Wekeza sasa kwa Scandinavia Express ijayo | Biashara ya Mabus

McRiyckeel

JF-Expert Member
Jun 21, 2017
2,066
12,056
Habari Wakuu,
Matumaini yangu mko njema na kwa wale wanaopitia heka heka na magumu Mungu abariki mihangaiko yenu iwe yenye kulipa fadhila la jasho lenu linalochuruzika kila kukicha.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye kiini cha uzi huu.

Kwa miaka kadhaa sasa baada ya anguko la iliyokuwa kampuni bora ya usafirishaji wa Abiria, Parcels na Mizigo ya kati na mikubwa ya Scandinavia Express, hakuja tokea kampuni yenye kutoa viwango vya huduma katika level waliyokuwa nayo.

Hii nikutokana na kuwa wafanyabiashara wengi wanaoingia katika tasnia hii kutokuweka kipaumbele katika utoaji wa huduma nikiwa na maana huduma za kabla ya kupanda basi (kukata tiketi, ukkabidhiji wa mizigo, booking system etc) na zile za baada ya abiria kupanda basi (kauli nzuri, chakula standard, mwendo mzuri wenye kuzingatia mashimo ama matuta usioumiza shingo wala mgongo)

Hivyo basi uzi huu ni special kabisa kwa wawekezaji wote watakaopenda kuwekeza kwenye kampuni tutakayoianzisha ambayo itaenda kuwa zaidi ya ilivyokuwa Scandinavia Express.

Nini tunapanga kuoffer kuweza kufikia ama kuzipita level za ilivyokuwa Scandinavia Express

1.Kutengeneza Private Stand zenye Standards bora kwa gharama nafuu

Hapa ikijumuisha design bora ya kuruhusu bus kuingia, kupark na kutoka kiurahisi.

Sehemu maalumu ya kupokea, kupangilia na kutumia mizigo ambapo tutaongezea na huduma za ziada kama custom packaging design za kampuni yetu ambapo itajumuisha printed sticker zinazoonyesha ni nani anatuma mzigo na nani ndiye mpokeaji....gharama hizi zitakuwa mficho kwenye gharama za utumaji mzigo.

Mfano Wake:
photo_5974089700039834221_y.jpg

2.Printed tickets
Tutatoa Tickets ambazo ziko printed instead ya zile za kuandikwa kwa mkono

3.Door to Door delivery
Baada ya mizigo kufika destination tutaweza kuwafanyia wateja wetu a door to door delivery kwa gharama za chini kuna project special ambayo kwa kuitumia tutaweza kuminimize cost kwenye ufanyaji huu wa delivery.

4.Standard Food na kwa bei affordable
Tutawezesha abiria kuweka booking ya chakula atakachohitaji through applikesheni ambayo bus host atakuwa nayo, gharama za chakula ni mficho kwenye nauli ya kusafiria.
Tutatengeneza simple resteurant ambayo ndiyo itakayokuwa inatengeneza chakula hicho kuhakikisha standards zimezingatiwa halikadhalika hatupotezi hela kwenda nje ya eco-system yetu.

5.Mafunzo kwa Madereva na Hostess
K
abla ya kampuni kuanza rasmi kusafirisha tutawapiga brush la nguvu hostess na madereva wetu, upande wa Madereva kuna special kozi kwa kushirikiana na Scania Tanzania wataweza kuipata juu ya namna bora ya uendeshaji wa Mabus yao etc

na hata baada ya kuanza rasmi kila siku kabla na baada ya safari watapitia kumbusho la mafunzo na msisitizo wa yapi yafanywe ama kutokufanywa kipindi chote cha safari hii yote ni kumaintain standards za huduma.

Haya ni machache kati ya mengi tutakayoweza kuyafanya kuhakikisha huduma zetu zinakuwa bora muda wote.

Mchanganuo wa Biashara kiufupi.
B
iashara ya Mabus si lelemama yahitaji usimamizi yakinifu wa kila siku ...

Nimebahatika kufanya mazungumz na kampuni 5 za watengenezaji wa Mabus,
1.Higer 2. Scania 3.Yutong 4. Asia Star 5. Volvo

Kwa kuzingatia huduma, upatikani wa vipuri, Guarantee ya uhakika gari kuwepo barabari kwa muda mrefu etc

Imeiweka mbele zaidi kampuni ya Scania kuwa chaguo letu bora zaidi

GHARAMA ZA UANZILISHWAJI WA PROJECT HII
1.Mabus 6

Ambapo kwa Scania wanatoa ofa ya mkopo kwa kulipia kianzio cha 25% cha bei ya bus huku mkikubaliana kipindi cha kufanya marejesho aidha siku,week,mwezi ama miezi etc

Bus moja ni Tsh. 710M
25% YA Bus ni Tsh. 177.5M
25% Kwa Mabus 6 ni Tsh. 1.065B

2. 3 (Three) Private Stands/Yard
Target yetu ni kuanza na route moja ya Dar - Dodoma
Hivyo tutakuwa na main two private stands + 1 stand itakayokuwepo Morogoro ikijumuisha na resteurant etc

Kila moja kuanzia gharama za kiwanja, matengenezo na vifaa tunakadiria 100M each hivyo kwa stand 3 itacost
Tsh. 300M

3.Total Cost
6 buses + Stands + Gharama mficho hadi kuanza kuingiza pato la mwanzo = Tsh 1.5B

KWA UZINGATIVU
K
wa watakaopenda kutoa maoni mawazo ama maswali uwanja huu ni wenu.

Uwekezaji wowote kuanzia Tsh. 500 000 unakaribishwa, karibu kwenye project itakayoenda kubadilisha ulimwengu wa usafirishaji Tanzania na East Africa

Mchanganuo huu ni kwa ufupi mno kwa yoyote atakaye hitaji kufanya uwekezaji basi ninaunda group WhatsApp
ambapo nitaweza kutoa ufafanuzi wa vipi faida utakavyoweza kuipata wewe muwekezaji na vipi usimamizi utakavyokuwa

Mshana Jr Bavaria Shimba ya Buyenze Kasie Herbalist Dr MziziMkavu Bujibuji Simba Nyamaume
 
Wabongo wanafundishika na kubadilika?
Watafanya kazi kwa maigizo kipindi cha kwanza baadaye ujuaji, jeuri na kiburi vinawajaa

Nashauri haya:
  1. Ajirini madereva wengi wa kike ni wasikivu
  2. Tumieni changamoto na adha na kero tunazopata abiria kwenye mabasi yaliyopo (tafuteni malalamiko humu, kuna kampuni zimelalamikiwa sana kwa kutoa huduma za hovyo lakini zimeshindwa kuwa discipline wafanyakazi wao kwakuwa tu ni wao pekee wenye mabasi mapya kila mwaka)
  3. Nashauri mabasi mtakayoagiza yasiwe na speakers kila row, yawe na speakers chache kwaajili ya matangazo tu entertainment nyingine za miziki na movies sauti ipite kwenye headphones kuondoa kero ya bus kuwa na kelele tangu mwanzo wa safari hadi mwisho usiku na mchana stress tupu (mfano halisi ni mabasi ya Abood ...kelele hakuna tofauti na bar)
  4. Usafi wa mara kwa mara uzingatiwe
  5. Mabasi yawe na vyoo
  6. Huduma za refreshmentsn
Nina ushauri mwingi wa kutoa kwasasa tafakarini haya machache ambayo nime observe kama changamoto kwa mabasi mengi nchini.
 
Hiyo namba 3 umeongea hoja ya msingi sana. Huwa sielewi ni nani aliwaambia wamiliki na watoa huduma ya mabasi ya mkoa kuwa zile kelele za muziki na mavideo zina umuhimu kwa wateja. Hivi kwann wasiweke mfumo wa earphones ambapo kila mteja atakuja na earphones zake na kutumia.

Ili watu waweze chagua kutumia wanachotaka kutumia
 
🙏
 
Kuna suala la breakdowns kwenye mabus ni kitu cha kawaida sana kipindi kile Scandinavia walikuwa wapo sharp sana kwenye kufaulisha abiria kwenye gari zao.
Kwa gari sita hakikisheni service za gari ziwe za uhakika sio za mashaka
 
Habari Wakuu,
Matumaini yangu mko njema na kwa wale wanaopitia heka heka na magumu Mungu abariki mihangaiko yenu iwe yenye kulipa fadhila la jasho lenu linalochuruzika kila kukicha.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye kiini cha uzi huu.

Kwa miaka kadhaa sasa baada ya anguko la iliyokuwa kampuni bora ya usafirishaji wa Abiria, Parcels na Mizigo ya kati na mikubwa ya Scandinavia Express, hakuja tokea kampuni yenye kutoa viwango vya huduma katika level waliyokuwa nayo.

Hii nikutokana na kuwa wafanyabiashara wengi wanaoingia katika tasnia hii kutokuweka kipaumbele katika utoaji wa huduma nikiwa na maana huduma za kabla ya kupanda basi (kukata tiketi, ukkabidhiji wa mizigo, booking system etc) na zile za baada ya abiria kupanda basi (kauli nzuri, chakula standard, mwendo mzuri wenye kuzingatia mashimo ama matuta usioumiza shingo wala mgongo)

Hivyo basi uzi huu ni special kabisa kwa wawekezaji wote watakaopenda kuwekeza kwenye kampuni tutakayoianzisha ambayo itaenda kuwa zaidi ya ilivyokuwa Scandinavia Express.

Nini tunapanga kuoffer kuweza kufikia ama kuzipita level za ilivyokuwa Scandinavia Express

1.Kutengeneza Private Stand zenye Standards bora kwa gharama nafuu

Hapa ikijumuisha design bora ya kuruhusu bus kuingia, kupark na kutoka kiurahisi.

Sehemu maalumu ya kupokea, kupangilia na kutumia mizigo ambapo tutaongezea na huduma za ziada kama custom packaging design za kampuni yetu ambapo itajumuisha printed sticker zinazoonyesha ni nani anatuma mzigo na nani ndiye mpokeaji....gharama hizi zitakuwa mficho kwenye gharama za utumaji mzigo.

Mfano Wake:
View attachment 2504999

2.Printed tickets
Tutatoa Tickets ambazo ziko printed instead ya zile za kuandikwa kwa mkono

3.Door to Door delivery
Baada ya mizigo kufika destination tutaweza kuwafanyia wateja wetu a door to door delivery kwa gharama za chini kuna project special ambayo kwa kuitumia tutaweza kuminimize cost kwenye ufanyaji huu wa delivery.

4.Standard Food na kwa bei affordable
Tutawezesha abiria kuweka booking ya chakula atakachohitaji through applikesheni ambayo bus host atakuwa nayo, gharama za chakula ni mficho kwenye nauli ya kusafiria.
Tutatengeneza simple resteurant ambayo ndiyo itakayokuwa inatengeneza chakula hicho kuhakikisha standards zimezingatiwa halikadhalika hatupotezi hela kwenda nje ya eco-system yetu.

5.Mafunzo kwa Madereva na Hostess
K
abla ya kampuni kuanza rasmi kusafirisha tutawapiga brush la nguvu hostess na madereva wetu, upande wa Madereva kuna special kozi kwa kushirikiana na Scania Tanzania wataweza kuipata juu ya namna bora ya uendeshaji wa Mabus yao etc

na hata baada ya kuanza rasmi kila siku kabla na baada ya safari watapitia kumbusho la mafunzo na msisitizo wa yapi yafanywe ama kutokufanywa kipindi chote cha safari hii yote ni kumaintain standards za huduma.

Haya ni machache kati ya mengi tutakayoweza kuyafanya kuhakikisha huduma zetu zinakuwa bora muda wote.

Mchanganuo wa Biashara kiufupi.
B
iashara ya Mabus si lelemama yahitaji usimamizi yakinifu wa kila siku ...

Nimebahatika kufanya mazungumz na kampuni 5 za watengenezaji wa Mabus,
1.Higer 2. Scania 3.Yutong 4. Asia Star 5. Volvo

Kwa kuzingatia huduma, upatikani wa vipuri, Guarantee ya uhakika gari kuwepo barabari kwa muda mrefu etc

Imeiweka mbele zaidi kampuni ya Scania kuwa chaguo letu bora zaidi

GHARAMA ZA UANZILISHWAJI WA PROJECT HII
1.Mabus 6

Ambapo kwa Scania wanatoa ofa ya mkopo kwa kulipia kianzio cha 25% cha bei ya bus huku mkikubaliana kipindi cha kufanya marejesho aidha siku,week,mwezi ama miezi etc

Bus moja ni Tsh. 710M
25% YA Bus ni Tsh. 177.5M
25% Kwa Mabus 6 ni Tsh. 1.065B

2. 3 (Three) Private Stands/Yard
Target yetu ni kuanza na route moja ya Dar - Dodoma
Hivyo tutakuwa na main two private stands + 1 stand itakayokuwepo Morogoro ikijumuisha na resteurant etc

Kila moja kuanzia gharama za kiwanja, matengenezo na vifaa tunakadiria 100M each hivyo kwa stand 3 itacost
Tsh. 300M

3.Total Cost
6 buses + Stands + Gharama mficho hadi kuanza kuingiza pato la mwanzo = Tsh 1.5B

KWA UZINGATIVU
K
wa watakaopenda kutoa maoni mawazo ama maswali uwanja huu ni wenu.

Uwekezaji wowote kuanzia Tsh. 500 000 unakaribishwa, karibu kwenye project itakayoenda kubadilisha ulimwengu wa usafirishaji Tanzania na East Africa

Mchanganuo huu ni kwa ufupi mno kwa yoyote atakaye hitaji kufanya uwekezaji basi ninaunda group WhatsApp
ambapo nitaweza kutoa ufafanuzi wa vipi faida utakavyoweza kuipata wewe muwekezaji na vipi usimamizi utakavyokuwa

Mshana Jr Bavaria Shimba ya Buyenze Kasie Herbalist Dr MziziMkavu Bujibuji Simba Nyamaume
Nimefika nipo hapa
 
Bila kuweka route ya Dar - Moro mtatunyima haki sisi wenye uwekezaji Moro tunaosafiri daily kati ya Dar na Moro

Kwanza nikushukuru mno kwa ichango yako, uko very positive kwenye mambo

Tukifanikisha tutakuwa na gari sita ambazo zinapokezana

4 zitakuwa barabarani Dar - Dodoma

1 itakuwa inasubiri kubadilishana kwa safari ya siku inayofuatia Dodoma, ambayo tunaweza ipa ruti fupi pia maybe Dodoma - Kondoa/Arusha/Singida au Iringa then likageuza Mchana

1 Italala Scania kwa Check-Up Saa 4 itaondoka pamoja na gari la Dodoma lenyewe likiishia Morogoro,
na jioni litarudi na Gari la kutoka Dodoma, lenyewe likigeuza tokea Morogoro kuja Dar.

Kupokezana huku ni kuzipa gari mapumziko na muda mzuri wa check-up
 
Mtaji unao kiasi gani brother, au mtaji wako ni hii business proposal?

proposal tu si Mtaji tosha nafahamu hilo, kuna mengi sijayaandika hapa ila yakufurahisha zaidi ni kuwa Business Plan halisi imepitia marekebisho kadhaa na kwa kutaja baadhi ya waliokosoa, kusahihisha ama kupitisha hadi kufikia hapa ni pamoja na baadhi ya waliokuwa wafanyakazi Scandinavia, pia imepitiwa na kutolewa baadhi ya comment na nyongeza na aliyekuwa Managing Director Scandinavia (Mzee Curussa)

hii yote ni kuhakikisha idea hii inaenda kufanya mageuzi mengine kwenye sekta hii ya usafirishaji wa abiria na mizigo
 
2. 3 (Three) Private Stands/Yard
Target yetu ni kuanza na route moja ya Dar - Dodoma
Hivyo tutakuwa na main two private stands + 1 stand itakayokuwepo Morogoro ikijumuisha na resteurant etc

Kila moja kuanzia gharama za kiwanja, matengenezo na vifaa tunakadiria 100M each hivyo kwa stand 3 itacost
Tsh. 300M
Naona kama hiyo figure ni ndogo..
Kwa bajeti hiyo, itawezekana tu kama hizo stand zitakuwa nje ya mji
 
Back
Top Bottom