Wanajeshi na askari police wameviishi viapo

Wanajeshi na askari police wameviishi viapo

Criss

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2011
Posts
1,959
Reaction score
3,172
Kwa upande wa Jeshi sina cha kuongeza kila mtu ameona namna walivyoviishi viapo kwa Taifa lao.

Kwa upande wa police nanyi mmeonyesha kumbe nanyi mpo conscious japo mwanzo nilikuwa nawatazama kwa sura hasi sana.

ufyatuaji wenu wa mabomu ya machozi umedhihirisha kuwa hamkuwa na nia ovu mioyoni mwenu, najua wengi wenu mnavidonda mioyoni, najua hamvutiwi na huu utekaji ,najua mnajua kuwa na ninyi ni zao la hii jamii inayonyanyasika nakubagazwa.

Wengine hapo mmesomeshwa kwa pesa za kaka na wadogo zenu wamachinga ,waendeshabidaboda na hata wakulima.

Najua mnaumia ,mmeumizwa na wengine bado vidonda vyenu havijapoa kwa vitendo walivyotendewa ndugu na hata rafiki zenu kutekwa ,kupakwa mafuta na hata wengine kuuwawa kisha wenzenu wanakuja kujitamba mbele zenu ,tafadhali ,msikubali kuibagaza hii jamii ya chini ambayo kimsingi sote tumejiunganisha nayo.

Ahsante kwa kuonyesha kumbe naninyi mnajitegemea kiakili .

Ongozeni raia maeneo ya kuguswa, tusafishe uchafu.

Tusimame kwa maslahi mapana ya Taifa,vyama vya siasa siyo waajiri wetu.


Tulipambanie Taifa letu.

Keep it up dude💪
 
Back
Top Bottom