WanaJF nipeni kazi au kibarua, maisha ya malezi yasije nishinda kuhudumia

Toto mol

JF-Expert Member
Oct 18, 2022
2,404
3,567
Habari za humu ndugu wana JF natumaini wazima wa afya na tunasonga mbele, kama kichwa cha habari kinavyosomeka,

Wadau nipeni kazi / kibarua nifanye nipate pesa za matumizi za kupata mahitaji ya mtoto mwaka kesho anaanza shule darasa la awali, chekechea, baadhi ya vifaa nimenunua kama kitambaa, t-shirt, begi,

Kilichobaki ni viatu, soksi, ada na mashonesho ya kaptura kwa fundi, kichwa kinapata moto huu mwisho wa mwaka vitu vitapanda bei, wadau nipeni kazi/kibarua nifanye mtu hawezi kukupa hela hivi hivi bure bila kumfanyia kazi!? Nipeni kazi,

Nb: location nipo musoma, sina ujuzi wowote zaidi ya kuelekezwa tu, nipeni kazi/kibarua nijikwamue adha hii😔🙏
 
Back
Top Bottom