirmation...
Kuuthibitishia ulimwengu na ndpo hapa walipa heshima kubwa sana nchini mwao na baran Africa kiujumla na ulimwengu wote.

Ieleweke kuwa ktk album ya kwanza ilipotoka kulitokea msuguano wa madaraka kati ya roga na guy kuwa nan aongoze kundi hlo... jambo hili lilipelekea guy kuonwa kma mwenye uchu wa madaraka ilihali amewakuta humo wakingwe wa kund...

Ukisikiliza album ya pili ni kama Guy fall hasikiki na Christian ambe lakn ukiwa makini utawaskia hapa wawili hawa hawakupewa nafas kubwa sana na pia kunaskika sauti ya doudou copa kwa sana aloletwa kundin na guy akitokea Roman Catholic kma mwanakwaya.

Ni baada ya msuguano huo Guy fall alikuwa wa kwanza kuondoka na kuwa solo artist... baadae waliuata watu watatu akiwemo dullel loemba, Christian ambe na Quentin moyasco sambamba na waimbaji wengne walokuwa benchi toka kwa roga.

Wakali hawa watatu walitoka na album ya super helico ambayo pamoja na ubora mzur ilivuma kidogo sana baadaya hapo walikwazana kimaslahi na alikuwa dullel na cChristian walotoka na kuunda Z1 international extra musica ikipewa jina la ERE D'E VERITE -Wakimshutumu Quentin kuwa si mkweli... neno hlo hapo juu lina maana ya yeye si mkweli...

Na baadae Quentin hakujibu mapigo zaid aliwambia MERCE -akiimaanisha asanten kwa shutuma zenu.

Christian ambe hajafa kimzk ndo kiongoz wa kund la Z1 huko anaitwa papa lutumba akiwa na dullel ambaye pia hukodiwa wakati mwingn na Quentin kpiga rythm gitaa.

kweli kaka vipi huyu jamaa Abilissi wapi habari zake?
 
Kimsingi nawapenda sana watu hawa ktk makundi haya

QUENTIN, DULLEL, CHRISTIAN AMBE

Vipi sauti ya Oxygene, Abilissi na Dou dou copa hazikugusi? Kiukweli christian amba hata mimi ananikosha sana hasa katika chagrin plus plus kipande anachoimba yeye balaa tu, Oxygene nampenda sana tena enzi zili akiimba na Quintin Moyascko wimbo kama Nakobala yo nako mambo yalikuwa poa.
 
Kiukweli abilissi huwa nampenda sana lakn kila nimwonapo akiimba huwa naumia sana make hunikumbusha Christian ambe na nazan alifuata nyayo zake kwa sauti.....

Doudou copa nampenda sana ana sauti ambayo inapendeza kwa rumba sana na kibwagizo sana...
 
Nikweli kabisa Abilissi kisauti alifanana sana na christian,sawa na Herman Ngassaki manu manu don mfumu alivyofanana kisauti na Guy guy fall. Na nadhani hii hufanywa makusudi ili kutopoteza identity ya kundi especially wanapotaka kupiga nyimbo za zamani.Lakini bado hujasema Abilisi wapi habari zake zilipo?
 
Back
Top Bottom