Pre GE2025 Rais Samia ametoa zaidi ya TSh. Milioni 26 kwa Wahanga wa ajali Mbeya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Sep 4, 2024
171
192
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan amekabidhi shilingi milioni 20 kwa familia nne za marehemu wa ajali iliyotokea Februari 25, 2025 jijini Mbeya na kukabidhi milioni 6 kwa majeruhi sita wanaoendelea kupewa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

1740723912165.png
Salamu hizo za pole kutoka kwa Dr Samia zimekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Februari 27, 2025 na Naibu Katibu Mkuu Ndg John Mongela wakati wa zoezi la kuaga miili ya watu wanne waliofariki kwenye ajali iliyohusisha gari la abiria kampuni ya CRN na gari la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iliyokuwa imebeba viongozi wa Chama cha Mapinduzi na waandishi wa habari wakitokea kwenye msafara ziara ya Mwenyekitiki wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM.

1740723937709.png
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndg Patrick Mwalunenge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dr Tulia Ackson wametoa salamu za pole kwa wafiwa huku wakiahidi kuhakikisha wanafanya kila linalowezekana kurejesha afya za mejeruhi wa ajali wanaoendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.


1740723999581.png
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Kwa hiyo ajali hii ndo imemgusa?
Mbeya tunalalamika kila mara ajali mlima Iwambi, hadi mkatuwekea na matrafiki barabarani wa kuzuia magari yawe yanapita kwa zamu wakati kuna alternative road nzuri tu ya Mbalizi hadi Iyunga hamuitengenezi.
 
Back
Top Bottom