Elections 2010 WanaJF: Natangaza nia kugombea jimbo la Lushoto Mjini

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
695
12
Nimechoshwa na ubabaishaji wa wabunge waliopita na aliyepo wa CCM, Shekifu kawa mbunge kwa vipindi viwili lushoto lakini bado huduma kwa jamii kama maji, shule, zahanati na barabara sio nzuri na awamu hii yupo Mshangama nae hakuna analofanya zaidi ya kusinzia bungeni na kuiacha wilaya hii ambayo ina rasilimali nyingi kama utalii na misitu ikiendelea kuwa nyuma kimaendeleo.

Mfano, haiwezekani wilaya kama hii yenye kuzalisha matunda mengi haina hata kiwanda cha kusindika hayo matunda, si hivyo tu bali hakuna sekondari za kutosha kukidhi mahitaji ya wanafunzi wanaofaulu, swala la barabara na lenyewe halifai, tangu wajerumani waweke lami barabara toka mombo hadi lushoto mjini basi hakuna tena barabara ya lami kuelekea maeneo mengine kama mlalo na kwekanga tena yenye vivutio na uwekezaji kama hotel, utalii wa mazingira n.k.

Kwa haya na mengine mengi NATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA KWENYE JIMBO HILI ILI NIWEZE KULETA MAENDELEO KWA WANANCHI WA LUSHOTO.

Naomba mniunge mkono wanaJF wenzangu. Aksanteni.
 
Mkuu hongera kwa uamuzi wa busara..Tuko pamoja nitakuPM ili unipe details zako kwaajili ya updates...
 
Mabadilko hayawezi kuja kwa kupitia CCM ni uamuzi mzuri ni matumaini yetu wengine wetu tuige mfano wako.
 
Hongera sana mkuu naamini huko kwa Wagosi wa Kaya lazima unyakue.
 
Kila la kheri nadhani utakuwa kwenye kinyang'anyiro na Mndolwa lakini huyu atakuwa kupitia Chama Cha Mafisadi
 
Safiii, wakati ukifika jiweke wazi tukupe support. Ndima ni mwenga du ! mgosi
 
Muhimu usimezwe na serikali...ukatapikwa ukwa kama Zitto...!! kila laheri.. mungu akutangulie ktk nia yako njema!:tinfoil3:
 
all the best mkuu.............mabadiliko tunaweza kuyaleta sisi wenyewe tu
 
Aluta continua.... tuko pamoja mkuu.
jamani tufanye mapinduzi ya ukweli kwenye majimbo yetu, mi naona bora kumchagua kiongozi mwingine kabisa kuliko hawa waliopo sasa manake nikichefuchefu kitupu, tuacheni uwoga tutumie haki zetu kwa ufasaha tutaogopa mpaka lini mtu unashindwa kutumia haki yako sasa sijui unasubiri kwenda kuitumia kaburini?!!!!
amkeni wazawahalisi.
 
Safiii, wakati ukifika jiweke wazi tukupe support. Ndima ni mwenga du ! mgosi

Kwi kwi!
Unayegombea ubunge kule kwa akina Kibiiti, Bendea na Ngoda, hongera sana.
Tuko pamoja, unapokaribia kuanza kampeni pls PM me nikusaidie mafuta. Mie kwetu pale Jergetal.

Kaibu Mgosi!
 
Hongera kwa uamuzi wako wa kutaka kuwa mwakilishi wa wananchi wa lushoto mjini na najua utakuwa na priorities zako lakini jamani hebu once in politics tuwe wakweli tuyalete hayo mabadiliko katika matendo......!!!lakini nina imani ni mtu makini ambaye hutaweza kurisk more than its worth...Nakuunga mkono!
 
Hii nsafi kwei kwei Zumbe, kama ni mbwai mbwai bwana, ne tivyeomba. Teh Teh he he!!!!


"Moringe wote ni wamasai lakini sio kila mmsai ni Moringe"
 
hongera mkuu, nakutakia kila la kheri.

Nataka nikujulishe tu kuwa kwa sasa jimbo la Lushoto mjini linashikiliwa na Mh Mshangama, ni kipindi chake cha kwanza yule Mh umri umesogea sana lkini bado anataka kuendelea, wakati Mshangama anachukua jimbo alifanya mambo mengi sana kabla ya kuingia ikiwa ni kujenga mashule kwa pesa zake na kusaidia sana jamii, lakini toka ameingia mdarakani amepoteza sana mvuto kwa wananchi wake na amekuwa sio mtendaji kama alivypkuwa kabla, lakini wakati ananchukua ubunge alimshinda Mh Shekifu, mtu ambaye alipendwa sana kabla, zipo hisia kwamba shekifu alizidiwa kete kiaina na Mshagama.

...hayo tuyaache...lakni kubwa ni kwamba sasa Shekifu anataka kurudi tena jimboni na kugombea japo hajatangaza nia rasmi, ila dalili zote ziko wazi kwani hata timu yake ipo inafanya kazi na kwakuwa yey ni kamanda wa UVCCM wa wilaya basi amesaanza kutumia nafasi yake kuzunga jimboni kushawishi arudi, ziara yake imemalizika jana tu,na vita yake na Mh Mshangana imeanza upya kwani Mh Mshangama kashaanza kulalamikia ziara za shekifu jimboni kwake....

Una nafasi nzuri ndugu yangu jipange tu usikate tamaa, anza mapema kujtangaza usiishie hapa JF tu, nenda jimboni, kama potential yako ni kubwa ndani ya CHADEMA waambie viongozi wako wakuunge mkono wakupeleke wakakutangaze chinchini kabla muda haujafika....

Wapo wagombea wengine waliojitokeza kupitia CCM ni kazi yako kuwajua wapinzani wako...

KILA LA KHERI...
 
Hongera Mkuu kuonyesha nia...Ila Chukua kwa umakini ushauri Wa MRALLEN usije ukawa kama ZITTO...ambaye Sii sii Em wamemrubuni mpaka Kafulia...Pia Nakushauri Uwaone viongozi Wa chama waeleze nia Subiri mchakato kubali matokeo Mwishoni
 
Hongera
mnakuunga mkono ingawa kura yangu itaenda kwa rais atakayependekezwa na chadema
 
Back
Top Bottom