KERO Wanafunzi wa MASTERS na Ph.D Hosteli za Ubungo - UDSM tunanunua maji ndoo moja Tsh. 1,000

KERO Wanafunzi wa MASTERS na Ph.D Hosteli za Ubungo - UDSM tunanunua maji ndoo moja Tsh. 1,000

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
WhatsApp Image 2026-02-17 at 11.41.08.jpeg
Kumekuwepo na ukosefu wa maji katika Hostel za Ubungo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunapoishi Wanafunzi wa Uzamili (Postgraduate Students) ambao tunasoma Master's Degrees na Ph.D!

Kipindi hiki hali imekuwa mbaya zaidi na tunalazimika kununua dumu moja la Lita 20 kwa Tsh. 1,000 ambayo ni sawa na ndoo moja, Wakazi wa Hostel tukiuliza uongozi wa Wanafunzi na Warden wa Hostel wanatuambia lipo nje ya uwezo wao.

Hali hiyo inatusikitisha sana hasa kwa kuwa sisi ni wapangaji tunaostahili kupatiwa huduma zote muhimu ikiwemo maji.
Screenshot 2026-02-17 122019.jpg

Screenshot 2026-02-17 122036.jpg

Kero hii ni ya muda mrefu, soma pia hapa: KERO - Ukosefu wa huduma muhimu ya maji na intaneti hosteli za UDSM za wanafunzi wa Masters na PhD ni mateso makubwa
 
Hahaha poleni sana hata huku mtaani tena uswaz tunanunua maji kupitia yale magar maalum na bajaji maalum ndoo tsh buku

Hivi hostel Zenu ndio za hapo karibu au kati ya ubungo plaza na stend ya mkoa wa zaman?
 
Unasoma PhD unakaa hostel?

Acha utoto, kama si mkazi wa Dar tafuta nyumba upange. Panga nyumba yenye mahitaji yote muhimu, kama unaishi kwa kujibana tafuta wenzako 'those you cordially click with' mchange pamoja mpange nyumba.
 
Unasoma PhD unakaa hostel? Acha utoto, kama si mkazi wa Dar tafuta nyumba upange. Panga nyumba yenye mahitaji yote muhimu, kama unaishi kwa kujibana tafuta wenzako 'those you cordially click with' mchange pamoja mpange nyumba.
Nusu ukweli nusu si sahihi... Kukaa Hosteli Kwa wengine ni kupunguza mambo ya kujihudumia kama mtu binafsi.

Wengine wapo Hosteli kwa kuwa wanahisi uzingativu (focus) unaongezeka zaidi wakiwa maeneo hayo.

Hapo hoja kuu ni kwamba Dar es salaam hakuna maji haijalishi unakaa Hosteli au mtaani.
 
Mbona huku kigamboni maji yapo kibao
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Kwani kukaa hostel kwa mtu wa masters au pHd ni aibu ??
Ishu hapo ni maji yapatikane ndiyo maana hostel zikawepo.
 
Back
Top Bottom