Wanafunzi waislamu watangaza maandamano! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi waislamu watangaza maandamano!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kiparah, Jan 18, 2012.

 1. k

  kiparah JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  NDUGU WANAHABARI
  Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu mola wa viumbewote. Pili tuna kushukuruni kwa kuitikia wito wetu licha ya kuwa namajukumu mengi ya kutoa taarifa kwa wananchi.Kwa mara ya kwanza
  tumeamua kukutana nanyi. Nasi tunatoa taarifa yetu hii kwenu ilimuifikishe kwa Watanzania na wapenda amani wote duniani. Tunakuusienijuu ya ukweli na uaminifu katika kuripoti taarifa hii.Tuna kuusieni
  tena kuripoti taarifa hii bila ya kupotosha maana iliyokusudiwa.Kutakuwa na nafasi ya maswali ili kuuliza ikiwa kunasehemu ambayohaikueleweka.

  NDUGU WANAHABARI
  Tuliowaita ni viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa KiislamuTanzania yaani Tanzania Muslim Students & Youth Association (TAMSYA).Jumuiya yetu inatambulika kisheria na inafanya kazi zake kwa kufuatasheria za nchi.

  NDUGU WANAHABARI
  Jumuiya yetu kama inavyojieleza inashughulika na malezi ya wanafunziwafuasi wa dini ya kiislamu waliopo katika shule, vyuo vya kati navyuo vikuu na vijana wa kiislamu kwa ujumla. Jumuiya hii inawalingania
  waishi kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Uislamu.

  NDUGU WANAHABARI
  Tumeamua kukutana nanyi ili kuzungumzia mambo ambayo yanawapatawanafunzi waislamu waliopo kwenye shule na vyuo vya serikali kwa mudamrefu. Wanafunzi waislamu wamekuwa wakinyanyaswa na kuwekewa
  vipingamizi vya makusudi ambavyo vinasababisha kufanya vibaya katikamasomo yao pindi wakiwapo shuleni.

  NDUGU WANAHABARI
  Sheria ya nchi inaruhusu uhuru wa kuabudu na kuchagua dini. Kwa mujibuwa dini yetu ya uislamu ibada haimaliziki kwa kuingia msikitini nakuswali tu bali Uislamu wenyewe ni mfumo kamili wa maisha. Ibada nikila jambo analolifanya muislamu na linaloridhiwa na Mwenyezi Mungulikiwa katika muundo wa vitendo au kauli za dhahiri na kificho.

  NDUGU WANAHABARI
  Tumepata malalamiko kutoka kwa wanafunzi waislamu wakikatazwa kuvaa HIJABU shuleni,
  Tumepata mashitaka kutoka kwa wanafunzi waislamu wakinyimwa sehemu zakusalia/kufanya ibada ya sala katika mazingira ya shule na vyuo.Tumepata mashitaka juu ya kupangwa makusudi matukio mbali mbali ya
  shule katika nyakati za sala za waislamu. Mfano sherehe za Mahafalizinapangwa kufanyika siku za Ijumaa muda wa sala, Ratiba za mitihanivyuo vikuu hazizingatii muda wa swala ya Ijumaa .kurefusha muda wa
  kusimama mstarini (Parade) mpaka muda wa swala unapita.Wanafunzi waislamu wamekuwa wakikatazwa kuvaa kofia au kanzu baada yamuda wa masomo katika shule za bweni huku wakristo wakiwa wanashinda
  na Rozari masaa 24.Waalimu wanaofundisha somo la maarifa ya uislamu wanawekewa vikwazo
  mbalimbali wakati wachungaji wanapishana katika shule bila vikwazo kwenda kufundisha baibal knowledge.
  Vipindi vya dini vinawekwa katika ratiba za shule muda wa saa saba mchana siku ya ijumaa wakati ambao wanafunzi wa kiislam wanapaswa kuenda msikitini kwa ajili ya swala ijumaa.

  NDUGU WANAHABARI
  Tutatoa mifano kadhaa katika maeneo tofauti ambayo wanafunzi waislamwamefanyiwa madhila, manyanyaso na udhalilishwaji ikiwa ni pamoja na kutukaniwa Mungu wao,mtume wao na kitabu chao (Quran tukufu) na TAMSYA imefuatilia bila ya mafanikio.

  SHULE YA SEKONDARI KIZUNGUZI WILAYANI KILOSA –MOROGORO
  Mwanafunzi wa kidato cha nne, Frank Thobias Cosmas, aliandika waraka ulioukashifu uislamu, Qurani tukufu na Mtume Muhammad Sallalahu alaihi wasallam.Wakati wanafunzi wakristo wakiwa wanaubandika katika mbao za matangazo shuleni hapo na kusambaziana waraka huo Tarehe 13/05/2011 mwanafunzi muislamu Saidi Suleiman aliupata na kuufikisha kwa viongozi wa wanafunzi waislamu na hatimaye malalamiko hayo yalifika kwa mkuu wa shule.Mkuu wa shule alimpa Adhabu Yule mwanafunzi aliye peleka taarifa na
  viongozi wa wanafunzi waislamu walisimamaishwa shule kwa muda wa siku 21, na Yule aliyendika waraka huo alibakishwa kufanya kazi za shule.Tukio hili liliripotiwa kwa Mkuu wa polisi Morogoro, Afisa Elimu
  Mkoa Morogoro na ofisi ya mkuu wa wilaya ambao walipuuza. Hatua hiyo ilisababisha waislamu wa Mkoa wa Morogoro kuandamana kwa amani siku ya Ijumaa tarehe 5 Agosti, 2011.

  PIA SHULE YA SEKONDARI ULONGONI – DAR ES SALAAM
  Siku ya Alhamisi,tarehe 27/01/2011Mkuu wa shule hiyo aliwalazimisha wanafunzi wa kike wa shule hiyo kuvua Hijabu wakati wa zoezi la kupiga picha kwa ajili ya Mtihani wa kidato cha nne.Alifanya hivyo kwa chuki za udini kwa sababu waraka wa baraza la mitihani unaotoa maelekezo ya namna na utaratibu wa kupiga picha kila mkuu wa shule amepatiwa na haukuagiza hivyo.


  SHULE YA SEKONDARI ENGUSERO KIBAYA –KITETO
  Mkuu wa shule hiyo kwa kushirikiana na Kaimu katibu Mkuu wa mkoa wa Manyara kwa barua yake ya Kumb.Na.FA.58/347/01/27 aliwaamrisha wanafunzi wavunje msikiti uliopo hapo shuleni kwa madai ya kwamba katika shule za serikali hairuhusiwi kujengwa nyumba ya ibaada. Lakini sikweli kwa kuwa zipo shule nyingi za serikali zilizo na nyumba za ibada makanisa tena makubwa sana. Mfano Shule ya sekondari Ndanda,
  Shule ya sekondari Umbwe, Lyamungo Sekondari, Pugu Sekondari Dar es salam na karibu shule zote kubwa za Serikali nchini. Huu ndio udini na mfumo kristo unaolalamikiwa na unaoliyumbisha taifa.

  SHULE YA SEKONDARI ALDERSGATE BABATI MANYARA
  Mkuu wa shule hiyo aliwanyima wanafunzi waislamu darasa kwa ajili ya kusomea somo la maarifa ya uislamu na kuwaambia kama wanataka kusoma somo la dini wachanganyike na wakristo ambao wamepewa chumba cha kusomea shuleni hapo, Jambo ambalo ni kinyume na sheria na kanuni za nchi.aidha alipiga marufuku uvaaji wa hijabu shuleni hapo kwa taarifa tuliyo letewa ya 17/03/2011.

  SHULE YA SEKONDARI LUGOBA
  Mwalimu aliwataka wanafunzi waislamu washerehekee Krismas walipokataa akawaambia tutaweka Taarabu maana waislamu mnapenda sana taarabu.Siku ya 21/01/2011 kwa makusudi Makamu Mkuu wa shule hiyo aliingia na viatu katika eneo la chumba wanachotumia waislamu kuswalia na kuwaamuru watoke katika chumba hicho wakati wa swala.Makamu Mkuu huyo alikwenda tena siku ya tarehe 31/01/2011 kwa hasira
  na kundi kubwa lililo sheheni wanfunzi wakristo kwa ajili ya kuwafanyia fujo waislamu waliokuwa wakiswali. jambo ambalo lileta tafrani kubwa shuleni hapo cha kusikitisha ni kuwa ukweli ulipotoshwa
  na hatimaye wanafunzi waislamu walionekana ndio chanzo cha tatizo.

  SHULE YA SEKONDARI ILBORU ARUSHA
  Mwanafunzi Juma Hassan alifukuzwa shule 13/01/ 2006 ikiwa ni wiki tatu
  kabla ya kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita. Sababu ya kufukuzwa
  shule ilidaiwa alimsukuma Mama Mkwizu mwalimu sheleni hapo alipotaka
  kuingia msikitini.

  SHULE YA UFUNDI TANGA JIJINI TANGA
  Mwaka 2006 Mkuu wa shule hiyo bwana T. Z. Kinala amekuwa na tabia ya Kutoa salamu ya HALELUYAH mstarini wakati wa PAREDI huku akijua kwamba wanafunzi walio mbele yake ni mchanganyiko wa waislamu,wakristo na watu wa dini nyingine.Lakini si hivyo tu, Tarehe 24/7/2006 mkuu wa shule alileta kikundi cha kwaya cha kanisa wakati PAREDI na kuimba nyimbo za ibada ya kikristo.
  Wakati alipo kuwa akiongea na wanafunzi wa, katika hafla fupi ya kuwakaribisha kidato cha tano mnamo tarehe 28/4/2006 Pia alitamka wazi wazi kuwaambia wanafunzi waislamu kuwa hapa shuleni hakuna kuswali
  swala tano kwani hii siyo seminari.Mnamo tarehe 18/06/2006 aliwaambia wanafunzi wa kiislamu wanaovaa
  mavazi yanayotambulisha uislamu wao, kama Kofia, Kanzu na Kilemba lau kama angeliwajua asingewachagua kujiunga na shule yake.Mnamo tarehe 02/08/2006 aliwaita waislamu wanaovaa mavazi ya kiislamu kama kanzu kuwa ni Mashoga

  NDUGU WANAHABARI CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
  Madhila haya na manyanyaso hayawasibu wanafunzi wa kiislam waliopo mashule tu lakini hata wale waliopo vyuo na vyuo vikuu pia hawajasalimika hapa tutatoa mfano wa chuo kimoja tu cha Dodoma (UDOM)
  ambako wanafunzi wa kiislam chuoni hapo wamekuwa wakidhalilishwa, kwa kutukaniwa dini yao na mtume wao mfano wa haya ni mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ambapo yalibandikwa matangazo yenye ujumbe unaowatukana na kukejeri uislam na waislam kuwa ni watu wasioweza na wasiostahiki kuongoza,jambo ambalo liliwafanya wanafunzi wakiislam chuoni hapo kuripoti katika uongozi wa chuo na vyombo vya usalama bila ya kupewa msada, hatimae waislam waliamua
  kujitowa katika mchakato huo wa kampeni na uchaguzi wakiwa na nia njema ya kujiepusha na uadui na uhasma baina yao na wanafunzi wa dini zingine, lakini hata hivyo baada ya uchaguzi walitukanwa na
  kukashifiwa wazi wazi na wakirsto wakishangilia kwa kusema Yesu ameshinda na Mohammad ameshindwa katika kona zote za chuo, bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria na mamlaka husika za chuo na serikali.

  NDUGU WANAHABARI
  Tukio kubwa na la kusikitisha kwa wakati huu ni hili la shule ya sekondari NDANDA iliyopo mkoa wa MTWARA wilaya ya Masasi tarafa ya Chikundi kata Mwena kijiji cha Ndanda. Mpaka hivi sasa tunapozungumza nanyi wanafunzi ishirini (20) wa kiislamu wamefukuzwa shule watano (5) wakiwa ni kidato cha tano na kumi na tano ni kidato cha sita ambao wanatarajiwa kufanya mtihani wa mwisho mwanzoni mwa mwezi wa pili.Aidha wengine waliosalimika kufukuzwa shule wamewekewa masharti magumu
  ya kusaini ikiwa wanataka kuendelea na shule hiyo ya serikali.Miongon mwa masharti hayo ni kutojihusisha na dini yao wakiwa shuleni sharti ambalo linapora haki ya kikatiba ya kuabudu.Sababu na kosa la kufukuzwa wanafunzi hao wa kiislam likiwa ni kuuomba uongozi wa shule uwape eneo maalumu la kufanyia ibada (Msikiti) kama vile walivyotengenezewa wanafunzi wakirsto kanisa kubwa shuleni hapo,kulalamika lugha za kashfa na dharau ambazo zinatolewa na mkuu wa shule dhidi ya wanafunzi wa kiislamu uislamu shuleni hapo.

  Kilichowaponza wanafunzi waislamu ni kupinga udini wa mkuu wa shule na upendeleo kwa wanafunzi wakristo, mfano kitendo cha mkuu wa shule kuteua viongozi wa serikali ya wanafunzi kiholela na kiupendeleo kwa wakirsto huku wakitoka nje ya shule wakishangilia na kusema Muhammad ameshindwa katika uchaguzi mwache bwana Yesu atawale shule!!! Haya yamefanyika mkuu wa shule akiyaona bila ya hata kukemea na
  kuwaadabisha wanafunzi wahusika jambo ambalo linaonesha wazi wazi kuwa ni mpango maalum ulio sanifiwa kwa mfumo maalum.

  NDUGU WANAHABARI
  TAMSYA mikoa, wilaya na matawi, shule na vyuo kwa muda mrefu imefanya jitihada mbalimbali za kuonana na wakuu wa shule na watendaji husikaNkatika kadhia hizi na kuishia kupuuzwa bali na kupewa majibu ya kejeli na jeuri. Na baadhi ya wakuu wa shule kuomba msamaha na kuahidikutorudia tena, lakini baada ya muda mfupi hurejea na kuendeleza dhulma na madhila kwa wanafunzi wakiislam kwa kasi ya ajabu.
  Pia walimu walezi wa wanafunzi wa kiislamu au hata walimu waislamu wanao thubutu kuhoji juu ya ubaguzi wa kidini pia huonekana vioja huku wakichekwa na hatimae kupewa adhabu ya kuhamishwa kituo cha kazi kiholela mfano dhahiri ni walimu wawili pekee wakiislam wa Ndanda Sekondari ambao wamefungashiwa virago vyao na kupelekwa vijiji vya mbali kosa lao likiwa ni kutaka haki itendeke baina ya wanafunzi wote,na wakati mwingine walimu waislam hujikuta wakiambulia vichapo na vipigo kama alivyofanyiwa mwalim Halima wa Ifunda sekondari pale alipopinga dhulma, uonevu na udhalilishwaji dhidi ya wanafunzi waislam
  shuleni hapo mwaka 2009 akajikuta anaambulia kipigo kutoka kwa mwalim wa kikristo.

  NDUGU WANAHABARI
  Hapa tumeonesha sehemu ndogo ya madhila yanayowasibu wanafunzi wa kiislam nchini kama mifano tu. kwani ni vigumu kueleza madhila ya kila shule au chuo kwa njia hii. Jambo la faraja ni kuwa kila mtanzania
  anajua haya hata watu wa kawaida pia Kwa kuwa tatizo hili ni la muda mrefu na baadhi ya viongozi wa
  serikali mfano Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Mh. Benjamin Mkapa alipoulizwa juu ya hali ya uwiano wa waislamu na wasiokuwa waislam katika sekta ya elimu alikiri kuwepo matatizo na uduni kwa upande wa
  waislam na matatizo mengi huku akisema kuwa si kosa la serikali bali ni tatizo la kihistoria.
  Sisi wanafunzi wa kiislam Tanzania tunasema wazi na tunao ushahidi kuwa hili si tatizo la kihistoria bali ni mpango maalum uliosanifiwa na serikali ya awamu ya kwanza kwa lengo la kuwadhulumu na
  kuwakandamiza waislam kielimu kwa mbinu mbalimali kama hizi zilizotumiwa na uongozi wa shule ya sekondari Ndanda na wanaharakati wengine wa mfumo kiristo katika sekta zote za elimu nchini.Wanafunzi wa kiislamu Tanzania tunajua kuwa kitendo kilichokifanywa na mkuu wa shule ya Ndanda na Bodi ya shule pamoja na maafisa elimu cha kuwafukuza shule wanafunzi ishirini (20) wa kiislam na wengine
  kuwekewa masharti magumu ya kuacha wito wa dini yao ili waruhusiwe kurudi shuleni si kitendo kipya bali ni muendelezo wa dhulma ambayo walifanyiwa babu na baba zetu ambapo walilazimishwa wachague aidha
  kuacha dini au kusoma, Alhamdul llah tunashukuru kwa kiasi Fulani walifanya maamuzi magumu ya kulazimika kuacha kusoma na kubaki na dini yao kwani kama wangechagua la pili basi huenda nasi leo tusingekuwa
  katika dini ya haki ya uislam. Ama leo hii sisi wanafunzi wa kiislamu Tunasema kusoma ni sehemu ya
  dini yetu kama tulivyoamrishwa na Allah (sw) Quran (96:1-5) kwa hiyo hatutokubali tena kuacha wito wa dini yetu kwa kutenganisha dini na elimu kwani ikiwa tutafanya hivyo basi itakuwa tumefanya dhulma kubwa
  kabisa. Hapa tunawapongeza wanafunzi wa kiislam wa Ndanda sekondari kwa kujitambua na kujua haki zao za kiiman na kikatiba kwa kutoutii uongozi wa kidhulma wa shule ya ndanda pale ulipowalazimisha kuacha
  wito wa dini yao ili wasome, wanafunzi wa Ndanda wamefanya jambo tukufu linalopaswa kuungwa mkono na kuigwa na kila mtu mwema. Na napenda kutoa wito kwa wanafunzi wakiislam nchini kote ya kuwa
  wanapaswa kuwaiga na kuungana na ndugu zao zao wa Ndanda sekondari kwa kutokubali dhulma ya namna yoyote ile.

  NDUGU WANAHABARI
  Kadhia ya Ndanda ni mzito sana ambayo imegusa hisia ya kila muislam na kila mtanzania mpenda amani na haki, ukweli wa hili unathibitika wazi wazi kwa kila mwenye uhuru wa kufikiri kwani vijana wale wa kidato cha sita waliofukuzwa ni nguvu kazi muhimu sana kwa ujenzi wa taifa ambao tayari kusoma kwao wangeweza kuiokomboa jamii na taifa kiujumla.Lakini jambo la kusikitisha ni kuona viongozi wenye dhamana katika
  wizara ya elimu wakilichukulia swala hili kisiasa kinyume na uhalisia wake. Kwa kufanya ziada na uchunguzi wa kubahatisha bila umakini hatimae kutoa taarifa zilizojaa usiasa ndani yake, kuwa eti maamuzi ya
  bodi ya kuwafukuza wanafunzi (20) wa kiislam ni sahihi huku akieleza kuwa amefika Mtwara na kuongea na Bodi ya shule, mkuu wa shule, walimu na serikali ya wanafunzi hatimae wanafunzi wote Paredi bila ya
  kuwaruhusu kuuliza maswali au kutoa maoni yao hatimae kutoa hukumu.Hukumu hii haiwezi kuwa sahihi kwani hajawashirikisha wahusika wa upande wa pili wa mgogoro ambao ni wanafunzi wa kiislam kwa
  kuwasikiliza hoja zao madai yao ya msingi, huku ni kuisaliti katiba ambayo wameapa kuilinda ambayo inarususu uhuru wa kutoa mawazo na kila mmoja kuheshimiwa kwa nafasi yake. Jambo zito zaidi ni kuona naibu waziri anaungana na watu madhalimu waliovunja katiba ya nchi kwa kuwalazimisha wanafunzi kuacha wito wa dini yao ili warudi shule sharti hili linavunja katiba Ibara ya (19:1-2) kinachozungumzia uhuru
  wa imani na kuabudu.Kutokana na uzito na unyeti wa kadhia hii na madhila haya
  yanayoendelea kufanywa dhidi ya wanafunzi wa kiislam nchini leo hii tunapenda tuutangazie uma kuwa sasa basi hatutaki kuendelea tena kudhulumiwa na kunyanyaswa, sisi ni watanzania na tuna haki zote kama
  wanajamii wengine.Kwahiyo tumeitaka serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kufanya
  mambo yafuatayo;
  Tunaitaka wizara ya elimu kuwarejesha wanafunzi wote walofukuzwa na
  wengine bila masharti yeyote ndani ya siku tano (5) kuanzia tarehe
  13/01/2012.

  Tunaitaka serikali kuunda Tume huru itakayo chunguza kero wanazopata
  wanafunzi waislamu katika shule za serikali nchi nzima.

  Tunaitaka serikali kuwawajibisha watendaji wa sekta ya elimu
  wanaoendekeza udini ubaguzi na unyanyasaji kwa wanafunzi wa kiislamu.

  Tunaitaka serikali ithibitishe au ikanushe juu ya madai ya mkuu wa
  shule Ndanda na badhi ya viongozi wa serikali kuwa mashule
  yaliyotaifishwa na serikali, serikali inamiliki majengo tu ama ardhi
  na mamlaka ya matumizi yake yako chini ya Taasisi zake za asili.

  Shule zote za serikali zitenge maeneo malum ya kufanyia ibada kwa
  ajili ya watu wa dini zote.
  Asilimia kubwa ya wakuu washule za sekondari za serikali ni wakristo,
  hivyo basi tunaomba serikali iweke mgawanyo sawa wa nafasi hizo.

  Kila jambo linapaswa kuwa na mwisho, hatuwezi kuendelelea kuvumilia uonevu wa wazi wazi siku zote.Hatuwezi tena kuendelea kuishi kama wanafunzi daraja la pili katika nchi yetu.Lazima haki sawa na uhuru upatikane kwa wanafunzi wa dini zote na sio kukandamiza waislamu. Hivyo basi tunalazimika kupaza sauti zetu kwaNkuingia barabarani kuonesha hisia zetu katika hali ya unyonge wetu

  NDUGU WANAHABARI
  Tunakusudia kufanya maandamano ya amani nchi nzima 20 Januari 2012 ambayo yatapeleka ujumbe kwa kila kiongozi wa Elimu katika mkoa yaani Afisa Elimu Mkoa na waislam wa Mkoa wa Dar es salaam watapeleka ujumbe moja kwa moja kwa waziri wa elimu.Kwa lengo la kutaka azingatie madai yetu ya kutonyanyaswa na kubaguliwa katika shule ya serikali.Lakini hatutoishia katika maandamano iwapo hali ya ubaguzi
  haitokoma.Tutatumia njia nyingine za kujikomboa katika madhila haya.Tunasema“tumenyanyaswa,tumedhaliliswa, tumebaguliwa kwa miaka 50 ya uhuru na tukavumilia na kusubiri vyakutosha leo tunasema inatosha na tumechoka tunaitaka serikali itambue haki,heshima na utu wetu kama wanavyoheshimiwa wanafunzi wa dini zingine mashuleni na mavyuoni.”Tunataka tuheshimiwe kama wanaadamu, kama wanatanzania huru, wanafunzi halali mashuleni na vyuoni kama wananyoheshimiwa wanafunzi wa dini zingine. Tumeanza muda mrefu kudai haki zetu kwa njia za kidiplomasia lakini hatujasikilizwa na leo tunatumia njia nyingine ya kidiplomasia na kikatiba ambayo ni MAANDAMANO ya amani huenda kwa njia hii serikali na jamii itasikia kilio chetu.

  ACHENI KUTUDHALILISHA NA KUTUNYANYASA WANAFUNZI WA KIISLAM MASHULENI
  NA MAVYUONI SASA BASI INATOSHA TUNAOMBA WAISLAM WOTE NA WAPENDA AMANI
  WOTE MTUUNGE MKONO KATIKA MAANDAMANO HAYA YA AMANI.

  Ahsanteni. JAFARI SAIDI MNEKE RAISI WA JUMUIYA YA WANAFUNZI NA VIJANA
  WA KIISLAMU TANZANIA (TAMSYA)

  Changanya na zako
  !
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,795
  Trophy Points: 280
  waislamu mnajizalilisha kwa kweli.
   
 3. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Mmmh haya....kama wakosaji wanajulikana na makosa yao pia..hivi kuandamana au kuwafungulia mashtaka (if applicable) nini kitakua dawa ya kudumu ???

  Tuendelee kujadili
   
 4. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Ni zaidi ya kujidhalilisha mkuu,....hata ukiwaona mashuleni na vyuoni wanafunzi wengi wafuasi wa dini hiyo wanapenda sana kulalamika na hasa kwenye mambo yasiyo ya msingi kama hayo,...wanaacha kusoma ili angalau waelimike wanaitisha maandamano na wanataka ndugu zao wawaunge mkono_utafikiri wanasiasa.
   
 5. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kwa nini kuwe na ulazima wa kujenga msikiti shuleni kama shule yenyewe inatoa huduma kwa wanafunzi wa kutoka madhehbu mbalimbali?
   
 6. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa_natafuta quran ya kiswahili ili nianze kuisoma nijue kuna nini ndani yake,maake asilimia kubwa ya waumini wa dini hii wanapenda kulalamika na vurugu,........inawezekana kuna mafundisho yanayochochea hivi vitu,.........help plz kwa yeyote mwenye nayo.
   
 7. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Angalieni hiyo michango ya kimaajabu hapa!
   
 8. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  unaboa na quot zako za kibazazi!!!
   
 9. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  11 Pia malaika wa BWANA akamwambia:

  "Wewe sasa una mimba nawe utamzaa mwana. Utamwita jina lake Ishmaelia, kwa sababu BWANA amesikia juu ya huzuni yako.
  12 Atakuwa punda mwitu katikati ya wanadamu, mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu na mkono wa kila mtu dhidi yake, naye ataishi kwa uhasama na ndugu zake wote.''

  (Mwanzo 16:11-12)
   
 10. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Udini upigwe marufuku Tanzania au Africa kama tunataka kuokoa jamii yetu... angalia utumbo wa shehe Mtanganyika akijipendekeza Zanzibar mzalendo.net (Kongamano la mfumo Kristo Pemba)
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  nawatakia maandamano mema.

  Na kasirikeni msirudi mashuleni mpaka msikiti ujengwe.

  Hata wakiujenga mwaka 2020,gomeni kusoma mpaka 2020.
  Muone hasara ya nani!
   
 12. Lyamungo

  Lyamungo Member

  #12
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lyamungo sec. hamna kanisa, shule zenye makanisa zilichukuliwa kutoka kwa wakristo kama Umbwe, Ashira n.k.
   
 13. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Maandamano pekee hayatoshi.
   
 14. g

  goodlucksanga Senior Member

  #14
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nipo udom ushahidi wa cd upo ambapo waislam wa hapa chuoni waliongea kuhusu jihadi yakuwa lazima udom iongozwe na saislamu nzkatikz kupitisha majina ya wagombea walipitishwa waislam tuuu, likagundulika uchaguzi ukaharibika uliporudiwa tena nawagombea wakiwa mchanganyiko waislamu kwa wakristo wakristo waliwapigia wakristo na waislam waliwapigia waislam ,sababu waislamu walisha tangaza jihadi na wakristo walitumia roho mtakatifu ,pia waislamu walifanyz vurugu na kumpiga kijana mkristo nusura ya kufa polisi wanajui hiliii.....
   
 15. b

  betty marandu JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 705
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 80
  Napata mashaka sana na dini yao,maana kazi yao ni kulalamika tu.si wanadai wana mungu hawa ?kwa ushauri tu kama kweli mnaamin mnaonewa mwombeni mungu wenu awasaidie acheni mayowe.unatia mfano wa Ndada kuwa na kanisa hata historia hujui Ndanda ilijengwa na nani?acha kulaklama ndugu zangu waishmael tafuten ukweli,na si kusimamisha magar kwa nyuma.
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hawa walimu wamefikia kiwango cha juu cha "udini" i.e. ukristo; wamefikia hatua ya kutisha hawaogopi tena wala hawana nidhamu kwa watoto wa kiislam wala waislam (very shocking and sad stories); tena kibaya zaidi wako kwenye taasisi za umma..

  a. wanawezaje kuwakataza watoto wa kike wa kiislam kuvaa hijab?? wanataka nini hasa? wanaumia nini mtoto wa kiislam kuvaa hijabu kama si chuki binafsi tena cha kiwango cha juu?

  b. Wanawezaje kukataza watoto kufanya ibada kama vile kusali, kufundishwa dini bila bughudha? wanakosa nini kwa watoto kufanya ibada yao? hivi hawa walimu wakristo wana akili kweli? wanawezaje kuvunja msikiti?? hivi waislamu mko hai?

  c. Wanawezaje kukashifu dini na mtume Muhammad?, wamekuwa nao pia wahubiri mashuleni? hivi wanafikia kiwango cha upofu kiasi hichi?

  d.wanawezaje kulazimisha watoto kusherehekea xmass? hivi wanaona dini yao ni superior kupita zote? hivi wakipenda watoto kufanyiwa hivyo na waislamu wenye nafasi kama hizo??, hivi wanawezaje kuongea kwenye paredi la watoto mambo ya haleluya, huu sasa ni ulimbukeni mkubwa..

  Jambo hili likemewe mara moja; na uchunguzi wa kina ufanywe
   
 17. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,116
  Trophy Points: 280
  Naona madai yenu ni uongo mtupu. UDOM uchaguzi wote uligubikwa na uislam, anzia tume nzima ya uchaguzi uislam tupu. Zaidi waliotoa waraka walikuwa waislam ambao walimpiga mkristo anayejua kiarabu baada ya kuusoma na kutafsiri kwa wenzake aliokuwa nao. Nakumbuka mpaka matokeo yalipotoka wakristo wakaanza kuimba mapambio usiku kucha mengine yakisema YESU ameshinda. Labda muwadanganye ambao hawakuwepo. Halafu pia mkiona mnanyanyaswa sana jengeni shule na vyuo vya kusoma peke yenu.
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Here we go again. The Wailers at work. Nyie gomeni tu, andamaneni tu lakini kumbuka mtihani wa kidato cha sita na kwa vyuo vikuu "semisteral exams" are @ hand.

  Zungukeni na pepa likija mfeli hafu msingizie "mfumo KRISTO"
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  si kweli
   
 20. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Dah kwa mwendo huu katiba mpya inabidi waislam tuwaweke kundi maalum (viti maalum bungeni) kuwe na upendeleo kidogo katika nyadhifa za juu kwa kigezo cha uislaam.
   
Loading...