Wanamgambo wa kiislam wadai wapo Tanzania

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,331
16,322
Kundi la wapiganaji wa kiislam limedai kua lipo tanzani hilo limeandamana na vidio inayosambaa katika mtandao wa tweeter ya dk 5 linalowataka waislam wa taifa hilo kujiunga na harakat zao
Wapiganaji hao katika vidio hiyo wanadai wapo mkoani tanga

Mwandishi wa bbc anaeangazia masuala ya usalama barani afrika tomi oladipo anasema hakuna ushahidi kua wapiganaji hao ni wa islamic state

Source BBC swahili

05d47c6a2fa330c5b0ee6e893f9e60e1.jpg
 
,kwanini hawajaenda misri,chad,djibout mpaka waje tanzania na wakati wanajua tanzania ni non-religious country
 
Hawa jamaa hata kama wanatania sio wa kuwapuuza hata kidogo, ni bora police wetu wafike yale maeneo yanayoonekana kwenye zile picha.
 
Kundi la wapiganaji wa kiislam limedai kua lipo tanzani hilo limeandamana na vidio inayosambaa katika mtandao wa tweeter ya dk 5 linalowataka waislam wa taifa hilo kujiunga na harakat zao
Wapiganaji hao katika vidio hiyo wanadai wapo mkoani tanga

Mwandishi wa bbc anaeangazia masuala ya usalama barani afrika tomi oladipo anasema hakuna ushahidi kua wapiganaji hao ni wa islamic state

Source bbc swahili

05d47c6a2fa330c5b0ee6e893f9e60e1.jpg
BBC...NI mabingwa wa kuteja attention za watu kwa Habari za kuzusha...
 
Mnazidi kusahaulishwa khs lugumi na sukari.
Kwa akil zetu hzi ndo itakuwa hot in town
 
Natumai kuona vikosi na spitali Tz vikiwa real bize karibuni (km habari ina ukweli).
 
Umeona mzee mwenzangu yani BBC sio kabisa ni wachochezi pia

Mkuu kitu cha kujiuliza hapa ni, je majority ya watangazaji wa idhaa ya kiswahili ya BBC wanatoka nchi gani?

Kitu kingine why Tanga i.e hizi propaganda za kuonyesha Tanga si salama lengo lake ni nini? Kuwatia hofu wawekezaji na watalii tukiweka maanani kwamba mahandaki yenyewe yanakwenda mpaka Mombasa - mimi sichukulii kama hili ni suala la Waislaam wenye itikadi kali, mbona tunaishi na Waislaam wa sect tofauti hatuna tatizo nao sisi.

Nashauri vyombo vya Dola viangalie saula hili kwa jicho la tatu.
 
Kuna watu wamekosa bomba kwa sababu wawekezaji wamekwepa magaidi ya alshabab huko kwao, sasa iweje baada ya bomba kuhamia Tanga eti na haya mafal.a nayo yameibukia hapo hapo! Alshabab wanadai kenya itoke somalia, sasa hapo Tanga magaidi yanadai nini? Kama kuna hujma flani vilee?
 
BBC imeegemea sana upande wa Majirani zetu up north. Isije ikawa ni state sponsored propaganda because majirani zetu bado wanauguza jeraha la kunyimwa bomba la mafuta!
Just saying!
 
Back
Top Bottom