Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 33,615
- 40,163
Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Iringa wamepata ajali ya gari leo Februari 5, 2026, wakati wakirejea kutoka kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), yaliyofanyika kimkoa katika Kata ya Idodi, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Kwa mujibu wa taarifa tulizopokea hadi sasa, ajali hiyo imehusisha gari lililokuwa limewabeba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Joseph Nzala Lyata, pamoja na waandishi wa habari akiwemo Frank Leonard, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa na mwandishi wa magazeti ya Serikali; Denis Mlowe wa Fullshangwe Blog; Clement Sanga wa Channel Ten; Herieth Mola wa Mkombozi Online TV; pamoja na Zuhura Zukheri wa Abood TV.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa hakuna kifo kilichotokea katika ajali hiyo. Hata hivyo, jitihada zinaendelea kufanyika ili kupata taarifa kamili kuhusu idadi na hali ya majeruhi.