WanaJF ingilieni kati huu msala

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
1,637
458
Nimepata kazi sehemu 2:

- Zote ni kampuni changa
- Nina wiki 1 kwenye kampuni A na tayari nina mkopo wa nusu mshahara
- Kampuni B imetoa ofa ya mshahara mara 2 ya kampuni A
- Sina hela za kulipa mkopo wa kampuni A
- Kampuni B nimewaambia kuwa nilikuwa sijaajiriwa
- Bado sijajaza mkataba na kampuni A, na atakuwa adui kama akijua ninaondoka

NIFANYEJE?
 
Sheria inaruhusu kuvunja mkataba wa ajira kwa upande wowote ule,mashari ga kuvunja mkataba inategemea terms za contract zimekaaje, but kwa upande wa mwajiri procedure zabkusitisha ajira ni ndefu saana tofauti na mfanyakazi,
 
Hivi umesoma content? kuna mahali nimesema nina mkataba na mwajiri? naomba wajibu walionielewa. usi mislead
 
Kama ni kweli mbona jibu liko wazi sana ama we unafanya kazi kwa kumridhisha mwajiri ama kwa kuangalia maslahi yako...Fanya kila uwezalo upate ela uwalipe hao A usepe na hata mkataba hauna nao mbona rahisi tu...
 
Huja sign mkataba maana yake huna ajira, kwa hiyo ni juu yako kuamua kurudisha pesa uliyokopeshwa na kujiunga na kampuni B kama kama kipaumbele chako ni Masilahi (Mshahara mnono) lkn kama interest yako ni kufanya kazi na kampuni A bila kujali tofauti ya mshahara unaopata basi waweza kuamua kuendelea na kampuni A sbb ulisha ridhika na kiwango walichokutajia mambo mengine yatajulikana mbele ya safari hasa uchapakazi na weledi wako utakuongezea kipato
 
Sheria inaruhusu kuvunja mkataba wa ajira kwa upande wowote ule,mashari ga kuvunja mkataba inategemea terms za contract zimekaaje, but kwa upande wa mwajiri procedure zabkusitisha ajira ni ndefu saana tofauti na mfanyakazi,
Kwa vyovyote vile kuwalipa haiwezi kukosekana kwenye terms of contract....
 
Nimepata kazi sehemu 2:

- Zote ni kampuni changa
- Nina wiki 1 kwenye kampuni A na tayari nina mkopo wa nusu mshahara
- Kampuni B imetoa ofa ya mshahara mara 2 ya kampuni A
- Sina hela za kulipa mkopo wa kampuni A
- Kampuni B nimewaambia kuwa nilikuwa sijaajiriwa
- Bado sijajaza mkataba na kampuni A, na atakuwa adui kama akijua ninaondoka

NIFANYEJE?
Nakushauri uendelee na uliko kopa ikiwa huwezi kulipa deni kwa sasa.m.
 
Mwajiri ndo kanipa mkuu.
Mkuu mkopo wa mwajiri ni issue ingekua ni wa benki ungehama nao kwenda kwa mwajiri B, huyu A atakua na kigezo cha kukugomea hadi umlioe hela yake, au kama kuna uwezekano fanya mpango upate hela ulipe huo mkopo then ndo uhame vinginvyo kampunii A itakua na kisingizio cha kukung'ang'ania ubaki.

ila nashauri pia uangalie terms and conditions za mkopo husika kama kuna kipengele kinachoeleza kuhusu mtu kuhama au kuacha kazi Je, anaweza kuendelea kulipa akiwa njebya kampuni Aau hadi amalize mkopo ndo asepe.?

Ni hayo tu mkuu
 
Nimepata kazi sehemu 2:

- Zote ni kampuni changa
- Nina wiki 1 kwenye kampuni A na tayari nina mkopo wa nusu mshahara
- Kampuni B imetoa ofa ya mshahara mara 2 ya kampuni A
- Sina hela za kulipa mkopo wa kampuni A
- Kampuni B nimewaambia kuwa nilikuwa sijaajiriwa
- Bado sijajaza mkataba na kampuni A, na atakuwa adui kama akijua ninaondoka

NIFANYEJE?
wiki moja na mkopo juu duh ......too bad......tafuta helaya kuwalipa nenda B, pia uko probabtion au tayari umeanza rasmi...maana 1 week af mkopo hapo fafanua wengi ukiwa rasmi ndiounapata mkopo..
 
Anza kazi haraka kwa B alafu kule A omba likizo ndefu haya mwezi au peleka ID,alafu kule B omba usign mkataba fasta kisha mwisho wa mwezi walipe A kiasi chote ulivuna kutoka B! Alafu waambie A unaenda kusoma nje ya nchi kisha waombe uingie nao mkataba kua utalilipa kidogo kidogo manake umepata scholarship ya kwenda kusoma nje! Wao ni watu km wewe watakuelewa bila shaka
 
Kama ni kweli mbona jibu liko wazi sana ama we unafanya kazi kwa kumridhisha mwajiri ama kwa kuangalia maslahi yako...Fanya kila uwezalo upate ela uwalipe hao A usepe na hata mkataba hauna nao mbona rahisi tu...
Pacodecor mmemzika? Poleeni sana mmeondokewa na mtu muhimu katika chama chenu
 
Sheria inaruhusu kuvunja mkataba wa ajira kwa upande wowote ule,mashari ga kuvunja mkataba inategemea terms za contract zimekaaje, but kwa upande wa mwajiri procedure zabkusitisha ajira ni ndefu saana tofauti na mfanyakazi,
Hivi umesoma content? kuna mahali nimesema nina mkataba na mwajiri? naomba wajibu walionielewa. usi mislead
Una zarau kwel wewe,, yan katumia mda wake kukueleza anachofaham afu unajidai unajua sheet" mbona ungemwelekeza tu""
nenda kampun C basi"" mijitu mingine bhana
 
A huna contract but mkopo kitanzi..pigana tafuta hela lipa..nenda B kapige mpunga mrefu provided nafsi yako ndicho inachotaka!
 
Back
Top Bottom