carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 398
- 1,016
Wanafunzi 20 wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari Dkt. Kalemani iliyopo Kata ya Bwongera, Wilaya ya Chato mkoani Geita, wamejeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakati mvua ikiendelea kunyesha.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Hamis Wambura, amesema tukio hilo limetokea wakati wanafunzi hao wakiwa ndani ya darasa wakijikinga na mvua.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Muganza, Dkt. Simoni Charles, amesema baada ya kupokea taarifa za tukio hilo walifika kwa wakati na kubaini wanafunzi 20 wamejeruhiwa, huku watatu wakiwa na majeraha makubwa.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Maiko Kachoma, amefika katika Kituo cha Afya Muganza kuwajulia hali majeruhi hao na kuwapa pole
Chanzo: Tbc digital