Wanafunzi wagoma wakidai kudhalilishwa kingono na walimu, polisi wawatawanya kwa mabomu

KUDHALILISHWA KINGONO! Naona hayo maneno pamoja na JIMBO KATOLIKI yamewekwa/tamkwa strategically! Hao wapuuzi sare rasmi za shule wanaenda kuzi-modify ili zi-fit upuuzi wao; wakiadhibiwa wanaleta visingizio! Timulia mbali wapuuzi hao.
Ni kweli hapa tusishabikie kabisa wanafunzi kwa sababu wamepata sehem ya kusemea wanaweza kufanya hvyo kuhalalisha upuuzi wao...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna excuse yoyote ya kumchania mtoto nguo..huo ni udhalilishaji.
Kama haifai mwambie atoe harafu mpatie adhabu inayostahili hata ikibidi afukuzwe shule.
Lakini kuchana nguo mbele ya wenzake sio poa hata kidogo.
Mi Africa sijui tukoje..tunakuwa na mambo ya kiajabu ajabu.
Sina hakika kama wewe ni mwalimu!!!

Kuna principle walimu wanaijua katika kudeal na baadhi ya makosa kwa mwanafunzi hasa ikifikia mahali anakuwa concord!!! Na hii pia huwa inatumiwa na maaskari sehemu ambayo kuna maandamano!!

Tusiwe wepesi wa kuhukum!! Watoto nao wa siku hizi ni shda kama ilivyoshida kwa walimu wa siku hizi so ili kubalance story uchunguzi utaonyesha nani konk zaidi ya mwenzie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KUDHALILISHWA KINGONO! Naona hayo maneno pamoja na JIMBO KATOLIKI yamewekwa/tamkwa strategically! Hao wapuuzi sare rasmi za shule wanaenda kuzi-modify ili zi-fit upuuzi wao; wakiadhibiwa wanaleta visingizio! Timulia mbali wapuuzi hao.
Point, hao mabinti wa majengo sec wakishonewa sketi wanapunguza, kusoma hawataki wanashinda redstone na black diamond, wazazi wakiwatafutia hostel hawataki wanaenda kupanga magheto ili wawe huru, waalimu wana kazi sana. Hilo kuzalilishwa kingono limeongezwa tu ili kuwakata maini waalimu. Hao watoto hawasomi ni ujinga ujinga tu, wakazi wa Moshi wanalijua hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
shida ya Watanzania ni uongo, mwalimu hawezi kukuchania sketi/suruali bila sababu lazima kuna sababu.
Hiyo adhabu ya kuchanikiwa sketi inatambulika na mamlaka husika au ni utashi tu wa Mwalimu?
 
Wazazi ndio wa kulaumiwa ina maana hawaoni mtoto anavaa nguo gani?? Kama wazazi wamekubari huo upuuzi basi jamii ndio inataka hivyo walimu hawana budi kuvumilia.
 
hahaahha mkuu acha utani basi, kuvaa sketi fupi ni mwanzo wa kujidharilisha ni mwanzo wa kuidharilisha shule pia

umeshonewa sketi ndefu unaikata unataka fupi yenye kukuweka wazi wazi ukiwekwa wazi et umedharilishwa duuuh
Kwa Hiyo ni bora wachaniwe wawe mapaja wazi kabisa wakiwa wanarudi nyumbani?

Nakumbuka kulikuwa na mgogoro wa kimavazi UDSM mambo ya pekosi na raizoni...wahadhiri waliwashamoto Sana na wanafunzi..Mwl. J.K aliingilia kati kasema wacha wavae tu watakavyo.

Kuvaa nguo Fupi ni kosa, ila kumchania mtoto nguo atembee uchi ni kumuweka vulnerable Zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bila ya kujua sababu ni nini?

shida mimi nimehisi "ni sketi fupi" lakini kama zinashonwa hapo na vipimo wanafahamu kwa nini uichane

kama zinashonwa hapo wana haki 100% kulalamika, ila kama zashonwa mtaani wajirekebishe washone zinazo endana na taratibu za shule.
Mkuu wanafunzi wanakata baada ya kushonwa.....chezea kizazi cha digitali , mdogo wg alirudishwa nyumbani arudi na wazazi ikabidi nimrudishe kwa niaba ya wazazi mzee alikuwa busy kufika kesi ya kuvaa sketi fupi ...kumbe dogo anazo nyingi anabadilisha cjui njiani cjui shule coz nyumbani akitoka anavaa sketi ndefu akifika anabadilisha ikabidi nimbane duh...Ana sketi kma tano hvi zingine za kimodomodo wakati mm nilimnunulia mawili .....nilichoka sana hawa watto wa kike tuwaombe tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni haki wakichaniwa. Watu wanabana surual ambayo kuvaa wanavaa kwa tabu, huko chini imebana kama soksi.wengine ili ipite huko chini wanaweka na zipu.
Wadada kukata sket ziwe vimini. Nimeyaona sana hayo pale. Dawa wachaniwe hivyo hivyo.
Kuzalilishwa kingono? Wamejizalilisha wenyewe mbona tangu walipoanza kubana na kukata hizo sare zao? Nina ndugu yangu pale na yeye ana huu ujinga.
Halafu kuchaniwa hiyo ipo kila mahali siyo hapo Majengo tuu hivyo hamna jipya wafuate maadili ya shule.

The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.
 
Hakuna excuse yoyote ya kumchania mtoto nguo..huo ni udhalilishaji.
Kama haifai mwambie atoe harafu mpatie adhabu inayostahili hata ikibidi afukuzwe shule.
Lakini kuchana nguo mbele ya wenzake sio poa hata kidogo.
Mi Africa sijui tukoje..tunakuwa na mambo ya kiajabu ajabu.
jamaaa mtoto afukuzwe shule kisa nguo fupi unajua gharama ya hili ulilo pendekeza? walimu sio wehu wana akili na elimu zao mtoto anae taka nguo fupi akatafute huko shule nyingine
 
Haiwezekani Walimu Kuwadhalilisha Wanafunzi Wao Kingono. Zipo Sheria Za Kumzuia Mwalimu Asifanye Upuuzi Huo Ndani Ya Maadili Ya Ualimu. Ikibainika Ni Kweli Adhabu Ni Kali Ikiwa Ni Kufukuzwa Kazi Na Utumishi Kisha Kupelekwa Mahakamani Kushtakiwa Kwa Sheria Za Nchi Na Hatimaye Kufungwa. Sasa Ni Mwalimu Gani Huyo Asiye Na Akili Avuruge Maisha Yake Kwa Kudhalilisha Kingono Wanafunzi Wake? Nidhamu Za Wanafunzi Zinatofautiana Sana Shule Na Shule Ama Kutokana Na Wamiliki Wake Wana Maadili Gani Au Shule Ipo Maeneo Gani. Utakuta Shule Zingine Wanafunzi Ni Wahuni Hawana Nidhamu Na Walimu Wao, Hawasomi Wala Kuandika Kazi Wanazopewa, Wanajadili Mambo Yaliyo Nje Ya Mada, Kelele Mtindo Mmoja Darasani, Misuguano Na Walimu Wao Haishi. Shule Zenye Nidhamu Hukuti Tuhuma Za Aibu Kama Hizi Na Wanafunzi Wanafaulu Vizuri Kwa Sababu Wanasikiliza Na Kuheshimu Walimu Wao
 
Point, hao mabinti wa majengo sec wakishonewa sketi wanapunguza, kusoma hawataki wanashinda redstone na black diamond, wazazi wakiwatafutia hostel hawataki wanaenda kupanga magheto ili wawe huru, waalimu wana kazi sana. Hilo kuzalilishwa kingono limeongezwa tu ili kuwakata maini waalimu. Hao watoto hawasomi ni ujinga ujinga tu, wakazi wa Moshi wanalijua hili.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wakazi wa Moshi ndio walimu na ndio wazazi wa watoto hawa na ndio wanaopashwa kukaa na Bodi ya shule pamoja na uongozi wa wanafunzi na si vinginevyo lakini sio kumwita Waziri wa Elimu eti akatatue ujinga wa wanafunzi wasiokuwa na adabu au kuuita utawala wa jimbo Katoliki upoteze muda kushughulikia utovu wa nidhamu wa wanafunzi, tusikubali kusikiliza upumbafu wao kwa gharama kubwa na kwa level ya juu kabisa bila sababu za msingi, hata hivyo mimi binafsi natoa lawama zaidi kwa wazazi ya kutofuatilia maendeleo ya watoto wao wanapokuwa shuleni na nyumbani na matokeo yake wataletewa bill ya maziwa bila kupenda
 
Kwa Hiyo ni bora wachaniwe wawe mapaja wazi kabisa wakiwa wanarudi nyumbani?

Nakumbuka kulikuwa na mgogoro wa kimavazi UDSM mambo ya pekosi na raizoni...wahadhiri waliwashamoto Sana na wanafunzi..Mwl. J.K aliingilia kati kasema wacha wavae tu watakavyo.

Kuvaa nguo Fupi ni kosa, ila kumchania mtoto nguo atembee uchi ni kumuweka vulnerable Zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app

yaani unarejea UD kutetea hawa wajinga wanao punguza sketi ambayo inatakiwa kufanana na wengine (sare) izo pekosi zilikuwa sare hapo shuleni

basi waruhusu hapo majengo kila mtu aende na sare yake wavae suti, pekosi, raizoni, kanyelamomo ili mradi tu wasome

mtoto wa fm 3 hana tofauti na muhudumu wa baa,anakata sketi kumvutia nani? mwalimu wakiwakaza mnarudi kulaumu tena humu.

kabla ya kuchaniwa tayari amesha punguza na kutembea mapaja wazi (alisha jidharirisha) huo ni mwendelezo tu
 
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limelazimika kutumia mabomu kuwatawanya wanafunzi wa shule ya sekondari Majengo baada ya kugoma kuingia madarasani kwa kile walichodai ni kudhalilishwa kingono na kuchaniwa nguo na walimu wao.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya wanafunzi hao kugoma kuingia darasani, kukataa kula chakula na kukusanyika mbele ya ofisi ya Mkuu wa shule hiyo huku wakitaka uongozi wa shule kufanya utatuzi wa sakata hilo.

Wakizungumza na Mtanzania Digital leo Ijumaa Februari 8, baadhi ya wanafunzi hao wamesema wamechoshwa na vitendo hivyo vya kikatili na udhalilishwaji wa kingono huko wakilitaka jimbo Katoliki la Moshi na Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako kuingilia kati.

Kiongozi wa serikali ya wanafunzi wa shule hiyo Gasto Lucas, amesema kuwa vitendo hivyo wanavyofanyiwa ni vya kudhalilisha utu wao kinyume na taratibu za nchi na wanapoulizia inakuwaje vitendo hivyo vinafanyika wanapigwa.

Kwa upande wake mwanafunzi Anithe Asenga amesema walimu wamekuwa wakiwanyanyasa wanafunzi wa kike na kuwadhalilisha huku wakichawachania sketi zao mbele na sehemu za kwenye mapaja.

“Tangu tumefungua shule hii ni sketi ya tatu nachaniwa tu jamani na sketi nimeshoneshewa hapa hapa shuleni nimelipia sh.20000 kwa kila sketi, “amesema.

Aidha akizungumza kwa niaba ya uongozi wa shule ya sekondari Majengo Mwalimu Mukindia Stephen amesema kuandamana siyo suluhisho hivyo aliwataka wanafunzi hao watawanyike warudi majumbani na uongozi wa shule utakaa na uongozi wa serikali ya wanafunzi kuzungumzia suala hilo.

Chanzo: Mtanzania
hao lazima walikuwa wanavaa vimini, mwl hawez anza kuchana sketi iliyo kwenye viwango vinavyohitajika.vijana nidhamu imeshuka sana,mwl nae ni binadamu na ana mambo mengi ya kufanya.hizo sketi-vimini ilipaswa zikusanywe ziwekwe store,kuchana akiwa amevaa sio wisdom.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimu sio vichaa hapo wanafunzi watakuwa wanachukua suruali walizopewa na kwenda kuzibana,binti nao wanakata sketi wanafunzi wakipita mtaani unakuta hamna tofautina teja au bamedi kwanini wasichaniwe sasa
 
Back
Top Bottom