Wanajamii, ushauri tafadhali...

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,502
11,248
Wanajamii kuna kisa kimoja kimemtokea rafiki yangu na kwa kweli amebaki kuchanganyikiwa. Kisa chenyewe ni kuwa jamaa ni ana rafiki yake wa kike (raia wa nchi nyingine) ambaye wanasoma naye na wapo karibu sana ingwa siyo wapenzi na wala hawajahi kuwa wapenzi wala ku-do.Huyu binti ana boyfriend wake na wanafahamiana vyema na huyu rafiki yangu, tena maelezo ya binti ni kuwa anategemea kuolewa na huyo boyfriend wake kwa kuwa wanatokea nchi moja na wanapendana.
Sasa kilichomtokea jamaa kwa kuwa wanakaribia kumaliza masomo kisha kila mmoja arejee nchini kwake, binti amemfata jamaa na ombi la kumpatia zawadi ambayo itakuwa kumbukumbu na kwa mujibu wake zawadi ya mimba itamfaa zaidi kwa maelezo kuwa huyu rafiki yangu ni mtu mwema sana na ni kijana mtulivu asiye na makuu na pia ana akili za darasani na hata za maisha hivyo anataka apate mtoto ambaye atakuwa na sifa kama za jamaa ili iwe kumbukumbu yake ya kudumu manake wanaweza wasionane tena.
Huyu mtu ni caring sana kwa kweli kiasi kwamba inapotokea binti akikwaruzana na bwana wake kimbilio lake kubwa ni kwa huyu rafiki yangu na hata bwana wa binti mwenyewe anamuheshimu sana huyu jamaa. Ila kwa hili la mimba anajihisi kuchanganyikiwa na amekuja kwangu kuomba ushauri. Hivyo wadau naomba mawazo angalau nipate pa kuanzia ili kumsevu mwana jamii mwenzetu.
 
huyo binti ni hatari.
mwambie jamaa yako akatae.
Mpingeni shetani, lakini ikimbieni zinaa.
 
Unasema uyo rafiki yako ni mtu mwema!!? uwo wema wake ndo unamfanya ajiulize zawadi ya mimba atoe au asitoe, iyo kali!!Na anachanganyikiwa kivipi?? Girlfriend wa mtu na wanampango wa ndoa yote anajua alafu anaambiwa zawadi ya mimba means to slip with her!! Means anatakiwa kuvuruga uhusiano wa watu!! Alafu uyo binti atamwambia uyo mchumba wake mimba ni ya nani?? Au atambambikia mtoto? Na yeye yupo tayari kuacha damu yake izagae?? Azae mtoto alafu basi??
 
Hayo mambo ya KU-do na mtu fulani ambaye ulimzimia lkn pengine hakujua au hukumwambia yapo sana mashuleni na vyuoni siku za mwisho. Nna dada yangu , mtoto wa baba yangu mdogo alifanya hivyo na ana mtoto sasa yupo darasa la saba baba yake hajulikani yupo wapi kwa upuuzi kama huo. Tukimuuliza anajidai bubu tu na baba yake mzazi hata kumshinikiza aseme hataki. atakayeteseka ni mtoto maana nyie mnafanya starehe, na matokeo ya starehe zenu ni mtoto, na mtoto anahitaji malezi ya baba na mama, mnafanya starehe zenu baadaye mtoto hamjui baba yake, AGHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHH
 
Dont try that..Ni mtego mbaya sana huo!..

Kama anathamini urafiki kati yake na huyo jamaake asikubali kumwabudu shetani...Hivi hajaona zawadi zingine hadi hiyo za uzinzi na kumfunulia dudu yake?..shiiit

Sasa akim'mimba, itakuwaje mbele ya safari?..huyu rafiki yake hatojua kwamba mtoto ni wa besti yake, na aamue kulipiza kisasi kwa namna yoyote?

Matatizo mengine ni ya kujitafutia kabisa...Shetani tunaishi nae hukuhuku kitaa..jamani!!!
 
Not all women are meant to be mothers.
TANMO mambo?
 
Last edited by a moderator:
Madhara ya kumpa hiyo zawadi hawezi kuiona sasa ila baadae atatumia ule usemi wa "ningejua"....
By the way, mi nikiambiwa mtu 'ana akili' basi uwa nadhani ana uwezo wa kutazama athari za vitendo vyake in the future.
 
Back
Top Bottom