WanaJF nawakumbusha UKIMWI upo,tuwe makini kwa hili

OME123

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,441
2,000
Natanguliza amani ya bwana kwenu,na heri ya mwaka mpya.
Awali ya yote nawakumbusha kuwa UKIMWI upo nilikuwa siamini lakini kwenye familia yangu umefika, mdogo wetu wa mwisho mtoto wa kike amepimwa amekutwa nao.

kwahiyo kwenye mchezo wenu huo chezeni kwa umakini. Baada ya kupata hizo taarifa nimeogopa sana. Inatakiwa tutulie na mmoja tulionao.
Aksanteni nawakilisha.
 
R Mbuna

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,162
2,000
Poleni sana mkuu kwa huo mtihani ulioingia kwenye familia yenu.

Mimi nimeshauguza hao wagonjwa kwenye familia yetu mpaka sasa hivi sina hofu sana na huo ugonjwa. Nina dada mdogo wangu wa kike na yeye anao sasa hivi inakaribia miaka sita ila afya yake bado ipo imara tu.

Mshauri tu mdogo wako asiwe na hasira na kuwaambukiza wengine kwani kama imetokea hivyo ni sawa na ajali tu na huo ugonjwa sasa hivi sio ishara ya kifo kwani watu wanaishi na wanazaa na familia inakuwa salama kabisa.
 
Farudume12

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
623
500
Natanguliza amani ya bwana kwenu,na heri ya mwaka mpya.Awali ya yote nawakumbusha kuwa UKIMWI upo nilikuwa siamini lakini kwenye familia yangu umefika, mdogo wetu wa mwisho mtoto wa kike amepimwa amekutwa nao.kwahiyo kwenye mchezo wenu huo chezeni kwa umakini.Baada ya kupata hizo tarifa nimeogopa sana.Inatikiwa tutulie na mmoja tulio nao.Aksanteni nawakilisha.
Watu wanapiga miaka 20 wakonao ukimwi. Kikubwa nikula vizuri, Fanya mazoezi, na tumia dawa kwawakati. NB: malaria yanauwa zaidi kuliko ukimwi.
 
py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,469
2,000
Hawa mademu wanaangalia pochi sana
Ndio maana wanapotea

Huku kitaa kuna madalali Fulani wa magari wameungua kila siku wanabadilisha mademu ,mademu wanadanganyika na magari

Na kuna mwingine dereva taxi anawamaliza sana

Mungu awalinde vijana..
Na hizi michepuko doh
 
mensaah

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
985
1,000
Usiogope mkuu... Ukimwi upo, ila haunatena makali kama miaka yanyuma... Relax mkuu
Mkuu mahope ya namna hiyo ndio yanafanya UKIMWI usiishe ila kila mmoja wetu akichukulia kama serious tutaupunguza kwa kasi na hatimae unaweza kuisha kabisa but kila mtu akichukulia kawaida kihivyo utaendelea kumalizia jamii yetu
 
Farudume12

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
623
500
Mkuu mahope ya namna hiyo ndio yanafanya UKIMWI usiishe ila kila mmoja wetu akichukulia kama serious tutaupunguza kwa kasi na hatimae unaweza kuisha kabisa but kila mtu akichukulia kawaida kihivyo utaendelea kumalizia jamii yetu
Ukipigania kuumaliza ukimwi, vipi EBOLA? vipi cancer ya ini?? Ukimwi ugonjwa wakawaida kabisa.
 
Alure

JF-Expert Member
Dec 27, 2014
1,103
2,000
Ukimwi upo ila una wenyewe si kila mtu anapata ukimwi ..... by the way si niliona kwenye gazeti chanjo ya ukimwi imepatikana au zilikuwa story za kurasa za mbele tu
 
Jephta2003

JF-Expert Member
Feb 27, 2008
5,312
2,000
Natanguliza amani ya bwana kwenu,na heri ya mwaka mpya.Awali ya yote nawakumbusha kuwa UKIMWI upo nilikuwa siamini lakini kwenye familia yangu umefika, mdogo wetu wa mwisho mtoto wa kike amepimwa amekutwa nao.kwahiyo kwenye mchezo wenu huo chezeni kwa umakini.Baada ya kupata hizo tarifa nimeogopa sana.Inatikiwa tutulie na mmoja tulio nao.Aksanteni nawakilisha.
Usigope ukimwi,ogopa kansa!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom